Deni La Taifa: Wabunge, Wanasiasa Wachumi Na Wachumi Wanasiasa

Deni La Taifa: Wabunge, Wanasiasa Wachumi Na Wachumi Wanasiasa

Karibu sana kwenye mjadala mkuu nguruvi3, tunakuhitaji sana jamvini;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Bongolander,

Umeuliza swali la msingi sana uliposema I quote “... hivi huwa najiuliza what are we doing to make us live better?”

Bongolander, ni wanasiasa wachache sana ambao they do what it takes to make you and others pamoja na vizazi vyenu to live better; Believe me, it’s a mere fact kwamba majority ya wanasiasa wetu (CCM) wanafanya all it takes to make them and their families to live better at the expense of majority of Tanzanians ambao wingi wao, umaskini wao na rasilimali zao zinazidi kuwekwa rehani kutajirisha mabepari wetu uchwara nchini na washirika wao huko nje; Kuna mifano mingi ya kutoa kama ushahidi wa hoja yangu hii lakini kwa sasas nitatoa mmoja:

Pamoja na malalamiko mengi ya wananchi kwa muda mrefu sana kuhusiana na hali ya maisha kuzidi kuwa ngumu day by day; pamoja na tafiti nyingi sana za ndani na nje ya nchi kuonyesha jinsi gani uliberali mamboleo unavyozidi kuangamiza maisha ya walio wengi (hasa vijijini) kila kukicha; pamoja na vilio vingi sana kwamba kwa zaidi ya miaka ishirini, nchi imekuwa haina dira wala mwelekeo, na pamoja na hofu kubwa kuzidi kujijenga miongoni mwa jamii juu ya timing bomb la ajira ya vijana, misuguano ya kidini n.k, bado world bank wanathubutu kuja na publication titled eti “Tanzania on a staircase to heaven”.

Kwa maana hii, iwapo unaelekeza swali lako kwa wanasiasa walio wengi CCM (sio wote) pamoja na vibaraka wao huko nje, jibu lao kwa swali lako ni rahisi sana: they are doing all it takes to make them and their families live better, not you, me and the majority of Tanzanians, otherwise they wouldn’t dare to come up with such reports/or they wouldn’t agree with such statements from the worldbank. So according to them, the country is on course, na ndio maana wengi wao hawawezi kabisa kukuelewa pale unaposema serikali ya ccm imeshindwa kumwendeleza mtanzania wa kawaida au ukija na hoja kwamba nchi haina mwelekeo, ni kutafuta nao ugomvi kwani una maana gani wakati World Bank wanasema tupo on course???? Vipimo vyao na vya washirika wao kuhusiana na mwelekeo mzuri wa nchi ni high GDP growth rate (hawajui jinsi gani WorldBank/IMF wapo karibu kupoteza vita dhidi ya matumizi ya kigezo cha ovyo (GDP) kupima afya ya uchumi wa nchi maskini, na kigezo hiki kitafutwa au kurekebishwa muda sio jmrefu kwani kinazidi kukosa credibility, sasa sijui wanasiasa hawa watajificha wapi); Pia wengi wao wanajenga hoja juu ya jinsi gani investments in infrastructure inavyofanywa na serikali ya ccm huku wakisahau kwamba fedha nyingi zinazojenga mabarabara ni fedha za wahisani/mikopo;

Lakini the fact kwamba barabara zinajengwa zaidi kwa mikopo kuliko fedha za ndani sio tatizo, tatizo ni je – hizo barabara zina linkages gani na economic activities and livelihoods za majority of Tanzanians in their production and commercial spheres, has kutokana na ukweli kwamba wao ndio walipa madeni haya? Jibu ni hakuna cha maana; Barabara nyingi zinaendeleza the same colonial pattern – dendritic structure whereby zinafuata tu kule kwenye raw materials and resources na kuendeleza chota chota (ya madini na mazao) from the hinterland kupeleka bandarini for exports; Hakuna barabara za maana zinazojengwa kwenda kwenye processing facilities to add japo value kwenye malighafi hizi hence tuwe na exports zenye thamani zaidi lakini pia processing factories zitoe ajira katika maeneo husika; Pia hakuna barabara linking for instance Village A and Village B strictly based on their local needs, hasa on a trade and commercial end, na ikitokea zipo, ni bahati tu kwamba barabara husika inapita karibu ikitokea shughuli za chota chota ya madini na mazo katika maeneo mbalimbali ya nchi for exports;

Fine, one may argue kwamba exports zinasaidia nchi kupata foreign exchange earnings, but swali linalofuatia ni je, how much of these earnings go back to where it came from - vijiji vilivyokuwa maeneo ya migodi au jamii za wakulima wanaozalisha mazao ya biashara (chai, kahawa, korosho n.k?); Pia katika hili, ukiangalia our debt service ratio utaumia sana i.e. how much of our export earnings goes to pay debt;

Kama nilivyojadili kwenye bandiko namba mojai, wanasiasa wetu hawapendi kuangalia debt service ratio to determine ukubwa wa deni letu, wanapenda kuangalia Debt to GDP ratio; The former is useful kwa uchumi unaokopa kwa kutumia foreign currency (hasa dollars) and the latter ni useful for uchumi unaokopa kwa kutumia local currency (hence shillingi ya kitanzania); But the irony is – serikali yetu imeanza kukopa locally tena kwa kasi ya ajabu and the trend has been more towards local sources than foreign sources; So kuna umuhimu wa kuangalia beyond Debt to GDP ratio if we are really serious to determine ukubwa na athari zilizopo kuhusiana na deni la taifa huko mbeleni;

Nimalizie kwa kurudia tena on fiscal discipline pamoja na kanuni zake; Katika hili, lengo kubwa hapa ni kuhakikisha kwamba mikopo inatumika zaidi to ‘finance’ aidha – vitu ambavyo vitalipwa na kizazi hicho hicho kilichokopa, au kuhakikisha kwamba matumizi ya mikopo hiyo pia itakuwa na manufaa kwa vizazi vijavyo ili iwe fair kwao kuja kulipa baadhi ya mikopo itakayo wakuta miaka ya huko mbeleni; Kwa maana hiyo, ni muhimu kwa serikali yetu kuanza kupunguza allocation ya bajeti zetu kuwa kubwa zaidi katika matumizi ya kawaida (posho za wabunge na watumishi wa serikali, mishahara, procurement zinazoendeshwa na kampuni za vigogo n.k), na badala yake iwekeze zaidi mikopo yetu katika development – hasa kuendeleza vita alivyoanzisha mwalimu Nyerere vya kupambana na umaskini, ujinga na maradhi;

Vinginevyo tunajenga a timing bomb nyingine ukiachana na tatizo la ajira; the new timing bomb ni the fact kwamba miaka mingi baadae, watoto na wajukuu zetu watakuja kugundua kwamba mikopo iliyochukuliwa na babu zao matumizi yake ndio maghorofa na mahekalu masaki, mikocheni, mbezi beach; matunzo ya gharama kubwa ya marais na mawaziri wakuu wastaafu ambao walikuwa sehemu ya tatizo enzi za uongozi wao; Landcruisers V8 mbovu zitakazokuja rundikana pale ujenzi kama scrapper n.k, , halafu eti bado wao ndio walipe madeni husika na wakiandamana wapigwa mabomu?!

Let’s be fair to the future generations!!

Cc patlending, nguruvi3, pasco et al..
 
Kuna vitu nimeviona hapa, Fiscal discipline, deficit, debt(internal and external), Revenue,GDP and Political will.

Mkuu Mchambuzi, bandiko lako #22 ''limeninyang'anya'' sehemu kubwa sana ya mchango wangu.
Sipendi kurudia uliyoyasema kwa undani na ukweli, ninachotaka kusema kwa uchache ni kuwa ndani ya bunge letu asilimia 95 kwa mtazamo wangu hawawezi kuongelea na wala hawajui haya ''Fiscal discipline, deficit, debt(internal and external), Revenue,GDP and Political will''

Kilichobaki kwao ni kile ulichokisema 'take care of today tomorrow will take care of itself''.
Kwanza, bungalow pili watoto watasoma wapi huko nje n.k. haya mengine ni by the way.

