Mkuu
Naantombe Mushi nina swali kidogo.
Kuna ubaya kukopa kwa ajili ya miradi ambayo haitoi "returns" za moja kwa moja kulipa deni husika na kulipa deni hilo kwa kutumia miradi mingine inayozalisha fedha ?
Nitatoa mfano.
Unakopa fedha kwa ajili ya miradi ya elimu, halafu fedha yako ambayo ulitakiwa kupeleka kwenye elimu, unaendeleza mradi wa mabasi ya mwendokasi, ili mradi huo (wa mwendokasi) ulipe "deni la elimu" ?
Hii kiuchumi imekaaje mkuu ?
Maana kwa mtazamo wangu naona miradi mingi inayogusa "wanyonge moja kwa moja" kama vile elimu, afya, maji, n.k "financial returns" zake ni "too slow" lakini miradi hii ni "very good agenda" za kuombea mikopo.