Demokrasia: Maana, misingi yake na faida kwa jamii

Demokrasia: Maana, misingi yake na faida kwa jamii

Kadhalika mimi pia hujanielewa vyema bro ! Ninaposema misingi ya jambo yaani humo taarifu (definitions) zote hazitok isipokuwa humo humo katika misingi hiyo.

Mfano misingi au msingi mkuu wa mfumo huu wa Demokrasia ni uhuru.

Sasa wewe unaezijua taarifu zote hizo unatakiwa kuielezea kila moja mapungufu yake kutokana na inavyojielezea.

Umegusia hiyo maana ya Demokrasia iliyoenda ndani zaidi kuhusu au inezingatia elimu,swali je ni elimu gani iliyokusudiwa katika maana hiyo ?

Sent using Jamii Forums mobile app
Elimu ya kuweza kuchagua unachotaka, zuri dhidi ya baya kwa mfano.

Unaweza kusema demokrasia ni kuwa na uchaguzi.

Sawa, unawapa watu uchaguzi, lakini hawaoni mijadala inavyokwenda bungeni (hawana TV, hawana umeme, hawana magazeti, hawajui mijadala inaendaje, hawajui nani anasema nini na kuetetea nini).

Ikija siku ya uchaguzi, unasema Tanzania ina demokrasia kwa sababu watu wana uhuru wa kuchagua, lakini kama hawajui tofauti ya kimoja na kingine, kwa sababu hawana elimu, watatumiaje uhuru huu kuchagua kinachowafaa?

Hapo utaona hiyo demokrasia ni geresha, ndiyo kama hi ya Tanzania.

Demokrasia ya uchaguzi, lakini watu hawana uhuru hata wa kuangalia Bunge live, au kufanya mikutano ya siasa.

Hiyo si demokrasia.

Sasa kama hatuja define vizuri demokrasia, tunaweza kusema Tanzania ina demokrasia ya vyama vingi, wakati kiukweli haina demokrasia.

Hapo ndipo umuhimu wa definition unapokuja.

Bila kuanza na definitions,tunaweza kuzungumzia demokrasia huku tunazungumzia.vitu viwili tofauti.
 
Ni mfumo wa utawala ambamo viongozi wa serikali huchaguliwa na wananchi wa nchi husikia kwa kupiga kura.

Wagombea wanaopata kura nyingi ndio wanaunda serikali kwa msingi wa wengi wape, yaani wale walioshindwa wanakubali kuongozwa na waliowashinda hata kama ushindi huo ni wa kura moja tu kati ya kura milioni 50, bado demokrasi inasema wengi wape. Hiyo ni fofauati na utawala wa kidikiteta ambapo mtu mmoja anatumia nguvu kuingia madarakani mara nyingi kwa njia ya mapinduzi ya mabavu bila kujali kama anaowangoza wanamkubali au hapana; kwa mfano utawala wa iddi Amini ulikuwa wa kidikteta.

Utawala mweingine wa kidikiteta, ambao ni ule ambao kunapigwa kura ya mtu mmoja tu, halafu anapata kura zote, kama ilivyokuwa wakati wa Utawala utawala wa Saadam na pia wakati wa Nyerere ingawe yaye aliruhusu Bunge liwe la kidemokrasia, uraisi haukuwa unapatikana kidemokrasia.

Haki za bianadamu hazina uhusiano kabisa na demokrasi ingawa serikali ya kidemokrasia sahihi itakuwa pia inafuata haki za binadamu. Utawala wa Ghadafi, kwa mfano haukuwa wa kidemokrasisa, lakini ni utawala uliokuwa unafuata sana haki za binadamu, wakati utawala wa Hitler ulikuwa wa kidemokrasia lakini haukuwa unafuata haki za binadamu; wao walikuwa na haki za wajerumani tu, wengine wote walijulikana kam subhuman.

Je utawala wentu tanzania uko kwenye mizani gani, maana nimesikia wakubwa wanasema hatuna demokrasia. Je tuna viongozi waliojinyakulia madaraka bila utashi wa wanachi wetu?
 
Demokrasia yetu ni ya kwenye makaratasi , ni ya kwenye katiba tu, hatuna tume huru ya uchaguzi. Chama kilichoko madarakani kinaweza kutawala milele kwa kutumia vyombo vya dola.

kikubwa kinachofanya wakubwa waanze kuingilia demokrasia yetu ni kwamba chama kilichopo madarakani sasa kimegeuka kuwa cha kigaidi, kinajibu hoja kwa vitisho na utekaji na mauaji. Na kinara wa vitendo hivyo ni Bashite.

