Deni La Taifa: Wabunge, Wanasiasa Wachumi Na Wachumi Wanasiasa

Deni La Taifa: Wabunge, Wanasiasa Wachumi Na Wachumi Wanasiasa

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2007
Posts
4,850
Reaction score
9,434
Deni la Taifa letu linazidi kupaa. Kwa mujibu wa takwimu za hizi karibuni, Deni hili tayari limeshavuka dollar za kimarekani Billion kumi na tano, sawa na takribani shillingi trilioni ishirini na tatu za Kitanzania.

Moja ya Vigezo muhimu vya kupima utendaji wa serikali yoyote ile duniani ni suala zima la nidhamu ya katika mfumo wake wa mapato na matumizi ya fedha za umma (Fiscal Discipline). Ukiachilia mbali ‘fiscal discipline’, vigezo vingine muhimu ni Ajira kwa raia wake, mfumo wake wa Elimu, mfumo wa Afya, Ufanisi Katika Mhimili wa Mahakama (Judicial Efficiency) n.k. Lakini mafanikio katika maeneo yote haya hutegemea sana kigezo muhimu kuliko vyote ambacho ni ‘Fiscal Discipline’ ya Serikali husika. Kwahiyo kwa leo Mada yangu italenga zaidi kwenye suala zima la Fiscal Discipline. Kinachonisukuma kuja na mada hii ni masuala makuu mawili:

Kwanza ni upotoshaji wa baadhi ya wanasiasa hasa ndani ya bunge letu kuhusiana na deni la taifa, hasa katika hoja zao mbili kwamba: Moja, hoja kwamba ‘ni jambo la kawaida kwa nchi kuwa na madeni, na Mbili, ni hoja ya baadhi ya wanasiasa kwamba ‘Deni letu la taifa ni dogo sana ikilinganishwa na nchi nyingine nyingi, hivyo wananchi hawana haja ya kuwa na wasiwasi wowote. Dhamira yangu ya pili kuja na mada hii imesukumwa na ukweli kwamba wabunge wetu wengi, licha ya kuwa na hoja za kizalendo zinazolenga kujadili juu hatari inayotukabili kama taifa kuhusiana na kuendekea kukua kwa deni la taifa kwa kasi, wabunge wengi hawapo ‘well informed to challenge’ vya kutosha serikali juu ya suala hili kwani mara nyingi hoja zao hupwaya na kuishia kuwa hoja za kisiasa, hivyo kushindwa nguvu kwa hoja za wanasiasa wasiojali nidhamu ya matumizi na mapato ya fedha za umma;

Nikiingia moja kwa moja katika hoja hizi za wanasiasa, kuna ukweli kwamba kwa taifa lolote, Deni la taifa/umma ni jambo la kawaida na la Lazima. Kwa kuangalia conventional methods za kupima iwapo deni la taifa ni mzigo au hapana ambapo vigezo kama vile ‘uwiano wa deni la taifa na pato la taifa’ (Debt to GDP Ratio) hutumika, kuna uwezekano wa umma kuaminishwa kwamba Tanzania ipo katika nafasi nafuu kuliko mataifa mengi in terms of national debt. Kwa mfano, kwa sasa, Debt to GDP ratio ya Tanzania ni around 47% huku kwa taifa kama marekani uwiano huu ni around 110% huku Japan Debt to GDP ratio ikiwa ni zaidi ya 200%. Katika hili, imekuwa jadi kwa wanasiasa (CCM) kujadili kujenga hoja zao nilizojadili awali, aidha kwa kujua au kutojua kwamba hoja zao zipo crafted zaidi kisiasa kuliko kiuchumi. Lakini katika mazingira yetu ambapo we glorify politics and defy economics, utamaduni huu sio jambo la ajabu.

Pengine at this juncture, ni muhimu kujadili, japo kidogo, dhana mbili muhimu ambazo ni kama chanda na pete katika mlinganyo mzima wa mfumo wa mapato na matumizi ya fedha za umma (fiscal system). Dhana hizi ni National Debt (Deni la Taifa/Umma) na Fiscal/Budget Deficit. Wengi mnaelewa maana yake dhana hizi hivyo nitajadili kwa ufupi sana kama njia ya kujenga muktadha wa mjadala.

1. Budget au Fiscal Deficit: Kwa lugha nyepesi,budget/fiscal deficit hujitokeza pale ambapo mapato ya serikali yanakuwa madogo kuliko matumizi ya serikali katika economic cycle husika. Hali hii ya mapato kuwa madogo kuliko matumizi ya serikali kwa ajili ya huduma mbalimbali za kijamii, na gharama za kuendesha shughuli za serikali kwa ujumla, hupelekea serikali huska kuchukua uamuzi wa kukopa kutoka vyanzo vikuu viwili – aidha vyanzo vya ndani, vyanzo vya nje au vyote kwa pamoja. Kila chanzo kina mchakato wake, faida zake lakini pia na changamoto zake, yote ambayo tutayadili huko mbeleni, lakini kwa sasa niseme tu kwamba tangia uhuru, kwa wastani, serikali imekuwa inategemea zaidi mikopo kutoka kwenye vyanzo vya nje (kwa zaidi ya 70%), huku vyanzo vya ndani vikitumika kwa kiwango kisichozidi 30%.

2. National Debt/Deni la Umma/Taifa - maana yake pia ni straight forward kwa walio wengi lakini pengine nisisitize tu kwamba – deni la taifa ni mrundikano wa Fiscal Deficits za economic cycles mbalimbali/ miaka nenda miaka rudi. Ni kutokana na hali hii, Deni la taifa na fiscal/budget deficit vina uhusiano wa karibu sana kwani kukopa/mikopo ‘represents a predominant source to finance deficit’ ya economic cycle husika. Kwahiyo deni la Umma/taifa pia hutazamwa kama asilimia ya pato la nchi ili kuakisi overall fiscal health ya uchumi husika;

Nikirudi katika hoja yangu ya msingi juu ya upotoshwaji unaofanywa na baadhi ya wanasiasa, ni jambo la kawaida kwa wanasiasa wetu to glorify politics and defy economics kwani to them, Politics is supreme to every kind of common sense and rationality. Porojo zao bungeni na maeneo mengine kutetea ukubwa wa fiscal deficit ni moja ya vituko vyao to defy economics and glorify politics. Nitafafanua. Katika nchi za wenzetu walioendelea kiuchumi, hasa nchi ambazo wanasiasa wetu huzifananisha na Tanzania in terms of Debt to GDP ratio kisha kujenga hoja kwamba ‘ratio’ zao zipo juu yetu (e.g. USA over 100%, & Japan over 200%) kuliko Tanzania (i.e. around 47%) na kusisitizia umma wetu kwamba tupo salama, wanasiasa hawa aidha kwa makusudi au mere ignorance, wanakosa ufahamu kwamba, suala zima la usimamizi wa mapato na matumizi katika mfumo wa fedha za umma kwa wenzetu huzingatia Sheria au Kanuni kuu mbili namely:

1. The Golden Fiscal Rule; na
2. The Sustainable Investment Rule.

Pengine ufafanuzi wangu juu ya kanuni hizi mbili utasaidia to shade more light kuhusu jinsi gani wanasiasa wetu wanavyokuwa wapotoshaji. Tukianza na Golden Fiscal Rule, kanuni hii inasema kwamba – katika mzunguko wa uchumi husika (in any given economic cycle), serikali inatakiwa kukopesha fedha na kuzitumia fedha hizo katika uwekezaji (investment) kuliko katika matumizi ya kawaida. Swali la kwanza la kujadili ni je:

· Kwa kiasi gani Wanasiasa wetu wanazingatia ‘Golden Fiscal Rule’ katika ujenzi wa hoja zao?

