Deni la Taifa in and out, kinachoumiza sio kukopa ni matumizi ya kinachokopwa

Deni la Taifa in and out, kinachoumiza sio kukopa ni matumizi ya kinachokopwa

Confirm tu mkuu.. ila itakuwa kwenye 140 Trillioni..

Kwa lugha ya kiuchumi na kwa kuangalia ratios kwamba deni letu ni pungufu ya 50% kesho Mwigulu atakuambia deni ni stahimilivu kwa sababu tu definition ya ustahimilivu wa deni kwa world bank wanasema at least 65% ya deni to gdp ni stahimilivu.

Ila tukirudi kwenye uhalisia haswa, na ukiangalia matumizi ya haya madeni.. utagundua ya kwamba deni sio stahimilivu kwa sababu mikopo imewekeza kwenye projects ambazo hazikuzi uchumi na kuongeza tax base na revenues ambayo ndio italipa madeni.

Pia mikopo yetu na matumizi yake imeshindwa kuvutia FDI ambayo itakupa fedha za kigeni ili ulipe hiyo mikopo..

So technically, ndo mana mimi binafsi naamini Tanzania ipo kwenye valley of death.. and its a matter of time..

Hili bomu lazima lilipuke tu
Sasa unatakaje ili hali miradi ilishaanzishwa na sasa ipo katikati?.Tukope tuikamilishe au tuache kukopa miradi hiyo ife?.
 
Ndugai kahoji tozo za miamala ya simu tulisema zitatumika kujenga shule. Iweje tena shule zimekopewa pesa aya madeni yatakua mzigo kwa taifa ili.

Majibu aliyokuja pewa ni muunganiki wa sgr, bwawa la nyerere
Kwa sababu muhuni wenu wa kaburini alikopa akayaanzisha mamiradi na kuyaacha katikati.Sasa mnataka mama asikope kuyakamilisha ili mpate sababu ya kupigia.
Sasa mama anajua janja yenu na lazima akope miradi hiyo iishe.
 
Deni la taifa ni pesa ndogo sana ukilinganisha na thamani ya madini yote yaliyopo wilaya moja tu ya TANZANIA yanalipa deni lote
 
Ndugai ana point mkuu... kunahitajika mjadala wa kitaifa kuhusu hii mikopo, matumizi yake, riba n.k

Yaani anayeponda hoja ya Ndugai hana akili.. Deni la taifa ni subject matter ya kila mtanzania
Tuanze na kuufuata ushauri wa Nape juu ya mikopo aliyochukua muhuni wa kaburini.
 
Baada ya tafakari ya muda mrefu sana nimelazimika kuyaelewa maneno ya Spika Job Ndugai. Naungana nae.
Ni wazi kuwa maneno yake yamekuja wakati sahihi. Ameongea kama mwananchi wa kawaida kabisa... Na kwa vile yupo ndani ndani huko kuna mengi anayajua!
Cha ajabu sisi wananchi wa kawaida ndo wale wale tunaompiga vita na kumkashifu...
Badala ya kuwa upande wa wapiga makofi na waimba sifa Tulipaswa tuwe na harakati huru na endelevu za kutaka kujua matumizi ya fedha za mikopo na zile za tozo! Isije ikawa tunatumika kama dhamana ya mikopo ili wateule wachache wazidi kuneemeka.
Dalili za matumizi ya kufuru na anasa zipo wazi kabla hata ya SSH...
Je, hatupaswi kwenda mbali zaidi kuhoji uhalali wa mikopo/tozo na matumizi yake?? Au tukishaambiwa na watawala basi tuufyate zaidi ya maandiko!
Kwa nini usiungane na Nape juu ya kulitaka bunge lipitie matumizi ya mikopo ya awamu ya 5 aliyokopa muhuni yule?
 
Kwa sababu muhuni wenu wa kaburini alikopa akayaanzisha mamiradi na kuyaacha katikati.Sasa mnataka mama asikope kuyakamilisha ili mpate sababu ya kupigia.
Sasa mama anajua janja yenu na lazima akope miradi hiyo iishe.