Watu wanaposema eti tupo katika hali nzuri kwa deni la taifa ukilinganisha na mataifa mengine inachekesha sana.
Marekani, Japan, China n.k wapo katika vita ''currency war'' kila mmoja akifanya devaluation ya currency yake katika ku-encourage export na kuweka uchumi katika hali nzuri. Nchi hizi ukiangalia GDP yake, fiscal discipline, debt management, revenue collection and political will, hatufanani hata kidogo, leo tunachukua namba 47% na kusema tunalingana nao!!

Marekani ina mzozo ndani ya senate na congress kuhusu debt ceiling. Kwamba serikali iwekewe ukomo wa kukopa hovyo ili kuleta fiscal discipline. Mtakumbuka hili ni moja ya mambo yaliyopeleke marakani kupoteza AAA katika credit rating.
Sasa tunapodhani wao wana debt to 100+% ni mbaya zaidi yetu ni kichekesho kingine kutoka kwa bunge letu

Fiscal discipline ni dira ya uongozi wa taifa lolote linalojitakia mema.
Kwamba lazima utumie kile unachopata. Ukiangalia Australia, UK, Japan, USA n.k. serikali inayokosa fiscal discipline inaondolewa madarakani haraka.Hata kwa akili za kawaida tu, huwezi kutumia zaidi ya unachokipata ukawa salama.

Kwa nchi yetu fiscal discipline hicho kitu hakuna. Kwanza hakuna mtu anayejua tunakopa wapi na kwanini na kwamba mkopo huo una return gani directly or indirectly.

Si bunge wala wananchi kwasababu juzi upinzani bungeni umeeleza kuwa deni la taifa lina uwalakini kwasababu 640 billions are unaccounted for. Sasa zilikopwa kwa kutumia sehemu gani ya utawala endapo bunge linaloidhinisha matumizi halijui?

Mambo kama hayo nduiyo yanaleta deni la taifa (internal na external).
Hata ukiangalia internal debt taarifa za CAG zimeonyesha embezzlement ya hali ya juu sana.
Hakuna mtu anayekuwa responsible kwasababu hakuna political will.
Kwa kadri deni linavyokaa ndivyo linavyokuwa na hili linakuwa mzigo kwetu sisi walipa kodi na vizazi vijavyo.

Kw vile hatuna fiscal discipline hatuwezi kuwa na effective revenue collections.
Pasco ameeleza vema scenario ambayo nadhani sote tunaijua.
Kwakukosa revenue tunaishia kuwa na deficit katika bajeti.
Na ili kufidia deficit tunalazimika kwenda kwa wajomba tukipitisha bakuli.

Wajomba wanatupa msaada sasa ni miaka 50. Dambisa Moyo katika kitabu chake ameeleza vema jinsi misaada inavyotulemaza waafrika. Alitolea mfano wa Nigeria nchi yenye utajiri wa mafuta.
Akasema tangu mwaka 1960+ hadi alipoandika kitabu chake nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta imepokea zaidi ya dollar billion 360 za msaada. Akauliza kama misaada inasiaidia iweje basi leo Nigeria iwe na idadi ya watu masikini sana?

Ukweli huo unatugusa sana kwasababu kama misaada inalenga kutuondoa katika umasikini na utegemezi kwanini basi miaka 50 sasa hakuna hata dalili ya kuweza ku-balance bajeti yetu.
Kwamba, tunaweza kujihudumia kwa basic needs kabla ya msaada.

Hapa tunarudi katika fiscal discipline. Hatuna kitu hicho kwasababu haiwezekani serikali ilete bajeti ambayo hailingani na revenue halafu wabunge wakubali tu. Wanakubali kwa kuelewa kuna mjomba na si wao kutumia akili zao na uwezo wao wa kimamlaka kuhoji.

Fiscal discipline inatakiwa iangalie mambo mengi sana.
Kwa mfano, nini kinaongeza matumizi kuliko mapato? Ni kwanini mapato hayakidhi matumizi? Je kuna njia mbadala za kuongeza mapato. Je, tunawekeza katika sehemu zinazotoa return au tunawekeza politically.

Tukiangalia kwa uchache, matumizi ni yale yanayoihusu serikali.
Inakuwaje nchi masikini kama yetu iwe na matumizi makubwa ya serikali.
Mathalani, katika mkoa mmoja wenye wilaya 5 kuna mkuu wa mkoa 1, wakuu wa wilaya 5, wabunge zaidi ya 5, maafisa tawala n.k. achilia mbali maafisa wa idara,wote hawa wanaongeza gharama zisizo za muhimu kwasababu mkuu wa mkoa mmoja ambaye ni effective anaweza kufanya kazi za wakuu wa wilaya bila tatizo.

Tuna serikali kubwa sana katika ngazi ya taifa na kila mahali.
Kibaya zaidi ukubwa huo si wa ufanisi bali sehemu za kutoa shukrani.
Tumeona ukuu wa wilaya ukigawiwa kama njugu, mawaziri na manaibu lukuki n.k.
Gharama za uendeshaji ni kubwa mmno kutokana na matumizi yasiyo ya lazima.

Ukubwa tu wa serikali unakuwa ni sababu ya kutokuwa na balanced budget na hivyo kuongeza deni hasa la ndani.
Ni vivyo hivyo katika ukusanyaji wa kodi. Serikali imebaki na kundi la wafanyakazi ambalo halina ujanja mbele ya kodi.
Makundi mengine yanapewa loophole za ima kulipa au kutolipa na hakuna anayejali.

Nilisikitika sana mwaka jana waziri wafedha aliongelea kuongeza mapato kwa kutumia kodi za simu za mikononi.
Kwamba nchi iliyojaa neema na mito, maziwa na bahari, madini, na uoto mzuri wa asili bado inategemea kodi ya text message kupata mapato. Kama ubunifu utakuwepo basi ni wa kugundua aina mpya ya soda na sigara ili kuwekewa kodi

Sasa katika fikra za namna hiyo ni nani anayejishughulisha na fiscal discipline, debt reduction, GDP,budget deficit na reveue collections.

Hebu tutue hapa kwanza kabala ya kuendelea
 
Nguruvi3,
Asante sana kwa hoja zako zilizojitosheleza, umenena yote hasa kuweka framework ya kutusaidia kubaini kiini cha tatizo husika lakini pia njia ya kupata ufumbuzi; nitarudi muda sio mrefu;

Ila pia napenda ku share na wewe kituko cha mbunge wa mtera ndugu lusinde akichangia hotuba ya ofisi ya waziri mkuu leo asubuhi, amejenga hoja kwamba:

"Thamani ya fedha yetu dhidi ya sarafu nyingine itapanda iwapo tu tutatoa picha za wanyama na kuweka picha ya nyerere na karume tu";

It is as simple as that!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Bongolander,
Awali ulijadili kwamba

Kwenye hiyo bluu naona hapo umenena kweli, inabidi tuangalie hawa watu wanaotaka urais 2015, wanataka sifa tu na madaraka na kutukuzwa, au wana nia ya kweli ya kuiendeleza Tanzania. So far kati ya wanaotajwa sioni hata mmoja wao anaelekea huko

The issue is, politicians in Tanzania wanashindana kutafuta uongozi hasa ccm not so much to servve Tanzanians as to win positions for power and privilege; To make matters worse, viongozi kama vile mawaziri wengi wao are not appointed based on how they can better use their wisdom and experience kwa manufaa ya maskini, badala yake ni kama vile kabla ya kula kiapo wanaitwa pembeni na kuambiwa kwamba what is expected of them na CCM ni ignorance, stubornness and dishonesty; Tazama baadhi ya mawaziri wasomi bungeni wanavayoendesha mambo kwa viroja;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Nguruvi3,
Ila pia napenda ku share na wewe kituko cha mbunge wa mtera ndugu lusinde akichangia hotuba ya ofisi ya waziri mkuu leo asubuhi, amejenga hoja kwamba:

