Hagwila
Member
- Apr 18, 2019
- 82
- 99
- Thread starter
- #121
Wanapambana kumchafua Majura wakiamini kuwa, kwa kufanya hivyo kuwasafisha Glory, Johari na Prisca.Nimewafuatilia kwa siku kadhaa sasa... Naona mnajaribu kuwa chafua wasiochafuka...
Gidamaa nilisoma maoni yako tangu siku ya kwanza ulivyoyatuma; niliamua kukaa kimya ili niendelee kusoma michango ya wanajukwaa wengine.Baada ya kupitia Mjadala huu Ushauri wangu kwa DED Magu, Ndugu; Lutengano Mwalwiba...
Nakuheshimu sana kwa usikivu wako, uhodari, ubunifu na uchapa kazi wako ukiwa kama Karani Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya Magu...
Aidha, naomba nikushauri ufanyie kazi mambo kadhaa ikikupendeza
1. Maofisa waliokaa zaidi ya Miaka kumi Wilayani Magu, ikikupendeza wakahudumie na Wilaya zingine..
Hapa usimsahau Afisa taaluma Nyakabona.... Yaani huyu awe wa kwanza kuondoka, amesha kuwa Mwananzengo anamtandao mkubwa wa walimu wakuu, walimu, Waratibu elimu kata.. Ni mkongwe sana huyu, wapo aliofundisha nao, wapo aliwafundisha juzi juzi hapa kwenye course zile za kuunga unga..Ha! Ha! Ha! Huoni hapa haguswi na Mtu.. Usisahau kuwa alijiandaa kuwa Afisa Elimu (DEO) utadhani Babu yake ndio anagawa Vyeo, sasa ilipogeuzwa gia angani hajawahi kukubali mpaka leo.. Usipoteze muda mshauri ahame kama utashindwa TAMISEMI watasikia tu, halafu Nyakabona sijui anakwama wapi? angeondoka Magu, naamini asingechelewa hivi na kugeuka kuwa Mkanga sumu....
Ili Madame Glory-DEO. Aweze kufanya mabadiliko ni lazima huu Mbuyu Udondoke..
2. Naomba uache kukumbatia hawa Maafisa Wachafu, Ooooh! Utachafuka... Najua wengine ni Marafiki zako, achana nao... Wakubalie waondoke... Hawa wanajua vyema figisu za huku Local Government..... Itakuja kula kwako siku moja... Ushauri wangu naomba ikikupendeza wakubalie waondoke...
3. Umewahi kujiuliza kwa nini Maafisa wa Wilaya ya Magu wakipata Uhamisho wa kwenda wilaya zingine wengi wao hukataa na kupangua uhamisho? Magu pazuri bwana...Ha! Ha! Ha! Shamba la Bibi, unakuja Maskini baada ya Muda wewe ni tajiri.... Sasa utakubali kuhama? Hivi huoni SLO- MAJURA anavyo lalamika nyuma ya pazia....ha! ha! ha! ha! Mbona hana hata miaka Miwili hapa Magu akitokea Ukerewe? Magu pakuchota hakuna mwenyewe....
4. Hawa walioshutumiwa wa chunguze lakini ukweli utabaki pale pale mikono yao ni mieupe kabisa... Unajua kwa nini wanashutumiwa? Ni kwa sababu DEO- Glory ameamua kufanya kazi nao, Mbona wakati wa DEO- Salyankanga walikuwa utumwani tu, japo kuwa Leo mmewangushia mzigo...
Kimsingi Migogoro katika utumishi haiwezi kuisha kwa sababu kila mtu anasaka tonge...
Rai yangu kwa Madame Glory -DEO, piga kazi achana na Wakanga sumu, watazinywa Wenyewe..... .Madaraka anatoa Mungu.... Simama katika ukweli, acha kusikiliza majungu, wapende walimu na Viongozi wao, watie moyo... utaona kazi itakapo pigwa na ufaulu utapanda Mara dufu katika wilaya ya Magu..
Kimsingi, Mchukie anaekuambia flani hawezi..Je? Nani anaweza? Kwa maana walimu hatusemeani vyema abadani..... Please JIAMINI WEWE NDIO DEO. Walinde wanawake wenzio hapo awali ilikuwa ngumu kwa Mwalimu wa kike kuhama kutoka Nyasato kuja Kahangara bila kuvuliwa chupi na wanazengo, kanyagia hapo hapo.. Ukisikia kelele jua limewapata..
