"Deep state" huu ni wakati wa kuandaa chama kingine kushika dola, kijani imeshindwa kutufikisha

Deep state = UVCCM

Hao kina Heri James, Kanani Kihongosi, Sabaya n.k

Kabla ya kuleta uzi tumia ubongo sio masaburi.
 
Uzi wangu huu!nilipost Mods wakatia kapuni!!
Mkuu pole yako kama uliandika kitu sensitive kama hichi pia wakatia kapuni. Moods na wenyewe wanapaswa kulinda kampuni yao inawalisha kila siku, kwahiyo siku unapoandika mambo nyeti, ujitahidi kufunga uzi wako kwa taswira, hiyo inasaidia kulinda kampuni na moods nyuzi zako watakuwa wanazipandisha. Lakini ukiuachia wazi kabisa uzi wako na umeandika mambo nyeti, uzi wako sidhani kama utapandishwa.
 
Si kina Kingunge hao, walijitoa na kwenda kufa.

Nadhani mzee huyo angelikuwa hai angelikuwa keaharudi Ccm.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona alipokua hoi hospitali na Mwendazake alipoenda kumtembelea alitoa kauli thabit. Alisema moyo wake upo CCM! Mwenda zake akamuuliza tena kama vile hajasikia vizuri na jibu likawa kama la mwanzo. Hakika angekua hai hadi leo, Mzee KNM angesharudi studio zetu Pugu Road
 
Kwanza kabisa niwapongeze "deep state" kwa kazi nzito na iliyotukuka mliyoifanya tangu Tanzania ipate uhuru hadi leo, mumekuwa muhimili muhimu kuhakikisha Tanzania inavuka salama katika nyakati zote ngumu, huku mukihakikisha kuwa amani ya nchi haichezewi wala kutiwa doa na mtu yeyote.

Kijani hii imetawala tangu tupate uhuru hadi leo ni miaka 60 sasa ,Ila ni dhahiri shahiri imeshindwa kutuvusha kama nchi kutoka kwenye lindi la umasikini, rushwa n.k, katika miaka 60 ya uhuru Tanzania bado afya, umeme, maji, elimu, miundombinu, yamekuwa matatizo yasiyo tibika kama cancer.

Ni wazi kwamba "elites" wa chama hichi cha kijani mawazo yao yamegota na sera zao zimekosa vision kabisa na zimepitwa na wakati, taifa halieleweki linaelekea wapi, hivyo hawawezi kutuvusha tena hapa, ni wamefika mwisho kisera, kifikra, kimkakati na kimbinu.

"Deep state" ni wakati wenu mwingine sasa kuandaa chama kingine kimkakati ili kushika dola, chama ambacho kitakuja na sera mpya, hali mpya na vision mpya ya kuliongoza taifa letu, chama ambacho kitatufanya kutoka hapa tulipo gota na kwenda kule watanzania wengi wanapokuota.

Najua mumejitahidi sana kuandaa na bado mnaendelea kuwaandaa baadhi ya viongozi kwenye chama cha kijani na nchi kwa ujumla kwa nia yenu nzuri tu ya kulivusha taifa ila wamewaangusha kutokana na sera mbovu za chama cha kijani, hivyo siyo vibaya sasa tujaribu na chama kingine tuone kitatufikisha wapi, kwani sera za chama cha kijani zimeshindwa kabisa kutuvusha.

Watanzania ni ngumu sana kujichukulia sheria mkononi kutokana na historia ya nchi hii, hivyo ni ngumu sana watanzania kuandamana au kufanya vurugu wakidai haki yao ya mageuzi kama nchi zingine, kwani nchi hii, haijawahi kuwa na migogoro ya ndani, kwahiyo hata wenzetu kupandikiza mamluku Tanzania kuchochea harakati za mabadiliko ni ngumu sana.

