Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
"Deep state" yako ya kufikirika ndiyo idara gani hiyo ama ni kikundi gani hicho?Kuhusu kutotunga sheria na kuhakikisha sheria hazivunjwi upo sahihi, Ila naomba nikuambie kwamba, hawa hawa wana uwezo wakuipiga chini hiyo sheria kama kuna jambo la kimkakati wanataka lifanyike na hakuna wa kuwauliza wala kuwazuia. Hivyo wakihamua jambo fulani liende wanavyotaka litaenda, au wakisema jambo fulani lisitishwe, linasitishwa mara moja na hamna wa kuwahoji.
Bado sijakuelewa mkuu.Kwa asili ya wizi wa WaTz, hiyo deep state itakuwa inakomba kupita maelezo, kama watazikwa nazo vile!
Kama ndiyo hao mwandishi alimaanisha, wanauwezo wa kufanya mageuzi hadi kuruhusu vyama pinzani kushika dola?Deep state ni CC ya chama tawala wana itikadi ila hawana brains
Wanasema “if they won’t kill you with NO EDUCATION they’ll kill you with POOR EDUCATION”
Hiyo ndo point kubwa CCM ime achieve na imefanikiwa kutawala hi nchi na itaenda kutawala tu, labd kutokee natural hazards ila sio kwa siasa.
Deep state ni ccm na ccm ni deep state,wakianzisha chama kingine ni hao hao ndiyo watunga sera,so Mambo yakua yaleyale,yaani konyagi ileile imewekwa kwenye chupa ya pepsiWanakubali kila kitu ndiyo, kwa sababu wanajua bila hao kuridhia, hawawezi kushika dola. Lakini sasa ndiyo hivyo kijani hawana jipya tena, hivyo ni wakati wa kuandaa chama kingine kushika dola ili tujaribu sera mpya.
Kwa haya uliyo yaandika itoshe kusema una ufahamu juu ya hili nililoliandika, vile vile wakati najiandaa kuwajibu member waliouliza nini maana yake, nashukuru umewasaidia kuwapa mwanga kwa kiasi chake. Pia nipende kukwambia ya kwamba hata Tanzania ipo na inaendelea kufanya kazi yake.Kwanza kabisa DEEP STATE ni serikali ndani ya serikali, kwa namna kubwa deep state huundwa na waasisi wa taifa ama washirika wa waasisi, inawezekana kwa upande wetu hapa waasisi na washirika wao wakawa na mlengo wa chama tawala.
Deep state pia huenda ikaundwa na jopo la wafanyabiashara wakubwa, ambao kwa namna pana wameshika uchumi wa taifa.
Deep state pia huenda ikawa imeundwa na maafisa wa ngazi ya juu wa majeshi ya ulinzi na usalama wa taifa.
Tuone kwa hapa kwetu kwa makundi hayo matatu.
Kundi la kwanza la waasisi, wao ndio walionunda chama tawala ambacho kimeshika dola tangu uhuru, ni ngumu hawa kukubali nchi ikawa chini ya chama kingine, kwani tayari huamini kwao ndipo hutoka watu wanaoifahamu nchi, A-Z na ikiwa kuna aliye bora kutoka nje, yapaswa aungane nao, hawa huwa tayari kwa namna yoyote kununua watu kutoka makundi mengine ya kisiasa. Kwa kuwa huamini wao ndio wanaoweza kushika dola na si vinginevyo.
Wafanyabiashara, nchi yetu ina “elites” ambao wengi wao ni watu wenye asili ya kutoka mashariki, hili kundi ndilo lenye ushawishi wa kiuchumi nyumbani kwetu, wala kusiwe na matarajio makubwa since watu hawa biashara zao zinamea na maslahi yao kukuwa kutokana na mfumo huu uliopo, they don’t have sense of nationalism, ndio mana wengi hawana feelings za harakati za kisiasa zaidi ya kuwa walamba nyao.
