Degree holder nimerudi kusoma VETA, hivi vyeti ni kupiga mikasi

Degree holder nimerudi kusoma VETA, hivi vyeti ni kupiga mikasi

Kwanza nianze kwa kumuombea dua kwa mwenyezi Mungu Rais wetu mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete, Mungu amlinde na kumpatia maisha marefu yenye furaha hapa Duniani.

Sijui mzee wetu Kikwete uliwezaje, maana ajira za kumwaga ulizokuwa ukitoa miaka 6 kurudi nyuma kwa kaka na Dada zetu leo kwa namna moja ama nyingine zimekuwa zikitusaidia na sisi majobless, leo unaweza kosa hata buku ya kula ukasaidiwa hata na ndugu ambae anakazi ya uhakika. Mungu akubariki sana muheshimiwa.

Wakati nikiwa advance shule yetu ilikuwa imepakana na chuo cha VETA, nilikuwa naona wale jamaa wamepotea njia kama sio kushindwa maisha. Kumbe bila kujua mimi ndio nilikuwa nimeenda kombo ya kiwango cha lami.

Najuta kupoteza muda, najuta kupoteza fedha ,najuta kutolitambua hili mapema, leo ninaishi kama nungunungu nisijue kesho yangu itakuwaje.

Ila mtafutaji hachoki, nimetuma maombi veta, nianze tena moja kusomea umeme wa magari. Mama Samia Hassan, nitoe pongezi kwako kwa kutufutia ile Value Retention Fee maana ilikuwa pigo kubwa kwa sisi majobless mungu akubariki sana mama.

Leo nimeamini cheti hakinunui bidhaa wala kulipa bili.
Ikiwa uko nako umeenda kusoma ili upate ajira jiandae kisaikolojia. Zama zimebadilika siyo kila homa ni malaria
 
sasa mshahara laki nne jamani si majanga haya
Kudharau mshahara wa laki 4 ndio mwanzo wa kufeli. Ukitaka kuanzia juu utaishia kupaona juu hivyo hivyo. Mambo si rahisi rahisi kama unavyofikiria. Rais wa sasa angedharau mishahara kama wewe aidhani kama angekuwa alipo, nadhani historia yake unaijua. Kama hujauatilia uliza wakuhadithie.
 
Tatizo unajifanya mjuaji, Nimeleta humu tangazo la kutaka ajira?
Hivi unasoma ulichokiandika?
We unalalama ajira hakuna wakati una GPA na uwezo wa kutosha,umehangaika kwenye interviews bila mafanikio ukitafuta ajira,sasa baada ya kuona mambo magumu umeamua kwenda veta ukasome upate cheti ili utafute tena ajira za umeme wa magari,huna lengo LA kujiajiri ndio maana unataka cheti,ungetaka kujiajiri kuna garage kibao kitaa za kujifunza kwakua una theoretical foundation ya kutosha isingechukua mda

Unadhani huko veta wanakuwekea ubongo mwengine?
 
Hivi unasoma ulichokiandika?
We unalalama ajira hakuna wakati una GPA na uwezo wa kutosha,umehangaika kwenye interviews bila mafanikio ukitafuta ajira,sasa baada ya kuona mambo magumu umeamua kwenda veta ukasema upate cheti ili utafute tena ajira za umeme wa magari,huna lengo LA kujiajiri ndio maana unataka cheti,ungetaka kujiajiri kuna garage kibao kitaa za kujifunza kwakua una theoretical foundation ya kutosha isingechukua mda

Unadhani huko veta wanakuwekea ubongo mwengine?
Inaonekana uelewa wako hata darasani ulikuwa mdogo maana huelewei wapi nimeleta tangazo la kuhitaji Ajira??
 
Inaonekana uelewa wako hata darasani ulikuwa mdogo maana huelewei wapi nimeleta tangazo la kuhitaji Ajira??
GPA kubwa akili zero,kilichokufanya uandike huu uzi ni nini?
Tujue na wewe ulipata GPA kubwa?
Umelalamika ajira hakuna,unachokataa sasa ivi ni nini?
 
Back
Top Bottom