DED Magu angalia sana Idara ya Elimu Msingi

DED Magu angalia sana Idara ya Elimu Msingi

We
Ngoja tumalizie kukusanya uozo wa DEO Geita vijijini anayejiita Afisa Usalama hafu tuuweke hapa ndio Aaak
QS
Weka mambo hadharani; hata kama ni afisa usalama, hajatumwa kuja kunyanyasa watu. Tena mimi naamini kama kweli huyo DEO wa Geita (V) ni afisa usalama, angekuwa mtendaji bora sana maana angekuwa ameiwa. Mfikishieni taarifa zake Mhe. Msukuma adili nae.
 
Hizi ni fitina kwakua tu hujapata!! Penye ridhiki hapakosi fitina!!

Ualimu ni kazi ya hovyo sana!
Wewe Lusungo hujui usemalo!! Unamdharau mwalimu ambaye ndiye alikufuta tongotongo! Tena inavyoelekea unawachukia waalimu tangu ukiwa shuleni, ndio maana hata uandishi wako unajionyesha!! Unasema: - Hizi ni fitina tu "kwakua" hujapata. Hakuna neno kwakua kwenye kiswahili, bali kuna maneno kwa kuwa au kwa sababu. Kwenye sentensi yako ya pili unasema: - penye "ridhiki" hapakosi fitina. Hakuna neno la kiswahili ridhiki, bali kuna riziki (mahitaji akirimiwayo mtu na Mwenyezi Mungu) na dhiki ( shida, au kutindikiwa).
Nakushauri, kama huna hoja za kupinga mada iliyoletwa humu, ni vema ukasoma tu ukapita kimyakimya kuliko kuandika mambo ambayo yanakufunua udhaifu wako tu.
 
Mheshimiwa DED MAGU salaam.

Napenda kukueleza machache kuhusu Idara yetu ya Elimu msingi kwenye Halmashauri yetu ya wilaya ya Magu kama ifuatavyo:-

Idara ya Elimu wilayani Magu imeyumba tangu alipohama Yesse Kanyuma, aliyekuwa Afisa Elimu Msingi (W) Magu.

Baada ya Kanyuma kuhamishwa; aliletwa Salyankanga kujaza nafasi hiyo. Mzee huyu Salyankanga (sasa amestaafu) alikuwa mla rushwa aliyekithiri; rushwa ya fedha kwa waalimu wa kiume, na rushwa ya ngono na fedha kwa waalimu wa kike.

Huduma zenye maslahi kwa waalimu wa shule za msingi; iwe ualimu mkuu, uratibu au huduma yeyote yenye maslahi kwa Mwalimu, mzee huyo alikuwa haitoi bila rushwa, ama ya fedha au ngono. Ilikuwa heri sana Salyankanga kustaafu maana chini ya uongozi wake aliwanyanyasa sana waalimu wa shule za msingi.

Bazazi huyo Salyankanga, alikuwa akifanya mambo yake hayo akishirikiana na watumishi kadhaa idarani hapo ambao ndio walikuwa kama mawakala wake hususan Johari na Prisca katika kuzikanyaga haki na stahili za waalimu.

Ameondoka Salyankanga ameletwa Madam Glory kuchukua nafasi hiyo, akitokea Ilemela ambako alikuwa Afisa Elimu Taaluma (Msingi).

Glory (mwenye digrii moja) amefika idarani amekutana na Johari na Prisca; wamempika ameiva, wamempa mikakati yao ovu, ameikubali na sasa rushwa na ukandamizaji dhidi ya waalimu wa msingi vinaendelea.

Glory hajiamini kwenye nafasi hiyo; anajua hatoshi, anawapiga vita maofisa wengine wenye elimu (masters) kumzidi yeye mwenye digrii moja akidhani watampoka cheo chake. Anatuamia "kufahamiana" kwake na R.E.O. Mwanza (kama na Johari "anavyofahamiana" nae) kuwasambaratisha maofisa idarani hapo, na anafanikiwa maana tayari ameshamhamisha Afisa Vifaa na Takwimu kwenda Misungwi; na anatamba eti bado mmoja!!

