DED: Nimeunda timu kuchunguza madai ya michezo michafu katika Machinjio ya Halmashauri ya Tunduma

DED: Nimeunda timu kuchunguza madai ya michezo michafu katika Machinjio ya Halmashauri ya Tunduma

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
1705677046838.jpg

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Mariam Chaurembo​
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Mariam Chaurembo, amesema ameunda timu huru ya wataalamu kuchunguza tuhuma za ukiukaji wa maadili na usafi katika machinjio ya mji huo zilizosambaa hivi karibuni kupitia video mitandaoni.

Chaurembo amefafanua kuwa timu hiyo itatoa ripoti kwake ili kubaini ukweli wa madai hayo na kuchukua hatua stahiki.

Amesema hayo baada ya Mdau wa JamiiForums.com kueleza kuwa Machinjio ya Halmashauri ya Mji wa Tunduma kuna Daktari wa Mifugo anayekagua nyama baada ya ng’ombe kuchinjwa, kisha kuchukua nyama anazodai hazifai kuliwa na binadamu kisha anakwenda kuziuza kinyemela kwa Wafanyabiashara wanaouza vyakula katika migahawa.

Pia Mdau akadai kuwa usafi wa mazingira wa eneo hilo ni kama hauzingatiwi, akatoa wito hatua zichukuliwe katika mambo yote hayo mawili kwa kuwa kinachotoka hapo kinahusisha afya za Watu wengi.

Hoja ya Mdau ~ Machinjio ya Mji wa Tunduma (Songwe) kuna michezo ‘michafu’ ya uuzaji wa nyama

Kuhusu Daktari wa Mifugo

Akijibu hoja kuhusu utambulisho wa msimamizi wa machinjio hayo, Chaurembo amesema "Yule ni daktari wa mifugo kitaaluma (professional doctor), ana sifa zote na anajua miiko ya kazi yake. Hatuwezi kumtuhumu moja kwa moja kabla ya ripoti ya timu huru niliyoiunda.”

Aliongeza kuwa daktari huyo anaendelea na majukumu yake akisaidiwa na wataalamu wengine wawili ili kuhakikisha nyama inayozalishwa ni salama kwa walaji.
Screenshot 2026-04-13 160028.jpg

Screenshot 2026-04-13 155913.jpg
Mpango wa Machinjio Mpya ya Kisasa
Kuhusu hali ya miundombinu ya machinjio ya sasa ambayo imekuwepo kwa zaidi ya miaka kumi, Mkurugenzi amekiri kuwa mji unakuwa kwa kasi na kuna haja ya kuwa na eneo kubwa na la kisasa zaidi.

Bajeti: Halmashauri imetenga kiasi cha TZS milioni 850 katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha (unaoanza Julai 2026) kwa ajili ya kujenga machinjio mpya ya kisasa katika Kata ya Katete.

Ukarabati wa Muda: Wakati mchakato wa ujenzi mpya ukiendelea, kiasi kingine cha fedha kimetengwa kwa ajili ya ukarabati wa haraka wa machinjio ya sasa. Mkurugenzi ameahidi kuwa mabadiliko makubwa ya usafi na miundombinu yataonekana ndani ya wiki mbili zijazo.

Usimamizi wa Mazingira
Chaurembo amesisitiza kuwa kwa sasa Mkuu wa Idara husika yupo eneo la machinjio kila wakati ili kusimamia usafi, hususan katika maeneo yanayozunguka machinjio ambapo biashara ndogondogo za vyakula (kama vichwa na mapafu) hufanyika.

"Tunafanya kazi kwa karibu na wananchi kuhakikisha afya zao zinalindwa. Machinjio mpya itakapokamilika, itakuwa nje kidogo ya mji ili kuondoa usumbufu uliopo sasa katikati ya makazi ya watu,"
alihitimisha Mkurugenzi huyo.
 
At least walirespond.

Ripoti ilitoka?
 
Back
Top Bottom