Deni la Taifa in and out, kinachoumiza sio kukopa ni matumizi ya kinachokopwa

Confirm tu mkuu.. ila itakuwa kwenye 140 Trillioni..
Ninachojua GDP yetu iko around 140T kama ulivyosema.

Kwa gdp hii uchumi wetu unasupport repayment ya deni? Tumeambiwa deni liko ndani ya viwango himilivu vya ulipaji.

Kama ni hivyo hoja ingekuwa mikopo inaenda kutumika kwenye miradi iliyokusudiwa ipasavyo?

Na usimamizi ni mzuri kiasi kwamba tunapata value for money? Na miundombinu inayosimikwa inafungua nchi kwa uzalishaji zaidi?



Sent using Jamii Forums mobile app
 
K
Kwel kabisa 💯
 
Umezunguka saana umeogopa kusema GDP ni ngapi ili ilinganishwe na 70T..
Confirm tu mkuu.. ila itakuwa kwenye 140 Trillioni..
Kwa lugha ya kiuchumi na kwa kuangalia ratios kwamba deni letu ni pungufu ya 50% kesho Mwigulu atakuambia deni ni stahimilivu kwa sababu tu definition ya ustahimilivu wa deni kwa world bank wanasema at least 65% ya deni to gdp ni stahimilivu.

Ila tukirudi kwenye uhalisia haswa, na ukiangalia matumizi ya haya madeni.. utagundua ya kwamba deni sio stahimilivu kwa sababu mikopo imewekeza kwenye projects ambazo hazikuzi uchumi na kuongeza tax base na revenues ambayo ndio italipa madeni.

Pia mikopo yetu na matumizi yake imeshindwa kuvutia FDI ambayo itakupa fedha za kigeni ili ulipe hiyo mikopo..

So technically, ndo mana mimi binafsi naamini Tanzania ipo kwenye valley of death.. and its a matter of time..

Hili bomu lazima lilipuke tu
 
Ukiona nadharia zimekuwa nyingi ujue kuna tatizo lazima...

Na kukimbia tatizo, hilo pia ni tatizo
 
Kwenye mambo ya uwekezaji kuna msemo huwa tunasema 'Market can remain irrational, for longer than you can stay solvent'

Unasema market itakuwa nzuri faida itapatikana.. je una uhakika gani kwamba by that time bado tutakuwa solvent?

Tafsiri ya ulichosema ni kwamba tutegemee speculation kwamba mambo yanaweza kuwa mazuri uko mbeleni.

Kwamba labda mji wa Chato utakuwa mkubwa watalii watamiminika, Uwanja wa chato utakuwa na economic benefit..

Hizo ni speculation ambazo hazipo supported na fundamentals zozote ndo mana huwa haishauriwi kufanya speculative decisions
 
Ni kwamba Deni letu hadi sasa ukiliangalia kwa takwimu za kiuchumi na sio kisiasa bado ni himilivu sana?.

Ukiangalia uwiano wa deni kwa pato la taifa kwa maana ya ratio of debt to GDP kama haijazidi 60% inamaana nchi ipo vizuri?.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Taifa linaanzisha mradi ambao haliwezi gharamia ata kwa asilimia 10, then mkopaji unakua endelevu kila uchwao. Kazi kweli kweli
 
Labda kama watu wanakuwa na wasiwasi wa je fedha tunayokopa inatumika kwa malengo tarajiwa na inatumika vizuri?

Kwenye uchumi we go with numbers not words ndio tofauti yake. Na hiyo setup ya world bank ndio inatumiwa na wachumi wote.

Unless tuseme hatuna uwezo wa kuli service hilo deni. Mbona marekani deni lao limeshavuka 100% na wanajiona wapo sawa tu kwasababu uwezo wa kuli service deni wanao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi naomba tu unifafanulie ikiwa tutashindwa kabisa kulipa deni nini kitatokea, kuna kitu napanga kufanya. Sijawahi kusikia nchi yoyote imekabidhiwa kwa madalali ipigwe mnada toka nizaliwe
 
Kuhusu mikopo ni muhimu kuzingatia masharti ya mkopo kuepuka masharti magumu mfano kiwango kikubwa cha riba na muda mfupi wa kurudisha deni .

Kuhusu ela ya tozo za Kwenye matumizi ya simu na miamala tungeomba nayo itangazwe na kuonyeshwa inavyotumika kama ilivyofanyika ela ya WB .
 
Hongera Mkuu kwa kudadavua na kufanya uelewa uwe mwepesi hadi mwenye elimu ya darasa la 7 aweze kuelewa
 
Kwenye page za TAMISEMI naona huwa wana toa takwimu
 
Hivi uwanja wa ndege Chato uligharimu shilingi bilioni ngapi maana ndiyo imekuwa kisingizio kutwa kucha
 
Mi naomba tu unifafanulie ikiwa tutashindwa kabisa kulipa deni nini kitatokea, kuna kitu napanga kufanya. Sijawahi kusikia nchi yoyote imekabidhiwa kwa madalali ipigwe mnada toka nizaliwe
Mkuu swali zuri.. actually madhara ya kushindwa kulipa deni yatachofanya ni kwamba, nchi itakuwa down graded na wakopeshaji.

Na ukiwa downgraded maana yake huwezi kukopesheka tena.

Lakini impact kubwa huwa inakuwa ni trickle down effect ya kitachotokea baada ya kushindwa kulipa madeni.

1. Wawekezeji watakimbia maana macro fundamentals zita deteriorate.

2. Mfumuko wa bei

3. Pesa itashuka thamani kwa kasi..

4. Nchi inaweza kushindwa kumudu baadhi ya matumizi ya muhimu kabisa..

Yaani ikitokea, impact yake itakuwa ni mambo mengi magumu yatatuandama sana kwenye uchumi
 
Statistically kwa sababu deni letu bado lipo bekow 65% of Gdp hiyo ni stahimilivu ila inapokuja uwezo wa kuli service deni sio stahimilivu..

Na hatuwez kujifananisha na America kwa sababu hata ukiangalia tax revenue to gdp ya Tanzania ipo chini ya asilimia 20% wakati kwa America Tax to Gdp ipo above 40%..

Kwahiyo hapo Debt to Gdp ya America inaweza kuwaruhusu hata kuwa 100% na wakawa stahimilivu... ila kwa Tanzania hata hii around 50% inaweza kuwa sio stahimilivu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…