HOJA Deni la Daraja la Kigamboni (Mwalimu Nyerere) litaisha lini?

HOJA Deni la Daraja la Kigamboni (Mwalimu Nyerere) litaisha lini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Unataka tuchangie nini zaidi ya kodi tunazotozwa katika mambo mengi? Au huoni hilo kuwa ni kuchangia. Na vipo tozo ya TANROADS katika kila lita ya diesel au petrol tunayonunua, bado haitoshi tu kwamba tunachangia?

Na kama ni halali sisi kuchangia hili daraja zaidi ya tozo za TANROADS na kodi, kwa nini hatuchangii kupita kwenye flyovers na madaraja mengine nchini?
Daraja hilo halijajengwa kwa kodi limejengwa kwa michango ya wafanyakazi NSSF, hela hizo lazima zirudi. Hizo msizolipia zinejengwa kwa kodi za wananchi wote.
 
Daraja hilo halijajengwa kwa kodi limejengwa kwa michango ya wafanyakazi NSSF, hela hizo lazima zirudi. Hizo msizolipia zinejengwa kwa kodi za wananchi wote.
Hujaelewa. Mwenye daraka la kuilipa NSSF ni serikali, kwa sababu sisi michango yetu ya kujenga hilo daraja tulishapeleka na tunaendelea kupeleka serikalini. Ndio maana hatutozwi kodi kupita kwenye Kijazi flyover au daraja la Mkapa
 
Acha hizo za kujifanya ni mzalendo sana. Huu ni ukamuaji tu wa serikali kwa wananchi wake. Tunachangia sana, na kodi zote za miundo mbinu ya barabara serikali ilisema itaweka tozo kwenye kila lita ya petroli na diesel. Kuchangia daraja hili ni kutozwa kodi ya barabara mara mbili
Hakuna cha uzalendo wala nini?? hutaki kulipia darajani usipite kwenye hilo daraja, hulazimishwi. Simple.
Madaraja mengi duniani na barabara i.e highways/motorways kuna road toll watu wanalipia pamoja na makodi kibao ya wenye magari, hutaki tumia usafiri wa public ili usilipie ila nao unalipia humo humo kwenye nauli.
Kwa taarifa yako nchi nyingi za Africa maendeleo yapo duni kwa vile majority ya wananchi wao hawalipi kodi ipasavyo.FACT.
 
Tozo bei rahisi sana hiyo,Congo wajapan sijui wachina wamejenga barabara zao kila sehemu sasa wao Tozo zao hakuna iliyo chini ya dola 50 na nyingine hadi dola 300 ile ya kasumbalesa..kutoka kasumbalesa mpk Kolwezi kwenda na kurudi unatoa Peage(tozo) hadi $ 2000
Sasa distance ya kilometer almost 400 utalinganisha na km za lile daraja la Nyerere?

Congo hakuna miundombinu ya kutosha hivyo kuacha wawekezaji wajenge na kutoza ni sawa tu maana itasaidia barabara kujengwa kwa kasi bila input ya serikali. Sasa hapa Tanzania ambapo tuna barabara, madaraja na flyover kibao kuna haja gani ya kutoza miaka 30?

Billion 300 si ingelipwa kwa bajeti za miaka 10, mbona tunatenga 1 Trillion ya safari na Matrilion kuandaa AFCON je hiyo 300B ni kitu gani?
 
Hakuna cha uzalendo wala nini?? hutaki kulipia darajani usipite kwenye hilo daraja, hulazimishwi. Simple.
Madaraja mengi duniani na barabara i.e highways/motorways kuna road toll watu wanalipia pamoja na makodi kibao ya wenye magari, hutaki tumia usafiri wa public ili usilipie ila nao unalipia humo humo kwenye nauli.
Kwa taarifa yako nchi nyingi za Africa maendeleo yapo duni kwa vile majority ya wananchi wao hawalipi kodi ipasavyo.FACT.
La ufisadi na ubadhirifu wa fedha za umma hujaona kabisaaaaa!
 