"Deep state" mumehepusha mengi na kufanya makubwa na mazuri zaidi, hivyo naamini nyinyi ndiyo watu wa kwanza ambao mnaweza kuleta "transformation" katika taifa hili na mkihamua kwanza, basi na watanzania watafuata.

Katiba mpya na iliyo bora ni muhimu sana na kupitia katiba mpya , mnaweza sasa kuandaa chama kingine kwa ajili ya kuliongoza taifa hili, kwani kwa sasa hamna chama chenye ubavu wa kuishinda kijani iliyo ota mizizi kila sehemu, lakini naamini mkiamua itawezekana kwani hakuna linaloshindikana mbele yenu.

Tambueni ya kwamba kwa "nature" ya taifa letu ni ngumu sana wananchi kudai mageuzi ya kiutawala kwa nyakati hizi hata wapitie katika kipindi kigumu kiasi gani, Ila nyinyi mkihamua kuanza kuleta hayo mageuzi hata wananchi watafuata pia, kwahiyo ni vyema mkaandaa chama kingine na kuwagroom viongozi wengine wapya kwa ajili ya kushika dola kwa wakati ujao, ili tuone kama tutavuka hapa ilipotufikisha kijani.

Kwa sasa si KIJANI wanaoweza kutufikisha pale tunapopakusudia kama taifa kwani wameishiwa na wamefika mwisho kifikra, bali ni nyinyi tu "deep state" wenye maamuzi ya juu zaidi yaliyobeba mustakabali na dira ya taifa letu.
Nimependa angle ya habari yako japo bado sio muarobaini wa kile tunachokihitaji kama Taifa.

Hili Taifa halina watu ambao wako committed, obligated, countable na akitokea mtu akawa na sifa hizo anajikuta kazungukwa na wachumia tumbo na wasio na malengo.

MTAZAMO WANGU
Tunapaswa kutenga miaka 20 kutoka muda wowote tutakaokuwa tayari ndipo tutaona mafanikio katika nyanya zote;

KIVIPI
Kwanza ni lazima Kila mtanzania atakaye kuwa na miaka 20 wakati huo awe na elimu ya kidato cha nne: Sababu kubwa ni kwamba miaka hii 14 yaani kindagaten 3+7+4, itakua ni filter ya kupata watu ambao wameppikwa kutokana na vipawa vyao kwa ajili ya kutake over hii nchi.

NINI KIFANYIKE
Serikali iandae mtaala wa muendelezo (continuous assessment) na sio wa kumtathmini mtahiniwa kwa single sitting baada ya kuhitimu miaka 3, 7, 4.

Mtaala upanue wigo wa fani ikianza na Sanaa zote, vipaji vingine kama uongozi, ukakamavu nk kuliko kukomea hapa kwenye HGK, HKL PGM and the likes.

PROFILING
Maafisa Usalama wachukue wigo huo kwa ajili ya kuandika historia za matendo ya vijana na kujua progress zao ndani na nje ya shule ili kudhibiti matendo ya kihalifu.

PROFILING inasaidia sana pale unapotokea uhalifu wanavuta kumbukumbu na kuanza ku narrow search kitu ambacho kitaondoa hizi mambo za vyombo vya usalama kutumia mateso kwa ajili ya ku retrieve info wakati profile yake ingeweza saidia.

Aidha mtaala unatakiwa kuwa na kipengele cha mazoezi kama utamaduni kwa ajili ya kuwa na Taifa la watu wakakamavu.

Wasalaam
 
Kwanza kabisa niwapongeze "deep state" kwa kazi nzito na iliyotukuka mliyoifanya tangu Tanzania ipate uhuru hadi leo, mumekuwa muhimili muhimu kuhakikisha Tanzania inavuka salama katika nyakati zote ngumu, huku mukihakikisha kuwa amani ya nchi haichezewi wala kutiwa doa na mtu yeyote.