Kama tutakavyojadili baadae, ni dhahiri kwamba tangia uhuru kanuni hii imekuwa inakiukwa. Kwa mfano zingatia jinsi gani serikali katika bajeti zake zote imekuwa iki ‘allocate’ sehemu kubwa ya fedha za umma katika matumizi ya kawaida (posho, mishahara, manunuzi ya umma n.k) kuliko kuwekeza katika maeneo yenye manufaa kwa umma. Bungeni wapo wanaojengahoja ju ya jinsi gani fungu la matumizi ya kawaida huwa kubwa zaidi ya lile la maendeleo, lakini kwa vile hoja zao hujengwa bila ya utashi wa kiuchumi, hasa unao challenge Serikali kwa misingi ya kanuni za kiuchumi, hoja nyingi za namna hii pamoja na umuhimu wake zinaishia kuwa defeated na hoja za wanasiasa waliokosa nidhamu ya usimamizi wa mapato na matumizi ya fedha za umma.

Tukiingia kwenye kanuni ya pili – The Sustainable Investment Rule, kanuni hii inasema kwamba – katika mzunguko wa uchumi husika (in any given economic cycle), uwiano baina ya sekta ya umma na pato la taifa (net public sector to GDP) has to be set within a stable and judicious/responsible level. Kwa mfano Waingereza wao kuna wakati kiwango chao walilenga kiwango chao kiwe chini ya 40% ya GDP.

Swali la pili la kujadili ni je:

· Kwa kiasi gani Wanasiasa wetu wanazingatia ‘the Sustainable Investment Rule’ katika ujenzi wa hoja zao?

Katika hili pia, kama tutakavyojadili, serikali katika miaka yake yote ya bajeti za mwaka imekuwa ikienda kinyume na kanuni/sheria hii yenye nia ya kuhakikisha kwamba kunakuwepo na fiscal discipline.

Ili kuufanya mjadala unoge na ueleweka zaidi, pengine tuzidi kutafuta majibu kwa maswali mengine mawili muhimu yafuatayo:

· Kwanini nchi za wenzetu walikuja na sheria/kanuni hizi?

Nikianza na ‘Golden Fiscal Rule’, sababu ya msingi ya kuja na sheria hii ambayo wabunge, wanasiasa na policy makers Tanzania ni muhimu waelewe ni kwamba - nia yake ni kuhakikisha kwamba ZIGO la matumizi ya umma yanayolazimisha mikopo lazima yaangukie across generations fairly; Idea hapa ni kwamba – angalau serikali iwe na ‘political will’ kujaribu kuhakikisha kwamba all public consumption zinazofaidisha kizazi cha sasa lazima ilipwe na kizazi kilichoingia katika deni/mkopo husika; Chini ya sheria hii, inatamka explicitly kabisa kwamba serikali haitakopesha kwa ajili ya matumizi ya kawaida yani (current spending or expenditure) bali kwa ajili ya investments. Nia hapa ni kuhakikisha kwamba hata kama vizazi vijavyo vitakutana na deni la mababu zao, basi angalau vizazi hivyo vifaidike na madeni watakayowakuta, hasa iwapo fedha hizo zilikuwa invested kwa faida ya vizazi vya wakati huo na vile vitakavyofuata.

Nikiingia kwenye Sustainable Investment Rule, kanuni au sheria hii ina compliment ile ya golden fiscal rule kwa nia ile ile ya kujaribu to avoid creation ya excessive burden ya debt repayments kwa vizazi vijavyo. Kwa sheria hii, serikali inahakikisha kwamba deni linadhibitiwa katika kiwango ambacho hakita prove kuwa unsustainable or unfair kwa vizazi vijavyo. Swali lingine muhimu kujadili ni je:

· How much Debt is too Much Debt?

Kama nilivyojadili awali, moja ya kipimo iwapo deni la taifa ni mzigo au sio mzigo kwa walipa kodi ni kwa kuangalia uwiano wa deni la taifa kwa pato la taifa i.e. Debt to GDP ratio. Ni katika hili ndipo tunaona nchi kama Marekani uwiano huu kwa sasa upo zaidi ya 100%, Japan zaidi ya 200%, wakati kwetu Tanzania kwa sasa uwiano ukiwa takribani 47%, suala lilalopelekea baadhi ya wanasiasa, wabunge na policy makers, aidha out of ignorance or arrogance, kujenga hoja kwamba tofauti na mataifa kama Japan na Marekani, sisi tupo salama salmini. Huu ni upotoshaji kwa maelezo yafuatayo:

Ni muhimu kwa viongozi wa namna hii kuelewa kwamba nchi kuwa na uwiano mdogo (i.e. Debt to GDP ratio) haina maana kwamba nchi hiyo ipo salama ai haipo katika hatari yaku default. As a matter of fact, historia ya uchumi wa kimataifa unaonyesha kwamba nchi nyingi ambazo zimekuwa ziki default madeni yao zile zenye Debt to GDP ratios way below 60%. Kwa maana hii, tofauti na wanasiasa wetu uchwara wanavyopenda umma wa watanzania uamini, Tanzania ipo katika hatari zaidi to default kuliko mataifa kama Japan, Uingereza au Marekani.

· Je kwanini nchi yenye high Debt to GDP ratio inaweza kuwa salama zaidi kuliko nchi yenye low ratio?

Jibu ni simple – sisi Tanzania tupo more likely kukopa fedha katika sarafu nyingine kubwa nje ya fedha zetu za madafu (shilling za kitanzania). Kwa mfano ukitazama historia ya uchumi wetu, vyanzo vikubwa vya mikopo yetu karibia mara zote imekuwa ni vyanzo vya nje ya nchi, hivyo kukopa in dollars kuliko kutoka vyanzo vya ndani ambavyo vingeweza kutegemea sarafu yetu (yani shillingi). Kwa wastani, uwiano baina ya deni letu la nje na la ndani miaka yote umekuwa sio chini ya 70% (nje) na sio zaidi ya 30% (ndani). Kwahiyo, tofauti na wenzetu kama Japan, UK au USA, sisi hatuwezi kutumia mfumuko wa bei (printing money) to devalue sehemu kubwa ya deni letu kwa ufanisi iwapo tunalemewa na madeni. Hivyo njia pekee inayobakia kwa ajili ya wokovu wetu ni aidha wakubwa (IMF, WorldBank na washirika zao) watufanyie debt restructuring, watusamehe with strings attached katika rasilimali zetu, vinginevyo kinachofuatia ni defaulting…;

Ni muhimu pia at this juncture tukafahamu kwamba mbali ya Debt to GDP ratiokuwa moja ya vipimo vikubwa vya severity ya deni la taifa, kipimo kingine muhimu ni kile cha ‘debt service ratio’ i.e. the ratio of debt service payments (principal plus interests) of a country to the export earnings of that particular country. Uwiano huu ukiwa chini, maanayake ni kwamba uchumi wa taifa husika una afya zaidi kuliko nchi yenye uwiano ulio juu.

Ni muhimu kwa wanasiasa wetu kuelewa kwamba tofauti iliyopo baina na matumizi ya debt to gdp ratio na ile ya debt service ratio. Kwa mfano, kipimo sahihi cha kubaini severity ya deni la taifa kwa nchi inayokopa kupitia vyanzo vyake vya ndani (local currency), key ratio to determine how large the debt is, ni debt service ratio. Na kwa nchi ambayo inakopa kupitia vyanzo vya nje (sarafu ya dollar), important ratio kuitazama ni debt to GDP ratio. Baadae tutaangalia ratio hizi kwa undani zaidi katika muktadha wa Tanzania ili kuelewa zaidi changamoto zinazotukabili. Kwa mfano, tutaona kwa undani zaidi jinsi gani Tanzania tunalipa more to service the debt kuliko tunavyotumia/wekeza kwenye sekta muhimu kama vile sekta ya Afya n.k.