Maafisa wa jeshi; kama ulikuwa hujui historia ya jeshi letu ni chama cha TANU, baada ya mgomo wa jeshi la uhuru (Tanganyika Rifles) ambalo kwa namna kubwa liliundwa na wazungu mwaka 1964, jeshi likabadilishwa, recruitment kubwa ikafanywa na vijana wa tawi la TANU (TANU Youth League) ambalo kwa leo ni kama (VUMCC) [emoji12] usije kutegemea strike, kwa sababu msingi wa jeshi ni kutumikia chama. Kwa hivyo wao ndio watakaopika viongozi na kukabidhi nchi, no matter upinzani kuna viongozi wazuri namna gani, aidha waungane nao.
Wanasema “if they won’t kill you with NO EDUCATION they’ll kill you with POOR EDUCATION”
Kundi kubwa la taifa ni knowledge dead heads, ama kundi lililoelimika ni half cooked. Sio deep state wakubadilisha, hata wao wanaangalia upepo wetu. [emoji41]
Ni hayo.
Naheshimu sana mawazo yako, lakini nipende kukwambia kwamba TISS nilichokiandika hapa hakiwahusu."Deep state" yako ya kufikirika ndiyo idara gani hiyo ama ni kikundi gani hicho?
Kama unamaanisha Tiss, umebugi na unajichelewesha sana kuwaza, maana hawawezi na hakuna nchi waliweza kufanya mageuzi ya kimapinduzi.
Wao ni pro government iliyoko madarakani na ni bendera fuata upepo tu hao, wanaitwa nusa nusa.
Wanaoweza kufanya mageuzi kirahisi ni wanajeshi.
Tatizo linalokuja kwa wanajeshi wa nchi hii wasiweze kufanya lolote na wawe ni mbwa wasio na meno hasa kuanzia utawala wa awamu ya nne ni maslahi manono wanayolipwa wakuu wao wa majeshi.
Mkuu wa majeshi kikatiba analipwa mshahara ghafi na stahili zake zingine zote za ulinzi, chakula, huduma ya usafiri na mafuta, wapishi, madereva nk bila kujali yupo kazini ama kastaafu, hiyo ni mpaka kufa.
Na wale senior officers ngazi za generals hawana dhiki wakiwa watumishi na pensheni zao ni za kuridhisha mno zinazoweza kuwafanya waishi maisha yao vyema hadi mwisho bila shida.
Sasa, watu kama hao moto wa machungu na mateso ya kimaisha ya nchi hii hauwawakii, hauwahusu.
Na haitokei hata siku1 waanze kujiorganize kuwaza na kupanga mambo hayo ya kubahatisha wakati walishatoshelezwa kimaisha, tena kwa dhiki gani waliyonayo kwa mfano!
Nchi hii itageuzwa na raia wenyewe baada ya kusema: "sasa imetosha"...."liwalo na liwe"
Maana hakuna cha kupoteza kama walivyifanya wenzetu wa mataifa ya Afrika kaskazini.
Sent using Jamii Forums mobile app
Unahitaji nguo mpya huku ulizonazo huwezi kuzifuaHuu ndo muda wa WANAHARAKATI ,UPINZANI na CHAMA KIPYA CHENYE NGUVU, kujiandaa kushika nchi
Sasa "deep state" ni kina nani hao?Naheshimu sana mawazo yako, lakini nipende kukwambia kwamba TISS nilichokiandika hapa hakiwahusu.
Nchi ya Stereo miaka hiyo, ilipata mfalme, mfalme yule akakabidhiwa jahazi akaambiwa jahazi lile lielekee mashariki lakini yeye akakaidi na kuelekea magharibi, akatumiwa ujumbe mfupi ukisema "mtukufu mfalme unaombwa jahazi ulipeleke mashariki", lakini mfalme yule akachukua kipaza sauti na kusema "mimi mtu na sipangiwi"........Deep state ni ccm na ccm ni deep state,wakianzisha chama kingine ni hao hao ndiyo watunga sera,so Mambo yakua yaleyale,yaani konyagi ileile imewekwa kwenye chupa ya pepsi
Point kubwa sana hiiWanasema “if they won’t kill you with NO EDUCATION they’ll kill you with POOR EDUCATION”
Hiyo ndo point kubwa CCM ime achieve na imefanikiwa kutawala hi nchi na itaenda kutawala tu, labd kutokee natural hazards ila sio kwa siasa.
Si kina Kingunge hao, walijitoa na kwenda kufa.Sijuwi mtaalamu wa Ufundi alishafariki