Deni la Taifa in and out, kinachoumiza sio kukopa ni matumizi ya kinachokopwa

Deni la Taifa in and out, kinachoumiza sio kukopa ni matumizi ya kinachokopwa

Ndugai kahoji tozo za miamala ya simu tulisema zitatumika kujenga shule. Iweje tena shule zimekopewa pesa aya madeni yatakua mzigo kwa taifa ili.

Majibu aliyokuja pewa ni muunganiki wa sgr, bwawa la nyerere
Ndugai ana point mkuu... kunahitajika mjadala wa kitaifa kuhusu hii mikopo, matumizi yake, riba n.k

Yaani anayeponda hoja ya Ndugai hana akili.. Deni la taifa ni subject matter ya kila mtanzania
 
... awamu ya 5 haikuwahi kukopa popote kwa ajili ya kuendeshea iwe shughuli za kiutawala au kimaendeleo maana fedha zilikuwepo tena fedha za ndani! Ghafla deni limefikaje 70 tr/-? Tunaomba majibu ya hili.
Fake news
 
Ndugai ana point mkuu... kunahitajika mjadala wa kitaifa kuhusu hii mikopo, matumizi yake, riba n.k

Yaani anayeponda hoja ya Ndugai hana akili.. Deni la taifa ni subject matter ya kila mtanzania
Mjadala sounds good

Lakini mjadala na nani? Sisi ambao tuko busy na chupa z soda? Simba na yanga? Mariam biriyani na misafara ya walevi wa arusha na moshi?

Don’t forget kwamba wanaojali serious stuff nchini hawazidi 6%

Hata bungeni na serikalini kuna watu wapo tu wanafukuzia pesa za kujenga
 
... awamu ya 5 haikuwahi kukopa popote kwa ajili ya kuendeshea iwe shughuli za kiutawala au kimaendeleo maana fedha zilikuwepo tena fedha za ndani! Ghafla deni limefikaje 70 tr/-? Tunaomba majibu ya hili.
Awamu ta tano imekopa 11 trillion Kwa miAka 4
 
Baada ya tafakari ya muda mrefu sana nimelazimika kuyaelewa maneno ya Spika Job Ndugai. Naungana nae.
Ni wazi kuwa maneno yake yamekuja wakati sahihi. Ameongea kama mwananchi wa kawaida kabisa... Na kwa vile yupo ndani ndani huko kuna mengi anayajua!
Cha ajabu sisi wananchi wa kawaida ndo wale wale tunaompiga vita na kumkashifu...
Badala ya kuwa upande wa wapiga makofi na waimba sifa Tulipaswa tuwe na harakati huru na endelevu za kutaka kujua matumizi ya fedha za mikopo na zile za tozo! Isije ikawa tunatumika kama dhamana ya mikopo ili wateule wachache wazidi kuneemeka.
Dalili za matumizi ya kufuru na anasa zipo wazi kabla hata ya SSH...
Je, hatupaswi kwenda mbali zaidi kuhoji uhalali wa mikopo/tozo na matumizi yake?? Au tukishaambiwa na watawala basi tuufyate zaidi ya maandiko!
 
Swali sio kutumia fedha za mikopo kujenga hayo sijui madude dude.. mauwanja etc.

Swali ni je, unawekeza kwenye economic viable projects?

Mfano labda kujenga bwawa la kufua umeme na SGR are these really economic viable projects?..

Maana yake ikiwa dunia inaelekea kwenye global warming, ukitokea ukame na maji yakiwa kidogo, maana yake hilo bwawa la umeme ni mimba..

So utakuwa unalipa mkopo wa watu halafu bado unabaki na mashida ya umeme..

Na vipi kama maji yasipo kauka?
 
Kuhusu mikopo ni muhimu kuzingatia masharti ya mkopo kuepuka masharti magumu mfano kiwango kikubwa cha riba na muda mfupi wa kurudisha deni .

Kuhusu ela ya tozo za Kwenye matumizi ya simu na miamala tungeomba nayo itangazwe na kuonyeshwa inavyotumika kama ilivyofanyika ela ya WB .

Hii nchi tatizo ni Wizi na uroho mkuu! Hawa viongozi ni wezi mbwa...!!! Unaweza kujiuliza kama ndo tulipo fikia nini kifanyike..... na wengi humu tunasema himilivu hili deni: je hatukopi tena?

Pesa za tozo zinakwend wapi na kufanya shughuli gani?
Sawa deni ni himilivu inamaana samia atatoka madarakani ataacha deni na atakaye kuja nae atataka akope unafikiri nini kitatokea?