La ufisadi na ubadhirifu wa fedha za umma hujaona kabisaaaaa!
Ufisadi ni mada ingine mkuu, ila hapo kwa ufisadi wabongo lazima mpigwe sana maana ni wazembe na wavivu muone TL anaozea jela mijitu anayoitetea wala haina habari. Akina Polepole, Mdude wamepotea mijitu imefubaa tu, ingekua nchi nyingine mafisadi ya serikali yangekiona cha moto. Nchi yetu ni ya amani mtuache bana kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake si ndio.
 
Hata ulichokiandika huitambui, nitakusaidiaje?

Jitahidi utembee uone vitu kisha ujifunze kuandika baadae kuongea, itakusaidia maishani.
bwege sana ww mm nimeandika kuhusu Congo ni sehemu ambayo naijua tangu nipo kijana mpk sasa namiliki malori yangu na yanaenda huko always,Ww upuuzi wako wa kutoelewa kilichoandikwa utajua mwenyewe na ufurambute wako huko ulipo usifikiri watu tunaongea hili kufurahisha genge,bahat nzuri hapa nilipo nina risiti ambayo nimelipia Peage/toll/tozo moja ya Lualaba mwez uliopita nilienda Congo mwenyewe.
IMG_20260804_160548.png
 
Attachments

  • IMG_20260804_160548.png
    IMG_20260804_160548.png
    2.6 MB · Views: 12
Hakuna cha uzalendo wala nini?? hutaki kulipia darajani usipite kwenye hilo daraja, hulazimishwi. Simple.
Madaraja mengi duniani na barabara i.e highways/motorways kuna road toll watu wanalipia pamoja na makodi kibao ya wenye magari, hutaki tumia usafiri wa public ili usilipie ila nao unalipia humo humo kwenye nauli.
Kwa taarifa yako nchi nyingi za Africa maendeleo yapo duni kwa vile majority ya wananchi wao hawalipi kodi ipasavyo.FACT.
Mbona hatulipii kijazi interchange? Mfugale Bridge? Daraja la mkapa? Malagarasi?

Unaweka toll kwenye luxury mfano Daraja la Tanzanite maana kuna mbadala wa serrander Bridge ambalo haliko mbali sasa pale daraja la Nyerere mtu ana mbadala gani? Azungukie mbagala au Ferry ilihali pale ndio shortest distance?

Watu wanalipa kodi sana Tanzania hasa indirect tax, unaposema hatulipi kodi unatumia hesabu ipi? Hivi unajua indirect tax ni 70% ya mapato yote ya Tanzania?

Kumbuka Wengi sio waajiriwa ni informal sector ndio maana huwezi ona Tax to GDP ratio inapaa maana informal sector haijarasimishwa eg bodaboda, madalali, mawinga, saidia fundi, social media influencers etc.
 
Cumulative Revenue: Over TZS 102.18 billion has been collected since operations began.
Purpose:
Toll collections are legally mandated to service the original $135–$136 million construction loan.

Future Outlook:
The bridge will completely transition to 100% free government public ownership once the full TZS 344 billion total project investment cost is fully recovered.
 
Sasa distance ya kilometer almost 400 utalinganisha na km za lile daraja la Nyerere?

Congo hakuna miundombinu ya kutosha hivyo kuacha wawekezaji wajenge na kutoza ni sawa tu maana itasaidia barabara kujengwa kwa kasi bila input ya serikali. Sasa hapa Tanzania ambapo tuna barabara, madaraja na flyover kibao kuna haja gani ya kutoza miaka 30?