Sipo hapa kubishana hovyo. Hoja ni ndugai na tozo za simu ayo yako kamueleze mzazi mwenzio
 
Ni kweli Ndugai kipindi cha Magufuli alizingua maana hakukemea hilo,lakini kwa sasa analikemea bado tunamu judge yeye badala ya Ku judge hoja yake.
Watu wamekaa kinafiki kumsifia Mama Samia huku naye anafanya makosa kama yale Yale ya Magufuli,Ndugai yupo sahihi kama badger yetu ni 30T na tunatumia 10 T Ku service mikopo unaona kabisa hapa Hanna future kwa Nchi financially.

Mama anatumia mikopo kujenga madarasa,sasa unajiiliza tozo zilizopihiwa kelele zinafanya kazi gani?? .Mikop inabidi itumike kwenye projects zitakazoongeza tax base,revenue,ajira na FDI na hiyo ujenzi wa madarasa.
 
Umezungumzia kitu sahihi kabisa "Multiplier effect"
Hiyo kitu haifanyi sawa kwa kila mradi, kwa bwawa la umeme yawezatumika. Lakini kwa miradi mingine mmmm..... hujaona watu wanaandika miradi wakionyesha FAIDA TAMU TAMU, lakini ukiingia kwenye uharisia ni majanga. Mfano angalia miradi au mawazo ya biashara yanayoandikwa humu JF kama mradi wa kuku, sijui kilimo cha papai eka kadhaa unapata mamilioni. UHARISIA WAKE NI CHANGAMOTO JAPO YAWEZEKANA KUFIKIA LENGO KWA KUFIKIRIKA.
 
Mkuu umetoa shule ya maana sana, naomba niichukue kama ilivyo na mimi nikawaelimishe kijiweni ninaposhinda, asante sana.
Kama sijaelewa utanisamehe.
Huoni kuwa ameongea kinyume na darasa lake mwenyewe?

Deni la taifa ni 70t, pato la taifa ni 30t(kama bado tunaendelea kukusanya angalau 1.2t kila mwezi + tozo na zinaingia hazina badala ya kwa akina Janu kama mifereji ya kufikisha msooga), hivyo kwa kutumia darasa lake, 70/30 ni himilivu? Rejea 70/145 aliyotumia.
 
Kama sijaelewa utanisamehe.
Huoni kuwa ameongea kinyume na darasa lake mwenyewe?

Deni la taifa ni 70t, pato la taifa ni 30t(kama bado tunaendelea kukusanya angalau 1.2t kila mwezi + tozo na zinaingia hazina badala ya kwa akina Janu kama mifereji ya kufikisha msooga), hivyo kwa kutumia darasa lake, 70/30 ni himilivu? Rejea 70/145 aliyotumia.
Uzuri ni kwamba elimu ya JF haichoshi, ngoja nirudi tena kwenye uzi husika.
 
Mkuu Naantombe Mushi nina swali kidogo.

Kuna ubaya kukopa kwa ajili ya miradi ambayo haitoi "returns" za moja kwa moja kulipa deni husika na kulipa deni hilo kwa kutumia miradi mingine inayozalisha fedha ?

Nitatoa mfano.
Unakopa fedha kwa ajili ya miradi ya elimu, halafu fedha yako ambayo ulitakiwa kupeleka kwenye elimu, unaendeleza mradi wa mabasi ya mwendokasi, ili mradi huo (wa mwendokasi) ulipe "deni la elimu" ?
Hii kiuchumi imekaaje mkuu ?

Maana kwa mtazamo wangu naona miradi mingi inayogusa "wanyonge moja kwa moja" kama vile elimu, afya, maji, n.k "financial returns" zake ni "too slow" lakini miradi hii ni "very good agenda" za kuombea mikopo.
Kukopa sio kubaya mkuu.. sema inatakiwa uhakikishe mkopo unaelekezwa kwenye viable projects.

Na unajua ambacho huwa kinagharimu ni zile projects the likes of Kununua mandege.. hizo tu mi ndo siafiki kama matumizi ya mkopo.

Mara mia ujenge shule maana shule inaongeza ubora wa human capital ya nchi
 
Back
Top Bottom