HOJA Deni la Daraja la Kigamboni (Mwalimu Nyerere) litaisha lini?

HOJA Deni la Daraja la Kigamboni (Mwalimu Nyerere) litaisha lini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
bwege sana ww mm nimeandika kuhusu Congo ni sehemu ambayo naijua tangu nipo kijana mpk sasa namiliki malori yangu na yanaenda huko always,Ww upuuzi wako wa kutoelewa kilichoandikwa utajua mwenyewe na ufurambute wako huko ulipo usifikiri watu tunaongea hili kufurahisha genge,bahat nzuri hapa nilipo nina risiti ambayo nimelipia Peage/toll/tozo moja ya Lualaba mwez uliopita nilienda Congo mwenyewe.View attachment 3643229
Nimepitia upya comment yako na nimeielewa. Ila mimi sio bwege, bwege mwenyewe.
 
Nimepitia upya comment yako na nimeielewa. Ila mimi sio bwege, bwege mwenyewe.
Poa ila nakushauri next time kuwa makini usikurupuke kushambulia mtu bila kuwa na uhakika..kumuita mwanaume mwenzio muongo ni matusi makubwa sana binafsi sipendi..Nina miaka zaidi ya 11 humu niliyojijengea ya kutokuwa mzee wa fiksi na chai,sasa kuniita muongo ni dharau kubwa sana kwangu
 
Hadi Julai 2024, katika miaka tisa ya uendeshaji, Tsh. Bilioni 102.18 zimekusanywa kupitia tozo mbalimbali." Pia alieleza kuwa, kwa mujibu wa upembuzi yakinifu, mradi unatarajiwa kurejesha Tsh. Bilioni 334 ndani ya kipindi cha miaka 30 kabla ya kukabidhiwa Serikalini.
Kwa miaka 9. Kwa hii hela.
Ni sawa na 31 Mill kila siku.

Nadhan ni fair enough. Nadhan hakuna ubadhilifu.

swali.
Je Miaka hiyo? .Serikali ya CCM haikuwa na Ilani ya Kujenga hili daraja la Kigamboni?.
au Ilan ilisema itaomba hela NSSF?.

Daraja la Kigongo - Busisi limegharimu 718 Billion.
Je wananchi wanatozwa tozo?.

Hapana . Hakuna Tozo.
 
Hata hivyo hiyo pesa ndogo Kwa sababu nssf ilikuwa inaingiza billion 120 Kwa mwezi ilifikia muda ilikuwa inaidai serikali trillion 6
 
Poa ila nakushauri next time kuwa makini usikurupuke kushambulia mtu bila kuwa na uhakika..kumuita mwanaume mwenzio muongo ni matusi makubwa sana binafsi sipendi..Nina miaka zaidi ya 11 humu niliyojijengea ya kutokuwa mzee wa fiksi na chai,sasa kuniita muongo ni dharau kubwa sana kwangu
Mkuu msamehe huyo Blank page 😁😁

Salute sana kwa kuleta true story which contains inspirations 🙏🫡🫡🫡
 
Kama Zembwela alivyosema ,Mbuzi wa bwana kheri na Shamba la Bwana Kheri hivyo yote KHERI.

Usitegemee waje waseme IMETOSHA Deni lishaisha maana anayekamuliwa ni THIRD PARTY hana visibility yeyote.

Nilitarajia kwamba sirikali haikusanyi faida means pesa yote inayokusanywa iende moja kwa moja kulipa Deni la NSSF na staffs wanaofanya kazi hapo watoke NSSF.
 
Billion 300 si ingelipwa kwa bajeti za miaka 10, mbona tunatenga 1 Trillion ya safari na Matrilion kuandaa AFCON je hiyo 300B ni kitu gani?
Naungana na wewe mkuu.
Serikali inunue mkataba wa ujenzi ili daraja litumike bure kama ilivyo kwa madaraja na miundombinu mingine.
Uwezo huo tunao hasa kutokana matumizi yasiyo ya lazima ambayo serikali imejibbesha na kuacha mambo ya msingi kama daraja la Nyerere.
 
binafsi sioni tatizo la kuchaji kutumia daraja hata kama siyo kulipia deni, msisahau kuna repair na matengenezo ya daraja pia na hiyo yote in gharama kubwa ila tatizo ni kwamba ilipaswa kuwe na uwazi hiyo pesa inakokwenda na jinsi inavyotumika kuwe na auditing kama inatumika kutunza miundo mbinu ya daraja kwangu ni sawa ila kama inakwenda mifukoni mwa irani ambapo uwezekano upo basi hapo siyo sawa …
Sio sawa
 
Nimeona hawa watangazaji wa Wasafi wakigusia kuhusu Daraja la Mwalimu Nyerere na kuhoji deni la ujenzi litaisha lini, kwa maana ya tozo zinazokusanywa kila siku, sasa ni lini deni la ujenzi wa daraja hilo litakuwa limekwisha.


Kwanza tufahamu kuwa Daraja la Kigamboni halikujengwa kwa mkopo wa kawaida wa serikali. Badala yake, lilijengwa kupitia mkataba wa aina ya DBFOT (Design, Build, Finance, Operate and Transfer). Chini ya mfumo huu, mwekezaji hubuni mradi, huujenga, hufadhili gharama za ujenzi, huendesha mradi na hukusanya mapato kwa kipindi kilichokubaliwa kabla ya kuukabidhi kwa serikali.