Billion 300 si ingelipwa kwa bajeti za miaka 10, mbona tunatenga 1 Trillion ya safari na Matrilion kuandaa AFCON je hiyo 300B ni kitu gani?
Nadhani ni mfumo wa kidunia hasa kuhusisha sector binafsi katika maendeleo ya miundombinu hasa kwa mfumo wa PPP..Hii kitu haipo Tanzania tu na congo hata Marekani kuna baadhi ya madaraja yanalipiwa kama Golden Gate Bridge lile daraja jekundu la San Fransisco nalo linalipiwa,Kenya tu hapo Nairobi expressway inalipiwa nayo ni ubia na wawekezaji binafsi

Mimi nadhani sio mbaya kuhusisha private sector zijihusishe kwenye ujenzi na maendeleo ya muundombinu maana hii pia inachangia sustainability ya private sector hasa hii mifuki ya kijamii inakuwa na hela inayozunguka baada ya kukaa nazo kuzikumbatia
 
binafsi sioni tatizo la kuchaji kutumia daraja hata kama siyo kulipia deni, msisahau kuna repair na matengenezo ya daraja pia na hiyo yote in gharama kubwa ila tatizo ni kwamba ilipaswa kuwe na uwazi hiyo pesa inakokwenda na jinsi inavyotumika kuwe na auditing kama inatumika kutunza miundo mbinu ya daraja kwangu ni sawa ila kama inakwenda mifukoni mwa irani ambapo uwezekano upo basi hapo siyo sawa …
wanafanya repair kwanini hatuoni daraja lingine likijengwa kwa faida ya hii draja kuna lile daraja la kuunganisha tanga na bagamoyo mpaka leo tupo kwenye upembuzi yakinifu
 
Sasa distance ya kilometer almost 400 utalinganisha na km za lile daraja la Nyerere?

Congo hakuna miundombinu ya kutosha hivyo kuacha wawekezaji wajenge na kutoza ni sawa tu maana itasaidia barabara kujengwa kwa kasi bila input ya serikali. Sasa hapa Tanzania ambapo tuna barabara, madaraja na flyover kibao kuna haja gani ya kutoza miaka 30?

Billion 300 si ingelipwa kwa bajeti za miaka 10, mbona tunatenga 1 Trillion ya safari na Matrilion kuandaa AFCON je hiyo 300B ni kitu gani?
Bil 300 ni hela ndogo Sana kwa serikali
 
bwege sana ww mm nimeandika kuhusu Congo ni sehemu ambayo naijua tangu nipo kijana mpk sasa namiliki malori yangu na yanaenda huko always,Ww upuuzi wako wa kutoelewa kilichoandikwa utajua mwenyewe na ufurambute wako huko ulipo usifikiri watu tunaongea hili kufurahisha genge,bahat nzuri hapa nilipo nina risiti ambayo nimelipia Peage/toll/tozo moja ya Lualaba mwez uliopita nilienda Congo mwenyewe.View attachment 3643229
Rist yako umenikumbusha Neno Korwezi.

Nilisikia kwenye Wimbo Luambo Makiadi

Korwezi baninga kwenye Kibao cha Azda
 
Naona umemuwekea na signature juu 😄

Ova
 
wanafanya repair kwanini hatuoni daraja lingine likijengwa kwa faida ya hii draja kuna lile daraja la kuunganisha tanga na bagamoyo mpaka leo tupo kwenye upembuzi yakinifu
Muwe mnatafuta taarifa sahihi kabla ya kuandika. Hilo daraja liko hatua za mwisho.
 
Kuondoa malipo ni ngumu
Labda kama faida yao imerudi,wangepunguza kidogo tozo tu ya magari kupita hapo

Ova
 
Rist yako umenikumbusha Neno Korwezi.

Nilisikia kwenye Wimbo Luambo Makiadi

Korwezi baninga kwenye Kibao cha Azda
Kolwezi kule DRC ni eneo ambalo ndilo lina Migodi ya hizo shaba migodi mikubwa tu kama Kamoa,Kamoto,TCC,CCR na mingine ipo katika jimbo la Lualaba mbele kidogo ya Lubumbashi,huko ndipo wahuni wa kikongo wanateka roli zima la shaba wanakuja hadi na Crane..Gari zote zinazikuwa zimebeba copper huwa zinapewa escort ya ulinzi wenye bunduki maana mnatekwa mchana kweupe watu wanachukua copper,na mzigo wa tani 30 za copper unafika hadi million 300
 
Back
Top Bottom