Haya mambo yanasikitisha sana. Mtoa Uzi huu ni mmoja ya wenye sifa ila hapewi nafasi nionavyo.
Ushauri wangu.
Unapoteza muda mwingi sana kutaka kupambana na system. Najua unaumia ila tu nikufahamishe serikalini kuna watumishi wazuri sana ila WAPUMBAVU ndio wenye madaraka. Wapumbavu hawapendi WELEVU hivyo huteuana wenyewe ili kulinda madaraka yao.
Nakushauri achana na kugombea madaraka, waachie wenyewe jipe muda utafute pesa ukizipata hutojali mambo ya uongozi. Hebu fikiria 250,000/= hizi hela ndogo sana ukizikosa kwa ajili ya madaraka. Amini maneno yangu kuwa na madaraka bila pesa ni bure tu au tuseme na wewe unataka madaraka ya kwenda kufunulia chupi za walimu?
Wewe Ligaba ni Premium Member kwenye jukwaa hili adhimu la JF; haitarajiwi uandike hoja zisizo na mashiko kama huyo anayetaka picha ya afisa aliyehamia Misungwi eti amzuie asilale na wake za watu!!
Unasema mimi ni mwenye sifa lakini sijapewa nafasi; mantiki ya kauli yako hiyo ni kwamba mimi naandika haya kwa sababu nawaonea gere au wivu Glory mtui, Johari Mwasha na Prisca.
Umekosea, mimi siyo mwalimu wala si mtumishi wa umma. Lakini kutokuwa mtumishi wa umma hakumaanishi kuwa sina uwezo wa kutambua mambo mbalimbali yanayonizunguka kiasi cha kushindwa kuyatathmini na kuyadadavua.
Nina uwezo huo kwa sababu ninayaona, nayasikia na mengine yananiathiri nikiwa raia wa nchi hii ambaye nastahili kuhudumiwa na watumishi wa umma kama madaktari, manesi, askari, maafisa ardhi, mahakimu, waalimu, na wengine wengi. Hawa ni watu ambao wapo miongoni mwetu, tunaishi nao, tunazungumza nao na tunashirikiana nao; kwa nini nishindwe kujua yanayoendelea kwenye ofisi hizo za umma wakati mimi ni mteja kwazo?
Siyo lazima matatizo yanayojiri katika ofisi za umma ziandikwe na mtumishi wa umma; zinaweza kuandikwa na mtu yeyote huru kama mwandishi wa habari, mwanaharakati, au raia yeyote wa kawaida mwenye uwezo wa kupata taarifa sahihi juu ya jambo analotaka kuliwasilisha kwa wahusika, ilimradi ana maslahi nalo; kama mimi nilivyofanya.
Nimemwandikia DED Magu ili achukue hatua ya kurekebisha udhaifu unaoendelea kwenye ofisi ya DEO Magu maana mimi ni mwana - Magu, mzazi mwenye watoto wanaosoma kwenye shule za umma wilayani Magu; kwa nini ninyamazie ubovu unaoendelea kwenye ofisi ya elimu kwenye halmashauri yetu?
Unasema niache kupambana na system!! Glory, Johari na Prisca wamekuwa system ya elimu Magu? Huyo Glory Mtui aachane na ujinga anaoufanya hapo ofisini kwa sababu ya kukamatwa masikio na Johari Mwasha; atamharibia kazi na atakuwa anazimia mara kwa mara hapo ofisini kama ilivyotokea juzi na leo ametinga ofisini akiwa na cannula, wakati mwenzake anadunda na juba lake tu.
Kufua chupi za maofisa wa elimu siyo kazi yangu, ingekuwa kazi yangu ningefua tu!! Wewe ni JF Premium member; mchango wako unatarajiwa kustawisha mjadala kwa kutoa hoja na si vinginevyo.
Bado wito wangu kwa DED Magu ni uleule; aangalie ofisi ya DEO Magu.