TANZIA Demi Agoglia Afariki Dunia Wakati Akifanyiwa Upasuwaji Wa Kuongeza Shepu

TANZIA Demi Agoglia Afariki Dunia Wakati Akifanyiwa Upasuwaji Wa Kuongeza Shepu

Mwanamke wa Uingereza aitwaye Demi Agoglia (26) amefariki dunia siku chache baada ya kufanya upasuaji wa kuongeza shepu (BBL) nchini Uturuki, Magazeti ya Uingereza yameripoti.

Demi ambaye alikua Mkazi kutoka Jiji la Manchester alipata mshtuko wa moyo saa chache kabla ya kuanza safari yake ya kurudi nyumbani Uingereza ambapo Mume wake alimpatia huduma ya dharura ya CPR kabla ya kumpeleka Hospitalini lakini jitihada zake hazikuzaa matunda.

Inaelezwa kwamba kiwango cha vifo vinavyotokana na upasuaji wa kuongeza makalio (BBL) ni kifo kimoja kati ya kila Watu 3000 ambapo upasuaji huo wa BBL ndio upasuaji wenye kiwango cha juu zaidi cha vifo vilivyorekodiwa kuliko upasuaji mwingine wowote wa urembo.

Upasuaji wa kuongeza makalio unakadiriwa kugharimu £3,500 (Tsh milioni 11.1) nchini Uturuki lakini hadi £10,000 (Tsh milioni 32) nchini Uingereza huku utafiti ukionesha kuwa ndio upasuaji hatarishi zaidi kuliko upasuaji mwingine wowote wa urembo.

Chanzo: Millard Ayo

View attachment 2868375
Ah kumbe Demi wa uingereza.....

Nkajua wa JF!!
 
watu mnahangaika kupendezesha mwili, badala ya roho. 1 Wafalme 18:21 Naye Eliya akawakaribia watu wote akanena, mtasitasita katikati ya mawazo mawili hata lini? Bwana akiwa ndiye Mungu mfuateni, bali ikiwa baali ni mungu haya mfuateni yeye. Yakobo 1:8 Mtu wa nia mbili husitasita katika njia zake zote.

Mtafuteni Mungu, pendeni zaidi vipawa vya rohoni badala ya kuutumikia mwili na tamaa zake. Yesu Kristo anarudi, yu malangoni, heri wazifuao nguo zao katika Damu ya Mwanakondoo.
Watu wa dini bhna,

Habari za yesu ni hadithi za watoto wadogo wanaoogopa paka
 
Watu wa dini bhna,

Habari za yesu ni hadithi za watoto wadogo wanaoogopa paka
labda kama wewe ni kumbe mwingine, yaani walee waliofurushwa mbinguni theluthi moja wakatupwa huko pamoja na shetani, hao ndio wanahangaika duniani na kuzimu wakilaghai watu ili wawapate wengi wa kwenda nao motoni. ila kama ni mwanadamu wa kawaida, hiki unachoongea kuna siku kitakutokea puani badala ya mdomoni.Mungu akurehemu. na Ushindwe Kwa Jina la Yesu Kristo.
 
Back
Top Bottom