Pia, baadae tutajadili kwa undani juu ya jinsi gani wanasiasa na policy makers wengi wamekuwa wakipuuzia management ya domestic debt na badala yake kujikita zaidi katika management ya external debt ambapo wamekuwa wakijikita na external debt management sana sana kutokana na pressure kutoka nje ya nchi kuliko ‘political will’. Vile vile tutajadili kwa undani jinsi gani external debt can be a threat to national security and nationa sovereignty, na kuna wakati baba wa taifa wakati ule anapingana na mzee mtei na kina IMF aliwahi kuhoji – Je, kwani hao ni wajomba wetu huko nje mpaka “watusaidua” fedha? Vile vile tutajadili kwa undani kuhusu suala zima la nani wanatukopesha, mchakato wake upo vipi, na transparency kwa walipa kodi…

Nihitimishe katika maeneo mawili: Kwanza ni msisitizo kwamba budget/fiscal deficit ni matokeo ya mapato ya serikali kuwa machache kuliko matumizi ya serikali in a given economic cycle. Kwa wenzetu wenye nidhamu ya juu kwenye suala hili (Fiscal Discipline), ongezeko la revenue ni matokeo ya ongezeko la output (GDP), income za individuals and income za businesses, na pia taxing the wealthy. Lakini kwetu Tanzania kuna kila ushahidi kwamba kasi ya kukua kwa uchumi (GDP growth) na ongezeko la vipato (biashara na individuals) havina uhusiano mkubwa na ongezeko la ukusanyaji wa kodi. Kwa mujibu wa utafiti mmoja, Tanzania ina potential ya kukusanya kodi at 21% of GDP. Kwa sasa, takwimu zinasema tupo somewhere around 16% lakini in reality, kiasi kinachokusanywa ni wa below the stated figure of 16%.

Pamoja na mapungufu haya, lengo la serikali ya Tanzania ni kufikishia mapato ya kodi kufikia 20% ya GDP ifikapo mwaka 2015 huku serikali pia ikilenga kupunguza utegemezi wa wahisani katika bajeti kufikia chini ya 10%; Kwa zaidi ya miaka 40, kiwango hiki kimekuwa kikicheza kati ya 30% na 40%; Katika miaka ya hivi karibuni, tumefanikiwa kushuka zaidi na kufikia in upper 20 percent. Swali linalobakia ni je, tuna mikakati gani endelevu ya kuhakikisha kwamba tunafikisha kiwango hiki kuwa in single digits i.e. kuifanya Tanzania iweze kujitegemea katika bajeti yake kwa at least 90% ifikapo 2015? Tunarudi pale pale – we defy economics and glorify politics. Huwa tuna malengo mengi lakini yanaishia hewani kutokana na Lack of “POLITICAL WILL.” Tumeona initiatives mbalimbali za kina Zitto Kabwe, January Makamba na wengine bungeni kuhusiana na masuala kama vile kuongeza makusanyo ya kodi on projects and investments that are natural resource based, kuja na sheria kali kudhibiti money laundering, suala la capital gains tax, property tax, regulation of the real estate sector n.k. Ni muhimu kwa wanasiasa kutambua kwamba deficits huchangiwa sana na uzembe katika maeneo muhimu kama haya., na bila kuweka political will katik maeneo kama haya, Taifa kufikia 90% katika kujitegemea kibajeti na taifa kufikia potential yake ya 21% of GDP in tax revenues itaendelea kuwa ndogo za mchana;

Pili na Mwisho, tuelewe tu kwamba mjadala hapa au hoja ya msingi hapa sio kwamba tunatarajia serikali yetu kulipa deni lake lote and make Tanzania become a debt free nation kwani katika taifa lolote lile, debts rarely gets repaid. So the issue sio serikali ilipe madeni yake yote bali kama nilivyojadili tuwe na political will kuzingatia masuala kama vile golden fiscal rule na sustainable investment rule. Pia ni muhimu kwa political will kuhakikisha kwamba debt levels do not crowd out indigenous/local businesses or reduce their confidence, kwani unlike multinationals ambazo nyingi aidha hazilipi kodi au hazina activities zenye backward and forward linkages that create values senye manufaa kwa wananchi walio wengi, local businesses ni key katika kufanikisha haya in terms expanding the tax base, creating jobs n.k; Mwisho, kuna umuhimu wa kuhakikisha kwamba serikali inakuwa na uwezi to service its debt bila ya kuathiri investments katika sekta muhimu za uchumi zenye kugusa maisha ya walio wengi kama vile Elimu, Afya na Kilimo. Serikali yetu imekuwa inalegalega sana katika kutenga fedha za kutosha per agreements mbalimbali za kimataifa kama vile bajeti ya kilimo kuwa at least 10% of the GDP, huku pia allocation of budgets as percentage of GDP kwenye sekta muhimu kama afya na nyinginezo, the government has been living below its commitments.
 
Suala la hatari inayoikabili Tanzania kutokana na kukua kwa deni la taifa linaeleweka. Serikali kupitia wataalamu wake wa uchumi na takwimu inaelewa fika nini kinaikabili kesho ya Tanzania kiuchumi. Tatizo ni kwamba hakuna political will. Mipango mingi ya serikali hivi sasa inaonekana kuelekezwa katika kutafuta kurejesha/kulinda imani yake kwa wananchi kwa njia za zimamoto kushinda uchaguzi wa mwaka 2015. Ushauri kutoka kwa baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani unatafsiriwa kama "kete ya kisiasa" na kutupiliwa mbali.

Kukosekana kwa dhamira ya kweli ya kutatua matatizo halisi ya Wananchi ndiyo chanzo cha kukua matatizo mbalimbali ya kimaendeleo tuliyonayo likiwemo hili la deni la taifa. Ninaamini hili tatizo la kukua kwa deni la taifa litafumbiwa macho sana tu kwasababu mwananchi wa kawaida haelewi kinachozungumziwa, na hivyo si rahisi kupata shinikizo kutoka kwa wananchi wengi au kuwamtumia kisiasa kwa hili.

Wanasiasa wetu wanaonekana kupenda kutaka kuonekana wana uchungu zaidi na maendeleo ya nchi kwa mambo ambayo yanaibua hisia kirahisi miongoni mwa raia na ni mtaji zaidi kisiasa. Mambo complex lakini ni muhimu kwa mwananchi kama hili la deni la taifa yanapuuziwa tu. Hata hapa jukwaani utaona kuwa wachangiaji ni wachache kwa mada kama hizi. Lakini zile za "Mulugo amefoji vyeti" etc wachangiaji lukuki.
 
Mkuu wangu Mchambuzi,

Hii thread inahitaji muda wa kutosha, kuisoma, kui-digest na kuijadili. Nazani ungeipeleka kule Jukwaa la GT, ingekuwa bora zaidi coz' hapa Jukwaa la Politics, inaweza kupotea mapema.....si unajua hili jukwaa?

Mtu akimuona Nchemba mitaani amejikwaa, atakuja hapa na kuanzisha thread na matokeo yake kuzi-push back threads za msingi.
 
Mkuu wangu Mchambuzi,
Hii thread inahitaji muda wa kutosha, kuisoma, kui-digest na kuijadili. Nazani ungeipeleka kule Jukwaa la GT, ingekuwa bora zaidi coz' hapa Jukwaa la Politics, inaweza kupotea mapema.....si unajua hili jukwaa? Mtu akimuona Nchemba mitaani amejikwaa, atakuja hapa na kuanzisha thread na matokeo yake kuzi-push back threads za msingi.
Word!!
 
Nikiingia moja kwa moja katika hoja hizi za wanasiasa, kuna ukweli kwamba kwa taifa lolote, Deni la taifa/umma ni jambo la kawaida na la Lazima. Kwa kuangalia conventional methods za kupima iwapo deni la taifa ni mzigo au hapana ambapo vigezo kama vile ‘uwiano wa deni la taifa na pato la taifa' (Debt to GDP Ratio) hutumika, kuna uwezekano wa umma kuaminishwa kwamba Tanzania ipo katika nafasi nafuu kuliko mataifa mengi in terms of national debt. Kwa mfano, kwa sasa, Debt to GDP ratio ya Tanzania ni around 47% huku kwa taifa kama marekani uwiano huu ni around 110% huku Japn Debt to GDP ratio ikiwa ni zaidi ya 200%. Katika hili, imekuwa jadi kwa wanasiasa (CCM) kujadili kujenga hoja zao nilizojadili awali, aidha kwa kujua au kutojua kwamba hoja zao zipo crafted zaidi kisiasa kuliko kiuchumi. Lakinir katika mazingira yetu ambapo we glorify politics and defy economics, utamaduni huu sio jambo la ajabu.
Economically, up to 60% of GDB-to-Debt Ratio is acceptable. However my concerns are whether available data are genuine and not tampered data! Under this context, tampered data are those data tampered intentionally or unintentionally; the former being for the purpose to deceive the donors/lenders and the later being due to incompetence of data collector and analysts!