Kwa muda wezi walizibitiwa lakini sasa hawa walafi wamerudi kwa kasi wanakopa wanaweka kwenye account zao imefika mahala sasa hivi hata hatujui makusanyo ya mwezi yanasemaje na wao hawatangazi tena!!!! Tuna kwenda kama malofa” hili deni Lao halivumiliki kabisa huo ndo ukweli ndugai sio chizi Eti kusema anamuhujumu mama uwo ni ufala pia kajaribu kutupa picha ya yajayo na asipuuzwe.... round hii tumeshikwa pabaya wandugu tumepata raisi wamipasho yeye nikuzodoa tu muda mwingine kubali kujifunza kupitia wengine, sio kila anaesema anakuwa hakupendi Hapana ila kiukweli niwe mkweli mama hamna kitu kabisa kabisa
 
Mkuu swali zuri.. actually madhara ya kushindwa kulipa deni yatachofanya ni kwamba, nchi itakuwa down graded na wakopeshaji.

Na ukiwa downgraded maana yake huwezi kukopesheka tena.

Lakini impact kubwa huwa inakuwa ni trickle down effect ya kitachotokea baada ya kushindwa kulipa madeni.

1. Wawekezeji watakimbia maana macro fundamentals zita deteriorate.

2. Mfumuko wa bei

3. Pesa itashuka thamani kwa kasi..

4. Nchi inaweza kushindwa kumudu baadhi ya matumizi ya muhimu kabisa..

Yaani ikitokea, impact yake itakuwa ni mambo mengi magumu yatatuandama sana kwenye uchumi
Thanks mkuu
 
Kukopa sio dhambi kama umezidiwa na mambo hayaendi tunachotaka watz ni matumizi sahihi ya mikopo mfano
Kumalizia miradi ya kimkakati aliyoiacha JPM mimi binafsi namuunga mkono akope tu hamna namna
Nyepesinyepesi nasikia JPM alikuwa anajuwa mali za viongozi wetu wa nchi na dini wamejipataje? Wengine wao kwa magumashi alikuwa anapiga pin account mwenye account anaitwa anaambiwa tuambia chanzo cha mali hizi wengi walikuwa hawana maelezo yakutosha wanachukua mpunga wa kutosha wanakubakishia unaolingana na kipato chako ndo maana wengi sasa hivi wanalia sana na kumkejeli na kutoa povu waliumizwa kwa style hiyo ila hawasemi ukweli kwa watu wanabaki tukukana tu hata mwenye JPM kuna wakati alisema hizi ndege ni fedha za mafisadi alizowapora ukifatiliwa wengi wanaomtusi aliwafilisi kwa style hiyo
 
Labda kama watu wanakuwa na wasiwasi wa je fedha tunayokopa inatumika kwa malengo tarajiwa na inatumika vizuri?

Kwenye uchumi we go with numbers not words ndio tofauti yake. Na hiyo setup ya world bank ndio inatumiwa na wachumi wote.

Unless tuseme hatuna uwezo wa kuli service hilo deni. Mbona marekani deni lao limeshavuka 100% na wanajiona wapo sawa tu kwasababu uwezo wa kuli service deni wanao

Sent using Jamii Forums mobile app
Miaka ya 80-90 world bank, IMF na mataifa ya magharibi walishinikiza nchi za kiafrika na nyingine masikini kukumbatia SAPs. Je, matokeo yalikuwaje? Wakati mwingine ushauri wa hao jamaa ni busara kukubalika with a pinch of salt. Mambo yakienda sivyo hutawaona tena. Tukumbuke Ugiriki ilipotikiswa kiuchumi kwa kuelemewa na mzigo wa madeni mjomba alijitokeza kwa jina na EU lakini kijasho kiliwatoka sana kwa mashaiti magumu waliyopewa. Mwenzako akinyolewa ...... malizia.
 
Mjadala sounds good

Lakini mjadala na nani? Sisi ambao tuko busy na chupa z soda? Simba na yanga? Mariam biriyani na misafara ya walevi wa arusha na moshi?

Don’t forget kwamba wanaojali serious stuff nchini hawazidi 6%

Hata bungeni na serikalini kuna watu wapo tu wanafukuzia pesa za kujenga
Huu ukweli uliouongea hapa unaumiza sana.
 
Mkuu Naantombe Mushi nina swali kidogo.

Kuna ubaya kukopa kwa ajili ya miradi ambayo haitoi "returns" za moja kwa moja kulipa deni husika na kulipa deni hilo kwa kutumia miradi mingine inayozalisha fedha ?

Nitatoa mfano.
Unakopa fedha kwa ajili ya miradi ya elimu, halafu fedha yako ambayo ulitakiwa kupeleka kwenye elimu, unaendeleza mradi wa mabasi ya mwendokasi, ili mradi huo (wa mwendokasi) ulipe "deni la elimu" ?
Hii kiuchumi imekaaje mkuu ?

Maana kwa mtazamo wangu naona miradi mingi inayogusa "wanyonge moja kwa moja" kama vile elimu, afya, maji, n.k "financial returns" zake ni "too slow" lakini miradi hii ni "very good agenda" za kuombea mikopo.
 
Back
Top Bottom