DED Magu, tafadhali shughulikia ofisi hiyo ya elimu maana usipofanya hivyo, hatimae hawa wadada watakuharibia. Yule Afisa aliyehamishiwa Misungwi ni mchapa kazi mzuri, na wewe unajua; sasa manpower hiyo imeondolewa kwa sababu ya majungu tu. Mheshimiwa Mbunge na Waheshimiwa Madiwani; msaidieni DED wetu kupangua watendaji vichomi kama hao wanaotuondolea watumishi mahiri katika wilaya yetu kwa kutumia influence zao na R.E.O. Mwanza.

Naamini hata matokeo ya darasa la VII mwaka huu Magu kushika nafasi ya tatu kimkoa, huyo afisa Vifaa na Takwimu amehusika pakubwa maana alikuwa anatembelea sana mashule na kuhimiza ufundishaji; tarajia mabadiliko Misungwi.

Naomba kuwasilisha; asante.
Sasa kama kahamishiwa Misungwi ubaya uko wapi? Kwani Misungwi wachapa kazi hawatakiwi?
Halafu mind set za wabongo wengi zimekaa hovyo sana. Mtu una masters unakaa kushindana na watu wa vidiploma na degree kwenye uafisa elimu badala ya kutumia elimu yako kutengeneza hela nje ya ofisi. Kusoma ni kuongeza maarifa sio kuongeza majungu!
 
Nyie walimu ni hovyo mno na taaluma yenu imejaa dhiki, laana na taabu.

Mwenzako akipata wamuonea kijicho
Wewe Lusungo hujui usemalo!! Unamdharau mwalimu ambaye ndiye alikufuta tongotongo! Tena inavyoelekea unawachukia waalimu tangu ukiwa shuleni, ndio maana hata uandishi wako unajionyesha!! Unasema: - Hizi ni fitina tu "kwakua" hujapata. Hakuna neno kwakua kwenye kiswahili, bali kuna maneno kwa kuwa au kwa sababu. Kwenye sentensi yako ya pili unaseme: - penye "ridhiki" hapakosi fitina. Hakuna neno la kiswahili ridhiki, bali kuna riziki (mahitaji akirimiwayo mtu na Mwenyezi Mungu) na dhiki ( shida, au kutindikiwa).
Nakushauri, kama huna hoja za kupinga mada iliyoletwa humu, ni vema ukasoma tu ukapita kimyakimya kuliko kuandika mambo ambayo yanakufunua udhaifu wako tu.
 
Sasa kama kahamishiwa Misungwi ubaya uko wapi? Kwani Misungwi wachapa kazi hawatakiwi?
Halafu mind set za wabongo wengi zimekaa hovyo sana. Mtu una masters unakaa kushindana na watu wa vidiploma na degree kwenye uafisa elimu badala ya kutumia elimu yako kutengeneza hela nje ya ofisi. Kusoma ni kuongeza maarifa sio kuongeza majungu!
[/QUOTE
Nionavyo mimi, mtoa mada baya wowote afisa huyo kuhamia
Sasa kama kahamishiwa Misungwi ubaya uko wapi? Kwani Misungwi wachapa kazi hawatakiwi?
Halafu mind set za wabongo wengi zimekaa hovyo sana. Mtu una masters unakaa kushindana na watu wa vidiploma na degree kwenye uafisa elimu badala ya kutumia elimu yako kutengeneza hela nje ya ofisi. Kusoma ni kuongeza maarifa sio kuongeza majungu!
Hakuna ubaya kwa afisa huyo kuhamishiwa Misungwi, maana hata kama ni mchapa kazi huko Kolomije nao wanahitaji hayo maendeleo.
Hoja ya mleta uzi nadhani ni mazingira yaliyosababisha afisa huyo kuhamishwa, ameeleza mwanzoni kuwa ni majungu na kutokujiamini kwa DEO ambaye ametumia influence yake na REO kumhamisha afisa huyo.
Piga picha, je kama watakuwepo maafisa wengine ambayo DEO huyo ana wasiwasi nao kwa kutokujiamini kwake, na yeye ni "mzigo" wa REO si ataendelea kuwapangua hapo ofisini? Huoni kuwa hali hiyo itaathiri utendaji wa ofisi kwa kubadilishabadilisha maofisa bila sababu za msingi? Huoni kwamba ni kuiingiza gharama serikali kwa kulipa fedha za uhamisho usiokuwa wa lazima kwa maofisa.
Lakini, licha ya uhamisho huo yapo pia malalamiko yaliyotolewa dhidi ya DEO na maofisa wengine. Kama ni ya kweli kwa nini DED Magu asiyafanyie kazi?
 