Not only that, As far as GDP-to-Debt Ratio inaangalia how healthy the economy is to repay the available debt; another concern may arise as well. Inawezekana kabisa ikawa our GDp-to-Debt Ratio ikawa ni kweli 47% thus implying kwamba our economy is still healthy to accommodate the available debt. Hapa pia tunapaswa kujiuliza. Our economy is that really healthy even in the Long Run? I am talking about sustainability of that economy to accommodate long Term Dues!

If, there's steady economic growth, then hapana haja ya kuliogopa Deni La Taifa provided the funds zinakuwa channeled kunakotakiwa.
 
Deni la Taifa letu linazidi kupaa. Kwa mujibu wa takwimu za hizi karibuni, Deni hili tayari limeshavuka dollar za kimarekani Billion kumi na tano, sawa na takribani shillingi trilioni ishirini na tatu za Kitanzania.

kuna wakati baba wa taifa wakati ule anapingana na mzee mtei na kina IMF aliwahi kuhoji – Je, kwani hao ni wajomba wetu huko nje mpaka “watusaidua” fedha? Vile vile tutajadili kwa undani kuhusu suala zima la nani wanatukopesha, mchakato wake upo vipi, na transparency kwa walipa kodi…

Nihitimishe katika maeneo mawili: Kwanza ni msisitizo kwamba budget/fiscal deficit ni matokeo ya mapato ya serikali kuwa machache kuliko matumizi ya serikali in a given economic cycle. Kwa wenzetu wenye nidhamu ya juu kwenye suala hili (Fiscal Discipline), ongezeko la revenue ni matokeo ya ongezeko la output (GDP), income za individuals and income za businesses, na pia taxing the wealthy. Lakini kwetu Tanzania kuna kila ushahidi kwamba kasi ya kukua kwa uchumi (GDP growth) na ongezeko la vipato (biashara na individuals) havina uhusiano mkubwa na ongezeko la ukusanyaji wa kodi. Kwa mujibu wa utafiti mmoja, Tanzania ina potential ya kukusanya kodi at 21% of GDP. Kwa sasa, takwimu zinasema tupo somewhere around 16% lakini in reality, kiasi kinachokusanywa ni wa below the stated figure of 16%.

Pamoja na mapungufu haya, lengo la serikali ya Tanzania ni kufikishia mapato ya kodi kufikia 20% ya GDP ifikapo mwaka 2015 huku serikali pia ikilenga kupunguza utegemezi wa wahisani katika bajeti kufikia chini ya 10%; Kwa zaidi ya miaka 40, kiwango hiki kimekuwa kikicheza kati ya 30% na 40%; Katika miaka ya hivi karibuni, tumefanikiwa kushuka zaidi na kufikia in upper 20 percent. Swali linalobakia ni je, tuna mikakati gani endelevu ya kuhakikisha kwamba tunafikisha kiwango hiki kuwa in single digits i.e. kuifanya Tanzania iweze kujitegemea katika bajeti yake kwa at least 90% ifikapo 2015? Tunarudi pale pale – we defy economics and glorify politics. Huwa tuna malengo mengi lakini yanaishia hewani kutokana na Lack of “POLITICAL WILL.” Tumeona initiatives mbalimbali za kina Zitto Kabwe, January Makamba na wengine bungeni kuhusiana na masuala kama vile kuongeza makusanyo ya kodi on projects and investments that are natural resource based, kuja na sheria kali kudhibiti money laundering, suala la capital gains tax, property tax, regulation of the real estate sector n.k. Ni muhimu kwa wanasiasa kutambua kwamba deficits huchangiwa sana na uzembe katika maeneo muhimu kama haya., na bila kuweka political will katik maeneo kama haya, Taifa kufikia 90% katika kujitegemea kibajeti na taifa kufikia potential yake ya 21% of GDP in tax revenues itaendelea kuwa ndogo za mchana;

the government has been living below its commitments.
Mkuu Mchambuzi, welcome back, long time hujashuka na nondo za jinsi hii, nakushukuru sana kutupiga lecture ya nguvu ya kiuchumi!, mwanzo nilikusifu sana kama mwanasiasa makini na mmoja wa ma great great thinkers humu jukwaani, hivyo nikawish cross upande wa pili, tukusumie jimbo lili lile, na utalisomba kama umeliokota!, nasali sana, CCM isikusimamishe wewe pale, maana uwepo wako utakuwa ni kikwazo kikubwa cha kupunguza idadi ya wabunge wa upinzani bungeni, japo tutakuwa tumeongeza Zitto, January, Deo type ya nguvu, na kuwa na more vibrant perliamentarians, ila baada ya lecture hii, naskushauri, please repoty chuo, kawapige watu darasa!.

Mimi nilisoma commerce O-Level, na chuo nikachukua Investment Law, International Bussiness Law na Capital Markets and Securities, ila baada ya kukusoma, nimejistukia kumbe nilikuwa mtupu kabisa katika deni la taifa!, labda kwa vile mimi nilikuwa "jongolist" sana chuoni, usikute wakati wenzangu wakipigwa somo hili, mimi nilikuwa kitaa!.

Nitachangia katika maeneo mawili, ukisanyaji kodi, na Dependency Syndrome!.

Nikianzia na ukusanyaji kodi, TRA wanatumia program ya Asycuda ++ katika track down mapato, katika kuelekea regional intergration, wenzetu Kenya na Uganda, wao wanatumia Simba, hivyo the system don't talk!. Ukwepaji mkubwa wa kwanza wa kodi, ni kwenye import!. Naifahamu kampuni moja maarufu sana kwa export import vyakula, wana Trading company ya ununua na kuuza vyakula local, then wana import na export company, wana freigt and forward company, wana shipping company, wana transport company, wana bonded ware house company na wana Insurance Company yao.

Kinachofanyika, wanangiza meli nzima ya mchele kupitia shipping company yao, huku documents zikionyesha huo mchele ni wa transit, to Malawi, Zambia, Rwanda, Burudi, Uganda, DRC etc. Mzigo ukifika, wanau clear kupitia clearing agents yao!, then mzigo unaingia kwenye bonded wherehouse yao. Then wanaupakia kwenye makontena na kuusafirisha kwenye zile nchi kupitia transport company yao. Kinachosafirishwa ni documents tuu, zikishafika border, wanajua wanachokifanya pale na TRA wanajua, (kwa msio jua), ukifika border post, kinachocross border ni documents only!. Ule mzigo unachange hands kupitia Trading company yao, unaingizwa kwenye maghala yao, na kuishia kusambazwa madukani na the bussiness ends there. From time to time, TRA huwa wanawabadili wale maofisa wake, na wakitokea wanoko, kutrace mzigo kwenye destination, taarifa zinakuja kuwa hakuna mzigo uliofika huko, ukiwarudia, unakutana na documents kuwa ule mzigo ulipotelea njiani, hivyo insurance copmya yao inashughulikia!. Kwa vile the systems dont speak, biashara huishia border post!. Serikali inapata kodi nil, hivyo kampuni inatumia majengo ya NHC, maghala ya NHC, Malori ya kukodisha!, hata wakurugenzi walikuwa wakiishi nyumba za Msajili, wanauwezo wa kuinunua korosho yote ya Mtwara!, hawana shamba, hawana land, hawana any investment in Tanzania, just a trading company ina reap bilions!, no one knows faida hii inapelekwa wapi, ukiondoa kuziona vogue, ferari na sports cars zao, nothing else!.

