Demokrasia ni adui wa maendeleo

Demokrasia ni adui wa maendeleo

Naunga mkono title ya mada hii. Demkkrasia inafaa kwa mataifa yaliyoendelea tayari. Lakini kwetu sisi ni upotezaji wa rasilimali muda, fedha na nguvukazi
Tuanze kumlaumu Nyerere kwa harakati zake za kuitaka demokrasia na kufukuza wazungu.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Nchi inaweza kupata maendeleo ikitawaliwa kidikteta lakini siyo guarantee. Mfano Shelisheli, Libya ya Ghaddafi, labda Misri na Hata Morocco iliyo kifalme. Lakini chini ya demokrasia ni kama haiwezekani kupata maendeleo.
Kumbe hata hiyo kidictator ni probability.
 
Na hapa ndipo umuhimu wa CHUMA unapokuja.

Yule jamaa kama angetawala extra 10yrs.

Tanzania na South Africa tungekua tunapelekana Anus 2anus katika maendeleo.
Umuhimu uanze kwa wazungu na lawama zotee apewe Nyerere kwa kufukuza Wazungu.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Acha kubadilisha hoja mkuu.

Unataka sasa tuanze ku-debate maendeleo ni nini?

Ukweli ni kwamba hata kabla ya kuja demokrasia AFRIKA ILIKUWA MASIKINI.

Katika kipindi ambacho dunia yote ilikuwa in dictatorship mode, still wa Afrika hata vijiko mlikuwa nashindwa kutengeneza.

Maana yake ni kwamba, msisingizie demokrasia.

Kuna sababu zenu za kutokuendelea lakini demokrasia is not one of them.

Nimekutolea mfano wa nchi ambazo hazikufuata demokrasia na bado ni masikini wa kutupa.

This should not be hard for you to comprehend
Sehemu ya kale kabisa ya ufuaji wa chuma ilipatikana Africa, CAR; Unawashutumuje kuhusu kijiko? Mtumbwi wa kale kabisa duniani ulipatikana Nigeria. Unashutumuje kuhusu umasikini? Kwako Wamisri waliojenga mifereji ya umwagiliaji na mapiramidi walikuwa masikini?
 
Tuige mfumo wa china,swali linakuja jeee mko tayari kunywongwa na kupigwa shaba mkifanya ubadhirifu wa mali za umma?

Kimsingi demokrasia sio mbaya shida ngozi nyeudi tumejaa,unafiki,uzandiki,nepotism na kila aina ya uchafu.

Hakuna integrity wala accountability,ni rushwa na kubebana mwanzo mwisho.
Ndio mleta mada akasema hili Suala lilipaswa kuangaliwa na mazingira ya nchi husika Kwa sababu tunatofautiana kitamaduni haiwezekani mtanzania awe na tamaduni kama za USA wakati Wana tofautiana kuanzia Akili life style Maono etc
 
Kwa hiyo unaweza kuwa na mtawala dikteta asiye na vision?
Very simple,.....mtawala mwenye vision kwenye nchi ya kidikteta ana resistance ndogo kwenye kutimiza mawazo yake,kuliko kwenye demokrasia,...
 
Sheria ni dhaifu sana kwa sababu ya kufuata misingi eti ya kidemokrasia !
Hivyo watu wanafanya Ukwapuaji na ubadhirifu huku wakijua watatoboa tu !

yule Mobutu ndio maana tukasema hao madikteta wawe ni wacha Mungu Waadilifu na wenye maono yamaendeleo !
Sio mradi tu awe Dikteta !
Mfano taifa gani la kidemokrasia lenye sheria dhaifu linalofuata misingi ya kidemokrasia ambapo watu wanafanya ufisadi na ubadhirifu huku wakijua watatoboa tu??
 
