Demokrasia inatupotezea sana muda na nguvu

Tatizo si mfumo tatizo ni watu ambao wakipata madaraka wanataka kuyang’ang’ania kwa gharama yoyote ile ikiwemo kufanya udikteta, dhuluma na udhalimu wa kusema uongo, ufisadi, wizi, ubadhirifu na hata mauaji na haya yanatokea sana Africa, South East Asia na South America.

Kama mfumo unaruhusu matatizo kwa karibu bara zima basi haufai kabisa. Au hautufai kabisa. Na si Africa tu, huko South Amerika na South East Asia shida tupu.
 
Ili usikike kwenye demokrasia lazima uwepo huko juu. Hili lipo hata kwenye udikteta na nchi za kifalme. Tatizo la demokrasia ni kutudanganya kuwa mtu wa chini anasikilizwa na ndiye anaendesha nchi.
Unatakiwa ujue kua mtu wa chini haimaanishi mtu moja mmoja bali ni wananchi wote kwa ujumla wao.Tatizo hapa ni sisi wananchi wenyewe tumeshindwa kujua thamani yetu ndo maana tunaonekana sio chochote ila nikwambie tu kua wananchi wanaweza kufanya lolote na likawezekana endapo wataamua kwa pamoja.
 
🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾

Mambo mengine inategemea na mwamko wa wananchi wenyewe ukoje.Kama uko kwenye jamii ya vilaza maana yake itachukua muda kustaarabika.lakini kwavile tuko kwenye zama za mabadiliko na ukuaji wa technolojia,inakua ni rahisi kuelimika kuliko uko tulikotoka.kwahiyo nadhan ni kizazi hichi cha kwetu ndio kizazi cha mwisho cha jamii ngumu kustaarabika ila kizazi kinachokua sasa kitakua tofauti sana na sisi.
 
Demokrasia imekuwa kitu cha hovyo sana kinachorudisha nchi nyuma, hasa nchi za kiafrika. Wanasiasa hawawazi tena maendeleo bali wanawaza jinsi ya kuingia madarakani na jinsi ya kubaki madarakani. Hakuna anayejali maslahi ya nchi. Kenya walianza kuongelea uchaguzi wa 2022 miaka 3 iliyopita.

Rais Samia anaongelea uchaguzi wa 2025 leo. Nchi haina dira yoyote bali ni kusikiliza kelele huku na huko na kuzifanyia kazi, imaendeshwa kwa matukio.

Kwenye demokrasia Serikali inatapanya mali, inakopa na kufuja ikijua kesho mzigo wa deni siyo wake. Ndiyo maana kila utawala mpya ukiingia utakuta unalalamika hazina imekombwa.

Tungerudi tu kwenye chama kimoja. Au tukae chini tuumize vichwa tuje na utaratibu mwingine na si demokrasia. Demokrasia ni uongo.
Chama kimoja kimetawala tangu uhuru mpaka 1982. Sijui kama ulikuwa umezaliwa. Ni maendeleo gani yaliyo patikana katika kipindi hicho? Nikubalianae nawe kwa hoja ya kuongeza kudumaza maendeleo. Wananchi wanaongezewa kodi ili iongezeke hela kupambana na upinzani.
 
Mawazo ya k

Mawazo ya kiprimitive haya. Hujui kama democrasia ndo maendeleo yenyewe. We unafikiri kusingekuwa na msuguano wa mawazo unafikiri ccm ya jpm si ingeua kila mtu kwa kisingizio eti anazua madaraja yasikengwe. Msingi wa demokrasia maana yake mwenye mawazo chanya mpe usinganganie yule yule ambaye hana anachojua tena.
 