Tukirudi kwenye domestic revenue collection, TRA wameintroduce TIN na fiscal devices, na kuweka sheria ya risiti, kwa ili ku track down every penny!. Masikini TRA wetu, hawana the capacity to trace any transactions, bado biashara kibao zinatoa risiti zetu zile!, na sisi tunaolipa VAT, nimekuwa aproached na mtu, akaniuliza kwa nini ulipe VAT ya 18% yote?, leta fiscal device yako, tukufanyie setting ya maujanja, sasa utalipa only 10% ila utalipa kwetu!, kule TRA kwenye VAT returns zako, zitaonyesha umelipa 18% na kijana atakupitishia remitance receipts zako ambazo "TRA" wamepokea malipo!. Na kweli ukisoma Z-Report kwenye device yako, every thing is fine!. Kama biashara ilivyo ngumu bongo, mtu anakushushia kodi kutoka 18% hadi 10% the paper work is fine!, why bother?!.

Hatuna any centralized payment system, hivyo there is no way to trace incomes za watu au biashara kwa sababu tunatumia cash!. Nimebeba boks UK enzi za £ 4.50 per hour!, ile siku Lady Di anafariki, wife alilia sana, akashauri nisiende job, sikupiga simu kuwataarifu nikihesabu huu ni msiba mkubwa wa taifa. Kesho yake naripoti, job, naambiwa nimekuwa fired, kwa no show, nikaambiwa nitalipwa 2 hours nilizofanya kazi kabla zijapata taarifa ya kuwa fired!, amini usiamini, niliandikiwa cheque ya £ 9!, wakati huo wanaocash cheques za illegal workers ni Wanaigeria, ilikatwa kodi, na wanakata chao!, I don't even remember niliambulia nini!. Kwa nini Tanzania tunalipa cash?, wanaokatwa kodi ni watumishi tuu walio katika payroll, vibarua wote na sekta binafsi tunalipa cashi na hakuna kodi yoyote ya income inaingizwa serikalini!, wenzetu wanajisikia proud kulipa kodi, sisi tunajitahidi kukwepa kodi ile mbaya, tena wengine ni makampuni makubwa yenye heshima kwenye jamii na kutoa misaada lukuki!, kumbe pia ni njia ya kuongeza expeses na kukwepa kodi, huku kwenye mahesabu yake eti kila siku yamekuwa yakipata hasara, kama Barrick wanavyodai they operate on losses!.

Nikimalizia na hili la Dependant Syndrome, tunatumia kuliko tunachokusanya kwa sababu Mjomba kila siku hutuletea lile kapu kubwa la mapesa "busket funding" na kutumwagia kwenye budget yetu kwa jina la "Gneral Budget Support!", sasa kama mjomba yupo na kila siku yupo!, why bother kupunguza matumizi huku mifweza ya bure ipo?!.

Wakati fulani nikitumika kwa mkoloni wetu, nikapewa task ya kufuatilia kama ni kweli, serikali imepunguza matumizi ya vitafunwa, warsha, semina na makongamano, ikiwemo kutonunua tena Mashangingi!, nikaripoti kuwa ni uwongo!, ila serikali lazima iwaeleza hivyo nyinyi wafadhali ili msije kughairi kuendelea kutuma lile kapu!. Kusema ukweli na Mungu atanisamehe, niliichongea nchi yangu kwa mkoloni wetu kwa kumweleza, nimeshuhudia kwa macho yangu a new fleet of State Cars sasa sio mashangingi tena, ni BMW X5!, na yale mapikipiki ya kupendezesha ni BMW za 1100 cc!, huku huku mwendo wake mwisho ni 5 KPH!, Si ni bora tungenunua tuu za Mchina tena kuwaomba watuwekee speed mwisho ni 30 tuu!.

Sio siri, ukifanya kazi kwa mzungu, kama sio mzalendo, unaweza kabisa kuiuza nchi yako!, baada ya kuripoti, nikaambiwa niandike opinion yangu, nini kifanyike ili kuishinikiza serikali yetu kupunguza matumizi!. Unajua nilishauri nini!, nilishauri "Stop the General Budget Support!" ili tutumie kile tuu tunachokusanya!. Du!, mama balozi alishtuka sana!, nikaitwa kwa round table discussion, wakasema tukisimamisha, wagonjwa mahositalini watakufa kwa kukosa dawa!, alimu itashuka kwa kukosa vitabu!, na maendeleo yatashuka, kwa kukosa fedha, kwa kuwa kumbe fungu lote la maendeleo, linatoka kwenye lile Kapu!, kila siku Magufuli anajitapa tunajenga mabarabara!, kumbe ni hela za mjomba!. Nkamjibu mama Balozi, kama mnatupatia fedha na mnashuhudia tukizitumbua, huku mnaendelea kutupa na tunazitumbua, hivi lengo lenu la hii misaada kweli ni Watanzania wasife, au tuendelee kuwa dependants, kila siku tumtume rais wetu akatembeze bakuli, hadi kuaibishwa kwa kuhongwa suti!. Why help mtu ambaye hajisaidii mwenyewe?!. Kikao kilivunjwa ila nilijifunza, kumbe sio kila misaada tunapewa ili kutusaidia, tunasaidiwa ili tuendelee kutegemea misaada!, na sasa ndio maana hata gesi yetu, inabidi tuwape bure kwa kukumbuka fadhila!. I fear the Greeks, especially when they bring gifts!",

Pasco.
 
Good idea
deni ni mzigo tena sana. Debt repayment inachukua fedha nyingi sana hivyo inarudisha nyuma maendeleo
 
Wakuu nasDaz na Pasco,

Asanteni sana kwa kushiriki na pia kwa michango yenu mizuri; nitarudi kujadili hoja zenu kwa kina;
 
Economically, up to 60% of GDB-to-Debt Ratio is acceptable.
Accepted in which context? did you follow my discussion on post number moja on why a high ratio doesn't necessarily mean kwamba an economy is in danger of defaulting/or how historically countries with ratios way below 60% ndio zimekuwa defaulting the most?

...If, there's steady economic growth, then hapana haja ya kuliogopa Deni La Taifa provided the funds zinakuwa channeled kunakotakiwa.

Ningependa kujadili hili la kasi ya kukua kwa uchumi kwani nalo wanasiasa wanalitumia sana kujenga hoja kwamba uchumi wetu ni wa mafanikio makubwa sana, hasa kutokana na ukweli kwamba kwa miaka karibia kumi na mbili MFULULIZO, average growth ya GDP kwa mwaka imekuwa karibia 7%; Katika mazingira ya kawaida, hii ni kasi kubwa sana, na kwa mataifa yaliyoendelea na yaliyojipanga kitaasisi, even a sustainable economic growth of 3% a year kwa miaka kumi mfululizo impact yake katika maisha ya wananchi itakuwa ni kubwa mno!! Watafiti wa worldbank waliwahi jadili huko nyuma kwamba iwapo nchi maskini inafanikiwa kuwa na wastani wa 7% and up kwa mwaka in terms of economic growth - sustainably nadhani for at least ten years?, basi nchi hiyo itafanikiwa kufikia MDGs; Leo hii MDGs hazipo mbali from expiry date huku mengi ya malengo yake yakiwa very much behind; Ni majuzi tu hizi IFIs zimefanya revision of some sort kwamba umaskini lengo ni kuutokomeza by 2030, sio tena 2015!!;

Nikirudi kwenye hoja yako kuhusiana na steady economic growth na jinsi gani inasaidia kupunguza hofu ya deni la taifa provided funds zinakuwa channed kunatotakiwa, you might have a point lakini umeacha hoja yako muhimu ikining'inia hasa kutokana na kutojadili uhusiano uliopo kati ya economic growth (GDP) na channeling of funds huko unaposema kunakotakiwa; Je unaweza kufafanua kidogo ulikuwa na maana gani?

