DENI LA TAIFA: Benki ya dunia yaitahadharisha Tanzania

DENI LA TAIFA: Benki ya dunia yaitahadharisha Tanzania

Nanukuu:

Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip mpango ametangaza kuwa deni la serikali limeongezeka kwa zaidi ya Trilioni moja.

"Deni la serikali limeongezeka na kufikia Sh.Trillioni 51.03 kutoka shilingi Trilioni 49.86 ya mwaka 2018 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 2.35". Alisema leo bungeni.


Mimi kama mwananchi wa kawaida naomba sana raisi atakayechaguliwa adili na vipaombele vya miaka 5 yaani 2020-2025 tusichoshane kutengeneza vitu vya vizazi vijavyo wakati tuliokupigia kura tunateseka tu mtaani katika vitunavyoona ni UPUUZI NA HAVINA MANUFAA KWA WAKATI TULIOPO NI MIRADI YA UJENZI KUWA MINGI KULIKO SEKTA YA KILIMO UVUVI NA HOSPITALI bado sana havijafikia kiwango kizuri hivyo basi wakati ujao tujaribu kuangalia na huku ..DENI NI KUBWA SANA maisha ni magumu kwa mtu mmoja mmoja😊😎
 
Asante mleta mada. Nipo napitia nukta kwa nukta hapa nije na maswali magumu kwa hii serikali ya......
 
Naona racist wamejaa kwenye hii thread hahaha, hamtaki tuambiwe ukweli kua tupunguze kukopa?
Kukopa tunakopa sana tu, japo tuna uafadhali kuliko mataifa mengi, ila still tunakopa na kukopa lazima ulipe. Hata marekani wana madeni kibao toka China, ila wanaweza pigana, sisi tuna uwezo huo?
 
Tuna Chato International Airport hata kama haikuwahi kuwa kwenye mpango wa Taifa wa maendeleo wa miaka mitano we don’t care
haha wenyewe (wenye nchi) wanakwambia chato ipo tanzania...kwahiyo freshi tuu
 
Reli ilikuwa na ulazima gani?

Tanzania ambayo hata viwanda vya nguo vilivyopo ni kichekesho

Barabara za lami zilitosha kabisa kuhudumia viwanda

Reli ilikuwepo tangia mjerumani anatawala nchi hii, iletwe assessment impact/mchango wa reli Ktk kupanuka kwa sekta viwanda

Leo hii miaka 50 baada ya Uhuru barabara bado ni kero kubwa maeneo ya interior za wilaya ni vumbi mtupu, miji yetu nayo imejaa barabara za vumbi

Angekopa hizo trillion 16 akajenga hata Magereza ili kupunguza misongamano Magerezani ningemuelewa
mkuu...kati ya reli na magereza wewe unaona magereza ni bora?? hii nchi ngumu aisee..
 
Tatizo sio kukopa tu. Ni aina ya mkopo na matumizi ya mukopo yenyewe. Mikopo ya mashirika makubwa inakuwa na riba ndogo. Mikopo kutoka benki za biashara ina riba mara mbili au hata tatu ya riba kutoka mashirika makubwa yanayotoa mikopo. CAG alinukuliwa akisema tatizo halipo kwenye kiwango cha mkopo bali ni kwa sababu mikopo yetu mingi ni ya kutoka kwenye mabenki ya biashara. Hapa tulipofika, tunatumia nusu au zaidi kidogo ya makusanyo yetu yote kulipa tu deni na riba yake. Na kwa vile hii mikopo inatumika kwenye miradi ambayo haitaanza kuzaa faida mpaka baada ya miaka kadhaa, pesa ambazo zingeingia mitaani "zizunguke" zinatumika kulipa hiyo mikopo na riba. Matokeo yake mzunguko wa fedha ni mdogo, na maisha yanakuwa magumu zaidi. Tena kilimo hakitengewi bajeti kubwa kwa vile pesa zinalipa madeni. Ndio maana japo uchumi unapanda, unapata tu kwenye kipato cha makampuni machache makubwa lakini kipato cha watu vijijini kinapungua. Itatubidi tusubiri mpaka hiyo miradi inayofanyiwa uwekezaji sasa ianze kulipa ndipo ugumu wa maisha utakapopungua. Tuendelee tu kumwomba Mungu.
 
Benki ya dunia imeitahadharisha Serikali ya Tanzania juu ya ukubwa wa deni lake lililofikia trillion 47+ kwa rekodi mpaka mwezi Mei mwaka huu.

Imetaja japo deni bado ni himilivu lakini Tanzania lazima iwe makini maana linaelekea kutokuhimilika

Chanzo: Mwananchi

====

Licha ya Serikali kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo inayotarajia kuboresha masisha ya wananchi, Benki ya Dunia imetahadharisha kuhusu ukopaji unaofanywa na Serikali.

Ingawa deni hilo bado ni himilivu, benki hiyo inasema umakini unahitajika kabla hali haijawa ngumu kwa Serikali kushindwa kutekeleza makubaliano.