Watu wanachekesha demokrasia gani unaiongelea wakati kura zimeibiwa na uchaguzi unapagwa!. Yaani kwa akili yako kuna demokrasia Tanzania!. Tanzania tunataka kuwa na demokrasia lakini haipo bado! wananchi kukutana na kuongelea katiba hairuhusiwi.... kuongelea katiba!!!. Ni visingizio tu kuna nchi zina maendeleo sana na zina demokrasia
Huu ni uongo mwingine wa demokrasia. Inatudanganya kuwa inaleta maendeleo. Na kuwa maendeleo hayawezi kupatikana bila demokrasia. Hiki ni kiini macho. Ukiona nchi ina demokrasia na imeendelea jua maendeleo yale hayahusiani na demokrasia yake.
 
Mpaka lini kustaarabika? Maana yake demokrasia inachagua aina ya watu? Na ushahidi unaonekana kuwa ili ufikie demokrasia au ili uokomaze unapaswa kupitia njia zisizo za kidemokrasia. Mfano Zimbabwe, mpaka keshi liingilie kati ndipo demokrasia kidogo ikakua. Sasa watakufa wangapi, tutapata hasara ngapi hadi hiyo demokrasia ikomae.
Ikiwa kuna hii Democracy ya kuombea Hela kwa beberu Hali ni hivi itakuwaje iwe hakuna mtu mmoja na kikundi Chake wabaki madarakani wakiaini wao ndio wanastahili

Sent from my CPH2179 using JamiiForums mobile app
 
Wakati mwingine ukifikiria sana kuhusu siasa ni kama haina maana na ni uchizi
Jamaa
Unatakiwa ujue kua mtu wa chini haimaanishi mtu moja mmoja bali ni wananchi wote kwa ujumla wao.Tatizo hapa ni sisi wananchi wenyewe tumeshindwa kujua thamani yetu ndo maana tunaonekana sio chochote ila nikwambie tu kua wananchi wanaweza kufanya lolote na likawezekana endapo wataamua kwa pamoja.
Mwananchi wa kawaida ni ngumu sana kufanya lolote. Demokrasia inatudanganya kuwa tuna nguvu hiyo.

Karibu mara zote mabadiliko huletwa na tabaka tawala. Kumtoa madarakani Mubarak Misri ni mpaka Majenerali wa jeshi waliporuhusu. Na wafaidika wa matunda yake ni wao. Nchi nyingi kupinduliwa ni mpaka tabaka tawala liruhusu. Jeshi lilikuwa wapi wakati rais wa Guinea anaua raia mwaka jana? Ni mpaka lenyewe liliporuhusu mabadiliko ndipo yakatokea.
 
Demokrasia inatudanganya kuwa mtu wa chini anaweza kuwa na sauti katika kuendesha nchi au sera za nchi. Hiki ni kiinimacho tumepigwa.
Sio demokrasia inadanganya, ndio ukweli. Tofauti ni kuwa watawala wanapoka madaraka hayo toka kwa wananchi. Kuwa na sauti ni wananchi kuwa na haki ya kuwachagua wawakilishi ktk ngazi zote za uwakilishi na hao wawakilishi kuwa na uwakilishi ulio kusudiwa. Nchi zote za kidikteta chaguzi haziko wazi na wanaopitishwa wanakuwa ni vibaraka wa serikali. Tanzania uchaguzi unasimamiwa na tume ya uchaguzi isio huru, watumishi wa serikali ndio wandika wapiga kura, wasimamizi wa vituo na zoezi la kuhesabu kura. Polisi ndio wabeba masanduku kupelekwa kwa mkurugenzi kurudia kuhesabu pindi CCM ikishindwa!
 
Mawazo ya k

Mawazo ya kiprimitive haya. Hujui kama democrasia ndo maendeleo yenyewe. We unafikiri kusingekuwa na msuguano wa mawazo unafikiri ccm ya jpm si ingeua kila mtu kwa kisingizio eti anazua madaraja yasikengwe. Msingi wa demokrasia maana yake mwenye mawazo chanya mpe usinganganie yule yule ambaye hana anachojua tena.
Demokrasia na maendeleo ni vitu tofauti kabisa. Si lazima kuwa na demokrasi ili kupata maendeleo, tena demokrasia ni adui wa maendeleo. Maana demokrasia na kodi/tozo kubwa ni kaka na dada.
 