Vinginevyo - high economic growth ambayo Tanzania tumekuwa 'tuna-enjoy' kwa miaka zaidi ya kumi mfululizo (average of almost 7% a year since the year 2000), have not led to elimination of poverty in any substantial way kwani viwango vya umaskini nchini ten years ago na leo hii ni kama havina tofauti yoyote meaningfully, licha ya a steady economic growth throughout the period; Why is it so? Ni kwa sababu economic growth haijatokea in sectors ambazo maskini au watanzania walio wengi earn their daily bread, bali kwenye sekta ambazo wawekezaji na washirika wao kwenye utawala ndio wana earn their daily bread; In other words, economic growth in the past ten years or so did not happen in the agricultural sector, ufugaji or rural areas where majority of the people (the poor) reside; or simply, such growth did not involve labour provided by the poor, hence hawajawa beneficiary of the income generated by such growth; Yet, ni hawa hawa maskini ambao wingi wao, unyonge wao, ujinga wao na rasilimali zao ndio zinawekwa rehani kuipatia nchi mikopo mikubwa mingine ikiwa ni kwenda kwenye miradi ya ovyo kabisa kunufaisha watawala fulani fulani na washirika wao, mikopo ambayo katika suala zima la public finance, inakiuka kanuni mbili nilizojadili awali - The Golden Fiscal Rule & The Sustainable Investment Rule. Lakini pamoja na hayo yote kukiukwa, walipaji wakuu wa madeni haya yasiyowahusu moja kwa moja wataendelea kuwa ni hawa hawa maskini/wakulima na wafugaji pamoja na vizazi vyao vya baadae;
 
Mkuu Pasco,

Nashukuru sana kwa mchango wako bandiko namba saba, lakini vile vile ushauri wako kuhusiana na mimi kwenda chuo kufundisha haya; naomba nikueleze tu kwamba nafanya hayo hivi tunavyoongea kwani kwangu mimi chuo kikuu ni mitaani ambapo kumejaa vijana wanao ishi katika maisha ya tabu katika nchi hii yenye neema nyingi, na wasiokuwa na uelewa wa masuala ya uchumi hata katika mambo ya msingi kabisa;

Nikianza na experience yako kuhusiana na suala la ukwepaji kodi, kwa kweli ni ya kusikitisha sana; hakika, tatizo letu kubwa has to do with the leakages in the system, nadhani matumizi ya neno deficit ni makosa kwetu; tutumie neno fiscal leakage or budget leakage, not budget or fiscal deficit; deficit hatuna, ni ya kujitengenezea wenyewe!!

Vinginevyo kutokana na kuzidi kupungua kwa fedha kutoka kwa wahisani to finance bajeti zetu katika muktadha wa crisis in the eurozone na continuing instability mashariki ya kati, kwa viongozi wowote wenye uzalendo na nchi yao, priority ingekuwa katika kuongeza mapato ya serikali kupitia kodi na vilevile proper management ya public resources kama nilivyojadili katika muktadha wa golden fiscal rule & sustainable investment rule; Vilevile, kwa viongozi wazalendo, maeneo mengine muhimu ambayo yalitakiwa kupewa kipaumbele ni pamoja na kuachana na usanii wa tax exemptions, kudhibiti tax evasion, na pia to formalize the informal sector kwa kuwapatia nyenzo na uwezo ili nao waingine katika mfumo rasmi wa uzalishaji, hence kuchangia zaidi katika GDP na revenues from taxes;

Hoja yako kuhusiana na dependency syndrome naiunga mkono; Kwa kifupi, kinachoendelea ni kwamba tyrants love aid, and they can hardly survive without it!! Na ikiwa lengo lako ni kutafuta madaraka ya urais ili uwe tajiri au uishi maisha y akifarari kwa mgongo wa walipa kodi, lazima utakuwa ni mwizi tu na pia utalinda wezi; Sasa inapotokea kwamba wahisani wanakuwa so generous in terms of AID flows into your country, mungu akupe nini tena, kwani unacho hitaji ni kupita ka-mtihani kadogo tu cha wahisani kuonyesha kwamba fedha zitatumika ipasavyo, lakini pia kazi yako itakuwa ni rahisi sana iwapo utaweka rehani jasho la maskini na rasilimali zao (migodi, mafuta, gesi n.k); na muhimu pia – ugavana wa benki, uwaziri wa fedha na ukatibu mkuu wizara ya fedha, weka watu wako;
 
Mjadala wa bajeti ofisi ya waziri mkuu imejaa kulaumiana kuliko positive criticisms; pia pande mbili zinashindwa kutambua kwamba kuna baadhi ya mambo ambayo kila mmoja needs to cross the aisle kwani bipartisanship is obvious kwenye mengine wakiamua kupunguza supremacy ya politics katika uendeshaji wa nchi;

Ofisi ya waziri mkuu ina msimamo gani kuhusiana na kukua kwa deni la taifa na nini ni mikakati yake kupambana na hilo? Au suala hili halimhusu waziri wa mawaziri??

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mkuu Pasco,

Nashukuru sana kwa mchango wako bandiko namba saba, lakini vile vile ushauri wako kuhusiana na mimi kwenda chuo kufundisha haya; naomba nikueleze tu kwamba nafanya hayo hivi tunavyoongea kwani kwangu mimi chuo kikuu ni mitaani ambapo kumejaa vijana wanao ishi katika maisha ya tabu katika nchi hii yenye neema nyingi, na wasiokuwa na uelewa wa masuala ya uchumi hata katika mambo ya msingi kabisa;

Nikianza na experience yako kuhusiana na suala la ukwepaji kodi, kwa kweli ni ya kusikitisha sana; hakika, tatizo letu kubwa has to do with the leakages in the system, nadhani matumizi ya neno deficit ni makosa kwetu; tutumie neno fiscal leakage or budget leakage, not budget or fiscal deficit; deficit hatuna, ni ya kujitengenezea wenyewe!!

Vinginevyo kutokana na kuzidi kupungua kwa fedha kutoka kwa wahisani to finance bajeti zetu katika muktadha wa crisis in the eurozone na continuing instability mashariki ya kati, kwa viongozi wowote wenye uzalendo na nchi yao, priority ingekuwa katika kuongeza mapato ya serikali kupitia kodi na vilevile proper management ya public resources kama nilivyojadili katika muktadha wa golden fiscal rule & sustainable investment rule; Vilevile, kwa viongozi wazalendo, maeneo mengine muhimu ambayo yalitakiwa kupewa kipaumbele ni pamoja na kuachana na usanii wa tax exemptions, kudhibiti tax evasion, na pia to formalize the informal sector kwa kuwapatia nyenzo na uwezo ili nao waingine katika mfumo rasmi wa uzalishaji, hence kuchangia zaidi katika GDP na revenues from taxes;

Hoja yako kuhusiana na dependency syndrome naiunga mkono; Kwa kifupi, kinachoendelea ni kwamba tyrants love aid, and they can hardly survive without it!! Na ikiwa lengo lako ni kutafuta madaraka ya urais ili uwe tajiri au uishi maisha y akifarari kwa mgongo wa walipa kodi, lazima utakuwa ni mwizi tu na pia utalinda wezi; Sasa inapotokea kwamba wahisani wanakuwa so generous in terms of AID flows into your country, mungu akupe nini tena, kwani unacho hitaji ni kupita ka-mtihani kadogo tu cha wahisani kuonyesha kwamba fedha zitatumika ipasavyo, lakini pia kazi yako itakuwa ni rahisi sana iwapo utaweka rehani jasho la maskini na rasilimali zao (migodi, mafuta, gesi n.k); na muhimu pia – ugavana wa benki, uwaziri wa fedha na ukatibu mkuu wizara ya fedha, weka watu wako;

Mchambuzi i do not get it, why do you want to call it budget leakage. Is it a leakage from government coffers, or it is a leakage before quids gets into gov coffers? or the government is not collecting taxes?