Nyie walimu ni hovyo mno na taaluma yenu imejaa dhiki, laana na taabu.

Mwenzako akipata wamuonea kijicho
Mimi siyo mwalimu na ndiye niliyeleta mada hii. Hata kama ningekuwa mwalimu; sijui wewe unafanya shughuli gani. Lakini iwe iwavyo, nimeshakueleza tangu awali kuwa hujui usemalo maana kwa mtu yeyote muungwana hawezi kudharau kazi ya mtu mwingine. Kazi maana yake ni shughuli halali anayoifanya mtu kwa ajili ya kujipatia riziki ili aendeshe maisha yake.
Unasema kazi ya ualimu ni ya hovyo, ina laana, ina dhiki na taabu; kazi yako wewe ni ipi ambayo haikupi taabu?
Kazi ni baraka wala siyo laana; maana bila kazi utaendeshaje maisha yako? Inaelekea wewe ni kilaza, huna hoja zaidi ya kashfa na huenda huna kazi yoyote zaidi ya uzururaji na u- mission town. Mtu anayejitambua hawezi kusema kuwa kazi ni laana badala ya baraka. Wewe unawazidi nini waalimu? Wanafanya kazi njema na adhimu ya kuwapata watoto elimu (ambayo wewe huna) maana ungekuwa nayo ungejitambua na usingeandika unayoandika. Ni watumishi wa umma, wanalipwa mishahara hata kama ni midogo lakini inawawezesha kujikimu; wana dhamana ya serikali, mwalimu wanaweza kukopa benki mpaka 20M/= kulingana na mshahara wake, anaweza kukopa nyumba, usafiri, ana bima ya afya yeye na familia yake na wazazi wake; mwisho wa ajira yake anatoka na kitita so chini ya 80M/=; wewe una nini na hatma yako ni ipi? Unajilisha upepo tu; pambana na hali yako.
 
Hata Idara ya ELIMU SEKONDARI -MAGU uozo ni ule ule, nipo naunganisha scene nitakuja na mkeka mzima.
 
Yesse kanyuma kashahamishiwa wizarani tangu Sept
Mtiririko wa safari yake ya utumishi unaonyesha mafanikio; alikuwa DEO Magu, akahamishiwa Shinyanga kuendelea kuwa DEO, baadae Geita kama Afisa Elimu Mkoa (REO); na sasa amehamishiwa wizarani. Inawezekana ana majukumu makubwa zaidi ya kikanda au kitaifa, ni mafanikio; hongera Yesse.
 
PM kufanya nini mkuu? Unadhani DED hajui upuuzi wa hao Johari na Glory? Uzi huu sioni kama umewachongea hao maafisa, wao pia wautumie kubadilika maana hata watendaji wa chini yao wasio walimu malalamiko yao DED ameyaona, ameyasikia na amewahi waonya. Hasa Johari alishaonywa live na DED.
Mkuu rkidilu; mimi siyo Afisa Elimu vifaa na takwimu wala si mwalimu. Kama hutajali njoo PM.
 