"Thamani ya fedha yetu dhidi ya sarafu nyingine itapanda iwapo tu tutatoa picha za wanyama na kuweka picha ya nyerere na karume tu";It is as simple as that!Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Mchambuzi, huyu ndiye tunategemea ajadili national debt, fiscal discipline n.k. Ndio maana nilikuambia kuna wakati nikisikiliza bunge huwa napata abrupt colic stomach upset
 
Nguruvi3,

Ningependa kujadili hoja zako muhimu kama ifuatavyo:

Kwanza naunga mkono hoja yako inayojadili jinsi gani bajeti zetu lack direction; tatizo hili ni matokeo ya nchi kukosa mwelekeo, hatuna dira inayotokana na wananchi, iliyoshibwa na kukubalika na wananchi; lakini bado viongozi wana hamasisha wananchi kuongeza bidii so as to face the future, but how can they face the future when they can't even face the facts?sera za maendeleo, maamuzi na justifications za vipaumbele kuhusiana na fedha zao - mapato na matumizi, sio tu kwamba wananchi hawashirikishwi,bali pia serikali haina muda wa kuwapatia wananchi taarifa za msingi;

Imekuwa jadi kwa bajeti zetu NOT to offer incentives ku boost growth in areas where majority ya watanzania practice their livelihood strategies kama vile kilimo, SMEs n.k; awali nilihoji GDP growth rate inayosifiwa na wanasiasa wa ccm hasa the fact kwamba kwa wastani in the past ten yrs ni kama 7% nikahoji je - hiyo growth ina linkages gani na majority ya watanzania in terms of OUTPUT, EMPLOYMENT, & distribution of INCOME na KEKI YA TAIFA? Hakuna kwa kweli, kwani the said growth isn't pro poor growth, na sidhani kama ina manufaa kwa zaidi ya 10pct of the population; growth isiyotokana na output ya majority, growth isiyotokana na input ya majority in terms of ajira, growth isiyopelekea increase in income to the majority is useless growth to the majority;Bajeti zote hasa kuanzia kipindi cha uliberali mamboleo zipo very far away from the socio-economic and ground reality kwani they don't address suala la pro poor growth;

Pia kuna suala la wanasiasa kupotosha takwimu za debt to GDP ratio, umejadili vizuri sana; msisitizo hapa ni kwamba, wenzetu currency zao zina nguvu sana na inapotokea wanahisi deni linaenda out of control, ni rahisi sana for them to devalue it kupitia inflation (printing money), tofauti na sisi ambapo most of our debt is in dollars ambayo inazidi kupaa relative to value ya sarafu yetu unless approach na mh. Lusinde kuondoa wanyama kwenye noti can work; vinginevyo hatuna uwezo sio tu to print dollars to devalue our debt but also we are suffering from poor export earnings kutokana na poor performance ya kilimo, misamaha mikubwa mapato ya madini, lakini pia the little dollars that we earn, most of it go to service deni hili la taifa; unakuta debt servicing ni kubwa kuliko hata allocation ya bajeti yetu kwenye sekta muhimu kama afya, elimu na nyingine zote zenye uhusiano wa moja kwa moja na maadui watatu wa maendeleo ya taifa letu - umaskini, maradhi na ujinga;ingawa ujamaa ulishindwa kutokana na uhaba wa fedha vis a vis surging population, but there was Political Will; where has this gone hasa nyakati hizi ambazo tupo in better position kupunguza kasi ya maadui zetu hawa watatu wa maendeleo?

Nitarejea for more...

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mchambuzi, huyu ndiye tunategemea ajadili national debt, fiscal discipline n.k. Ndio maana nilikuambia kuna wakati nikisikiliza bunge huwa napata abrupt colic stomach upset
Hawa ndio wachumi wanasiasa, na tofauti na wanasiasa wanasiasa wachumi kama mwigulu nchemba ni kama hakuna kwani wote ni useless kwa maendeleo ya wananchi walio wengi; huyu mwigulu angekuja humu na digrii yake ya uchumi daraja la kwanza ambayo ni kwa manufaa ya watanzania daraja ya kwanza, nadhani angetusaidia zaidi kutuelimisha wananchi nje ya daraja la kwanza, vinginevyo ni dhahiri hawezi thubutu kuja humu kujadili uchumi wetu kwa hoja;


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Hawa ndio wachumi wanasiasa, na tofauti na wanasiasa wanasiasa wachumi kama mwigulu nchemba ni kama hakuna kwani wote ni useless kwa maendeleo ya wananchi walio wengi; huyu mwigulu angekuja humu na digrii yake ya uchumi daraja la kwanza ambayo ni kwa manufaa ya watanzania daraja ya kwanza, nadhani angetusaidia zaidi kutuelimisha wananchi nje ya daraja la kwanza, vinginevyo ni dhahiri hawezi thubutu kuja humu kujadili uchumi wetu kwa hoja;Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Ngoja tumpe cc Mwigulu Nchemba.

Tuendelee na mada yetu
 
Nguruvi3,

Nimerudi kuendelea na mjadala; hoja yako nyingine hapo awali inahusiana na ripoti ya CAG revealing over 600 billion katika deni la taifa is unaccounted for; We should know that tyrants love aid, because it helps them stay in power and contribute to underdevelopment;

Half of world Aid has been reserved for africa, na Tanzania throughout tumekuwa one of the top recipients of Aid in the continent; Ndio maana sisi ni mmoja wa wadaiwa wakubwa, not only in Africa bali LDCs; Swali linalofuatia ni je - where has all aid gone? Majibu ndio hayo kwa CAG huku Dada yetu Moyo nae akielezea mambo rellevant to our situation kuhusiana na root cause ya matatizo yetu; imagine if this aid kwa miaka hamsini ingekuwa imeenda zaidi china au india, wangekuwa mbali zaidi ya walipo leo kwani its obvious kwamba for the past half century wamekuwa better in economic management, wamekuwa na more practical policies to tackle poverty na wanadhbiti rushwa kwa ufanisi kuliko sisi; na nchi hizi kwa pamoja zina population karibia mara tatu ya bara la afrika lakini hili kwao halijawa kikwazo kwani at the centre they put the people and political will;

Sisi we don't borrow wisely na ripoti ya CAG has revealed it all; mbali ya hilo, we careless kwani we loose millions of dollars kila mwaka kwenye export opportunities ambazo zinhetusaidia sana kukabiliana na debt; kwa mfano, serikali ya marekani ilikuja na mpango wake wa AGOA, ni wakulima wangapi Tanzania walifahamu uwepo wa opportunity hii? Sisi nadhani ni miongoni mwa nchi chache sana ambazo zimezembea sana kutumia fursa hii;wengine wanaweza kuwa na sababu zinazoeleweka kama instability n.k lakini sisi tulikuwa na kila sababu ya kuhakikisha majority of Tanzania who depend on kilimo kwa ajira na kipato wanapewa rellevant info, na pia kuwezeshwa kwa kila namna kwani ingesaidia export earnings ambazo ni muhimu to curb the debt;

Nikiwa bado kwenye suala la viongozi wetu kuzembea opportunities available for growth sekta ya kilimo, pia katika suala la Trade,zipo taarifa jinsi gani viongozi wetu walioenda cancun walishiriki kukwamisha negotiations zenye manufaa kwa taifa; kuna mtu mmoja senior worldbank Washington alinieleza jinsi gani alishangazwa na msafara wetu cancun kuwa miongoni mwa audience iliyopiga makofi to cheer kufeli kwa negotiations husika; viongozi hao wengine bado wapo madarakani na wanaendelea kupewa dhamana kuongoza vitengo vyenye uhusiano wa moja kwa moja na maisha ya watanzania;

Kwa kweli its obvious kwamba its the government and some officials who are beneficiaries of donors' generosity, its not the poor men and women in our country; tutazame wenzetu kama indonesia:

There is nothing accidental about their success; tofauti na sisi hasa baada ya Mwalimu kung'atuka, policy makers indonesia walianza with good housekeeping - hasa keeping government deficits and inflation in check, borrowing wisely, paying debt on time, na pia to act pre-emptively kukabiliana na changamoto zote kubwa, hasa kutokana na uwepo wa dira na vipaumbele ambavyo wananchi participated in the planning process;

The heart of the strategy ya wenzetu hawa ilikuwa ni kuwekeza sehemu kubwa ya mapato ya natural resources kwenye programs zinazolenga kuboresha rural growth na rural income; pgms hizi included strict family planning policies, programs za kuongeza productivity katika kilimo cha mchele kama vile extension services, rural irrigation, adult literacy, basic health care etc; walielewa mapema kwamba Human Capital ni matokeo sio tu ya jamii iliyoelimika bali pia yenye afya!Matokeo yake ikawa - indonesia ambayo awali ilikuwa moja ya importers wakubwa wa mchele duniani wakageuka sio tu self sufficient bali pia net exporters ndani ya kizazi kimoja tu;

Haya yote yapo ndani ya uwezo wetu, it doesn't need rocket science kuleta mabadiliko ya kunufaisha watanzania wa 2040 or 50, but it takes selfish leaders kama hawa wa sasa kutofanikisha haya; otherwise key is political will, uzalendo, fiscal discipline, among other things;

Changamoto iliyopo ni kwamba CCM is the magnet for the corrupt, not just the talented, especially youth ambao utendaji wa wengi wao ni kama umepigwa ufunguo wa ku operate in extreme ignorance, dishonesty and stubornness; watazame wengi waliopo bungeni na lumumba;

Nitarudi for more...

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mkuu Mchambuzi/wakuu wa jamvi
Kwanza shukran kwa bandiko zako mbili.
Nilitazama tatizo letu kwa njia nyingine. Tumeona kuwa lipo tatizo la kukusanya kodi, kwamba kodi zinatoka kwa wafanyakazi. Hata hao wafanyakazi wapo wasiolipa kodi kabisa. Hakuna system inayohakikisha kuwa kila mtu analipa kodi.

Wale watu wanaofanya kazi hasa katika sekta binafsi wamekuwa wanalipwa kwa cash. Hii ni kwasababu waajiri wanaogopa kulipa mambo kama ya NSSF n.k. kwahiyo sehemu kubwa sana ya private sector imekuwa inakwepwa kodi.
Kwa nchi za wenzetu, kile kitu kinachoitwa tax filing kwa kila mtu kina maana ya kuhakikisha kuwa kila mtu analipa kodi na kama sivyo basi ijulikane ni kwanini. Kwa mpango huo wamekuwa wanatumia social insurance number n.k.

Wao wanaweza kujua kiasi mtu alichotengeneza, kodi aliyolipa na amelipa wapi.
Katika nchi yetu hilo halipo. Hii si kweli kuwa haiwezekani,la hasa, ni kukosa ubunifu tu na hasa kukosa political will.

Sehemu nyingine ambayo ni tatizo ni ile ya matumizi. Ninashangaa sana kuona kuwa mradi uliotengewa fedha mwaka wa fedha 20xx/20xy na kwa uhakika wa kumalizika, mradi huo utatengewa pesa katika bajeti mbili au tatu zijazo.

Hapa kuna embezzlement ya hali ya juu sana. Haiwezekani kuwepo na makadirio ya mwaka X halafu mradi uvuke mwaka huo ukiwa haujakamilika. Tumeona hili katika kandarasi hasa za bara bara. Maana yake ni kuwa laxity ya serikali inahusisha mafao kwa baadhi ya watendaji.

Na sehemu nyingine ni kutokuwa na utaratibu wa udhibiti wa fedha. Hivi inakuwaje shirika, halamshauri au wizara xyz zipatikane na hati chafu ya matumizi ya fedha halafu waombe tena fedha zaidi ya hizo na watengewe?
Maana yake ni ile ile ya ''tumbo street''

Sasa hatua za awali kabisa za kurekebisha matatizo tuliyo nayo ni kwanza kuangalia fiscal discipline, pili kuongeza revenue collection, tatu kusimamia matumizi,nne kuweka wazi mikopo ya serikali, kuangalia wapi serikali iwekeze na kwanini na ukomo wa madeni''debt celing''
Haya yapo katika uwezo kabisa tena bila kutumia hata senti katika kuyatekeleza.

Swali ni je yanawekana mahali pasipo na political will?

Tukiangalia nchi kama za Asia ambazo zimepiga hatua, utaona wao walikuwa na vipaumbele katika baadhi ya mambo.
India ni wazuri sana katika teknolojia ya mawasiliano na hilo tu limekuwa sehemu kubwa sana ya uchumi wa nchi yao.
Malaysia wao wameamua kuwekeza katika kilimo na sasa wanatuuzia mawese ambayo yapo Kigoma.

FAO inakadiria kuwa kutakuwa na tatizo la uhaba wa chakula katika miaka 10 ijayo. Hivi karibuni tumeona ukame uliozikumba nchi za kiafrika na jinsi nchi hizo zilivyokuwa katika wakati mgumu sana.
Tunaona mfano wa Kenya kuja kununua mahindi kwa bei mbaya sana kwa magendo. Ndivyo ilivyo kwa somalia,Ethiopia na nchi nyingine.

Tukiwa na arable land nzuri hatujaweza kuwekeza katika kilimo eneo ambalo lingeweza sana kuipataia serikali fedha.
Hapa simaanishi serikali ichukue jukumu, nina maana serikali iweke mazingira mazuri ya watu kunufaika na kilimo.
Ndivyo serikali za dunia ya kwanza zinavyofanya. Fikiria kwanini wao watoe ruzuku kwa wakulima wao au wawe na protectionism ya producer wao.

Labda tujiulize kidogo, kwanini serikali iagize chakula wakati huo huo chakula kama mahindi yanavushwa kwenda nchi jirani. Kwamba ni rahisi zaidi kuagiza mchele au kusbiri mchele wa Japan kuliko mchele wa Kyale au Shinyanga.
Hapa ni ukosefu tu wa strategy. Kama kuna umakini serikali ingeweza kupata mapato hata bila kuwa na bwana shamba hata mmoja.

Sasa viwanda vichache vya kuanzia tumeua, kilimo tumeua! tumebaki na nini?
Matokeo ya haya ni kuwa importer na siyo exporter. Stability ya currency itatoka wapi.
 
Katika siku niliyotoa tongotongo kuhusu deni la taifa,basi ni leo......\

Mkuu Mchambuzi,kipindi ile cha mjomba Ben,ambapo alikua veery busy kulipa madeni,kuna rumors kwamba mzee Nyerere aliwahi kumwita mjomba Ben mpuuzi.....!!!!Sikuwahi kupata mantiki ya mzee hadi hii leo.Je,tukiacha kulipa haya madeni,kuna athari zozote??Je wanao'support bajeti yetu wataacha kutupatia pesa ya kutumbua??
Thanks for your Post!!:clap2:
 
Last edited by a moderator:
Heshima sana Mchambuzi

Ni bahati mbaya nimeiona hii thread leo sijui nilikuwa wapi pengine ungekuwa una mention baadhi ya wanajamvi ingesaidia sana kutokupitwa na nondo muhimu kama hizi.

Mambo yaliyozungumzwa ni mengi na yote yana mashiko makubwa.

Deni la taifa linazidi kupaa,ni kweli tena litazidi kuwa kubwa kama serekali hii ya CCM itafanikiwa kushinda uchaguzi wa mwaka 2015 kwa kishindo.Umezungumzia masuala ya fiscal discipline,ajira,afya,mfumo wa elimu na efficiency ya mahakama zetu na nk.

