Demokrasia ni adui wa maendeleo

LKY alikuwa dikteta jambo ambalo hata yeye binafsi hakuwahi kupinga sifa hiyo na siku zote alikuwa proud kuonekana hivyo na hakuwahi kuipenda demokrasia katika maisha yake.

Nimeweka records sawa
LKY alikuwa dikteta katika mambo gani?
Ni mambo gani aliyoyafanya yaliyomtambulisha kama dikteta??
 
Unayoiongelea siyo demokrasia. Ni kundi la wanafiki
 
Mijitu mivivu na mijizi sikuzote hulaumu...
 
Kwahiyo Wizi wa kura ndio mfumo mzuri kwa Nchi?!
Nyerere alitutawala kwa mfumo wa Authoritarian Maendeleo yalikiwepo?
 
Ili kufahamu kama ni demokrasia au udikteta ndio unaohitajika Tanzania tutazame demokrasia tuliyonayo. Utagundua kwamba misingi ya demokrasia ambayo inahusisha chaguzi kila baada ya miaka mitano ipo lakini misingi mingine ya demokrasia haipo. Misingi hii mingine ni kama uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa maoni kuhusu maswala ya nchi kutoka Kwa wananchi, uhuru wa fikra na hata uwepo wa upinzani kama afya kwenye demokrasia. Chama tawala kina wanyima wananchi haki za msingi ambazo ni muhimu kwenye demokrasia yoyote. Elewa kwamba demokrasia iliyopo Tanzania ni "Illiberal democracy" , ambayo haina tofauti sana na udikteta. Ila nina kubaliana na wewe, udikteta unahitaji uhakika wa Rais anayegombea na serikali yake. Jambo hili limewashinda wengi na benovelance kwenye nafasi ya authority ni Jambo ambalo haliendani na ubinadamu wa kawaida. Kama demokrasia itaendelea kudumu, misingi yote inatakiwa kitiliwa maanani na kutekelezwa Kwa manufaa ya wananchi.
 
Kule kutajwa tu kuwa ni Nchi zinazofuata Utawala wa kidemokrasia hata kama haki za kidemokrasia hazifuatwi tayari zimo kwenye matatizo kama alivyofafanua mleta hii mada !!

Viongizi wa Africa,wakiapishwa hawana tena Cha kuwaza zaidi ya uchaguzi ujao, ayo maendeleo unayoyasema kwa mlolongo huo utayapataje?na ilo ni zao la kulazimisha mifumo isiyoendana na sisi katika nchi zetu kama iyo democrasia. Mtoa mada yupo sawa

Congo Brazzaville, Cameroon, Lesotho, Eswatini, Sudan, Uganda etc zina maendeleo gani ilhali hazina democracy?
 
LKY alikuwa dikteta katika mambo gani?
Ni mambo gani aliyoyafanya yaliyomtambulisha kama dikteta??
Alifunga wapinzani wake kisiasa,zuia maandamano ya kisiasa, alizuia harakati zote za kisiasa zilizokuwa kinyume na mtazamo wake na wa chama chake.
 
Idiamin alikuwa dictator aliifanyia nini Uganda?Hatuna demokrasia Africa kuna Domokrasia
 
Una uhakika??
Marais wote wazungu wa south afrika walichaguliwa kidemokrasia
Uchaguzi huru wa south afrika, mahakam imara msingi wake ulitengenezwa kipindi cha apartheid

Kumbuka apartheid ni mbaya ila ina-mazuri yake
 
Kwa maana hiyo hoja yako unaona ni bora tubadili Katiba na Sheria zetu ili turudi mahameni siyo (chama kimoja kushika hatamu za uongozi)
Swali; toka mwaka 1961 hadi 1992 (30 yrs) wakati tunabadili katiba yetu ni maendelea gani chanya yalitokea ambayo unaweza kuyatumia kama vielelezo ili kujenga hoja yako ipate nguvu.
 
Tanzania hakuna demokrasia sababu msingi wa demokrasia ni kuwepo kwa uchaguzi huru, bunge na huru mahakama Mfano nchi za demokrasia Rais akiwa nje ya madaraka anaweza shtakiwa na kufungwa
 
Kama nakuelewa vile...!
 