DODOMA huku watu wanapeleka Hadi 2M wilaya siitaji. Uratibu huu huu
Huyo Mare man anayesema uratibu hauna mafangu yeyote hajafanya utafiti. Mratibu ana posho ya 250,000/= kila mwezi, anapewa usafiri wa pikipiki, anapewa posho ya mafuta kila mwezi hata kama ni 150,000/= akichanganya zinakuwa 400,000/=. Hiyo ni hela ndefu sana nje ya mshahara, ambayo mratibu anaweza kuikopea benki kwa makato ya laki 3 kila mwezi; kwa mwaka ni M3.6/=; akichukua mkopo wa miaka mitano tu anabeba M18/= kwa posho tu; hayo siyo maslahi?
 
Halmashauri, Manispaa, Majiji, kuna majungu na mambo ya ajabu ya sana!
Ahsante Mungu kuniepusha na hicho kikombe!
Wacha tubanane huku serikali kuu
 
Huyo aliyehamishiwa Misungwi hafai kabisa maana ameharibu ndoa za walimu, mtukanaji hakuna cha maana alichokifanya hafai kabisa, tutamkumbua JJ aliyekuwa mtumishi hodari mwenye utu
 
Huduma zenye maslahi kwa waalimu wa shule za msingi; iwe ualimu mkuu, uratibu au huduma yeyote yenye maslahi kwa Mwalimu, mzee huyo alikuwa haitoi bila rushwa, ama ya fedha au ngono. Ilikuwa heri sana Salyankanga kustaafu maana chini ya uongozi wake aliwanyanyasa sana waalimu wa shule za msingi.


Kwanini hukutoa taarifa kwa mamlaka husika zimkamate kwa wakati huo? Ninyi walimu kwanini hampendani?
 
Hapo DED achukue hatua aisee ,lakini pia waalim nao wamezidi umbulula wanashindwa kuyaanika hayo maovu? Mbona viongozi wapo wengi wa kupelekewa taarifa?
Hizo tuhuma hazina ukweli wowote,palipo na mafanikio ..

majungu lazima...D.o anafanya kazi vizuri sana...na Magu imekuwa ya tatu kimkoa sababu ya kusimamia taaluma hUyo AFISA aliyehamishwa ilikuwa na Tabia mbaya....

.uzinzi ...KATEMBEA NA WAKE ZA WATU WENGI,

WENGINE NI WAALIMU AMEWAVUA MPK CHUPI kuwasaidia kupata ruhusa za kwenda masomoni

....na mwisho hata huko alikokwenda bado kuna WAKE ZA WATU KWA NINI ANGANGANIE MAGU TU??? ...HII NI AIBU ABADILIKE
 