Ningependa kuanza na serekali yenyewe.Kwanza ukubwa wa serekali ni tatizo kubwa na litaendela kuwa tatizo ikiwa hapatakuwa na juhudi za dhati za kupunguza ukubwa serekali.Ukubwa ninaosema ni kuanzia serekali kuu (mawizara) hadi serekali za mitaa na maofisi ya wakuu wa wilaya na mikoa.Huko kote ukitembela utakutana na maafisa wengi wa serekali wasiokuwa na hata kazi za kufanya lakini wenye mishahara mikubwa ambayo inagharamiwa na Hazina yetu.Nafikiri ifike kipindi tuangalie katika wilaya zetu kama bado tuna haja ya kuwa na wakuu wa wilaya,wakurugenzi wa halmashauri,wabunge na meya katika wilaya moja.Piga hesabu Tanzania bara ina wilaya ngapi,fikiria kasi ya kuanzisha wilaya na mikoa ilivyokubwa.Gharama zote za kuendesha maofisi ya wilaya zetu zingeweza kuelekezwa katika miradi ya maendeleo sijui kama nitakuwa sahihi mishahara ya watumishi wa umma inamega % kubwa sana.

Tanzania nadhani ni nchi inayoongoza kwa kuwa na wizara nyingi jirani zetu waKenya wamefanikiwa kuweka katika katiba yao idadi ya mawaziri isiyozidi 22 sisi tuna mawari 60 ukichanganya na manaibu wao.Unapokuwa na idadi kubwa ya mawaziri uwezekano ni mkubwa kwa baadhi ya mawaziri na mawizara kutokuwa na kazi za kutosha lakini wenye kulipwa marupurupu makubwa sana ikiwemo nyumba usisahau tuliuza nyumba mawaziri,makatibu wakuu,majaji na maafisa wengi wa serekali wanapokosa nyumba wanakimbilia kuishi kwenye mahotel ya gharama kubwa.Bado kuna matumizi ya magari ya kifahari na safari za nje ambazo mabalozi wetu wangeweza kutuwakilisha vizuri.

(a) Wingi wa wizara hauna husiano na ufanisi badala yake unazidi kufyonza fedha ambazo zingeweza kupelekwa kwenye miradi ya maendeleo eg ujenzi wa majosho na mabwawa,ujenzi wa zahanati,ujenzi wa masoko vijijini,ujenzi wa barabara za vijijini.

(b) Uanzishwaji wa wilaya na mikoa mipya hauna uhusiano na utatuzi wa kero za mwananchi wa kawaida.Nimeshuhudia mara kadhaa ofisi hizo zikianzishwa kisiasa zaidi kutegemea na wakuu wetu wanatokea sehemu gani.Mahitaji ya wananchi wengi vijijini ni pembejeo kwaajili ya na kilimo si mashangingi ya wakuu wa wilaya,wafugaji wanahitaji majosho ya kuogesha mifugo yao,wanahitaji masoko ya uhakika na si majengo ya wakuu wa wilaya.Sasa unapotuambia unaanzisha wilaya mpya ili kusogeza maendeleo kwa wananchi nashindwa kuelewa wakuu wa wilaya wanamchango gani wa maendeleo kwa taifa letu !.

Serekali haina vipaumbele ambavyo vina uhusiano wa maendeleo ya wananchi wengi.Ikiwa asilimia 75 ya waTanzania wanaishi vijijini basi sera na mipango ya serekali ingelekezwa vijijini.Ungetegemea wakulima wa matunda wa mikoa ya Tanga,Morogoro na Pwani wangehakikishiwa soko zuri la mazao yao kwa kujengewa viwanda vya kusindika matunda.Serekali ingeongeza ajira na hakikisho la kodi lisiloepukika.

Hakuna serekali makini dunia itakayokubali usafiri wa reli ufe,hili linawezekana Tanzania TAZARA na reli ya kati zimeachwa kama watoto yatima.Sekta ya usafiri inayokazaniwa sasa ni barabara !.Ukitaka kusafirisha mizigo ya Uganda,Kongo,Zambia,Burundi na Rwanda kwa gharama nafuu zaidi ni lazima tutumie usafiri wa reli.Reli ya TAZARA ipo kwanini inasuasua.Kwanini hatuunganshi mikoa na wilaya zetu kwa reli.Jibu ni moja watawala wetu pamoja na kupanua ukubwa wa serekali na kujaza watumishi wa umma wasiokuwa na kazi bado haiwazi kuhusu Tanzania ya kesho na keshokutwa,wanafikiri habari za leo,wanawaza habari zao na familia zao.

Unapokuwa na aina ya uongozi wa aina hii usitegemee kama kuna siku watawaza deni la taifa,unapokuwa na mbunge anatamka ndani ya bunge kwamba shilingi yetu inashuka thamani kwasababu ya kukosekana picha ya Nyerere na Karume !.
 
Majany,

Karibu sana kwenye mjadala na asante kwa swali zuri hapo juu; sina majibu ya kujitosheleza lakini nina imani nguruvi3 na wadau wengine watachangia mawazo yao; mimi nitasema tu machache kama ifuatavyo:

Mwalimu alikuwa ni mmoja wa wapinzani wakubwa wa ukoloni mamboleo kwa vitendo. Neo-colonialism is the geopolitical practice ambayo hutumia vitu kama mfumo wa ubepari,utandawazi na cultural imperialism kuthibiti nchi maskini kijeshi au kwa dirisha la liberal democracy ili kuweza influence policy decisions za nchi maskini kwa faida ya nchi tajiri, hasa kiuchumi na kibiashara - pia tazama dhana ya dependency theory kuelewa zaidi suala hili;

Mwalimu Nyerere throughout uongozi wake na hata alipostaafu alisimamia alichoamini na kujaribu kulinda taifa letu dhidi ya ukoloni mamboleo kwa nguvu zote lakini sote tunaelewa kwanini alishindwa licha ya political will on his part;

Mwalimu Nyerere, licha ya kuonekana kushindwa Tanzania na azimio la arusha hivyo kuachia ngazi, nchi nyingine za dunia ya tatu zaidi ya sitini ziligundua right from the outset kwamba vision ya mwalimu ilikuwa very rellevant kwao wote, ndio maana miaka miwili baada ya kun'gatuka, ikaundwa south south commission na kina dr. mahathir mohamed waziri mkuu wa zamani wa malaysia, dr. Boutros ghali katibu wa zamani wa UN etc ambao wakamwomba Nyerere sio tu awasaidie kuunda tume bali pia awe chairman wa commission na akakubali; Maeneo muhimu ambayo tume hii iliyafanyia kazi ni pamoja na madeni ya mataifa maskini na madhara yake, high interest rates katika mikopo, bei ndogo kwa mazao yetu soko la dunia, protectionism katika masoko yao etc;Ni kutokana na kazi ya tume hii ndio lobbying against debt ikazidi kushika kasi na hatimaye nchi tajiri gave in na kuja na kitu kinaitwa Highly Indebted Poor Countries (HIPC) initiaties in mid to late nineties;

Nadhani hoja ya mwalimu kwa mkapa sasa unaelewa msingi wake hasa kutokana na ukweli kwamba HIPC ilipelekea misamaha ya madeni chini ya rais mkapa;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mkuu Ngongo,
Umegusia suala la mawasiliano hasa ya reli. Huko nyuma Mchambuzi ameeleza kuwa kuna uwekezaji usiozingatia principle bali utashi wa kisiasa. Yeye alisema bara bara zinazojengwa ni dendric badala ya pipeline la economy.

Katika mataifa yanayosonga mbele usafiri wa reli ni muhimu sana, utashangaa nchi kubwa kama Marekani na Uingereza bado zinatumia huku China ikija kwa kasi sana. Reli ni lifeline ya nchi zilizobahatika kuwa nazo. Sielewi kwanini reli ya kaskazini imekufa! hakuna sababu! Hata atakayesingizia mkonge na kahawa bado anapaswa kujiuliza malori yanayosafiri kila siku yanapeleka nini, mabasi yanapeleka nini.

