Chris wood
JF-Expert Member
- Dec 21, 2020
- 1,667
- 5,043
Kwanza nianze kwa kumuombea dua kwa mwenyezi Mungu Rais wetu mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete, Mungu amlinde na kumpatia maisha marefu yenye furaha hapa Duniani.
Sijui mzee wetu Kikwete uliwezaje, maana ajira za kumwaga ulizokuwa ukitoa miaka 6 kurudi nyuma kwa kaka na Dada zetu leo kwa namna moja ama nyingine zimekuwa zikitusaidia na sisi majobless, leo unaweza kosa hata buku ya kula ukasaidiwa hata na ndugu ambae anakazi ya uhakika. Mungu akubariki sana muheshimiwa.
Wakati nikiwa advance shule yetu ilikuwa imepakana na chuo cha VETA, nilikuwa naona wale jamaa wamepotea njia kama sio kushindwa maisha. Kumbe bila kujua mimi ndio nilikuwa nimeenda kombo ya kiwango cha lami.
Najuta kupoteza muda, najuta kupoteza fedha ,najuta kutolitambua hili mapema, leo ninaishi kama nungunungu nisijue kesho yangu itakuwaje.
Ila mtafutaji hachoki, nimetuma maombi veta, nianze tena moja kusomea umeme wa magari. Mama Samia Hassan, nitoe pongezi kwako kwa kutufutia ile Value Retention Fee maana ilikuwa pigo kubwa kwa sisi majobless mungu akubariki sana mama.
Leo nimeamini cheti hakinunui bidhaa wala kulipa bili