Soma: Tozo kwenye daraja la Nyerere Kigamboni zashushwa kwa bodaboda na bajaji. Bodaboda sasa kuvuka ni Tsh 300

Katika mradi huu, Serikali ya Tanzania ilichangia takribani asilimia 40 ya gharama za ujenzi, huku NSSF ikichangia takribani asilimia 60. Kutokana na uwekezaji huo, daraja liliwekwa mfumo wa tozo (toll) ili NSSF irejeshe fedha ilizowekeza pamoja na gharama za uendeshaji na matengenezo.

Kwa mujibu wa makubaliano ya mradi, kipindi cha ukusanyaji wa tozo ni miaka 30 tangu daraja lianze kutumika. Kwa kuwa daraja lilifunguliwa mwaka 2016, kipindi hicho kinatarajiwa kuendelea hadi takribani mwaka 2046, isipokuwa makubaliano hayo yabadilishwe rasmi.


Tozo zinazolipwa hutegemea aina ya chombo cha usafiri:

Pikipiki:
Kuanzia Tsh. 300/-
Bajaji: Kuanzia Tsh. 5,00/-
Gari dogo binafsi: Tsh. 1,500 kwa safari moja.
Mabasi, Malori na magari makubwa: Hutozwa viwango vya juu zaidi kulingana na aina na uzito wa gari.

Pia kuna mfumo wa bando (bundle passes) kwa watumiaji wa mara kwa mara ambao hupunguza gharama kwa kila safari.

Ni muhimu kufahamu kuwa fedha zinazokusanywa si ulipaji wa “deni la taifa” kwa maana ya mkopo wa kawaida, bali ni urejeshaji wa uwekezaji wa NSSF chini ya makubaliano ya mradi. Hadi sasa, hakuna tangazo rasmi la kubadilisha kipindi cha miaka 30 au kutangaza tarehe tofauti ya kusitisha tozo.

Gharama za Mradi wa Daraja la Kigamboni (Daraja la Mwalimu Nyerere)

Kwa mujibu wa taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), gharama ya awali ya mradi wa Daraja la Kigamboni pamoja na barabara zake za kuunganisha, kama ilivyoainishwa kwenye Mkataba wa Ufadhili wa mwaka 2014, ilikuwa Dola Milioni 143.50, sawa na takribani Tsh. Bilioni 238.71 kwa thamani ya fedha wakati huo. Gharama hiyo baadaye ilirekebishwa mwaka 2016 na kufikia takribani Tsh. Bilioni 328.90.


Mgawanyo wa Gharama

Kwa kuwa mradi ulitekelezwa kwa mfumo wa ubia kati ya NSSF na Serikali, mgawanyo ulikuwa:

NSSF – asilimia 60
Serikali ya Tanzania – asilimia 40

Gharama ya Awali USD milioni 143.50 (takriban TZS bilioni 238.71)
Gharama Iliyorekebishwa (2016) Takriban TZS bilioni 328.90

Hoja ya Malipo ya Serikali kwa NSSF

Ripoti ya CAG ilieleza kuwa kutokana na uwezo mdogo wa kifedha wa Serikali wakati wa utekelezaji, NSSF ilifadhili gharama yote ya mradi kwa wakati huo, na Serikali ilikubali kuirejeshea NSSF sehemu yake ya mchango pamoja na gharama zinazohusiana na kuchelewa kwa malipo (riba).

Ripoti ya CAG 2019/20 (Ukurasa wa 147):

CAG alieleza kuwa licha ya kuwepo kwa Finance Agreement, Mkataba wa Uendeshaji (Concession Agreement) uliotakiwa kusainiwa kati ya Wizara ya Ujenzi na NSSF ulikuwa haujasainiwa, jambo lililoibua hoja kuhusu uhalali wa uendeshaji wa daraja na ukusanyaji wa tozo.


Mradi huu ni mfano wa ubia kati ya Serikali na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). Kwa kuwa daraja lilifunguliwa mwaka 2016, kipindi cha miaka 30 cha uendeshaji wa NSSF kinatarajiwa kufikia karibu mwaka 2046.

Aliyekuwa Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Patrobas Katambi, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kigamboni, Dkt. Faustine Ndugulile, bungeni Agosti 27, 2024.

Alisema:

"Hadi Julai 2024, katika miaka tisa ya uendeshaji, Tsh. Bilioni 102.18 zimekusanywa kupitia tozo mbalimbali." Pia alieleza kuwa, kwa mujibu wa upembuzi yakinifu, mradi unatarajiwahii nchi ina mambo ya kikwuma dana kurejesha Tsh. Bilioni 334 ndani ya kipindi cha miaka 30 kabla ya kukabidhiwa Serikalini.

Hata hivyo, kuondolewa au kusitishwa rasmi kwa tozo kutaamuliwa kulingana na masharti ya mikataba, urejeshaji wa gharama, na maamuzi ya kiserikali.
Hii nchi ina mambo ya kikwuma sana.
 
bwege sana ww mm nimeandika kuhusu Congo ni sehemu ambayo naijua tangu nipo kijana mpk sasa namiliki malori yangu na yanaenda huko always,Ww upuuzi wako wa kutoelewa kilichoandikwa utajua mwenyewe na ufurambute wako huko ulipo usifikiri watu tunaongea hili kufurahisha genge,bahat nzuri hapa nilipo nina risiti ambayo nimelipia Peage/toll/tozo moja ya Lualaba mwez uliopita nilienda Congo mwenyewe.View attachment 3643229
Heshima yako mkuu.
 
Back
Top Bottom