Degree 5 Bora Zinazotakiwa Kupewa Heshima

Hakuna cha mkubwa yule ni muwakilishi wa Wananchi usimkuze sana mkubwa ni Mungu tu hawa wengine wameshika vijivyeo tu vya muda sio vya milele maana akitoka yeye atakaa mwingine na awamu ijayo hatokua yeye atakua mwingine kwa hio atengue kauli yake mapema before it's too late
Yeah. Kweli bro. hiyo sio kauli ya inayotegemewa kutoka kwa kiongozi ngazi ya juu kama yeye. Tulitegemea kutoka kwake lipatikane suluhisho lakini dah! Yeye tena amekuwa ni sehemu ya tatizo.
 
Hakuna digrii iliyo bora kuliko nyingine. Kinacho matter ni jinsi unavyoitumia. Ingawa wengi hawana digrii lakini bila wazibua/ watapishaji vyoo na wazoa takataka tusingeweza kuishi mjini. Kipato kikubwa sio ishara ya umuhimu wake.

Amandla...
Twende Veta tukajifunze kufyatua Tofali au sio? Haya Majaliwa atuonyeshe Cheti chake alichoenda kusomea Veta ufundi wa Magari au basi tuseme yeye hakwenda atuonyeshee CHETI cha mwanae hata mmoja aliempeleka Veta akajifunze kupamba maharusi, sawa hana basi atuonyeshe Cheti cha kiongozi yoyote alieenda kusoma Veta, ikiwa na hii hana basi arudi kutengua kauli yake
 
Yeah. Kweli bro. hiyo sio kauli ya inayotegemewa kutoka kwa kiongozi ngazi ya juu kama yeye. Tulitegemea kutoka kwake lipatikane suluhisho lakini dah! Yeye tena amekuwa ni sehemu ya tatizo.
Ka Simu ni Ka Simu tu
 
Mtu kuamua kurudi kusoma Veta sio dalili ya kudhalilika. Mojawapo ya fani zinazoweza kulipa sana ni upishi. Chef ambae restaurant yake ina Michelin star anaingiza pesa nyini kuliko karibu wasomi wetu wote hapa. Na hata heshima anapewa kuliko wasomi wengi. Wafinyanzi hivyo hivyo. Ma fashion designer wazuri wengi ni mafundi wazuri wa kukata na kushona nguo. Wafinyanzi pia. Tatizo letu tunaamini kuwa kikaratasi ndio kitakupa heshima badala ya unachokifanya. Sio hivyo.

Weka hapa Cheti chako cha Upishi kutoka Veta,
 
Twende Veta tukajifunze kufyatua Tofali au sio? Haya Majaliwa atuonyeshe Cheti chake alichoenda kusomea Veta ufundi wa Magari au basi tuseme yeye hakwenda atuonyeshee CHETI cha mwanae hata mmoja aliempeleka Veta akajifunze kupamba maharusi, sawa hana basi atuonyeshe Cheti cha kiongozi yoyote alieenda kusoma Veta, ikiwa na hii hana basi arudi kutengua kauli yake
Ndipo unapokosea. Veta hawafundishi kufyatua matofali tu. Wewe kama una digrii ya ivil lakini hauna kazi ni bora uende Veta ukajifunze ufundi uashi, useremala ili ukianzisha kampuni yako ya ujenzi usimtegemee mtu na usimamizi wako uwe bora zaidi. Ukiona kazi yako hailipi una hasara gani ukienda Veta ukajifunza umekanika na udereva bora ili uendeshe gari yako ya abiria vizuri zaidi? Matajiri wengi katika nchi hii hawana digrii. Mabinti kama Shishi wanatengeza hela nzuri katika vibiashara vyao. Kwa nini msomi usiende Veta ili uwape ushindani katika hizo biashara? Kuna ubaya gani kujifunza kupamba maharusi kama inalipa na ni kazi ambayo jamii inaihitaji? Kila fani na kzi halali inastahili heshima. Nchi yetu tupo tulipo kwa sababu hatuthamini michango ya walimu wa praimari na manesi Tunawathamini maprofesa na madaktari ambao bila hao tunaowadharau wasingefika walipofika.

Amandla...
 
