Mkuu Waterloo, naheshimu sana mchango wa mawazo yako kama mkongwe katika jukwaa hili. Una hakika kwamba malalamiko yanayotolewa dhidi ya maofisa hao wa Idara ya elimu Magu ni majungu? Sijui wewe uko wapi, lakini mimi niko Kisesa wilayani Magu na wala siyo mwalimu; lakini madhira wanayoyapata waalimu hapa wilayani kwetu nayaona, maana wapo miongoni mwetu na tunaishi nao kwenye jamii na wengine ni ndugu zetu!! Hata huyo Salyankanga anaishi hapa Kisesa, namfahamu na yeye ananifahamu katika maisha yetu ya kawaida, japo naamini hanijui kwenye jukwaa hili la JF.
Unapojumuisha tu kwamba waalimu wanapenda majungu huwatendei haki ndugu Waterloo. Hawa ni watumishi wa umma ambao wana wajibu wao kwa mwajiri wao na Taifa kwa ujumla, lakini pia wana haki zao kama watumishi kwa mujibu wa taratibu za kiutumishi.
Mambo mengi yanalalamikiwa na waalimu hawa kwa maofisa niliowataja, ambayo baadhi yake nimeyataja kama rushwa, ubadhirifu, unyanyasaji wa kisaikolojia, kingono, udanganyifu katika mitihani, kudhulumiwa malipo yao ya nauli, likizo, posho mbalimbali kama za madaraka, semina n.k kwa kupunjwa kwa makusudi, kulazimishwa kugawana na maofisa hao, kupewa maagizo nusunusu na ya kujirudiarudia yanayowagharimu waalimu muda na fedha kiasi cha kuwafanya muda mwingi washinde kwenye ma-stationery na ofisini kwa DEO na kushindwa kuwa vituoni mwao n.k.
Mambo yote haya kwa ujumla wake yanashusha morali na tija, jambo ambalo lina athari kubwa kwa hatma ya watoto wetu. Labda wewe watoto wako wanasoma IST, St. Mary's, ISM,IISM, Breuban, St. Constantine n.k. Kama ndivyo, huwezi kuona athari zinazowapata watoto wanaosoma shule za umma kutokana na waalimu wao kukosa morali kwa sababu ya matatizo niliyoyaeleza kwenye andiko hili.
Bado hoja yangu iko palepale, namsihi Mkurugenzi wetu wa Magu DC, ashughulikie udhaifu uliopo katika ofisi yetu ya DEO Magu; hats kama hao maofisa wenye appointments kutoka kwa Katibu Mkuu Tamisemi hawezi kuwaondoa; atumie uwezo wake ili washughulikiwe na waliowaweka hapo. DED ni Mteule wa Rais; yeye ndiye msimamizi wa shughuli za wizara zote za nchi ukiacha chache tu katika wilaya yetu, na mwakilishi wa Rais wetu ni DC ambaye anaingia wizara zote; wote ni vijana mahiri, wasomi wabobezi na wazalendo; kwa nini waachie taswira ya elimu wilayani Magu iharibiwe Glory, Johari, Prisca na wengine wowote wanaofrustrate waalimu na watumishi wenzao mahiri kwa kutokujiamini kwao kwa sababu ya elimu ndogo? No Way!!