Kijani hii imetawala tangu tupate uhuru hadi leo ni miaka 60 sasa ,Ila ni dhahiri shahiri imeshindwa kutuvusha kama nchi kutoka kwenye lindi la umasikini, rushwa n.k, katika miaka 60 ya uhuru Tanzania bado afya, umeme, maji, elimu, miundombinu, yamekuwa matatizo yasiyo tibika kama cancer.

Ni wazi kwamba "elites" wa chama hichi cha kijani mawazo yao yamegota na sera zao zimekosa vision kabisa na zimepitwa na wakati, taifa halieleweki linaelekea wapi, hivyo hawawezi kutuvusha tena hapa, ni wamefika mwisho kisera, kifikra, kimkakati na kimbinu.

"Deep state" ni wakati wenu mwingine sasa kuandaa chama kingine kimkakati ili kushika dola, chama ambacho kitakuja na sera mpya, hali mpya na vision mpya ya kuliongoza taifa letu, chama ambacho kitatufanya kutoka hapa tulipo gota na kwenda kule watanzania wengi wanapokuota.

Najua mumejitahidi sana kuandaa na bado mnaendelea kuwaandaa baadhi ya viongozi kwenye chama cha kijani na nchi kwa ujumla kwa nia yenu nzuri tu ya kulivusha taifa ila wamewaangusha kutokana na sera mbovu za chama cha kijani, hivyo siyo vibaya sasa tujaribu na chama kingine tuone kitatufikisha wapi, kwani sera za chama cha kijani zimeshindwa kabisa kutuvusha.

Watanzania ni ngumu sana kujichukulia sheria mkononi kutokana na historia ya nchi hii, hivyo ni ngumu sana watanzania kuandamana au kufanya vurugu wakidai haki yao ya mageuzi kama nchi zingine, kwani nchi hii, haijawahi kuwa na migogoro ya ndani, kwahiyo hata wenzetu kupandikiza mamluku Tanzania kuchochea harakati za mabadiliko ni ngumu sana.

"Deep state" mumehepusha mengi na kufanya makubwa na mazuri zaidi, hivyo naamini nyinyi ndiyo watu wa kwanza ambao mnaweza kuleta "transformation" katika taifa hili na mkihamua kwanza, basi na watanzania watafuata.

Katiba mpya na iliyo bora ni muhimu sana na kupitia katiba mpya , mnaweza sasa kuandaa chama kingine kwa ajili ya kuliongoza taifa hili, kwani kwa sasa hamna chama chenye ubavu wa kuishinda kijani iliyo ota mizizi kila sehemu, lakini naamini mkiamua itawezekana kwani hakuna linaloshindikana mbele yenu.

Tambueni ya kwamba kwa "nature" ya taifa letu ni ngumu sana wananchi kudai mageuzi ya kiutawala kwa nyakati hizi hata wapitie katika kipindi kigumu kiasi gani, Ila nyinyi mkihamua kuanza kuleta hayo mageuzi hata wananchi watafuata pia, kwahiyo ni vyema mkaandaa chama kingine na kuwagroom viongozi wengine wapya kwa ajili ya kushika dola kwa wakati ujao, ili tuone kama tutavuka hapa ilipotufikisha kijani.

Kwa sasa si KIJANI wanaoweza kutufikisha pale tunapopakusudia kama taifa kwani wameishiwa na wamefika mwisho kifikra, bali ni nyinyi tu "deep state" wenye maamuzi ya juu zaidi yaliyobeba mustakabali na dira ya taifa letu.
Hakuna deep state Tanzania wewe,usidanganywe
 
Deep State ambayo haikuiona Dowans, meremeta, kagoda, escrow, deep state ambayo haiweki ulinzi madhubuti mipakani ambapo kwa sasa kuna tishio la ugaidi, yaani nchi pekee ambayo mgeni anaweza kuingia kupitia mipakani asikaguliwe hata na ditecta, deep state ambayo inaangalia CCM wakipora na kuvuruga uchaguzi, deep state ambayo inaruhusu Rwanda avuke na jeshi aende msumbiji aweke kambi huko anatarajia kukaa miaka minne hadi mitano huku akifanya ujasusi na mataifa mengine kama huko Tanzania, hiyo deep state haipo makini nadhani haipo kabisa
 
Deep State yetu iko ughaibuni (Mabeberu). Huko ndo wanatuamulia kwa kutumia watu wao walioko huku. Itoshe tu kusema nakubaliana na wewe.
 
