Degree holder nimerudi kusoma VETA, hivi vyeti ni kupiga mikasi

Degree holder nimerudi kusoma VETA, hivi vyeti ni kupiga mikasi

Kama lengo lako ni kuajiriwa nakushauri achana na umeme wa magari, soma boiler maker (Welding ) inaweza kua muhimu zaidi kuliko hiyo ya auto electricians; hiyo fani vijipesa vyake ni vidogo vidogo sana. Muhimu nakupongeza kua na vyeti vyote 2, VETA na Degree. Nchi zingine ambazo zimekua na vyuo vikuu vingi, vijana wake wengi wana degree zaidi ya moja kwa fani tofauti tofauti, yaani unakuta kijana ana degree ya uhasibu, sheria na hata manunuzi, lengo ni kua multi purposes, kwa BONGO i wouldnt suggest that cause we have other things to do or study kama hyo ya VETA.
 
Maamuzi mazuri sana umefanya, hapo weka juhudi darasani kwenye practical na mtaani ukifanya hivyo utafika mbali sana maana maarifa yoyote yapo kwenye practical ukifanikiwa hapo hela zitakutafuta zenyewe hata ukisha anza kuelewa utafute kazi za kujitolea gereji Ili uwe mzoefu na elimu yako ya theory ya chuo kikuu itakusaidia kuvijua vitu kwa usahihi maana utakuwa unavifanyia kazi.
 
Kama lengo lako ni kuajiriwa nakushauri achana na umeme wa magari, soma boiler maker (Welding ) inaweza kua muhimu zaidi kuliko hiyo ya auto electricians; hiyo fani vijipesa vyake ni vidogo vidogo sana. Muhimu nakupongeza kua na vyeti vyote 2, VETA na Degree. Nchi zingine ambazo zimekua na vyuo vikuu vingi, vijana wake wengi wana degree zaidi ya moja kwa fani tofauti tofauti, yaani unakuta kijana ana degree ya uhasibu, sheria na hata manunuzi, lengo ni kua multi purposes, kwa BONGO i wouldnt suggest that cause we have other things to do or study kama hyo ya VETA.
Una uhakika umeme wa magari pesa yake ni ndogo ?
 
Kuna jamaa alipata degree SUA,alvyorud mtaan akakuta tayar magufuri ameshaanza madudu yake ikabid akasome diploma ya clinical medicine,sahv n CO vijijin huko na mshahara wake wa laki 4
Uko SUA alichukua degree ya nini?
Sema nini uyo jamaa yako ni kiazi sana
 
Umeenda shule kweli wewe? Hiyo sio overall GPA, hiyo ni ya semister
Usipanic sana ndugu hiyo GPA ni yangu sio yako
Halafu hiyo 3.8 ni GPA ya second year
Hiko Kibox cha juu ni matokeo ya first year nilipata GPA zaidi ya 4.wastani wa B+
Hakuna mwaka niliopata gpa chini ya 3.7 Udsm hapo
Kama nikija kujiendeleza vigezo vya kufundisha ninavyo
 
Jamaa ulipewa sijui 15M na broo ulishindwa hata kuweka 1.5M Tigopesa ukawa unaingiza hata 10K kwasiku uku unapiga mruzii tu kweli Dunia sijui inaendeshaje mambo yake.
 
Kwanza nianze kwa kumuombea dua kwa mwenyezi Mungu Rais wetu mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete, Mungu amlinde na kumpatia maisha marefu yenye furaha hapa Duniani.

Sijui mzee wetu Kikwete uliwezaje, maana ajira za kumwaga ulizokuwa ukitoa miaka 6 kurudi nyuma kwa kaka na Dada zetu leo kwa namna moja ama nyingine zimekuwa zikitusaidia na sisi majobless, leo unaweza kosa hata buku ya kula ukasaidiwa hata na ndugu ambae anakazi ya uhakika. Mungu akubariki sana muheshimiwa.

Wakati nikiwa advance shule yetu ilikuwa imepakana na chuo cha VETA, nilikuwa naona wale jamaa wamepotea njia kama sio kushindwa maisha. Kumbe bila kujua mimi ndio nilikuwa nimeenda kombo ya kiwango cha lami.

Najuta kupoteza muda, najuta kupoteza fedha ,najuta kutolitambua hili mapema, leo ninaishi kama nungunungu nisijue kesho yangu itakuwaje.

Ila mtafutaji hachoki, nimetuma maombi veta, nianze tena moja kusomea umeme wa magari. Mama Samia Hassan, nitoe pongezi kwako kwa kutufutia ile Value Retention Fee maana ilikuwa pigo kubwa kwa sisi majobless mungu akubariki sana mama.

Leo nimeamini cheti hakinunui bidhaa wala kulipa bili.

Ninadhani kitu ambacho haujui ni kuwa hela zote ni mali ya serikali na wao ndio wanaweza kuzimwaga mtaani au kuzitoa mtaani.

Kinachoendelea sasa ni kuwa pesa hakuna mtaani na hao waliosoma elimu ya ufundi huko VETA hawana kazi kwa maana wapo wengi na hakuna mtu anayejenga nyumba kwa sasa hivyo hakuna dili za kupaka rangi, kufanya wiring wala kuchomea mageti.

Njaa ipo kwa watu wote white colar na blue colar. Kinachokusumbua wewe ni kuwa upo desparate na maisha unataka kufanana na wenzako ambao tayari walibahatika kupata kazi bank na wameoa.

Tuliza akili kwa maana kwa mwendo huo unaweza kwenda VETA na ukirurudi mtaani ukakosa dili, unaweza kujiua kwa stress.

Stay Calm mdogo wangu.
 
Back
Top Bottom