Katika kipindi hiki cha EAC reli zile zingekuwa ni investment kwa nchi jirani. TAZARA ipo underutilized na reli ya kati iking'olewa mataruma na wawekezaji wa kihindi kwa kushirikiana na viongozi wa serikali kwa kitu kinachoitwa 10%.
It's abdurd, outrageous and insane.

Juzi kumezinduliwa mradi wa bandari ya Bagamoyo. Hii ya Dar ni underutilized and negleted.
Ukiangalia kwa makini ili bandari ya bagamoyo iwe effective na productive lazima iwe na link na railways ambazo zinaanzia Dar.Labda wanajamvi mniambie kutoka economic point of view the sustainability and viablility of Bagamoyo port.

Kuhusu ukubwa serikali, hili nalo tumeliongelea. Kwahakika hilo ni tatizo kubwa sana.
Unapokuwa na baraza la mawaziri kubwa kuliko nchi ya Ufaransa au Uingereza kuna tatizo.
Matokeo yake ni watu kutokuwa na kazi za kufanya na kujiingiza katika kupitisha miradi yao kama tulivyoona bandari.

Mkuu Majany, kelele za Nyerere zilikuwa kuhusu mataifa makubwa kutoa mikopo halafu kuchukua pesa nyingi kutoka mikopo hiyo. Mchambuzi ameeleza kuhusu south south commission na agenda zake.

Kwa ufupi alichokuwa anasema Nyerere ni kuwa badala ya kujaza mikopo kwa nchi masikini halafu kuchukua kwa mkono mwingine kikubwa zaidi ya walichotoa, nchi hizi zingetoa unafuu wa mikopo na riba au kufuta baadhi ya madeni.
Hili lingesaidia vinchi masikini vijenge uwezo wa kuweza kukopa baadaye na kulipa.

Sasa kwa upande wa Mkapa, yeye alikuwa analipa madeni kupunguza deni la taifa na riba zitokanazo.
Wakati hayo yakifanyika huduma za jamii na zile za kuwakwamua masikini zinakuwa zinazorota. Kwa maneno mengi baada ya kulipa deni tutarudi kukopa tena kwasababu hakuna uwezo uliojengwa ili kutuwezesha kuwa wakopaji na walipaji.

Ni kelele za akina Nyerere ndizo zilishtua wakubwa kwa kiasi fulani na kuja na HIPC ambayo ilitokana na mazungumzo ya Paris Club.

Tunaweza kutokubaliana kwa mambo mengi kuhusu Mwalim, lakini lazima tujiulize katika miaka zaidi ya 30 tangu ameondoka madarakani kuna mikopo gani ambayo imewekezwa kama yeye alivyofanya?

Hapa naomba kutoka nje kidogo ya mada na kuwa 'biased' bila kuudhi au kukirihisha mtu.
Nyerere alikuwa na Political will ndiyo maana project zake zililenga zaidi katika kuhakikisha tunajitosheleza kwa uchache na tunajiendeleza kutokana na nyakati.

1. Aliwekeza katika miundo mbinu. Hakuna miundo mbinu iliyojengwa au inayojengwa sasa ambayo haina blue print ya utawala wa Nyerere. Akawekeza katika vitu kama TAZARA, Reli ya Kaskazini n.k. ambazo leo zinabaki kuwa sehemu muhimu sana ya uchumi.

2. Akawekeza katika viwanda ili kuhakikisha kuwa kama hatuwezi kuuza ''AGOA'' basi tuuze kwa jirani. Ndivyo ilivyokuwa katika baadhi ya bidhaa za viwanda kama nguo, matairi, betri, maziwa kwa uchache.

Akawekeza katika kuhakikisha kuwa spea zinapatikana hapa zile za uwezo wetu, food proceesing industries n.k.
Yote yalihakikisha kuwa si tu yanakuwa na faida kiuchumi lakini yanakuwa na social impact katika vitu kama ajira.

Mazingira yanabadilika na hatutegemei hali ingebaki hivyo, lakini basi tulipaswa kuanzia alipoachia.
Sasa tumeua viwanda, miundo mbinu halafu tunakopa kuwekeza katika miundo mbinu ile ile n.k.

Nimalizie kwa kusema ili kuweza ku-tackle tatizo lazima kwanza tuanze na fiscal discipline, tupunguze leakage, tuongeze revenue kwa njia za kisasa na kitaalamu(tuache kutegemea kodi za bia na vocha za simu), tuwe na management ya kukopa na tuwe na uwezo wa ku-invest kwa kuona return iwe direct or indirect.

Tunaweza kabisa kwa muda mfupi,if and only if the ''political will'' will prevail.
 
Nguruvi3,

Napenda kujadili hoja zako za bandiko namba 31 kama ifuatavyo:

Kwanza ni kuhusiana na kukerwa kwako na tabia yetu sugu ya kuendelea kuagiza vyakula kutoka nje wakati tuna uwezo mkubwa tu wa kuwa net exporters wa mazao husika iwapo tutaamua; Nadhani utakubaliana nami kwamba moja ya sababu ya uwepo wa tatizo hili ni pamoja na ulaji mkubwa sana unaendelea katika mfuko wa ‘import support', vinginevyo tukianza kuwa self sufficient, mafisadi watakula wapi? Mbali ya suala la import support scheme, pia ni uzembe wetu katika ku - create economic and business linkages katika uchumi wa ndani; Huko nyuma nilijadili jinsi gani Serikali imepwaya katika hili ingawa inajisifia sana katika ujenzi wa barabara nchini;

Miradi ya barabara ina mapungufu mengi ukiachilia suala la fedha kuliwa kama ulivyojadili i.e. kila mwaka fedha za walipa kodi kutengewa fedha katika miradi isiyo kwisha; Mbali ya tatizo hili, miradi hii don't deliver towards the creation of perfect market information kwa wakulima in order to stimulate internal trade, badala yake, zinazidi tu kufungua our hinterland kwa faida ya mabepari wa nje kwa utaratibu ule ule wa kikoloni; Na ni utaratibu huu ndio unaleta ‘impressive growth' ya GDP ambayo haina manufaa kwa wananchi walio wengi kwani kwanza, kinachotoka hakirudi kwao, lakini pili, sehemu kubwa ya GDP growth haitokani na labour ya watanzania walio wengi bali capital intensive schemes kwenye migodi n.k, of which mapato ya kodi huko ni ya kusikitisha sana;

Pamoja na umuhimu wa Barabara hizi, the whole thing is not systematic, kwani kila inapotokea jamii Fulani fulani zinanufaika na barabara tunazojisifia nazo, basi ni aidha kwao kuna madini, mazao ya biashara au wanaishi karibia na maeneo ambapo wanakumbwa na bahati ya kuwa karibia na barabara kuu ambazo literally zipo kwa ajili ya ‘somba somba' ya mazao na madini kuelekea bandarini as raw as possible (not even processed suala ambalo lingetoa ajira kwa wanavijiji); Mfumo wetu wa barabara ni dendritic, na ndio maana hata market information nchini is still so imperfect kiasi kwamba, ni jambo la kawaida kwa mtanzania anayeishi dar-es-salaam kuwa na taarifa ya soko la Kigoma kuliko Mtanzania wa Tabora ambae yupo karibu zaidi, kuwa na taarifa juu ya soko la Kigoma;