Deep State ambayo haikuiona Dowans, meremeta, kagoda, escrow, deep state ambayo haiweki ulinzi madhubuti mipakani ambapo kwa sasa kuna tishio la ugaidi, yaani nchi pekee ambayo mgeni anaweza kuingia kupitia mipakani asikaguliwe hata na ditecta, deep state ambayo inaangalia CCM wakipora na kuvuruga uchaguzi, deep state ambayo inaruhusu Rwanda avuke na jeshi aende msumbiji aweke kambi huko anatarajia kukaa miaka minne hadi mitano huku akifanya ujasusi na mataifa mengine kama huko Tanzania, hiyo deep state haipo makini nadhani haipo kabisa
Labda nikwambie tu kwamba operations za kijeshi za Tanzania waga ni za kimkakati na ufanisi wa hali juu, JWTZ wapo Msumbiji muda mrefu, lakini usitarajie kusikia matangazo kama Rwanda.
 
kuna vitu unapaswa kuvijua kwanza...

Nani ni dip state..
CCM ni nani.
Malengo ya dip state ni nini kwa Tanzania.
Dip state anategemea nini kutoka kwa CCM..

tafuta uprofesa kwanza na hivyo vitu vinne, japo unaweza kuishia njiani, either kwa kuwa chizi ukawa kama dr shika au rev mtikila au ukafa kwa deppression kama sio elimination..
 
Deep State ambayo haikuiona Dowans, meremeta, kagoda, escrow, deep state ambayo haiweki ulinzi madhubuti mipakani ambapo kwa sasa kuna tishio la ugaidi, yaani nchi pekee ambayo mgeni anaweza kuingia kupitia mipakani asikaguliwe hata na ditecta, deep state ambayo inaangalia CCM wakipora na kuvuruga uchaguzi, deep state ambayo inaruhusu Rwanda avuke na jeshi aende msumbiji aweke kambi huko anatarajia kukaa miaka minne hadi mitano huku akifanya ujasusi na mataifa mengine kama huko Tanzania, hiyo deep state haipo makini nadhani haipo kabisa
Mkuu huo wizi ndio unaleta mzunguko wa hela mtaani watu wananeemeka tena sana tu!!!Wewe unafikiri bila upigaji hapa mjini hela itazungukaje sasa???!!
 
N
Deep State ambayo haikuiona Dowans, meremeta, kagoda, escrow, deep state ambayo haiweki ulinzi madhubuti mipakani ambapo kwa sasa kuna tishio la ugaidi, yaani nchi pekee ambayo mgeni anaweza kuingia kupitia mipakani asikaguliwe hata na ditecta, deep state ambayo inaangalia CCM wakipora na kuvuruga uchaguzi, deep state ambayo inaruhusu Rwanda avuke na jeshi aende msumbiji aweke kambi huko anatarajia kukaa miaka minne hadi mitano huku akifanya ujasusi na mataifa mengine kama huko Tanzania, hiyo deep state haipo makini nadhani haipo kabisa
Nyie vipi swala apeleke taarifa kwa simba huku akijua simba yupo mawindoni
 
Ndani ya jeshi kuna kitu kinaitwa MI [emoji16] (Military Intelligence) ukiwajua hawa, ndio uanze kubwabwaja humu, mana naona wengi tunatoa comments ambazo ni ubashiri tuu
 
Back
Top Bottom