Degree holder nimerudi kusoma VETA, hivi vyeti ni kupiga mikasi

Degree holder nimerudi kusoma VETA, hivi vyeti ni kupiga mikasi

Kwanza nianze kwa kumuombea dua kwa mwenyezi Mungu Rais wetu mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete, Mungu amlinde na kumpatia maisha marefu yenye furaha hapa Duniani.

Sijui mzee wetu Kikwete uliwezaje, maana ajira za kumwaga ulizokuwa ukitoa miaka 6 kurudi nyuma kwa kaka na Dada zetu leo kwa namna moja ama nyingine zimekuwa zikitusaidia na sisi majobless, leo unaweza kosa hata buku ya kula ukasaidiwa hata na ndugu ambae anakazi ya uhakika. Mungu akubariki sana muheshimiwa.

Wakati nikiwa advance shule yetu ilikuwa imepakana na chuo cha VETA, nilikuwa naona wale jamaa wamepotea njia kama sio kushindwa maisha. Kumbe bila kujua mimi ndio nilikuwa nimeenda kombo ya kiwango cha lami.

Najuta kupoteza muda, najuta kupoteza fedha ,najuta kutolitambua hili mapema, leo ninaishi kama nungunungu nisijue kesho yangu itakuwaje.

Ila mtafutaji hachoki, nimetuma maombi veta, nianze tena moja kusomea umeme wa magari. Mama Samia Hassan, nitoe pongezi kwako kwa kutufutia ile Value Retention Fee maana ilikuwa pigo kubwa kwa sisi majobless mungu akubariki sana mama.

Leo nimeamini cheti hakinunui bidhaa wala kulipa bili.

Ukiwa fundi toka veta hata deni la hesleb hulipi Wala kudaiwa.

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Nakumbuka mwaka juzi nilipata kabahati utumishi, aisee nafasi 2 tukaitwa 2000.. nikasema no sweat uchawi hauendi kwa mentali, ila ile idadi nimefika nikaikuta, nikasema dah Bongo noma sana..
Rea tuliitwa watu zaidi ya 900 kugombania nafasi moja .Sijui tunaenda wapi.
Mwaka jana Tra walitia fora watu 6000 nafasi 7
 
Ninadhani kitu ambacho haujui ni kuwa hela zote ni mali ya serikali na wao ndio wanaweza kuzimwaga mtaani au kuzitoa mtaani.

Kinachoendelea sasa ni kuwa pesa hakuna mtaani na hao waliosoma elimu ya ufundi huko VETA hawana kazi kwa maana wapo wengi na hakuna mtu anayejenga nyumba kwa sasa hivyo hakuna dili za kupaka rangi, kufanya wiring wala kuchomea mageti.

Njaa ipo kwa watu wote white colar na blue colar. Kinachokusumbua wewe ni kuwa upo desparate na maisha unataka kufanana na wenzako ambao tayari walibahatika kupata kazi bank na wameoa.

Tuliza akili kwa maana kwa mwendo huo unaweza kwenda VETA na ukirurudi mtaani ukakosa dili, unaweza kujiua kwa stress.

Stay Calm mdogo wangu.
Kama vijana hali ndio imekua hivyo tufanye nini sasa mimi naona bora nikapate ujuzi wakati nikiendelea kusubiri baraka za mama samia
 
Jamaa ulipewa sijui 15M na broo ulishindwa hata kuweka 1.5M Tigopesa ukawa unaingiza hata 10K kwasiku uku unapiga mruzii tu kweli Dunia sijui inaendeshaje mambo yake.
Million 17 sio kweli
 
Aaaah! Aseee we jamaa narudia Tena umeshindwa kuapply kabisa yale uliyo ya Soma na umesema ulichosoma kinaendana na umeme wa magari sasa si Bora huo umeme wa magari ungesoma mwenyewe na kujitolea sehemu mbalimbali na ada ibaki kama mtaji au unafikilia kuwa huko veta Kuna practical Sana Mimi na hisi unajichomesha tu maana veta ada yako itaishia kukufundisha vitu ambavyo ni secondary then na ufundi kiduchu then Kwisha kazi.

Maana hata humu vyuoni tunanganyana kuwa Kuna ujuzi kumbe ni uzumbukuu ada zinatumika kulipa malecture wanao tutungia mtihani. Mm binafsi nilianza kuwa muhumini wa audictism baada ya kumaliza form six nikaingia kitaa nikapingwa na jamii ile mbaya nikasema ngoja niende DIT kuchukua diploma ya mech eng lakini nilikili kuwa nilikuawa sahihi kuendelea na informal education kutokana na kwamba chuo imegeuka kuwa sehemu ya kufanyishana mitihani na kurudisha miaka nikasoma mwaka mmoja nikachukua matokeo ya NTA 4 ni kasepa now naona Kama ningeendeleaga na formal education ile ningekuwa so far. Ila kwako we jamaa hii ni noma Kama vijana mnashauriana hivi basi hii Kali.