Kwa sasa, taarifa ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inaonyesha deni la nje linalohusisha lile la umma na sekta binafsi lilikuwa Dola 21.6 bilioni (takriban Sh49 trilioni) na la ndani ni Sh15.5 trilioni. Takwimu hizo ni mpaka Mei mwaka huu.

Hata hivyo, Benki ya Dunia inasema uwiano wa deni la Taifa na pato la taifa (GDP) kwa mwaka 2018 ulikuwa asilimia 40.1 zikiongezeka kutoka asilimia 37 za mwaka uliotangulia. Pamoja na ukweli huo, uwiano huo ni chini ya ukomo wa asilimia 70 unaopendekezwa kimataifa.

“Ingawa deni ni himilivu lakini ongezeko la mikopo ya kibiashara kutoka benki linapaswa kutazamwa kwa umakini,” inasomeka sehemu ya ripoti ya benki hiyo.

Hivi karibuni, Benki ya Dunia imeindua ripoti ya 12 ya hali ya uchumi Tanzania iliyoangazia umuhimu wa rasilimaliwatu katika kukuza utajiri ambayo pamoja na mambo mengine imetoa ushauri wa namna ya kuboresha ukuzaji uchumi na maisha ya wananchi.

Mwaka 2010/11 ripoti hiyo inasema mikopo kutoka benki za biashara ilikuwa asilimia nne tu ya deni zima lakini imeongezeka mpaka asilimia 30 mwaka 2016/17 hivyo kuipa Serikali gharama kubwa za marejesho.

Kutokana na ongezeko hilo, ripoti inasema Tanzania inatumia asilimia 43 ya mapato yake ya ndani kulipa deni la Taifa ingawa ulipaji wa deni la ndani umekuwa mdogo.

“Mei 2018 Serikali ilianzisha uhakiki wa madeni ya wakanadarasi na wazabuni ili kuharakisha ulipaji na Sh1 trilioni zilitengwa kwa ajili hiyo kwenye bajeti ya mwaka 2018/19 lakini kwenye nusu ya kwanza ya mwaka huo ni Sh322 bilioni pekee zilikuwa zimelipwa,” inasema ripoti hiyo.

Uuzaji nje

Kutokana na bei ndogo iliyopendekezwa na wanunuzi, Serikali ilizuia uuzaji wa korosho kwa kampuni zilizojitokeza mwaka jana na ikaamua kuzinunua yenyewe. Jeshi la wananchi lilihusishwa kwenye mchakato huo.

Kiasi kikubwa cha zaidi ya tani 200,000 za korosho zilizonunuliwa na Serikali hakikuuzwa nje ya nchi hivyo kushusha mapato ya fedha za kigeni kwa asilimia 3.9 kutokana na mapato ya zao hilo kushuka kutoka Dola 529.6 milioni hadi Dola 196.5 milioni.

Wakati uuzaji nje ukipungua kwa kiasi hicho, ununuaji uliongezeka kwa asilimia 7.8 kutoka Dola 2.7 bilioni hadi Dola 3.2 bilioni kulikochangiwa na ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) na upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam.

“Hata hiyo, mapato yatokanayo na huduma hasa utalii yalifika Dola 189 milioni yakilinganishwa na malipo yaliyofanywa nje, Dola 56 milioni. Mapato hayo yalichangiwa na ongezeko la watalii na usafirishaji wa bidha kwenye nchi jirani,’ inasema ripoti hiyo.

Kushuka kwa akiba ya fedha za kigeni kumechangiwa na kupungua kwa uuzaji wa mauzo nje ya nchi kulikosababishwa na kutouzwa kwa korosho (page 20).

Utajiri wa wananchi umeshuka kutoka Dola 20,900 mwaka 1995 hadi Dola 17,451 mwaka 2014. (page 43).

Changamoto ya kwanza inayoifanya Tanzania ishindwe kukabiliana na umasikini hivyo kuboresha maisha ya wananchi wake ni kasi kubwa ya kuzaliana. Ongezeko la watu nchini ni asilimia 3.1 kwa mwaka, kiwango cha juu ikilinganishwa na asilimia 2.7 kwa nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara.

Kupunguza idadi ya watoto kwa kila mwanamke, kuimarisha elimu kwa mabinti, kupunguza ndoa na mimba za utotoni na kuongeza ushiriki wa wanawake kwenye shughuli za uchumi ni miongoni mwa njia za kukabili changamoto hiyo.

Udumavu na umasikini

Ingawa utajiri wa Tanzania umeongezeka kwa zaidi ya asilimia 45 kwa miongo miwili iliyopita, kasi kubwa ya ongezeko la watu imeshusha utajiri wa kila mwananchi kwa Dola 3,500.

Mwaka 2014 utajiri wa Tanzania unaojumuisha thamani ya rasilimali zote ilizonazoukitoa madeni ulikuwa Dola 904.33 bilioni ukilinganishwa na Dola 624.99 bilioni mwaka 1995. Lakini, utajiri wa kila raia ulipungua kutoka Dola 20,900 mwaka 1995 hadi Dola 17,451 mwaka 2014.