Hoja nyingine uliyogusia inahusiana na madhaifu katika ukusanyaji wa kodi; Nakubaliana na wewe kimsingi katika hili; Kama ulivyojadili, tatizo kubwa ni kwamba we have a narrow tax base, hivyo kupelekea taifa letu kuendelea kuwa ‘taifa tegemezi'; Katikati ya mwaka jana (2012) Muungano wa taasisi za kidini Tanzania ulikuja na ripoti iliyotoa takwimu muhimu sana kuhusiana na mwenendo wa ukusanyaji kodi Tanzania; Kwa mujibu wa ripoti hii, 70% ya mapato yote ya Ndani yanatokana na Makampuni 400 tu nchi nzima, huku SMEs ziki account for the remaining 30%; Hii ni ajabu kidogo kwani kwa uelewa wangu, makampuni ya wawekezaji kutoka Afrika ya Kusini peke yake nchini Tanzania yanazidi makampuni 100; Ukiachilia mbali makampuni kutoka Afrika ya Kusini, yapo mengine mengi sana kutoka Kenya, India, UAE, Uturuki, EU, USA, Australia, na ukichanganya haya na mengine mengi ya wazawa ambayo ni beyond SME levels in terms of business turnover, Tanzania inatakiwa iwe na large tax payers way over 400; Nadhani sote humu tunafahamu many wealthy individuals (wazawa) wenye kuendesha biashara zenye turnovers beyond SME level (over Tsh 800 million kwa Mwaka) na wapo professional and successful kibiashara lakini hawalipi kodi kwa sababu mbalimbali ambazo baadhi yake umezijadili;

Vile vile umezungumzia suala la informal sector and taxation; kwa mujibu wa takwimu zilizopo, informal sector in Tanzania accounts for about 50% of GDP and about 70% of total workforce, yet it largely remains untaxed; Hili ni tatizo, na sina maana kwamba poor farmers and petty traders mijini waanze kutozwa kodi; Maana yangu hapa ni kwamba serikali makini inaweza kuwajengea uwezo wote hawa kwa kuwapatia incentives mbalimbali for growth and eventually formalize them hasa on condition kwamba they register na Brela na TRA kabla ya kusaidiwa katika hatua za mbele zaidi; Umakini ukifanyika, mimi sidhani kama watanzania hawa watashindwa to comply na sheria za kodi; Mkuu bongolander, katika hoja yangu ya awali kuhusiana na leakages in the circular flow of income nchini, hoja yangu ilikuwa katika muktadha huu;

Mkuu nguruvi3, kwahiyo upo sahihi ( at least kwa mtazamo wangu) kwamba idadi ya walipa kodi Tanzania ni ndogo kuliko our potential kwani kwa mujibu wa TRA, potential number ya walipa kodi Tanzania ni watanzania milioni 15 (kumi na tano), lakini actual tax payers to-date haizidi watanzania milioni mbili. Kwa maana hii, watanzania wenye uwezo wa kulipa kodi na ambao hawalipi kodi ni zaidi ya 85%; Nguruvi3, kwa mtazamo wako, tunageuzaje takwimu hizi ili walipa kodi Tanzania wawe angalau hata 50% ya watanzania wote wenye uwezo wa kulipa kodi na tuweke targets zipi na kwa vigezo gani?
 
Mkuu Ngongo,

Karibu sana katika mjadaal; Samahani kwa kuto tag wadau mbalimbali kwani mara nyingine huwa naona kama ni kuwaletea usumbufu kwani mtu ukiwa na interest, aidha you tag/subscribe user unayemfuatilia ili akiweka posts upate taarifa, au unatembelea tu threads mbalimbali kwa wakati wako; Pengine sipo sahihi katika mtazamo huu, lakini next time nitajitahidi kurekebisha hilo; Lakini all in all, haujachelewa katika mjadala, ndio kwanza tupo ukurasa wa pili, so karibu sana;

Katika bandiko lako namba 33, umejadili mambo kadhaa muhimu sana ambayo ningependa kuingia moja kwa moja kuyajadili kama ifuatavyo:

Kwanza ni suala la loss of focus ya serikali yetu katika kuelekeza resources zilizopo towards rural development; Hili ni tatizo kubwa sana ambalo Mwalimu aliliona mapema sana na kuhimiza juu ya umuhimu wa kuendeleza vijiji kwani sio tu kwamba huko ndio majority ya watanzania wanaishi bali pia, (1) Nguvu kazi kubwa ipo vijijini kupitia kilimo i.e. 70% of the work force in Tanzania (2) wanavijiji ndio wazalishaji wakuu wa taifa letu ambao wanatulisha vyakula mijini na pia wanatusaidia kupata mapato ya fedha za kigeni tunazotumia to import oil, machinery, mashangingi, kulipa mishahara ya wabunge na watumishi wa serikali n.k; Miaka ya 1960s, Nyerere alipata kusema:

["…nor would borrowing help us. Whether it is used to build schools, hospitals, houses or factories etc, it still has to be repaid. Where, then shall we get it from? We shall get it from the villages and from agriculture…If we are not careful we might get to the position where the real exploitation in Tanzania is that of the town dwellers exploiting the peasants"]

Nadhani it is fair to say kwamba scenario hii ndio inayoendelea nchini na serikali yetu keeps on entertaining it, ndio maana upinzani ukienda vijijini na kufungua macho maskini, the wave of change inaitikisa sana CCM…

Pili, umejadili suala la big government; Naunga mkono hoja; Wapo baadhi ya wana CCM wanaojaribu kutetea hoja hii lakini as not only a matter of fact, bali also matter of principle kwamba the bigger the government, the more it has to tax people in order to operate; that's the bottom line; Kwahiyo link baina ya big government na poverty reduction kwa kweli is very hard to establish, hasa katika nchi maskini kama Tanzania; Tukiachilia madhara yake kwa mlipa kodi in terms of more taxes, pia yapo madhara mengine ambayo wengi huwa wana overlook kama vile:


  • Kwanza, a larger government inaongeza michakato, hasa ya bureaucracy to get things done kwani wanaosimamia kwa mfano utekelezaji wa sera na miradi ya maendeleo wanakuwa ni wengi zaidi tofauti na mazingira ambayo kunakuwa na watu wachache; Wewe nadhani pia na mdau mwingine mmejadili suala la wakuu wa mikoa na utitiri wa wakuu wa wilaya katika usimamizi wa sera na miradi ya maendeleo;
  • Pili, a larger government pia implies kwamba fedha nyingi zinachukuliwa kutoka katika miradi muhimu ya maendeleo ili kwenda to support spending kama vile mishahara na posho; nah ii hufanyika bila hata ya kufanya analysis ya opportunity costs;
  • Tatu, the larger the government, the more the rules and regulations kwa wananchi to follow, suala ambalo linaongeza red tape; Red tape is what chokes maendeleo mengi sana nchini, kwa mfano, ili mzawa kuanzisha biashara (SME) bado kuna so much red tape kiasi kwamba kwa wengine wanaona it's not worth it be formalize as an SME, suala ambalo linachangia sana ukwepaji kodi; SMEs ni backbone ya uchumi wowote lakini wanasiasa wetu kwa hili wapo more rhetoric kuliko walking their talk; Its such an irony kwamba viongozi wetu ambao wali embrace uliberali mamboleo na azimio la Zanzibar kupisha private enterprise kwa mbwembe, leo hii hao hao have become anti – business, especially in terms of creating a conducive environment for SMEs to flourish ili zitoe mchango katika taifa in terms of employment, output and tax revenues;
Suala la tatu na la mwisho ulilojadili linahusiana na Miundombinu, hasa ya reli; There is no doubt kwamba kuna a direct link baina ya miundo mbini (infrastructure) na economic growth, hasa reli, barabara, viwanja vya ndege na bandari na nguruvi3 on post no.35 amelijadili vizuri sana; Kwahiyo link hii kati ya infrastructure development na economic growth haina mjadala; tatizo langu linakuja kwenye suala la miuondo mbinu ya barabara ambayo ujenzi wake haulengi sana kuinua uchumi wa ndani bali export economy kama nilivyojadili awali; Lakini mbali ya hilo, wanasiasa wa CCM wanaojimwagia sifa kuhusiana na ujenzi wa barabara mbalimbali wanasahau kitu kimoja:

  • Pamoja na umuhimu wa barabara on economic growth and poverty reduction, suala hili sio open ended kama wana CCM wengi wanavyodhani kwani kuna optimum level; Nitafafanua:
Barabara is an important input in the aggregate production katika uchumi wa nchi husika lakini it comes at a cost – a reduction in the investments of other important capitals – hasa HUMAN CAPITAL, ambayo ni ELIMU na AFYA; These two types of Capital actually ni pre-requisite for other forms of capital kama barabara kuwa na tija katika taifa, hasa in the context of poverty reduction; Kwani bila ya kuwa na producers wenye skills, elimu na afya bora, hawawezi kuwa in a position ya kuzalisha mazao bora, kwahiyo hizo barabara zitaishia tu kusafirisha "BORA MAZAO", na sio "MAZAO BORA";