Ungesema huna mtaji mazingira hayapo sawa ningekuelewa. Ila ndio umeona degree kua bure kabisa. Na mtaji unao duu hii Kali

Ko uwezi kutoa chochote kutoka

Degree
Advance level
O level
Past experience
Huu uzi inabidi tumuonyeshe ndali chako na mh suluhu
 
Kuna jamaa alipata degree SUA,alvyorud mtaan akakuta tayar magufuri ameshaanza madudu yake ikabid akasome diploma ya clinical medicine,sahv n CO vijijin huko na mshahara wake wa laki 4
sasa mshahara laki nne jamani si majanga haya
 
Kwanini umeme wa magari mkuu?

Maana nlikua nna wazo pia la kusoma umeme wa magari, ila sijajua soko lake.
ndio tunapoelekea huko , ila usome uwe deep sio kipole pole ,
soko lipo na chances za kuendelea zipo juu
 
Huyu ndiyo kati ya watu wenye elimu bila maarifa na hawa ndio mabingwa wa kuilaumu serikali.
Usijifanye unajua sana ndugu,. Wewe hapo elimu yako imekusaidia nini?
 
Kwahyo ukienda veta ndo utaajiriwa ama..we si unatafta ajira....yan kwel umeshindwa chakata akil ukakoosa cha kufanya..wew kwel akil zilikua za kukarir

Yaan unaenda tena poteza hela et unaenda fundishwa..watu skuhiz wanapata knowledge youtube kwenye majarida ..or else hata kujulia kaz field..umeshindwa hata jiunga na garage za uswaz wakufundishe..tena uma degree..yaan unaenda toa pesa upate tena cheti...kwel nmeamin
 
Kwahyo ukienda veta ndo utaajiriwa ama..we si unatafta ajira....yan kwel umeshindwa chakata akil ukakoosa cha kufanya..wew kwel akil zilikua za kukarir

Yaan unaenda tena poteza hela et unaenda fundishwa..watu skuhiz wanapata knowledge youtube kwenye majarida ..or else hata kujulia kaz field..umeshindwa hata jiunga na garage za uswaz wakufundishe..tena uma degree..yaan unaenda toa pesa upate tena cheti...kwel nmeamin
Nataka nikajifunze kwa vitendo, siwezi tumia YouTube tu wakati sina karakana na vitendea kazi
 
Nataka nikajifunze kwa vitendo, siwezi tumia YouTube tu wakati sina karakana na vitendea kazi
Ndugu yangu .una shida pahala.na usipobadilika mindset..hata ukitoka hapo veta utahis bado unawiwa....

Hiv unapotembeaga mitaan.masokon.kariakoo..hiv unaonaga watu na biashara zao kuanzia machinga mpaka wafanya biashara wakubwa.unahis wana degree au hvyo vyet vya veta?

Yaan umeshindwa fanya chochote kitu.had wa darasa la saba anakushinda mkuu...

Amini kwamba...mkuu una tatzo..

Bas kama umeshindwa kabisa..iga wanachofanya wenzio mitaan bas .au ndo pride inakuzingua.
 
Ndugu yangu .una shida pahala.na usipobadilika mindset..hata ukitoka hapo veta utahis bado unawiwa....

Hiv unapotembeaga mitaan.masokon.kariakoo..hiv unaonaga watu na biashara zao kuanzia machinga mpaka wafanya biashara wakubwa.unahis wana degree au hvyo vyet vya veta?

Yaan umeshindwa fanya chochote kitu.had wa darasa la saba anakushinda mkuu...

Amini kwamba...mkuu una tatzo..

Bas kama umeshindwa kabisa..iga wanachofanya wenzio mitaan bas .au ndo pride inakuzingua.
Ndugu ningekuwa nandoto za kuwa chinga ningalikwisha kuwa kitambo sana. Kila mtu ananjia anayo amini. Mimi naamini katika ujuzi.

Sio kwamba mimi mimi sina uwezo ila hali ninayo kutananayo kwenye interview inakatosha tamaa hali ni mbaya sana sana.

Nimepoteza miaka minne chuo sasa nataka tena nitumie mwaka mmoja nibobee kwenye magari, naamini ninaiwezo mkubwa wa kujifunza.
Kisha nije nifungue kijiwe changu mwenyewe, Hilo ndio ninalo amini
 
Back
Top Bottom