Mtu kuamua kurudi kusoma Veta sio dalili ya kudhalilika. Mojawapo ya fani zinazoweza kulipa sana ni upishi. Chef ambae restaurant yake ina Michelin star anaingiza pesa nyini kuliko karibu wasomi wetu wote hapa. Na hata heshima anapewa kuliko wasomi wengi. Wafinyanzi hivyo hivyo. Ma fashion designer wazuri wengi ni mafundi wazuri wa kukata na kushona nguo. Wafinyanzi pia. Tatizo letu tunaamini kuwa kikaratasi ndio kitakupa heshima badala ya unachokifanya. Sio hivyo.

Amandla...
Umenena vyema; lakini hapo ingekuwa iachwe na iwe ni maamuzi ya mtu binafsi na sio kwa shinikizo au agizo tena la kutoka juu kwa mtu mwenye wadhifa huo. Usishangae akatokea na mtu mwingine akaliweka kama lile Azimio la Musoma ambalo mpaka leo linadumu na linatekelezwa kikamilifu.
 
Weka hapa Cheti chako cha Upishi kutoka Veta,
kazi yangu ya ufundi mchundo inanitosha. Na kwa hiyo "puerile argument " yako inaonyesha kuwa hata kama unna digrii haujaelimika. Bila shaka umefremu hako kadigrii kako na umekaning'iniza ukutane ukiamini kuwa ndicho kitakupa heshima.

Amandla...
 
Umenena vyema; lakini hapo ingekuwa iachwe na iwe ni maamuzi ya mtu binafsi na sio kwa shinikizo au agizo tena la kutoka juu kwa mtu mwenye wadhifa huo. Usishangae akatokea na mtu mwingine akaliweka kama lile Azimio la Musoma ambalo mpaka leo linadumu na linatekelezwa kikamilifu.
Ule ulikuwa ni ushauri. Ni uamuzi wa mtu kuupokea au kuukataa. Unfortunately, wasomi wetu wengi hawana la kujivunia zaidi ya kikaratasi walichopata Chuo Kikuu.

Amandla...
 
kazi yangu ya ufundi mchundo inanitosha. Na kwa hiyo "puerile argument " yako inaonyesha kuwa hata kama unna digrii haujaelimika. Bila shaka umefremu hako kadigrii kako na umekaning'iniza ukutane ukiamini kuwa ndicho kitakupa heshima.

Amandla...
Babu kelele nyingi za nini? Weka hapa Cheti chako cha Upishi kutoka Veta usituletee porojo zako km Majaliwa
 
Ndipo unapokosea. Veta hawafundishi kufyatua matofali tu. Wewe kama una digrii ya ivil lakini hauna kazi ni bora uende Veta ukajifunze ufundi uashi, useremala ili ukianzisha kampuni yako ya ujenzi usimtegemee mtu na usimamizi wako uwe bora zaidi. Ukiona kazi yako hailipi una hasara gani ukienda Veta ukajifunza umekanika na udereva bora ili uendeshe gari yako ya abiria vizuri zaidi? Matajiri wengi katika nchi hii hawana digrii. Mabinti kama Shishi wanatengeza hela nzuri katika vibiashara vyao. Kwa nini msomi usiende Veta ili uwape ushindani katika hizo biashara? Kuna ubaya gani kujifunza kupamba maharusi kama inalipa na ni kazi ambayo jamii inaihitaji? Kila fani na kzi halali inastahili heshima. Nchi yetu tupo tulipo kwa sababu hatuthamini michango ya walimu wa praimari na manesi Tunawathamini maprofesa na madaktari ambao bila hao tunaowadharau wasingefika walipofika.

Amandla...
Hapana. Hoja hapa sio kuna wanaodharaulika. Hoja ni wasomi ngazi ya degree wameambiwa waende VETA kupata ujuzi ili waweze kujiajiri. Hapo inamaanisha wenye deg. wote hawana ujuzi - kitu ambacho sio kweli au sahihi. Tena kuwenda VETA sio kigezo cha mtu kuweza kujiajiri. e.g. Kwani maafisa usafirishaji wameenda VETA? Wakulima wa nyanya wameenda Veta? Mbona wamejiajiri. Kitendo cha mheshimiwa kuwalenga wasomi esp.Deg. holders kinaleta ukakasi. Kwani ni Deg. holders tu ndo hawana ajira? What's so special with the deg.holders? Wamemkosea nini?
 