Huyo Afisa aliyehamishwa ilikuwa kichomi KBS

KATEMBEA NA WAKE ZA WATU WENGI TABIA YAKE HAIKUWA NZURI KABISA,

WALIMU WENGI WA KIKE KAWALAGHAI KUWA ATAWASAIDIA KUPATA RUHUZA ZA KWENDA MASOMONI

...HATA HUKO ALIKOPELEKWA AENDE TU SI KUNA WANAWAKE...NANI ASIYEMJUA
Ni kweli; acha na mimi nizungumze machache ninayoyajua kuhusu hiyo ofisi ya DEO Magu ambayo imekumbwa na kashfa nyingi tangu enzi za Saryankanga. Huyu DEO wa sasa ni mpiga hela tu; amekutana na mchagga mwezake Johari rushwa mtindo mmoja.
Naanza na mfano mmoja ambao hata DED Lutengano ataukumbuka. Hivi karibuni tu kuna Mratibu (mama mjane) alihamishiwa kata ya Itumbili kwa uhamisho wa malipo. Mama huyo baada ya kulipwa, DEO Glory na timu yake walimtoza yule mratibu pesa kama shukrani kwao!! Mama yule alikwenda kulalamika kwa DED Lutengano; sijui hatua zilizochukuliwa na DED kama zipo.
Wewe mwenyewe DED, siku za karibuni uliitisha kikao cha Finance ambapo wakuu wa idara walikuwepo. Uliwapongeza wajumbe kwa matokeo mazuri ya mitihani ya darasa la VII; na Katibu wa TSD alichangia kwa kuitaka ofisi ya elimu kuwa na ushirikiano miongoni mwao, badala ya kupigana majungu na kuchongeana hadi kufikia kuhamishwa baadhi ya watendaji chapa kazi kama SLO aliyehamishwa alivyopigwa jungu. Baada ya kikao DEO Glory alimfuata Katibu huyo wa TSD na kuanza kumshambulia kwa maneno; mpaka sasa mahusiano ya watu hao wawili siyo mazuri; lakini pia mahusiano kati ya DEO na Mkaguzi Mkuu siyo mazuri vilevile kwa sababu ya ofisi ya DEO kupanga wasimamizi kwa mapatano na baadhi ya waalimu wakuu ili watahiniwa wa darasa la VII katika shule zao wasaidiwe. Kwa mahusiano haya hafifu kazi zitafanyikaje kwa ufanisi?
Palifanyika semina au kongamano la Juma la Elimu ya Watu Wazima kimkoa hivi karibuni kule Buchosa. Maofisa wanne wafuatao:- SLO aliyehamishwa, Afisa Elimu ya Watu Wazima, DEO Glory na Johari walilipwa posho kwa ajili ya kuhudhuria na kushiriki kongamano hilo la Juma la Elimu ya Watu Wazima. Waliokwenda Buchosa ni wawilo tu; SLO aliyehamishwa na Afisa Elimu ya Watu Wazima. DEO Glory na Johari hawakwenda Buchosa licha ya kulipwa posho, wala hawakuwa ofisini Magu siku zote za kongamano hilo. Huyo ni ubadhirifu wa mali ya umma.
Uhamisho wa SLO kwenda Misungwi pia ni ubadhirifu kwa sababu umetolewa kwa majungu. Afisa huyo amekaa Magu kwa muda wa chini ya mwaka mmoja toka alipohamia Magu akitokea Ukerewe na alilipwa. Kwa uhamisho huu amelipwa tena kumhamishia Misungwi kwa sababu tu Glory na Johari wamekwenda kulalamika kwa Afisa Elimu Mkoa Mwanza eti SLO huyo anawanyima raha!! R.E.O. Mwanza nae kwa sababu hao wawili wote ni wapenzi wake (kama hawajui wajijue sasa), akaamua kufanya alivyofanya TAMISEMI hatimae SLO amehamishwa!!
Mhe. Jaffo, Mhe. Ndalichako, Mhe. Mkuchika afande wangu, tafadhali fuatilieni mambo haya; kuna watu bado hawajamwelewa Mheshimiwa Rais wetu mpendwa Dr. John Pombe Magufuli kwamba dhamira yake kwa dhati ya moyo wake amekusudia kuipeleka mbele nchi yetu. Baadhi ya watendaji wanafanya yao tu bila kuzingatia Vision, Mission wala Spirit ya Rais wetu. Nitakwenda Magu kumweleza Rais uozo huu siku akija kuzindua mradi wa maji; tutaonana wabaya.
 
PM kufanya nini mkuu? Unadhani DED hajui upuuzi wa hao Johari na Glory? Uzi huu sioni kama umewachongea hao maafisa, wao pia wautumie kubadilika maana hata watendaji wa chini yao wasio walimu malalamiko yao DED ameyaona, ameyasikia na amewahi waonya. Hasa Johari alishaonywa live na DED.
Mkuu kandukamo1; umeimarisha hoja ya mleta mada na inaelekea uko well informed na kinachoendelea hapo halmashaurini kuhusu ofisi ya DEO.
Inavyoelekea huyu Johari ndiyo mastermind au brain ya hiyo ofisi ya DEO kwa hiyo amewavuta wenzake masikio!! Mkurugenzi anapaswa kufanya kitu sasa!!
 
Back
Top Bottom