Si lazima. Libya iliendeshwa kibabe na ilikuwa tulivu kwa miaka mingi. Huko North Korea hatusikii watu kuuuana kama walivyouawa watu Zanzibar mwaka jana, au Kenya 2008.
Hakuna utulivu, ni watu wanaoishi wameelekezwa mitutu ya bunduki. Nao huchoka na hatimae kukubali kufa kuliko hayo maisha.
 
Huu ni uongo mwingine wa demokrasia. Inatudanganya kuwa inaleta maendeleo. Na kuwa maendeleo hayawezi kupatikana bila demokrasia. Hiki ni kiini macho. Ukiona nchi ina demokrasia na imeendelea jua maendeleo yale hayahusiani na demokrasia yake.

Unasoma kwenye magazeti na kusikiliza kwenye magenge au una uzoefu. Mimi nimekaa US and Canada kwa miaka 20. Nime tembelea zaidi ya nchi kumi nyingine hivyo naongea kwa uzoefu. Mfumo wa demokrasia ni bora kuliko mifumo mingine yote. Mifumo mengine ni lazima kutakuwa na matabaka au ukabila. lakini kibaya ni kulazimishana mfano huko China kutoa mimba ni sera ya serikali! kuna waislamu zaidi ya milioni wamewekwa kwenye kambi kwasababu tu ya dini yao hawana makosa yeyote!. Huko Urusi watu wanapigwa risasi waziwazi. Hata nchi za kiarabu mtoto anazaliwa lakini kama sio mtu wa kwao mtoto anakuwa hana haki nenda Dubai na nchi nyingine za ukanda ule uone.
 
Chama kimoja kimetawala tangu uhuru mpaka 1982. Sijui kama ulikuwa umezaliwa. Ni maendeleo gani yaliyo patikana katika kipindi hicho? Nikubalianae nawe kwa hoja ya kuongeza kudumaza maendeleo. Wananchi wanaongezewa kodi ili iongezeke hela kupambana na upinzani.
Kukosa kwetu maendeleo kulisababishwa na sera mbovu ya kiuchumi, ya ujamaa na si kukosa demokrasia. Na kuwa na sera nzuri za kiuchumi si lazima uwe na demokrasia
 
Mambo mengine inategemea na mwamko wa wananchi wenyewe ukoje.Kama uko kwenye jamii ya vilaza maana yake itachukua muda kustaarabika.lakini kwavile tuko kwenye zama za mabadiliko na ukuaji wa technolojia,inakua ni rahisi kuelimika kuliko uko tulikotoka.kwahiyo nadhan ni kizazi hichi cha kwetu ndio kizazi cha mwisho cha jamii ngumu kustaarabika ila kizazi kinachokua sasa kitakua tofauti sana na sisi.
Na ni kizazi cha mwisho kutawaliwa kwa mfumo uliopo. Kizazi kijacho watu watakuwa wameelimika zaidi, na ni vigumu kumtawala mtu alielimika, japo ni rahisi sana kumwongoza.
 
Uko duniani wanajiandaa kwa mapinduzi ya technologia ya awamu ingine...

Sisi bado tunazindua matundu ya vyoo mashuleni na madawati mapya
Waziri mkuu kagoma kuzindua kibanda cha Mlinzi kilichojengwa kwa tsh.7mil.

Ndio habari ya mjini hio.
 