Umeletwa mada nzuri sana kama unaishi katika mawazo yangu.
Asante sana kwa hoja nzuri zenye nguvu na mifano halisi kiasi kwamba kila mwenye akili ameelewa matatizo ya hili balaa linaloitwa demokrasia tulilowekewa na mabeberu toka ulaya.
Shida ni namna gani tunaweza kubadili mfumo huu muovu ambao unazidi kuzoeleka pamoja na kwamba ni mgumu kutekelezeka na kurudi kwenye utawala wetu wa asili
(utawala wa watemi na machifu )!
Utawala wa watemi na machief huko hata sishauri 🤣🤣🤣

Ni vyema Tu tukaiga kile ambacho kimefanyika UAE ama Qatar pamoja na china huwenda kikatufikisha ktk nchi ya Ahadi
 
Demokrasia kwako ina maana gani??

Mfano wa nchi gani ambazo unafikiri zina Demokrasia?
Democrasia ni utawala wa watu. Yaani watu wote wana mamlaka ya kuamua nchi iendeshwaje. Iwe moja kwa moja au kupitia wawakilishi. Leo hii nchi kama Uingereza, Marekani na SK ni za kidemokrasia kwa kiwango kikubwa.
 
Sehemu ya kale kabisa ya ufuaji wa chuma ilipatikana Africa, CAR; Unawashutumuje kuhusu kijiko? Mtumbwi wa kale kabisa duniani ulipatikana Nigeria. Unashutumuje kuhusu umasikini? Kwako Wamisri waliojenga mifereji ya umwagiliaji na mapiramidi walikuwa masikini?

Kwa hiyo kama waligundua ndo nini yani?
Standard yao ya maisha Wa afrika ilikuwaje? Wa Afrika hawakuwa masikini?

Au ndo mlikuwa matajiri alafu mkaletewa democracy ndo mkaanza kuwa masikini?

Yaani unajisifia kugundua mtumbwi?

Najua unataka u-spin hii hoja lakini ni ngumu sana.

Afrika ni Afrika tu. Umasikini ulianza kitambo sana.

Acha kusingizia demokrasia
 
Utawala wa watemi na machief huko hata sishauri 🤣🤣🤣

Ni vyema Tu tukaiga kile ambacho kimefanyika UAE ama Qatar pamoja na china huwenda kikatufikisha ktk nchi ya Ahadi
Kwa mafano hapa Tanzania ni familia gani au kabila gani unaona inafaa itutawale kifalme kama UAE au QATAR ili tupate maendeleo makubwa?
Unaweza kukubali Wachaga Warombo wawe kabila la kifalme kutuletea maendeleo makubwa?
 
Kwa hiyo kama waligundua ndo nini yani?
Standard yao ya maisha Wa afrika ilikuwaje? Wa Afrika hawakuwa masikini?

Au ndo mlikuwa matajiri alafu mkaletewa democracy ndo mkaanza kuwa masikini?

Yaani unajisikia kugundua mtumbwi?

Najua unataka u-spin hii hoja lakini ni ngumu sana.

Afrika ni Afrika tu. Umasikini ulianza kitambo sana.

Acha kusingizia demokrasia
Mtumbwi siyo wa maana ila kijiko ndiyo cha maana!!? Pia hii mada hujaielewa. Inasema kuwa demokrasia ni adui wa maendeleo. Nchi masikini haiwezi kuendelea ikiwa inatawaliwa kidemokrasia? Kama una ushahidi wa kupinga hili kutoka sehemu mbalimbali duniani ulete?
 
Democrasia ni utawala wa watu. Yaani watu wote wana mamlaka ya kuamua nchi iendeshwaje. Iwe moja kwa moja au kupitia wawakilishi. Leo hii nchi kama Uingereza, Marekani na SK ni za kidemokrasia kwa kiwango kikubwa.
Unamaanisha nini unaposema watu WOTE wana mamlaka ya kuamua nchi iendeshwaje??

Marekani, Uingereza na South Korea watu WOTE wanaamua nchi iendeshwaje?
 
Back
Top Bottom