Hizi mindset zenu za kufurahia vifo vya walio kinyume na ideology zenu, nanyi aisee!
Huko siasani mnafundishana upuuzi kwamba kifo sio haki au kifo ni adhabu tena yamstahili mpinzani wako wa mawazo, upuuzi kiwango Cha juu Sana kudhani kifo ni adhabu kwa usiempenda.
Kwahiyo wakifa wa chama chenu mnaojipa utakatifu kutafuta huruma kwenye maslahi yenu ya kisiasa, nao chaitwaje kifo chao?
Kifo Cha mtu mwingine sio faraja kwako kwakuwa nawe lazima ufe wakati ukifika. Pambaneni kwa hoja zenu za kisiasa na si kuhusianisha kifo na tofauti zenu za kisiasa ilhali kila mja yampasa kifo.
Roho ya mwendazake ipumzike kwa amani.