Demokrasia inatupotezea sana muda na nguvu


Kama kwa mawazo yako uchaguzi wa mwaka jana ulikuwa wa huru na haki na hakuna kura zimeibiwa basi hatutaweza kuelewana. Imefika wakati wa kuwaacha watu wamebishane na wenzao wanaopenda ligi za mabishano yasiyo na tija mimi sina muda huo. Siku ukiaamka ndugu yangu tutakutana kwenye hoja lakini endelea kulala!. Uelewa wa vijana wetu siku hizi unatisha kwa uduni kuliko hata udikteta. Hawa ndiyo viongozi wetu wajao ambao tutawapa nchi waendeshe wakati wanajidanganya mpaka nafsi.
 
Demokrasia na maendeleo ni vitu tofauti kabisa. Si lazima kuwa na demokrasi ili kupata maendeleo, tena demokrasia ni adui wa maendeleo. Maana demokrasia na kodi/tozo kubwa ni kaka na dada.
Mbona jpm alizima demokrasia lakini nchi ilikuwa inaenda ICU kwa wawekezaji wote kukimbia na mzunguko wa pesa kukata
 
Mbona jpm alizima demokrasia lakini nchi ilikuwa inaenda ICU kwa wawekezaji wote kukimbia na mzunguko wa pesa kukata
Wawekezaji hawakukimbia sababu ya kukosekana kwa demokrasia, walikimbia sababu ya sera za kiuchumi za JPM. Hazikuwa rafiki kwao.
 
Wewe ni miongoni mwa hao wakwamishao Afrika kupiga hatua kwasababu ya viashiria vyako vya ubinafsi mkubwa ulivyovionyesha.

(Samahani kwa kukushut namna hii)

Demokrasia unayoilaani inaelekeza watu kujadili mambo yao kwa ukweli na uwazi ili kupata suluhisho. Wewe unaonekana kupenda zile kauri za kufanya kila kitu siri - huko kwenye siri ndiko hujaa wabadhirifu wenye vichwa mgando wasio na utu wala aibu.

Kinachotokea Afrika ni ushamba wa madaraka. Mtu akipata madaraka anajiona yeye si binadamu wa kawaida na kujiona kuwa ana akili kuliko watu wote walio chini yake.

Mtazame yule mama wa Ujerumani(nchi yenye demokrasia hata USA wakasome) Yule mama kila linapotokea jambo huita mawaziri wake hukaa pamoja wakijadiri tena wakati mwingine live kwenye tv, uamuzi unaotolewa kila mtu anakubaliana nao.


Itazame Ujerumani iliyokuwa chini ya mataifa yaliyoshinda WW2 hadi mwaka 90 yakipora mali ya Ujerumani kwa kisingizio cha kujilipa hasara ya vita. Ujerumani ya leo baada ya 1990 imekuwa ni nguzo ya Ulaya.

Tunachotakiwa kukifanya ni kupigania kupata wawakilishi wetu walio sahihi kwenye uongozi wa nchi. Tunapokosa uwakilishwaji ulio sahihi ndipo hutokea utopolo wote huo unaousikia.
Amen[emoji120]
 
Hoja mujarabu kabisa, hii kitu sio ya Africa, pia hii inadhihirisha ni kwa kiasi gani vuguvugu la ukombozi wa Africa kupitia kina Nyerere, Kenyatta, Nkurumah, Lumumba na wengineo lilivyokwama au kufeli kabisa.

Ikiwa mfumo wako wa uongozi ni lamiza, bila hiyari kuwa Copy and Paste kutoka kwa jirani budi kujitafakari uhuru wako wa maamuzi.
Kama mfumo unaruhusu matatizo kwa karibu bara zima basi haufai kabisa. Au hautufai kabisa. Na si Africa tu, huko South Amerika na South East Asia shida tupu.
 
Wawekezaji hawakukimbia sababu ya kukosekana kwa demokrasia, walikimbia sababu ya sera za kiuchumi za JPM. Hazikuwa rafiki kwao.
Ndo demokrasia yenyewe otherwise huelewi maana ya demokrasia. Rudi shule
 
Ndo demokrasia yenyewe otherwise huelewi maana ya demokrasia. Rudi shule
Demokrasia na sera nzuri za kiuchumi ni vitu mbalimbali. Zaidi zaidi demokrasia huzalisha sera mbovu za uchumi na kodi kubwa.
 
Wavivu wengi hukimbilia kwenye kulalama

Na demokrasia is a very good Avenue for that
 
Wavivu wengi hukimbilia kwenye kulalama

Na demokrasia is a very good Avenue for that
Na watu wanapredict itakuja kuharibu mambo kama ujamaa tu. Sababu watu wanapiga kelele, na kwenye demokrasia wengi wanaopiga kelele wanasikilizwa. Unapaswa kuwapa wanachotaka la sivyo wanakuangusha. Wanapiga kelele wanapewa bima ya afya kwa kila mtu, wanapiga tena kelele wanapewa elimu bure, wanapiga tena kelele wanapewa hiki na kile bure. Sasa serikali inapata wapi pesa zote hizo? Inazidi kuongeza tozo na mwisho wa siku ni mkwamo mkubwa wa uchumi, na shida tupu. Mwisho wa siku serikali haitaweza kufanya chochote zaidi ya kuhudumia mahitaji yasiyoisha ya wapiga kelele. Wanapredict hiyo ndiyo hatima ya welfare state zinazozalishwa na demokrasia.
 
Tatizo sii Demokrasia ila ni mfumo wa chama kimoja kungangania kubaki madarakani il-hali wanajua hawapendwi tena na wananchi. Matumizi ya dola kubaki madaraki ndicho kitu kingine kinachoichafulia nchi.
 
Si lazima. Libya iliendeshwa kibabe na ilikuwa tulivu kwa miaka mingi. Huko North Korea hatusikii watu kuuuana kama walivyouawa watu Zanzibar mwaka jana, au Kenya 2008.
Ndugu, kwa mifano hiyo ya utawala HAPANA.
Libya ya Gadafi ilikandamiza makabila madogo ya kusini mwa nchi na iilkuwa kichaka cha magaidi waliosumbua sana dunia. .
North Korea; Ukitofautiana na MKUU unapotezwa kama yaliyomtokea hata KAKA mtu pale Kuala Lumpur International Airport, Malaysia.
Kote huko yawezekana panakuwa na utulivu kwa kiasi fulani, ingawaje PIA inategemeana hilo linasemwa na nani.
Lakini juu ya yote kinachohitajika katika nchi ni AMANI. Huu ndio msingi wa haki na hatimae MAENDELEO.
 
umenikumbusha kipindi cha wimbi la kununua viongozi wa wapinzani, wabunge na madiwani aisee kilikuwa kipindi cha mavuno kweli kweli
Aliyechezea fursa ni kigogo pekee ndo alipishana live na hela za jiwe.Waunga juhudi walimdisi jiwe kutengeneza cv ya kununuliwa na jiwe kwa bei juu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…