Deni la Taifa: Kukopa sio tatizo, lakini tumefanyia nini huo mkopo?

Deni la Taifa: Kukopa sio tatizo, lakini tumefanyia nini huo mkopo?

Mdude_Nyagali

Member
Joined
Dec 11, 2022
Posts
79
Reaction score
1,444
Binafsi nimepata mshtuko mkubwa baada ya kuona ongezeko kubwa la deni la taifa kufikia trillion 91 kutoka trillion 60.9 mwezi April 2021 wakati Samia anashika madaraka. Kwa hesabu ya haraka ni kwamba kwa mwaka mmoja serikali ya Rais Samia imekopa trillion 30 kiasi ambacho kimevunja rekodi kwani tangia tupate uhuru serikali haikuwahi kukopa pesa nyingi kwa kipindi kifupi kama ilivyotokea sasa.

Kabla ya kuendelea kutoa maoni yangu kuhusu ukopaji huu wa serikali ya Samia na matumizi yake hebu tuangazie deni la taifa tangu uhuru.

Mwalimu Nyerere kwa miaka 24 aliyokaa madarakani deni la taifa aliloliacha ni trillion 3.

Mzee wetu Mwinyi alilitoa deni kutoka trillion 3 mpaka trillion 18. Maana yake mzee mwinyi kwa miaka 10 alikopa trillion 15.

Mzee Mkapa alipoingia madarakani alikuta deni ni trillion 18. Akaanza juhudi za kupunguza deni bila kukopa na mpaka anaondoka madarakani 2005 deni la taifa lilibakia trillion 10 kutoka trillion 18 ya awali.

Mzee Kikwete alilitoa deni kutoka trillion 10 mpaka trillion 35. Maana yake Mzee Kikwete alikopa trillion 25 kwa miaka 10 aliyokaa madarakani.

Magufuli alilitoa deni kutoka trillion 35 mpaka trillion 60.9. Maana yake Magufuli alikopa trion 25.9 kwa miaka mitano aliyokuwepo madarakani.

Rais Samia amelitoa deni kutoka trillion 60.9 mpaka trillion 91. Maana yake ni kwamba mwaka mwaka mmoja na miezi Samia kakopa trillion 30+. Sawa na wastani wa kukopa trillion 1.5 kwa kila mwezi, bilion 50 kila siku, bilion 2.08 kwa saa na milion 34.7 kwa sekunde. Hiyo ni hesabu ya miezi 20 ya Rais Samia madarakani.

Na mimi niliamini kwamba pengine serikali ya Samia kuongeza kodi mpya ambazo hazikuwepo hapo awali zikiwemo tozo ililenga kufanya maendeleo kwa makusanyo ya pesa zetu wenyewe bila kukopa lakini ongezeko la deni la taifa limenishtua. Nimeshtuka kweli na kuogopa hasa ukizingatia taarifa za ukusanyaji mapato zinazotolewa na TRA kuvuka malengo.

𝑺𝒂𝒔𝒂 𝒕𝒖𝒓𝒖𝒅𝒊 𝒌𝒘𝒆𝒏𝒚𝒆 𝒉𝒐𝒋𝒂 𝒚𝒂 𝒎𝒔𝒊𝒏𝒈𝒊 𝒌𝒘𝒂𝒎𝒃𝒂 𝒕𝒖𝒎𝒆𝒌𝒐𝒑𝒂 𝒍𝒂𝒌𝒊𝒏𝒊 𝒕𝒖𝒎𝒆𝒇𝒂𝒏𝒚𝒊𝒂 𝒏𝒊𝒏𝒊?

Sisi wananchi ambao ndio dhamana ya nchi hii tungependa kuona kasi ya deni la taifa iendane na kasi ya maendeleo ya taifa. Binafsi naumia kuona kasi ya ukopaji ni kubwa kuliko maendeleo ya taifa. Kwamba serikali inakopa kwa kasi ya Nyumbu anayefukuzwa na Simba halafu maendeleo kasi yake ni ya Kinyonga, inasikitisha.

Magufuli alikopa trillion 25.9 kwa miaka mitano. Pamoja na kwamba tulilalamika aina ya ukopaji wake ambao mara nyingi haukuzingatia sheria lakini angalau mikopo yake ilionekana imefanya kazi gani japo kazi zenyewe zilizingatia utashi wake zaidi kuliko ushauri wa wataalamu.

Tuliona mikopo ya serikali ya Magufuli ikinunua ndege hata kama hakukuwa na Business Plan lakini angalau tuliona matokeo ya mkopo hata kama ndege hizo nyingi zimepaki kutokana na changamoto lakini tunaziona. Magufuli alianzisha ujenzi wa reli ya kisasa SGR, bwawa la umeme la mwalimu Nyerere, uwanja wa ndege Chato n.k.

Sasa hivyohivyo kwa Samia tulitegemea kuona maendeleo yanayoendana na mkopo huo hata kama ni ya hovyo lakini yaonekane na thamani yake iendane. Ukiacha uagizaji wa vichwa na mabehewa ya tren ya SGR ambayo thamani yake haiwezi kuzidi hata 5% ya mkopo wote ambao serikali imekopa kwa mwaka mmoja ni mradi gani mwingine ambao unaweza kuleta matumaini yanayoendana na mkopo huo?