Naona umeamua kuvaa silaha za vita (kama hujavalishwa na Glory, Johari na Prisca) ili upambane na Nyagabona, ambaye kwa mawazo yako na hao waliokutuma, mnaamini kwamba Nyagabona au Majura ndio walioandika malalamiko haya kwa DED; mnajidanganya!!
Mnawaza hivyo kwa sababu dhamiri zenu zinawasuta kwani huyo Glory (akichagizwa na Johari) ndiye chanzo cha kuhamishwa kwa Majura; na mkakati wa kumhamisha Nyagabona unaendelea kwa kumtumia REO Mwanza kama mlivyofanya kwa Majura.
Unasema Nyagabona lazima ahame Magu eti kwa sababu amekuwa mwananzengo kwa hiyo ameweka mizizi. Ni kosa kwa kiongozi kuwa na mahusiano mema na watu anaowaongoza? Kwa mtazamo wako wewe mahusiano hasi kati ya kiongozi na watumishi anaowaongoza ndiyo yenye tija mahala pa kazi? Hujui usemalo, wala siamini kama DED anaweza kuchukua ushauri wako huo wa hovyo!!
Wapo maafisa wengi tu waandamizi hapo halmashaurini waliokaa muda mrefu kwa mfano Mkaguzi Mkuu Kaswa, Mkaguzi Mwandamizi mkewe Tungu Kasiga, na wengineo hata huyo mswahilina mwitu Johari (mchana baibui, usiku kwa Mbochi); mbona huwataji hao kuwataka wahamishwe?
Unadiriki kusema eti Nyagabona alikuwa anautarajia u-DEO kana kwamba babu yake ndiye anayegawa vyeo!! Vipi wewe?
Nyagabona ana uwezo, hata kama hamtaki kukubali; amekuwa Afisa Elimu Taaluma msingi tangu enzi za DEO Mtunga, Massaga, Kanyuma, Saryankanga na sasa Glory.
Kwa nini Nyagabona aonekane sasa kwamba ni tishio kwa cheo cha Glory?
Msiwe na tabia kama za mbwa mwenye kichaa; ambaye huwa anang'ata kila anachokiona mbele yake, iwe jiwe, mti, mnyama mwingine au mwanadamu akidhani kwamba hicho anachoking'ata ndicho kinachomsababishia shida kichwani mwake, kumbe shida imo kichwani mwake mwenyewe!!
Shida ya Glory haiko kwa Majura wala Nyagabona, but the problem is within herself!! Hajiamini kutokana na namna alivyopata madaraka hayo; anajua hana vigezo na hatoshi kuwa DEO. Anakijua kilichomwezesha kupata u-DEO lakini siyo vigezo.
Gidamaa unataka watu waliokaa muda mrefu Magu wahamishe kwa sababu tu wamekaa muda mrefu? Kukaa muda mrefu eneo moja la kazi siyo kigezo pekee cha kumhamisha mtumishi, unless viwepo vigezo vingine vinavyoambatana na kigezo hicho.
Unamchagiza DEO Glory awatie moyo waalimu wanawake wenzie maana wakati wa Saryankanga walikuwa utumwani kwa kuvuliwa chupi na hilo bazazi!! Siamini kama Glory anaweza kuwa kiongozi mzuri iwe kwa waalimu wa kike ama wa kiume kwa sababu, kwanza wanawake wenyewe wana tabia ya kupigana vita, kudharauliana na kuonyeshana umwamba, kila mmoja akijiona yuko juu na huwa wanapenda kukomoana zaidi kuliko kusaidiana, especially kwenye mambo ya kiofisi.
Kwa waalimu wa kiume, huyu Glory siamini kama atawatendea haki kwa sababu ya ile hali ya kutojiamini kwake, kutokuwa na vigezo na namna alivyopata madaraka hayo. Atakabiliana na matatizo hayo kwa kuwa strict kupita kiasi, akiamini kwamba atawatiisha waalimu kwa kuwatisha badala ya kuwa humble na cooperative.
Juzi Alhamisi, DED Magu amemsifia sana DEO Glory na timu yake kwenye semina ya Mtihani wa DRS la IV 2019 iliyofanyika Mugini; kwamba eti wanafanya kazi nzuri, wasijali mambo yanayoandikwa kwenye mitandao; n.k Mkurugenzi ni kiongozi mkuu wa halmashauri, haitegemewi a-crush utendaji wa ofisi ya elimu mahali kama pale, lakini ukweli anaujua.
Bado natoa wito kwako DED Magu, waondoe ofisi ya elimu Magu DEO Glory, Johari na Prisca.