Deni la Taifa in and out, kinachoumiza sio kukopa ni matumizi ya kinachokopwa


Hizo hapo juu ndio athari zinazozipata nchi zinazoshindwa kulipa madeni yake [ INSOLVENT; NOT CREDIT WORTHY} Na nchi ikifikia hatua hizo ndio utasikia nchi ina machafuko, haitawaliki kwa sababu ya vurugu, yakiwemo maandamano yasiyokwisha na hatimaye JESHI huingilia kati na kupindua serikali!!!!
 

Umeelimisha vizuri ukaharibu ulipoanza kumshambulia Hayati JPM. Hili zimwi la kuhangaika na marehemu sijui litaisha lini akili mwa baadhi ya Watanzania.

Yuko mwengine akasema kwa miaka mitano JPM amekopa zaidi ya miaka 10 Mkapa na miaka 10 Jakaya.

Mzee Mwinyi aliongea vizuri wakati flani akasema kwa miaka 5 JPM mambo aliyo yafanya yametufunika sisi tuliomtangulia wote.

So tumpogeze Rais SSH alivyo mjibu Spika Ndugai kuhusu hoja yake ya deni la Taifa. Tumpongeze Ndugai kwa uthubutu wake. Haya mengine ya kumshambulia Spika ni kufilisika kisiasa. Nyerere JK alishafafanua vizuri juu ya muflisi wa kisiasa. Pengine former CAG atapata pakutokea safari hii. Huyu hawezi msahau Ndugai kwa ile TKO.
 
Kukopa sio kubaya mkuu.. sema inatakiwa uhakikishe mkopo unaelekezwa kwenye viable projects.

Kukopa sio kubaya lakini ukope kwa akili sio kwa kufuata hisia; Kumbuka kuwa mkopeshaji anafanya biashara hivyo kama utakopa na kurudisha mkopo na riba basi hatasita kukukopesha zaidi. In fact kukopa kunaweza kukuletea sifa kama unakopa na kuweza kurudisha mikopo!!

Hakuna uwekezaji wa kijinga umewahi kufanyika nchini kama ule wa kwenda kununua ndege za ATCL zaidi ili hali zilizopo hazitumiki at full capacity!!! Hawasemi lakini fedha nyingine walizokopa walizitumia kununua hiyo mindege. Hasara ya shirika ni mzigo mzito sana wanabebeshwa wananchi bila kuonewa huruma na watawala kwani wanazidi kuongeza TOZO tu ili kupata mapato zaidi!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…