Unasoma kwenye magazeti na kusikiliza kwenye magenge au una uzoefu. Mimi nimekaa US and Canada kwa miaka 20. Nime tembelea zaidi ya nchi kumi nyingine hivyo naongea kwa uzoefu. Mfumo wa demokrasia ni bora kuliko mifumo mingine yote. Mifumo mengine ni lazima kutakuwa na matabaka au ukabila. lakini kibaya ni kulazimishana mfano huko China kutoa mimba ni sera ya serikali! kuna waislamu zaidi ya milioni wamewekwa kwenye kambi kwasababu tu ya dini yao hawana makosa yeyote!. Huko Urusi watu wanapigwa risasi waziwazi. Hata nchi za kiarabu mtoto anazaliwa lakini kama sio mtu wa kwao mtoto anakuwa hana haki nenda Dubai na nchi nyingine za ukanda ule uone.
Nchi hizo zimeendelea hivyo sababu ya sera nzuri za kiuchumi. Na kuwa na sera nzuri si lazima uwe na demokrasia. Huku kwetu tuna sera mbaya za kiuchumi na mzigo wa demokrasia juu. Watu wameanza kupigania sera nzuri za kiuchumi huko Uingereza kabla hata ya demokrasia. Mfano mmoja ni walipinga kuongezewa kodi bila kushirikishwa.

Watu wanaweza kuwa huru bila demokrasia, na watu wanaweza kukandamizwa hata kwenye demokrasia.
 
Unatakiwa ujue kua mtu wa chini haimaanishi mtu moja mmoja bali ni wananchi wote kwa ujumla wao.Tatizo hapa ni sisi wananchi wenyewe tumeshindwa kujua thamani yetu ndo maana tunaonekana sio chochote ila nikwambie tu kua wananchi wanaweza kufanya lolote na likawezekana endapo wataamua kwa pamoja.
Tanzania bado hajafikia hapo. Maliasili za nchi zinaporwa na watawala lakini bado mwananchi kijijini anasehemu ya kukanyaga na kuweka tuta la muhogo, mjini bado ukiwa na sh 200 unaweza kununua kipande cha muhogo ukanywa maji na siku ikapita. Lakini muda unao kuja si rafiki kwa wote, tunaenda kwenye boiling point.
 
Nchi hizo zimeendelea hivyo sababu ya sera nzuri za kiuchumi. Na kuwa na sera nzuri si lazima uwe na demokrasia. Huku kwetu tuna sera mbaya za kiuchumi na mzigo wa demokrasia juu. Watu wameanza kupigania sera nzuri za kiuchumi huko Uingereza kabla hata ya demokrasia. Mfano mmoja ni walipinga kuongezewa kodi bila kushirikishwa.

Watu wanaweza kuwa huru bila demokrasia, na watu wanaweza kukandamizwa hata kwenye demokrasia.

Sera mbaya zinachangiwa na kutokuwa na demokrasia. Sasa utakuwaje na sera nzuri kama watunga sera wote wanachaguliwa na mtu mmoja !. Hata kujadili mabadiliko ya katiba hayaruhusiwi sasa tutarekebisha vipi hizo sheria
 
Hapo Tatizo ni demokrasia au tatizo ni sisi waafrika?.Elekeza lawama zako sehemu sahihi maana demokrasia ni pana na iko sehemu nyingi duniani ila sehemu kubwa ya matatizo uliyoyataja yako Afrika.kwahiyo hadi hapo tatizo ni sisi wakazi wazawa wa Afrika nasio demokrasia.
Ombi langu kwa mara nyingine. Kwa upana wake hiyo demokrasia, nitajie nchi moja tu iliyoendelea kwa sbabu ya demokrasia. Nasema moja tu!
 
Kukosa kwetu maendeleo kulisababishwa na sera mbovu ya kiuchumi, ya ujamaa na si kukosa demokrasia. Na kuwa na sera nzuri za kiuchumi si lazima uwe na demokrasia
Binadamu kwa asili ni kiumbe mwenye tamaa, bila mipaka na misingi ya kutawala , hizo sera nzuri bila kuwa na mifumo thabiti ya kuwahoji wanayo iandaa, unatudanganya. Wewe inaonekana ni kutokea tawala za kitemi. Mipango ya mtemi kuwakamua wananchi na kujilimbikizia mali kwako ni sera nzuri za uchumi.
 
Back
Top Bottom