Hivi tunajua thamani ya hiyo trillion 30 ambayo serikali ya Samia imekopa ndani ya miezi 20? Mfano tungeamua kujenga barabara ya lami njia nne (Sio mbili) ili kupunguza msangamano na ajali kutoka Dar es Salaam mpaka Tunduma tungetumia trion 3.9 tu kati ya hizo trion 30 zilizokopwa kwa mwaka mzima. Kutokana na shida ya maji iliyopo nchini basi bilion 400 zilikuwa zinatosha kununua magari ya kuchimba visima na vifaa vyake katika halmashauri zote nchini pamoja na kujenga mradi wa maji bwawa la Kitunda kwa upande wa Dar. Ujenzi wa vituo vya afya vilivyobakia nchi nzima pamoja na kukomesha adha ya uhaba wa madarasa pamoja na madawati ulihitaji asilimia 16 ya hizo trillion 30 zilizokopwa kwa ndani ya miezi 20.

Pengine kupitia hiyo trillion 30 hatukupaswa kusikia shida ya maji kwenye vijiji na miji yote katika halmashauri zetu. Hatukupaswa kusikia shida ya madarasa, zahanati ama vituo vya afya.

𝐒𝐰𝐚𝐥𝐢 𝐥𝐚𝐧𝐠𝐮 𝐣𝐞 𝐡𝐢𝐲𝐨 𝐭𝐫𝐢𝐥𝐥𝐢𝐨𝐧 𝟑𝟎 𝐢𝐥𝐢𝐲𝐨𝐤𝐨𝐩𝐰𝐚 𝐧𝐚 𝐬𝐞𝐫𝐢𝐤𝐚𝐥𝐢 𝐲𝐚 𝐑𝐚𝐢𝐬 𝐒𝐚𝐦𝐢𝐚 𝐤𝐰𝐚 𝐦𝐰𝐚𝐤𝐚 𝐦𝐦𝐨𝐣𝐚 𝐢𝐧𝐚𝐞𝐧𝐝𝐚𝐧𝐚 𝐧𝐚 𝐦𝐚𝐞𝐧𝐝𝐞𝐥𝐞𝐨 𝐚𝐥𝐢𝐲𝐨𝐲𝐚𝐟𝐚𝐧𝐲𝐚?

𝑴𝒅𝒖𝒅𝒆 𝑵𝒚𝒂𝒈𝒂𝒍𝒊 7 x 70 Sumu ya Nyigu.
 
Sasa tunafanya makusanyo ya pesa ya kuwapa wakuu wa vyombo vya dola wakati wa uchaguzi 2025 ili tuendelee kutawala.

Sababu ya wananchi kuwa mazuzu na mazwazwa pia vilaza tutawapa kofia,chumvi nk watasahau shida zote na kuimba nyimbo pendwa ya "wataisoma namba CCM mbele kwa mbele"

"Ujinga wa fikra ni mbaya Sana katika dunia"

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
𝐒𝐰𝐚𝐥𝐢 𝐥𝐚𝐧𝐠𝐮 𝐣𝐞 𝐡𝐢𝐲𝐨 𝐭𝐫𝐢𝐥𝐥𝐢𝐨𝐧 𝟑𝟎 𝐢𝐥𝐢𝐲𝐨𝐤𝐨𝐩𝐰𝐚 𝐧𝐚 𝐬𝐞𝐫𝐢𝐤𝐚𝐥𝐢 𝐲𝐚 𝐑𝐚𝐢𝐬 𝐒𝐚𝐦𝐢𝐚 𝐤𝐰𝐚 𝐦𝐰𝐚𝐤𝐚 𝐦𝐦𝐨𝐣𝐚 𝐢𝐧𝐚𝐞𝐧𝐝𝐚𝐧𝐚 𝐧𝐚 𝐦𝐚𝐞𝐧𝐝𝐞𝐥𝐞𝐨 𝐚𝐥𝐢𝐲𝐨𝐲𝐚𝐟𝐚𝐧𝐲𝐚?
Karibu sana Mdude!!

Swali lako halitajibiwa na wala hujakosea kuuliza bali unaowauliza huwa hawana majibu kwa maswali wanayoulizwa.
 
Apatikane jasiri mmoja atuunganishe tuingie barabarani kuikomboa nchi yetu kutoka kwenye makucha ya majambazi bila hivyo ndugu zangu tutaendelea kulalamika tu afu haya mambuzi yanachekelea.Mtaani watu wamechoka aisee wanasubiri mtu aanzishe mapambano watu waingie barabarani
 
Awamu hii ingejikita kwenye suala la nishati haswa ya gesi asili, viwanda na teknolonia ...

Ingeharakisha uwepo wa plant ya CNG, usambazaji wa gesi kama nishati ya kupikia kwa wananchi, usambazaji wa vituo vya CNG kwa magari n.k
 
Back
Top Bottom