"Deep state" huu ni wakati wa kuandaa chama kingine kushika dola, kijani imeshindwa kutufikisha

Wanasema “if they won’t kill you with NO EDUCATION they’ll kill you with POOR EDUCATION”

Hiyo ndo point kubwa CCM ime achieve na imefanikiwa kutawala hi nchi na itaenda kutawala tu, labd kutokee natural hazards ila sio kwa siasa.
 
"Deep state" yako ya kufikirika ndiyo idara gani hiyo ama ni kikundi gani hicho?

Kama unamaanisha Tiss, umebugi na unajichelewesha sana kuwaza, maana hawawezi na hakuna nchi waliweza kufanya mageuzi ya kimapinduzi.

Wao ni pro government iliyoko madarakani na ni bendera fuata upepo tu hao, wanaitwa nusa nusa.

Wanaoweza kufanya mageuzi kirahisi ni wanajeshi.

Tatizo linalokuja kwa wanajeshi wa nchi hii wasiweze kufanya lolote na wawe ni mbwa wasio na meno hasa kuanzia utawala wa awamu ya nne ni maslahi manono wanayolipwa wakuu wao wa majeshi.

Mkuu wa majeshi kikatiba analipwa mshahara ghafi na stahili zake zingine zote za ulinzi, chakula, huduma ya usafiri na mafuta, wapishi, madereva nk bila kujali yupo kazini ama kastaafu, hiyo ni mpaka kufa.

Na wale senior officers ngazi za generals hawana dhiki wakiwa watumishi na pensheni zao ni za kuridhisha mno zinazoweza kuwafanya waishi maisha yao vyema hadi mwisho bila shida.

Sasa, watu kama hao moto wa machungu na mateso ya kimaisha ya nchi hii hauwawakii, hauwahusu.

Na haitokei hata siku1 waanze kujiorganize kuwaza na kupanga mambo hayo ya kubahatisha wakati walishatoshelezwa kimaisha, tena kwa dhiki gani waliyonayo kwa mfano!

Nchi hii itageuzwa na raia wenyewe baada ya kusema: "sasa imetosha"...."liwalo na liwe"
Maana hakuna cha kupoteza kama walivyifanya wenzetu wa mataifa ya Afrika kaskazini.
 
Deep state ni CC ya chama tawala wana itikadi ila hawana brains
Kama ndiyo hao mwandishi alimaanisha, wanauwezo wa kufanya mageuzi hadi kuruhusu vyama pinzani kushika dola?

Hao ushawishi wao labda ni kuishinikiza serikali kuhusu katiba mpya.

Tena nao kwa kuangaliana usoni kama mapanya, ni nani awe wa kwanza kulifunga paka kengele!

Maana watawala wakimjua tu, wanampokonya kadi kumkata mbawa na mizengwe mingine kibao ili kumziba mdomo kwa ngebe zake.

Mageuzi ya nchi hii hadi sisi raia tuliochoshwa, kwa umoja wetu tutakaposema: "sasa basi, imetosha, liwalo na liwe" na hatuna cha kupoteza.
 

Ukubwa wa chama cha mapinduzi sio chama tu as taasisi ya kisiasa, bali ni chama as kiranja wa taasisi za kitaifa ambazo hazipaswi kunajisiwa na siasa zozote zile
 
Wanakubali kila kitu ndiyo, kwa sababu wanajua bila hao kuridhia, hawawezi kushika dola. Lakini sasa ndiyo hivyo kijani hawana jipya tena, hivyo ni wakati wa kuandaa chama kingine kushika dola ili tujaribu sera mpya.
Deep state ni ccm na ccm ni deep state,wakianzisha chama kingine ni hao hao ndiyo watunga sera,so Mambo yakua yaleyale,yaani konyagi ileile imewekwa kwenye chupa ya pepsi
 
Siku ukielewa Waafrika tulivyo utakoma kuwapa kazi hao deep state sijui CCM,
Au CHADEMA.

Uafrika ni laana.
 
Kwa haya uliyo yaandika itoshe kusema una ufahamu juu ya hili nililoliandika, vile vile wakati najiandaa kuwajibu member waliouliza nini maana yake, nashukuru umewasaidia kuwapa mwanga kwa kiasi chake. Pia nipende kukwambia ya kwamba hata Tanzania ipo na inaendelea kufanya kazi yake.
 
Naheshimu sana mawazo yako, lakini nipende kukwambia kwamba TISS nilichokiandika hapa hakiwahusu.
 
Deep state ni ccm na ccm ni deep state,wakianzisha chama kingine ni hao hao ndiyo watunga sera,so Mambo yakua yaleyale,yaani konyagi ileile imewekwa kwenye chupa ya pepsi
Nchi ya Stereo miaka hiyo, ilipata mfalme, mfalme yule akakabidhiwa jahazi akaambiwa jahazi lile lielekee mashariki lakini yeye akakaidi na kuelekea magharibi, akatumiwa ujumbe mfupi ukisema "mtukufu mfalme unaombwa jahazi ulipeleke mashariki", lakini mfalme yule akachukua kipaza sauti na kusema "mimi mtu na sipangiwi"........
 
Point kubwa sana hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…