Licha ya kupungua kwa utajiri wa kila mwananchi, idadi ya masikini imeongezeka pia kutoka milioni 12.3 waliokuwepo mwaka 2012 hadi milioni 13.3 mwaka 2016. Ndani ya miaka minne, masikini milioni moja wameongezeka.

Mtafiti na mchumi mwandamizi, Profesa Samwel Wangwe anasema hiyo inaweza kuwa imechangiwa na ukuaji mkubwa wa sekta zisizoajiri watu wengi zaidi.

“Watanzania wengi ni wakulima au wafanyabiashara wadogo. Tunahitaji mipango itakayowainua waliopo kwenye maeneo hayo ili kuufanya uchumi wetu uwe jumuishi,” anasema Profesa Wangwe.

Kuhusu ongezeko kubwa la watu, naibu waziri wa afya, Dk Fustine Ndugulile anasema kunachangiwa na mambo mengi ikiwamo jitihada za Serikali kuboresha huduma za afya hasa chanjo kwa watoto.

“Hata hivyo, udhaifu wa sheria na ukosefu wa elimu ni chanzo cha ndoa na mimba nyingi za utotoni,’ anasema Dk Ndugulile.

Mkurugenzi mkazi wa Benki ya Dunia nchini, Bella Bird anasema wananchi wanahitaji kuelimishwa ili kukabiliana na changamoto zilizopo. Elimu, anasema itawasaidia kuboresha maisha, kukuza kipato na kuwa na uzazi unaohimilika.

“Elimu ya mama ni muhimu kwa maendeleo ya baadaye ya mtoto kielimu na kiuchumi. Watoto milioni tatu chini ya miaka mitano nchini wana udumavu. Msichana mmoja katika kila watatu anaolewa akiwa na chini ya miaka 18 na mmoja katika kila wanne anazaa akiwa chini ya umri huo,” anasema Bella.

Chanzo: Mwananchi
Safi. Tupunguze Sana matumizi ya kujenga mabarabara, shule, Maji, nk. Tulipane tu mishahara na kulipa madeni tuliyokupo zamani. Kama Alivyofanya Rais Mkapa 1995/2000 ndipo tuaze kujenga na kununua Trein na ndege. Mabarabara na maji Kama tunaogopa madeni ya taifa
 
Nanukuu:

Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip mpango ametangaza kuwa deni la serikali limeongezeka kwa zaidi ya Trilioni moja.

"Deni la serikali limeongezeka na kufikia Sh.Trillioni 51.03 kutoka shilingi Trilioni 49.86 ya mwaka 2018 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 2.35". Alisema leo bungeni.


Mimi kama mwananchi wa kawaida naomba sana raisi atakayechaguliwa adili na vipaombele vya miaka 5 yaani 2020-2025 tusichoshane kutengeneza vitu vya vizazi vijavyo wakati tuliokupigia kura tunateseka tu mtaani katika vitunavyoona ni UPUUZI NA HAVINA MANUFAA KWA WAKATI TULIOPO NI MIRADI YA UJENZI KUWA MINGI KULIKO SEKTA YA KILIMO UVUVI NA HOSPITALI bado sana havijafikia kiwango kizuri hivyo basi wakati ujao tujaribu kuangalia na huku ..DENI NI KUBWA SANA maisha ni magumu kwa mtu mmoja mmoja😊😎
Mkuu kwa ubinafsi huo ndiyo maana leo tupo hapa, sisi watu weusi tuna ubinafsi sana na tutachelewa miaka yote.

Mtu aanze kudili na vitu vya leo halafu wajukuu zako wakija watakua wanalia hivihivi kama tunavolia sisi.

Tatizo ni kwamba tunataka maisha ya wenzetu ambao mababu zao waliteseka kwaajili yao, tunatakiwa tupambane kwaajili ya vizazi vijavyo ili nao hapo baadae wasijekulia kama tunavolia sisi.

Mkuu unafikiri wale mababu zao akina David Livingstone wangekubali kuja huku kwetu kutafuta maisha ya taabu huku wakipatwa na maradhi mpaka wanakufa hukuhuku Africa kwa mawazo yako walikua wajinga?

Walikua wanapambana ili vizazi vya baadae visipate shida.
 
mkuu...kati ya reli na magereza wewe unaona magereza ni bora?? hii nchi ngumu aisee..


Mkuu watuhumiwa/mahabusu wamerundikwa huko Magereza, mi nilisuggest tu maana options zipo nyingi

Hiyo trillion 16 ingewekezwa kujenga barabaraza lami, vyuo vya beta na vyuo vikuu na sio reli

Sekta ya viwanda nchini kwetu sio kubwa sana kiasi cha kufanya tujenge reli ya gharama ambazo ni sawa na makusanyo ya Kodi ya mwaka mzima ya Central government


Kujenga barabara za lami tulikuwa tunapiga ndege wawili kwa Jiwe moja, maana wakulima na wenye viwanda barabara za lami zingewaservice vizuri tu
 
Kwa hela zetu za ndani!.....hahaha[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
IMG_20200708_164946.jpg
 
Back
Top Bottom