In the short run, tutaona increase in exports n.k lakini over time, washindani wetu huko nje ambao wanazalisha mazao bora kutokana na jinsi walivyowekeza katika afya na elimu (Human Capital), watatushinda katika soko kwa vigezo vya ubora wa mazao, hivyo kupelekea rural incomes to decline over time; Kwahiyo pamoja na umuhimu wa barabara zinazopigiwa debe na serikali, ni muhimu kina magufuli et al wajue kwamba this comes with a cost especially kutokana na tabia yao to deal na suala hili kama ni open ended badala ya kuwa na optimum levels vichwani mwao; Ni muhimu kwa wabunge wetu wenye kuguswa na hali ya umaskini Tanzania, kulitazama hili katika mijadala ya bajeti huko bungeni;

cc Nguruvi3, Bongolander, majany, Zakumi, et al
 
Mkuu Mchambuzi nashukuru kwa huu uzi ambao unatufikirisha. Nimetumia muda kuusoma japo kwa bahati mbaya sijasoma post nyingi za wachangiaji. Nimesoma rules za investment.

Mkuu labda kitu kimoja ambacho tunamiss kwenye hii mikopo ni kujua ni wapi expenditure zinafanyika. Inakuwa kama tunawakopea watu kwa kuwa expenditure kubwa hazifanyiki hapa na matokeo yake ni kwamba haturealize multiplier effect ambayo tungeitegemea. Kwamba tunakopa mamilioni ya dollar lakini wanaokuja kufanya kazi kama za kandarasi kwenye barabara na miradi ya maji ni hao hao ambao wanatupatia mikopo/misaada na matokeo yake ni pesa kurudi kwao. Watu wetu wanalipwa kidogo sana; wao wanalipwa mamilioni na vifaa vingi vinatoka kwao. Kwa maana nyingine kama umekopa dollar 100 basi huenda tunabaki na dollar 1 zingine 99 zinarudi ughaibuni. Hapa inatakiwa tuwe na uamuzi wa makusudi kabisa kuhakikisha kwamba tunabakisha pesa za mikopo hapa nchini.

Hapa ndipo ninapokubaliana na wazo la Waziri Magufuli kwamba wazawa waungane kujijengea uwezo waweze kupata kandarasi kubwa za barabara. Hii ikifanikiwa itasaidia kuleta multiplier effect kubwa nchini kwa mikopo. Mfano kama kampuni ya Tanzania ndiyo ingekuwa inajenga miundo mbinu ya magari yaendayo kasi (mara haraka hata sijui ipi sahihi) basi pesa za ule mkopo ninaousikia kwamba unatoka benki ya dunia zingebaki hapa lakini miundombinu hii inajengwa na kampuni ya ujerumani hivyo pesa zitaenda kuujenga uchumi wa ujereumani.

Hilo na Magufuli linaweza kuwa limechelewa lakini ni muhimu. Hili linatakiwa lifanyike kwa makusudi kwenye sekta zote kuanzia kilimo, ujenzi, nk. Wenzetu wa Malaysia na Singapore walifanya hivi na uchumi wao kuinuka.

 
Majany,

Karibu sana kwenye mjadala na asante kwa swali zuri hapo juu; sina majibu ya kujitosheleza lakini nina imani nguruvi3 na wadau wengine watachangia mawazo yao; mimi nitasema tu machache kama ifuatavyo:

Mwalimu alikuwa ni mmoja wa wapinzani wakubwa wa ukoloni mamboleo kwa vitendo. Neo-colonialism is the geopolitical practice ambayo hutumia vitu kama mfumo wa ubepari,utandawazi na cultural imperialism kuthibiti nchi maskini kijeshi au kwa dirisha la liberal democracy ili kuweza influence policy decisions za nchi maskini kwa faida ya nchi tajiri, hasa kiuchumi na kibiashara - pia tazama dhana ya dependency theory kuelewa zaidi suala hili;

Mwalimu Nyerere throughout uongozi wake na hata alipostaafu alisimamia alichoamini na kujaribu kulinda taifa letu dhidi ya ukoloni mamboleo kwa nguvu zote lakini sote tunaelewa kwanini alishindwa licha ya political will on his part;

Mwalimu Nyerere, licha ya kuonekana kushindwa Tanzania na azimio la arusha hivyo kuachia ngazi, nchi nyingine za dunia ya tatu zaidi ya sitini ziligundua right from the outset kwamba vision ya mwalimu ilikuwa very rellevant kwao wote, ndio maana miaka miwili baada ya kun'gatuka, ikaundwa south south commission na kina dr. mahathir mohamed waziri mkuu wa zamani wa malaysia, dr. Boutros ghali katibu wa zamani wa UN etc ambao wakamwomba Nyerere sio tu awasaidie kuunda tume bali pia awe chairman wa commission na akakubali; Maeneo muhimu ambayo tume hii iliyafanyia kazi ni pamoja na madeni ya mataifa maskini na madhara yake, high interest rates katika mikopo, bei ndogo kwa mazao yetu soko la dunia, protectionism katika masoko yao etc;Ni kutokana na kazi ya tume hii ndio lobbying against debt ikazidi kushika kasi na hatimaye nchi tajiri gave in na kuja na kitu kinaitwa Highly Indebted Poor Countries (HIPC) initiaties in mid to late nineties;

Nadhani hoja ya mwalimu kwa mkapa sasa unaelewa msingi wake hasa kutokana na ukweli kwamba HIPC ilipelekea misamaha ya madeni chini ya rais mkapa;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Asante sana Mchambuzi,angalau naanza kumuona bwana Ben katika jicho la tatu....!!!!Kweli kuna tatizo hapa!!:tape2:
 
Kimbunga,

Karibu sana katika mjadala; hoja zako hapo juu ni very compeling; Kuna two main arguments supporting nchi kukopa - political and economic arguments:

Nikianza na economic argument for borrowing ni kwamba borrowing is desirable as long as the rate of return on the said investments exceeds the cost of capital; investments hapa again maana yake ni zile kanuni za fiscal discipline kwamba mkopo lazima utumike zaidi on investments katika sekta zenye direct impact kwa maisha yalio wengi kama vile afya, elimu, kilimo, sio kutumia mikopo kwa ajili ya matumizio ya kawaida (mishahara na posho za watumishi wa serikali, wabunge, procurement deals za kampuni za wakubwa etc);

The second argument supporting borrowing ni political ambayo inasema kwamba - faida za mikopo will be felt with the current generation while mzigo wa kulipa madeni utabebwa na kizazi kingine; debt crisis ya Argentina ni mfano mzuri wa jinsi gani political argument ilitumika kufaidisha kikazi kimoja na kuja kuwa balaa kwa kikazi kingine;

In our case, hata hiyo economic argument haina mashiko kwani its obvious kwamba we borrow even at times when the rate of return falls below the cost of capital; kujua hili, tazama our debt service na jinsi gani ni kubwa kuliko hata our investments in Education and Health sectors;

Political argument kwetu Tanzania nayo haina mashiko licha ya ukweli kwamba hata ingekuwa na mashiko, it violates zile kanuni mbili za fiscal discipline, hasa the sustainable investment rule yenye lengo to avoid creation of an excessive burden ya debt repayments kwa vizazi vijavyo; Lakini hata kama for political reasons tuna amua kuvunja hii kanuni, bado the political argument supporting borrowing haina maana Tanzania kwa sababu gains of borrowing are not felt by the majority of the current generation bali wachache wanaofaidi mabilioni yasiyojulikana yapo wapi per CAG report;

Cc Nguruvi3, Bongolander

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom