Demokrasia Marekani kubwa sababu wanasiasa wana shughuli za kuwaingizia vipato nje ya siasa tofauti na Tanzania

Shotocan

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2023
Posts
6,650
Reaction score
12,711
Demokrasia Marekani kubwa sababu wanasiasa wana shughuli za kuwaingizia vipato vya kutosha nje ya siasa tofauti na Tanzania

Kwa Tanzania ukianzia upinzani hadi Chama tawala wengi waganga njaa tu hawana shughuli za maana za kuwaingizia kipato cha kutosha zaidi ya kuwinda tu fursa za kisiasa wawe Chadema au CCM nk ndio maana hata chaguzi tu ndani ya vyama ni mshike mshike watu wasio na vipato vya kuelekwa nje ya siasa wakiwinda pesa kwenye siasa

Marekani wao huangalia kwanza mtu ana nini ? Ana mali au kipato gani cha kutosha nje ya siasa ndio humpa nafasi

Tanzania nadhani tunapenda wapiga mayowe tu ndio maana nchi haiendelei na vyama hasa vya upinzani havifanyi vizuri sana kwenye chaguzi ziwe za ndani au chaguzi za kitaifa .Wanajaza zaidi wapiga mayowe wasio na kipato cha kutosha hakikika nje ya siasa

Watu wa aina hiyo kuifikisha nchi au chama cha siasa mbali ni changamoto sio rahisi
 
Kuzunguka kwako kote ulikuwa u awalenga wapunzani ila umejifanya kutaja CCM ila hiyo aya ya mwisho imedhihirisha ulikuwa unalenga nini
 
Demokrasia Marekani kubwa sababu wanasiasa wana shughuli za kuwaingizia vipato vya kutosha nje ya siasa tofauti na Tanzania

Kwa Tanzania ukianzia upinzani hadi Chama tawala wengi waganga njaa tu hawana shughuli za maana za kuwaingizia kipato cha kutosha zaidi ya kuwinda tu fursa za kisiasa wawe Chadema au CCM nk ndio maana hata chaguzi tu ndani ya vyama ni mshike mshike watu wasio na vipato vya kuelekwa nje ya siasa wakiwinda pesa kwenye siasa

Marekani wao huangalia kwanza mtu ana nini ? Ana mali au kipato gani cha kutosha nje ya siasa ndio humpa nafasi

Tanzania nadhani tunapenda wapiga mayowe tu ndio maana nchi haiendelei na vyama hasa vya upinzani havifanyi vizuri sana kwenye chaguzi ziwe za ndani au chaguzi za kitaifa .Wanajaza zaidi wapiga mayowe wasio na kipato cha kutosha hakikika nje ya siasa

Watu wa aina hiyo kuifikisha nchi au chama cha siasa mbali ni changamoto sio rahisi
Mtu Kama Lissu hana kitu zaidi ya lile tumbo unategemea atafanya nini zaidi ya kuchukia wenye nacho?
 
Tanzania mazingira ya kujiajiri kibiashara ni magumu ndo maana wanasiasa wanashindwa kuendesha shughuli halali nje ya siasa
 
Siasa za Tanzania na Africa zimetawaliwa na uchawa
Uchawa = umaskini wa kipato.
 
Ni sisi wenyewe hapa hapa JF huwa tunalalamika kuwaweka wafanya biashara kuwa kwenye nafasi za uongozi, tukisema wanatunga sera na sheria kwa manufaa ya biashara zao.
Wewe tena unalalamika wasio na kipato kuwa viongozi.

Hatueleweki..!!!!
 
Back
Top Bottom