Ule ulikuwa ni ushauri. Ni uamuzi wa mtu kuupokea au kuukataa. Unfortunately, wasomi wetu wengi hawana la kujivunia zaidi ya kikaratasi walichopata Chuo Kikuu.

Amandla...
Kikaratasi? Nyie acheni usengewenu km ni kikaratasi basi fungeni mavyuo yote msileteusenge wa ngumi, kenge nini nyinyi
 
Malalamiko mengi humu ni wasomi kuambiwa waende Veta. Sidhani kama kuna mahali amesema kuwa wasomi wenye digrii wote hawana ujuzi. Ukweli ni kuwa wasomi wetu wengi hawana ujuzi (skills) wao ni academicians zaidi. Veta itawapa skills zinazohitajika kama wameshindwa kupata kazi zinazoendana na usomi wao. Wengi wa hao unaowataja wangefaidika zaidi katika fani zao kama wakienda Veta. Nadhani amewataja digrii holders kwa sababu wao ndio mara nyingi wanalalamika kutopata ajira serikalini pamoja na wao kuwa wasomi. Anacho washauri ni kuwa inabidi waanze kuangalia maeneo mengine yatakayowawezesha kujiajiri. Maeneo hayo ni pamoja na ufundi uashi, ufundi seremala, ufundi wa mitambo, upishi, ushonaji, ufundi bomba, ufundi wa kutengeneza simu n.k. Kama msomi umeridhika na hapo ulipo, ushauri wake haukuhusu. Mpotezee tu.

Amandla...
 
Ukweli ni kuwa wasomi wetu wengi hawana ujuzi (skills) wao ni academicians zaidi.
Sio ukweli ndio maana nimekwambia nionyeshe Cheti chako cha Veta, sipingi watu kwenda kusoma Veta ila kauli ya PM haijatoka kwa wakati sahihi it's all about timing
 
Kikaratasi? Nyie acheni usengewenu km ni kikaratasi basi fungeni mavyuo yote msileteusenge wa ngumi, kenge nini nyinyi
Kwaheri. Nimefanya kazi na wengi wenye hivyo vikaratasi na kwa kweli wakti mwingine ni bora kuwa na fundi aliyejifunza kwa fundi mwenzie. Kama wewe kitu pekee kinachokufanya ujione mtu ni hicho kikaratasi basi una tatizo kubwa. Ungethamini uliofundishwa mpaka upate kuwa na hicho kikaratasi usingediriki kutumia lugha unayo tumia. Kama nilivyosema, inawezekana umeenda shule lakini haujaelimika. Mawazo kama hayo ndio yanayofanya Law School ifelishe wasomi kama nyinyi kibao!

Amandla...
 
Ule ulikuwa ni ushauri. Ni uamuzi wa mtu kuupokea au kuukataa. Unfortunately, wasomi wetu wengi hawana la kujivunia zaidi ya kikaratasi walichopata Chuo Kikuu.

Amandla...
Mkuu; Usisahau "Ushauri wa mkubwa ni Agizo". Usipoupokea, wewe ni Mkaidi. Mtu mkaidi hafai, hana nidhamu na anaweza kuchukuliwa hatua za kisheria.
Mfano: Wewe ni fundi na nimekuajiri uutumie ufundi wako kujenga nyumba ninayoitaka mimi. Tumekubaliana na kazi ikaanza. Lakini baadaye kidogo nikaja na wazo na nikakushauri kwamba kule kwenye vyumba vya kulala usiweke Tiles kwani nimesikia zina madhara ya kiafya.
Kama ww ni fundi unayejifahamu utapokea na kutekeleza kama nilivyokushauri. Tofauti na hapo (ukikaidi)nitakufukuza kazi.
 
Sio ukweli ndio maana nimekwambia nionyeshe Cheti chako cha Veta, sipingi watu kwenda kusoma Veta ila kauli ya PM haijatoka kwa wakati sahihi it's all about timing
Matokeo ya Law School ni uthibitisho wa hoja yangu. Cheti changu kitakuthibitishia nini maana hakitaandikwa Fundi Mchundo. Kumbe sio tuu hauna skills hata kwenye "argumentation" haumo. Ungekuwa "comforatle in your skin" kauli ya PM wala isingekusumbua maana haikuondolei utu wako.