Ukiangalia kwa undani nchi yetu kwa sasa haina mwelekeo. Kila siku huwa najiuliza as a country what are we doing to make us live better? Mtu wa kawaida ukiamka unajua kuwa leo nafanya kazi hii, kesho nafanya kazi hii na baada ya mwezi mmoja kitakuwa hiki. Lakini kwa serikali yetu ni vigumu sana kupata jibu simply because hakuna. Au angalia sehemu unayoishi sasa ilinganishe na miaka miwili iliyopita, na angalia itakuwaje baada ya mwaka, kama kutakuwa na mabadiliko.

There is still a lot can be done without depending on kutembeza bakuli, we can still collect more Taxes, we can have more revenue in our coffers, and we can do more for the development of our country. Lakini ukitaka uwe na pesa nyingi, kwanza inabidi usakanye kwa nguvu, pili usitumie hovyo, tatu unapotumia utumie katika maeneo ambayo yatukusaidia kupata nyingine. Tanzania hatufanyi yote.

Ukiangalia utaona kuwa sehemu kubwa ya mapato ya ndani yanakwenda kwenye current expenditure (mkono kinywani) na pesa nyingi sana zinakuwa misused. Kuna watu wanalipwa kupita kiasi na pasipo na ulazima, na kuna ubadhirifu mkubwa, wengine wanatumia ovyo sana raslimali za serikali bila uangalizi wa maana, kuna kununua magari ya ajabu mpaka unashgangaa, wakati huenda hata pikipiki inaweza kufaa. Kwa hili, labda naweza kusema ni ufisadi tu, sio leakage wala deficit. Deficit unaweza kuitengeneza kwenye karatasi kwa kupanga namba, kwa hiyo tukipanga namba vizuri tunaweza kuwa na surplus, or we can plug in all holes and do away with the leakage.

Kwenye hiyo bluu naona hapo umenena kweli, inabidi tuangalie hawa watu wanaotaka urais 2015, wanataka sifa tu na madaraka na kutukuzwa, au wana nia ya kweli ya kuiendeleza Tanzania. So far kati ya wanaotajwa sioni hata mmoja wao anaelekea huko.
 
Mkuu Bongolander,

Karibu sana katika mjadala,umepotea kidogo; naomba nijibu swali lako la leakages halafu ntarudia hoja zako nyingine muhimu baadae kidogo;

Umeliweka swali vizuri sana iwapo nina maana leakages kwa whatever collected au kwa vile un accounted for; nilichomaanisha ni kwamba ukiangalia circular flow of income in an economy, utaona main actors ni households, firms and government; kwa maana hii,whether the system is formalized or part of it remains informal, bado kuna circular flow income in the general economy; kama tunakubaliana na hili, it follows kwamba in the context of development planning,leakage ni fedha ambazo serikali imeshindwa kuzi inject into the budget by expanding the tax base esp kwa ku formalize zaidi uchumi by means of kuwapatia mitaji wananchi kibiashara on condition kwamba they register with brela and tra, pia by,minimizing tax evasion (ambayo ni kinyume cha sheria) na by minimizing tax exemptions (ambazo zinalindwa kisheria at times);mbali ya upande wa potential revenues nchini ambayo worldbank wanasema ni 21pct of GDP huku official data now shows its around 16pct wakati kiukweli its just above 10pct, hata zile zinazokusanywa na kufisadiwa nazo ni leakage in the context of budgeting development; in other words - if our starting point is the circular flow of income ambayo ipo with actors watatu as gvnt,households and firms, na this flow ipo regardless kuna formal and informal economy, blk mkt etc, the actual GDP should reflect totality ya haya yote, otherwise Waziri Mgimwa mwaka jana anaposema lengo ni kufikisha revenue collection kufikia 21% of GDP, if not attained si ni kwasababu leakages are greater than injections? Sina theoritical ground to support this thesis, so kama nimekosea, nisahihishe mkuu;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kwanza shukrani sana kwa kuleta suala la maana hapa jamvini, nyuzi zenye maudhui muhimu kama hii zimekuwa adimu siku hizi.

Naomba turudi kuzipitia "kanuni" hizi ulizozileta za usimamizi wa madeni ya umma na mahusiano yake na hali ya uchumi ya taifa. Mosi ni vyema tukajiridhisha ni kwa nini kanuni hizi zipo. Kanuni hizi zinatokana na nadharia ya uchumi mpana (macroeconomic theory) inayoainisha ya kwamba endapo kila kitu kitabakia katika hali yake (ceteris paribus), ongezeko la deni la serikali au nchi huchangia kupandisha gharama za ukopaji na riba jambo ambalo huathiri uwekezaji kutokana na kwamba taasisi za fedha huwa hazioni tija kukopesha wawekezaji binafsi na hivyo kupendelea kuwekeza kwenye dhamana za umma/serikali ambako faida huwa ni kubwa na uwezekano wa mikopo kufeli kuwa mdogo. Jambo hili tayari tumeshaanza kuliona kwenye minada mbalimbali ya dhamana za serikali ikiwa ni pamoja na wigo mpana wa riba za uwekezaji na ukopeshaji tunazotozwa watanzania na taasisi zetu za fedha (interest rate spread). Kanuni hizi za usimamizi wa madeni ya umma husema pia endapo uwekezaji wa mikopo hii hautokuwa katika miradi yenye faida linganishi na ile ya sekta binafsi (mara nyingi hii ni miradi ya maendeleo kama vile afya, elimu, miundombinu, teknohama, n.k)basi uwezo wa serikali kulimbikiza mitaji (capital accumulation) hupungua jambo ambalo huathiri ukuaji wa uchumi kutokana na kuwa mikopo haikuzalisha.
attachment.php

Nadharia hii ni ya kawaida sana na ni ambayo wanadamu wengi huitumia pindi tunapotaka kukopa sisi wenyewe hususani katika mazingira ya biashara. Mkuu, jambo ambalo linawafanya watunga sera wetu wajiamini katika suala hili la madeni ni kutokana na kwamba kitakwimu, uchumi wetu unaviashiria vyote vya afya njema. Ukiangalia kielelezo cha kwanza hapo chini utaona ya kwamba katika kipindii cha 2000-2013, pamoja na kwamba deni la taifa limekuwa likiongezeka toka mwaka 2008 (mstari mwekundu), uwekezaji nchini pamoja uwezo wa taifa kutengeneza ziada/akiba umekuwa pia ukiongezeka (mistari ya bluu na kahawia) jambo ambalo linalifanya taifa kuendelea kuwa ni mkopaji mzuri kwa maana lina uwezo wa kurejesha madeni yake. Kwa viashiria hivi taifa lina ziada ya ya rasilimali zinazotosheleza kama rehani. Jambo la kusikitisha ni taifa kushindwa kupunguza nakisi yetu ya mauzo ya nje (mstari wa njano) ambayo inachangia kupunguza uwezo wetu wa kuweza kuhimili misukosuko ya uchumi na pia kurejesha mikopo ya nje.

attachment.php

Mkuu ukweli ni kwamba ni hizi investments katika sekta ambazo ziko capital intensive kama madini, gesi na kwa kiasi fulani barabara ambazo zinasaidia kuleta mantiki ya taifa kuendelea kukopa na kuwa na uwezo wa kurejesha.

Pili, hofu zilizopo kutokana na ongezeko hili ya madeni, ni hofu halali kwani pamoja na viashiria vyote hivi mwisho wa siku sehemu ya madeni yetu yatalipwa na mimi na wewe kupitia kodi zetu jambo ambalo lina uhusiano wa karibu na namna jinsi mikopo hii tunvyoitumia. NI wazi kwamba hakuna mtu atakayekubali kukatwa kodi zaidi kurejesha mkopo ambao matumizi yake yalikuwa ni aidha kulipa mishahara, anasa au kujaza akaunti za wakubwa. Katika hili ni vyema wananchi kupitia wawakilishi wetu tukawa madhubuti katika kutambua nia ya mikopo, matumizi na usimamizi wake. Ni matumaini yangu kwamba mchakato huu wa katiba mpya utatumika vyema katika kuweka misingi ya matumizi ya rasilimali na mikopo ya taifa na sio kumwachia waziri mwenye dhamana uhuru wa kuamua.

