Iyerdoy
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,755
- 1,939
Mkuu; hizo degrees au tuseme hatujaanza kuwa na wasomi leo. Wasomi wamekuwepo toka kitambo na waliajiriwa bila kwenda veta. au nadanganya bro?Malalamiko mengi humu ni wasomi kuambiwa waende Veta. Sidhani kama kuna mahali amesema kuwa wasomi wenye digrii wote hawana ujuzi. Ukweli ni kuwa wasomi wetu wengi hawana ujuzi (skills) wao ni academicians zaidi. Veta itawapa skills zinazohitajika kama wameshindwa kupata kazi zinazoendana na usomi wao. Wengi wa hao unaowataja wangefaidika zaidi katika fani zao kama wakienda Veta. Nadhani amewataja digrii holders kwa sababu wao ndio mara nyingi wanalalamika kutopata ajira serikalini pamoja na wao kuwa wasomi. Anaco washauri ni kuwa inabidi waanze kuangalia maeneo mengine yatakayowawezesha kujiajiri. Maeneo hayo ni pamoja na ufundi uashi, ufundi seremala, ufundi wa mitambo, upishi, ushonaji, ufundi bomba, ufundi wa kutengeneza simu n.k. Kama msomi umeridhika na hapo ulipo, ushauri wake haukuhusu. Mpotezee tu.
Amandla...
Veta ilitumika sana kwa vijana Std 7 ambao hawakubahatika kuendelea na masomo Sekondari, vijana F4 ambao hawakufaulu kuendelea na masomo A-level au vijana waliokatiza masomo yao kwa sababu fulani.
Sasa unapowaelekeza (kwa ushauri au agizo -whatever) wale waliokwishapita A-level na kumaliza chuo wafanye U-turn waende VETA huoni ni kama unawadhalilisha? Yan mheshimiwa anataka kusema hao vijana wasomi walikuwa vipofu (walijizima data/walijitoa ufahamu) hawakuiona VETA walipokuwa wanajiunga vyuoni???
Ujuzi wa kiwango cha juu ni ule unaopatikana kutokana na uzoefu(Field Experiance) kazini. Huko VETA ni mojawapo ya maeneo ya kujifunzia na kutoa cheti kuthibitisha umejifunzia wapi Utaalam wako. Vyuo vya VETA ni kama vyuo vingine ila ni chuo kwa kada za awali.
Kumwambia deg. holder aende veta ni sawa na kumwambia daktari arudi O-level akajifunze biology. Hiyo sio poa.