Alifunga wapinzani wake kisiasa,zuia maandamano ya kisiasa, alizuia harakati zote za kisiasa zilizokuwa kinyume na mtazamo wake na wa chama chake.
Nitajie hao wapinzani wake waliofungwa?
 
Hata hizo Nchi zilizoendelea kuna Deep state ambayo ipo juu ya sheria, Nchi kama Usa Raisi sio kiongozi mkubwa kabisa, kuna watu ambao raisi hawezi wagusa, Deep state = Disctator = Mfalme etc
 
Nitajie hao wapinzani wake waliofungwa?
Operation coldstore 1963 zaidi ya wakomunisti 100 walikamatwa.

Lee did not believe that "democracy necessarily leads to development" and that "the exuberance of democracy leads to undisciplined and disorderly conditions which are inimical to development".

So when people say, 'Oh, ask the people!' It's childish rubbish. We are leaders. We know the consequences. You mean that ice-water man knows the consequences of his vote? They say people can think for themselves? Do you honestly believe that the chap who can't pass primary six knows the consequences of his choice when he answers a question viscerally on language, culture and religion? —Lee Kuan Yew, 1998.

Lee was an outspoken critic of Western ideals of democracy, stating that "with a few exceptions, democracy has not brought good government to developing countries." He argued that in states such as China, the concept of democracy was simply "not workable", because of the large population size that had to be canvassed, while in India, the results of democracy "have not been spectacular". He believed in the state interference of the media and personal lives of citizens. He has been criticised for using his political power to wage lawsuits to bankrupt and imprison his political opponents, as in the case of J. B. Jeyaretnam and Chee Soon Juan. Francis Seow, the former solicitor-general of Singapore, has described Lee as such:

he prime minister uses the courts… to intimidate, bankrupt, or cripple the political opposition. Distinguishing himself in a caseful of legal suits commenced against dissidents and detractors for alleged defamation…, he has won them all.
 
Tanzania hakuna demokrasia sababu msingi wa demokrasia ni kuwepo kwa uchaguzi huru, bunge na huru mahakama Mfano nchi za demokrasia Rais akiwa nje ya madaraka anaweza shtakiwa na kufungwa
 
Naona umekariri tu vitu visivyo na muunganiko. Kigezo cha kwanza kikuu cha demokrasia ni uchaguzi huru na wa haki, Singapore imeshafanya chaguzi 13 tangu uhuru ambazo hazijawa na malalamiko ya wizi wa kura au uchakachuaji wa matokeo. Ni huyo Lee pia ambaye alisema ni muhimu sana kwenye nchi raia wakachagua viongozi wanaowataka wao kuwaongoza ili nchi ifanikiwe.
 
..Udikteta umeshindwa kuleta maendeleo Afrika, ndio maana kumekuwepo na kelele za kudai demokrasia.
Ghadafi mfano mzuri na Morocco Nchi zao huwezi fananisha na Zetu, pia Hata hapa Tanzania Nyerere alifeli tu sera za Uchumi ila other aspects kama Elimu tulikua vizuri tu, moja ya data kali za Nyerere miaka ya 1970 literacy rate ya Tanzania ilikua asilimia 90, compare na sasa literacy rate imeshuka hadi asilimia 80 na bado quality ya elimu ni mbovu mno compare na Zamani.
 
Morocco ni nchi ya uchumi wa kawaida tu lakini yenye rasilimali nyingi sana.
 
Naona umekariri tu vitu visivyo na muunganiko. Kigezo cha kwanza kikuu cha demokrasia ni uchaguzi huru na wa haki, Singapore imeshafanya chaguzi 13 tangu uhuru ambazo hazijawa na malalamiko ya wizi wa kura au uchakachuaji wa matokeo.
Nini unacho jaribu kupinga na kutetea kuhusu Singapore ya LKY maana hata hueleweki
Unaita vipi nchi ya kidemokrasia mahali ambapo wapinzani wana gandamizwa ? Na kiongozi mkuu asiye amini katika huo utaratibu wa kidemokrasia unaoutetea wewe ?
Kuna vitu vya kutetea lakini sio Singapore ya Lee ambaye yeye mwenyewe mfumo mzima wa kidemokrasia alikuwa kinyume nao na alikuwa proud of Singapore mpaka leo hii haitoi uhuru bora wa maandamano moja ya legacy ya huyo LKY unaye mtetea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…