Mkuu, nimeambatanisha vielelezo vingine viwili hapo chini vya nchi kadhaa hivi, je unaweza ukaona mahusiano kati ya madeni ya umma, viwango vya uwekezaji/akiba na hali halisi hivi sasa duniani? USA is an exception in this instance due to the dollar hegemony.
 
Attachments

  • tz.jpg
    tz.jpg
    36 KB · Views: 900
  • debt.jpg
    debt.jpg
    33.1 KB · Views: 47
  • savings.jpg
    savings.jpg
    33.6 KB · Views: 883
Nikirudi kwenye hoja yako kuhusiana na steady economic growth na jinsi gani inasaidia kupunguza hofu ya deni la taifa provided funds zinakuwa channed kunatotakiwa, you might have a point lakini umeacha hoja yako muhimu ikining'inia hasa kutokana na kutojadili uhusiano uliopo kati ya economic growth (GDP) na channeling of funds huko unaposema kunakotakiwa; Je unaweza kufafanua kidogo ulikuwa na maana gani?

Vinginevyo - high economic growth ambayo Tanzania tumekuwa 'tuna-enjoy' kwa miaka zaidi ya kumi mfululizo (average of almost 7% a year since the year 2000), have not led to elimination of poverty in any substantial way kwani viwango vya umaskini nchini ten years ago na leo hii ni kama havina tofauti yoyote meaningfully, licha ya a steady economic growth throughout the period; Why is it so? Ni kwa sababu economic growth haijatokea in sectors ambazo maskini au watanzania walio wengi earn their daily bread, bali kwenye sekta ambazo wawekezaji na washirika wao kwenye utawala ndio wana earn their daily bread; In other words, economic growth in the past ten years or so did not happen in the agricultural sector, ufugaji or rural areas where majority of the people (the poor) reside; or simply, such growth did not involve labour provided by the poor, hence hawajawa beneficiary of the income generated by such growth; Yet, ni hawa hawa maskini ambao wingi wao, unyonge wao, ujinga wao na rasilimali zao ndio zinawekwa rehani kuipatia nchi mikopo mikubwa mingine ikiwa ni kwenda kwenye miradi ya ovyo kabisa kunufaisha watawala fulani fulani na washirika wao, mikopo ambayo katika suala zima la public finance, inakiuka kanuni mbili nilizojadili awali - The Golden Fiscal Rule & The Sustainable Investment Rule. Lakini pamoja na hayo yote kukiukwa, walipaji wakuu wa madeni haya yasiyowahusu moja kwa moja wataendelea kuwa ni hawa hawa maskini/wakulima na wafugaji pamoja na vizazi vyao vya baadae;

Application of the two public finance "rules" notwithstanding, there is an inherent need to first appreciate the multidimensionality of poverty and second not to allow ourselves to get brainwashed by political rhetoric in relation to growth. Allow me to expand albeit briefly, for starters on the basis of the proclaimed guides on public finance, the use of loans in social spending such as education and healthcare seems to fall in line with the need to invest in aggregate units of production. However, as we all know there is a considerable lag in realizing returns to investment in human capital, in the case of education through the time it takes to fully train the labour force and in health through the time it takes to tangibly translate gains in say a vaccination programme or improvements in health facilities and care. That is one cannot expect to invest in education today and start reaping the rewards the next day, it may even take a generation for this to happen.

Secondly, growth figures widely reported tend to be nominal and do not take into account the debilitating effects of population growth and inflation. That is a nominal annual growth of say 8% is actually pittance and doesn't mean anyone else is better off if in that 12 month period the cost of living went up by 8 or more percent. Furthermore, growth shouldn't necessarily be assumed to lead declining poverty rates as there are finer issues related to distribution and welfare both of which are critical to the various dimensions of poverty (Atkinson and Lugo, 2010; Osberg and Bandarra, 2011). Kwa hiyo ndugu yangu it is high time we began to pay more attention NOT to the growth statistics rather where is this growth coming from.
 
Patpending,

Nitakurudia na hoja zako muhimu sana shortly, asante kwa mchango wako, hasa kwa kuhimiza juu ya tatizo la ignorance and arrogance miongoni mwa wanasiasa wetu waliopewa dhamana ya kutoa maamuzi ya kiuchumi lakini muhimu zaidi kuusimamia uchumi wetu;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mkuu bongolander,

Karibu sana katika mjadala,umepotea kidogo; naomba nijibu swali lako la leakages halafu ntarudia hoja zako nyingine muhimu baadae kidogo;

Umeliweka swali vizuri sana iwapo nina maana leakages kwa whatever collected au kwa vile un accounted for; nilichomaanisha ni kwamba ukiangalia circular flow of income in an economy, utaona main actors ni households, firms and government; kwa maana hii,whether the system is formalized or part of it remains informal, bado kuna circular flow income in the general economy; kama tunakubaliana na hili, it follows kwamba in the context of development planning,leakage ni fedha ambazo serikali imeshindwa kuzi inject into the budget by expanding the tax base esp kwa ku formalize zaidi uchumi by means of kuwapatia mitaji wananchi kibiashara on condition kwamba they register with brela and tra, pia by,minimizing tax evasion (ambayo ni kinyume cha sheria) na by minimizing tax exemptions (ambazo zinalindwa kisheria at times);mbali ya upande wa potential revenues nchini ambayo worldbank wanasema ni 21pct of GDP huku official data now shows its around 16pct wakati kiukweli its just above 10pct, hata zile zinazokusanywa na kufisadiwa nazo ni leakage in the context of budgeting development; in other words - if our starting point is the circular flow of income ambayo ipo with actors watatu as gvnt,households and firms, na this flow ipo regardless kuna formal and informal economy, blk mkt etc, the actual GDP should reflect totality ya haya yote, otherwise Waziri Mgimwa mwaka jana anaposema lengo ni kufikisha revenue collection kufikia 21% of GDP, if not attained si ni kwasababu leakages are greater than injections? Sina theoritical ground to support this thesis, so kama nimekosea, nisahihishe mkuu;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Mchambuzi ukweli ni kwamba baadhi ya mawaziri wetu wanaongea kisiasa na kutetea dosari zilizopo ndani ya mfumo wa budgeting . Sikufuatilia hotuba ya Mh Mgimwa, lakini sikubaliani na kauli kuwa leakages si kubwa kuliko injections. Leakages ni kubwa hasa tuliangalia vyanzo vya kodi ambavyo havijatumiwa, na tukiangalia matumizi mabaya ya revenue ambayo ni makubwa kuliko tunavyodhani, si lazima yawe zaidi kuliko injections lakini ni significant kwa kiasi cha kuweza kuwa kikwazo cha maendeleo.

Unajua viongozi wetu wanapenda kucheza na takwimu na kupuuza facts, kwa ajili ya kuonesha kuwa wanafanya kazi lakini inafact hawafanyi kazi. Kimisngi naona suala la bajeti bado sio bomu la kisiasa kwa waliomadarakani, kwa hiyo wanajua tu bajeti itajadiliwa kwa siku mbili au tatu na itapitishwa bila kupingwa, lakini suala la bajeti na jinsi tunavyomanage finances inatakiwa lingaliwe kwa makini zaidi.
 
Naam! Wakuu wote hapo juu heshima mbele.
Kuna vitu nimeviona hapa, Fiscal discipline, deficit, debt(internal and external), Revenue,GDP and Political will.
Ukiviangalia vitu vyote hivyo halafu ukasikia kuna mtu analinganisha nchi yetu na nyingine napata maradhi ya tumbo.

Nalitafutia muda kidogo ili nitie senti sumuni. Mada nzuri na muhimu sana.
 
Back
Top Bottom