Wamarekani hawataki wakija nchini mwetu waishi kwa hofu ya kutekwa au kukamatwa. Na hawataki mtu muhalifu hata kama anafadhiliwa na mfumo wa nchi yake akanyage ardhi yao.

Hivyo basi wakubwa wanatuhimiza turudi kwenye misingi ya demokrasia na utawala bora ili tusizalishe akina bashite wengine , ni hatari kwa dunia. Wanataka wananchi wa Tanzania wawe na nguvu ya kuchagua viongozi wanaowataka na kuwaondoa madarakani muda wowote watakapokengeuka.

Tukiwa na demokrasia na utawala bora wakubwa watajisikia amani kuja nchini kuwekeza na kupumzika na kuleta misaada na watajisikia amani tuendapo nchi zao.
 
Kufuatana na maelezo yako ya maana ya demokrasia, huyo anayechaguliwa hata kura moja ya ziada anapoingia madarakani na kujitwalia mamlaka yote yeye, bado hapo tutakuwa tunatambua kwamba kiongozi huyo anaongoza kidemokrasia.

Anapoingia madarakani, na kupewa nyenzo zote za taifa na kuzifanya zake, na kuzitumia ziwanyime hao waliompa kura milioni 50+1 wasiweze tena kuwa na uhuru wa kuchagua tena, hiyo bado tutaiita demokrasia bila ya kuichanganya na 'utawala bora', kwa maana vitu hivi viwili ni mbalimbali kabisa!

Mtu tunayemchagua kwa kura moja ya ziada, anapoamua katiba na sheria zilizowekwa na taratibu zote tulizokwishajiwekea yeye anachambua anazotaka kuzifuata na anazotaka kuzikataa kwa matakwa yake, bado tutakuwa na haki kwamba nchi yetu ni ya kidemokrasia, hata kama tunajua 'utawala bora' hauwezi kutenganishwa na matakwa ya kidemokrasia?

Bunge, Mahakama, mihimili inayojulikana kuwa sehemu ya demokrasia nchi zote, yeye tuliyemchagua kwa kura moja ya ziada ikimpendeza mihimili hii aiweke chini ya' mzizi wake uliojichimbia chini zaidi" hapo bado tutafurahi na kushangilia kiongozi wetu huyu tuliyemchagua kwa imani ya wengi wape!

Na wabunge je, wawakilishi wa wananchi ambao pia wamechaguliwa kwa kura hizo hizo za 'kidemokrasia', yaani ya maana ya "wengi wape" huyo tuliyempa kura moja ya ziada, anapoamua wawakilishi wetu hawa anaweza kuwatumia apendavyo yeye, hata bila ya matakwa yetu tuliopiga kura, bado inatubidi tumwimbie wimbo mtamu wa 'demokrasia' hata anapowanunua au kuwatia misukosuko hao tuliowachagua sisi?

Hiyo maana ya demokrasia uliyoieleza hapo kwenye mada yako itakuwa ni demokrasia yenye hitilafu kubwa.

Kama demokrasia maana yake ni "wengi wape", hata ile iliyokuwepo wakati wa chama kimoja basi itabaki kuwa ilikuwa ni demokrasia.
Watu walikuwa na uhuru wa kumpigia kura Mwalimu Nyerere au kukipigia kura kivuli. Wengi wangechagua kivuli, kwa nini uchaguzi huo tusiuite kuwa ni wa kidemokrasia?
 
Kwa tafsir ya Abraham Lncolin alielezea demokrasia kuwa Ni mfumo wa keserikali wa watu unaondeshwa na watu kwa manufaa ya watu" Ukizungumza watu na tafsir hii ni vitu viwili visivyokubaliana na maumbile kuwa na tamaa ni maumbile na ayo ndo yaliyopelekea mfumo huu wa kidemokrasia kushindwa leo kila mmoja amekuwa mbinafsi,kwenye siasa za upinzani bado wanaamini katika demokrasia mbali ya kuwa na mapungufu makubwa kwa mfano nilimsikia mama yangu au dada Fatma karume yaan ukimtja tu jina unaona Ni mbepari hlf anajiita muumini wa demokrasia.
 
Back
Top Bottom