BTW, ukinitukana tena nita ku ignore.

Amandla...
 
Kwaheri. Nimefanya kazi na wengi wenye hivyo vikaratasi na kwa kweli wakti mwingine ni bora kuwa na fundi aliyejifunza kwa fundi mwenzie. Kama wewe kitu pekee kinachokufanya ujione mtu ni hicho kikaratasi basi una tatizo kubwa. Ungethamini uliofundishwa mpaka upate kuwa na hicho kikaratasi usingediriki kutumia lugha unayo tumia. Kama nilivyosema, inawezekana umeenda shule lakini haujaelimika. Mawazo kama hayo ndio yanayofanya Law School ifelishe wasomi kama nyinyi kibao!

Amandla...
Una dharau sana watu walioenda shule na sasa hawana kazi hamtaki kuwapa ajira tatizo lenu ndio linaanzia hapo mnapachikana wenyewe
 
Mkuu; Usisahau "Ushauri wa mkubwa ni Agizo". Usipoupokea, wewe ni Mkaidi. Mtu mkaidi hafai, hana nidhamu na anaweza kuchukuliwa hatua za kisheria.
Mfano: Wewe ni fundi na nimekuajiri uutumie ufundi wako kujenga nyumba ninayoitaka mimi. Tumekubaliana na kazi ikaanza. Lakini baadaye kidogo nikaja na wazo na nikakushauri kwamba kule kwenye vyumba vya kulala usiweke Tiles kwani nimesikia zina madhara ya kiafya.
Kama ww ni fundi unayejifahamu utapokea na kutekeleza kama nilivyokushauri. Tofauti na hapo (ukikaidi)nitakufukuza kazi.
Ushauri halali ndio agizo. Angesema wenye digrii wote wafukuzwe ili waajiriwe wenye vya Veta, yeyote ambae angemtii angeshughulikiwa na Mahakama au taasisi nyingine.
Mfano wako sio sahihi. Kamw wewe umeniajiri una haki ya kuniagiza unachotaka ili mradi kisilete madhara katika usalama wa nyumba. Ukiniagiza nitoe tiles nitazitoa kwa sababu haitahatarisha usalama wa wanaotumia nyumba. Au ukiniletea tile za kichina wakati nimekushauri zitumike za Spain siwezi kukataa kuziweka.

Lakini ukiniambia nipunguze nguzo, hapo nakuachia kazi. Ni kama wale mafundi Kariakoo ambao waliambiwa waongeze basement na wakatii ingawa walihofia kuwa itaathiri jengo? Walipaswa kukataa. Au kama wewe ni daktari halafu akaingia PM katika chumba cha operation akasema kuwa anadhani uondoe miguu yote ya mgonjwa kwa sababu anaamini yote ime oza, utaikata kwa sababu wazo la Mkubwa ni amri? Hivyo hivyo katika huu ushauri wa PM. Wale wanao ona unawafaa waufuate, na wale wanaoona hauwafai waachane nao.

Amandla...
 
Una dharau sana watu walioenda shule na sasa hawana kazi hamtaki kuwapa ajira tatizo lenu ndio linaanzia hapo mnapachikana wenyewe
Kwa taarifa yako hakuna nchi ambayo serikali ina wajibu wa kutoa ajira kwa wananchi wake. Serikali inaweka mazingira ya ajira kupatikana. Serikali haikuambii usomee nini. Ni wajibu wako kuangalia soko (ikiwa pamoja na serikali) linahitaji fani gani. Hauwezi kuilaumu serikali kama wewe leo utaamua kusomea typing halafu ukakosa kazi kwa sababu serikali haina typewriter. Jukumu la kuhakikisha kuwa una elimu itakayokuwezesha kuajiriwa au kujiajiri ni lako. Sio la serikali.

Kwa taarifa yako hata wahitimu wa Veta wameenda shule. Sio nyinyi peke yenu mlioenda vyuoni ndio mmeenda shule.

Amandla...
 
Back
Top Bottom