Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,657
- 20,967
Demokrasia imekuwa kitu cha hovyo sana kinachorudisha nchi nyuma, hasa nchi za kiafrika. Wanasiasa hawawazi tena maendeleo bali wanawaza jinsi ya kuingia madarakani na jinsi ya kubaki madarakani. Hakuna anayejali maslahi ya nchi. Kenya walianza kuongelea uchaguzi wa 2022 miaka 3 iliyopita.
Rais Samia anaongelea uchaguzi wa 2025 leo. Nchi haina dira yoyote bali ni kusikiliza kelele huku na huko na kuzifanyia kazi, imaendeshwa kwa matukio.
Kwenye demokrasia Serikali inatapanya mali, inakopa na kufuja ikijua kesho mzigo wa deni siyo wake. Ndiyo maana kila utawala mpya ukiingia utakuta unalalamika hazina imekombwa.
Tungerudi tu kwenye chama kimoja. Au tukae chini tuumize vichwa tuje na utaratibu mwingine na si demokrasia. Demokrasia ni uongo.