Deni La Taifa: Wabunge, Wanasiasa Wachumi Na Wachumi Wanasiasa

Deni La Taifa: Wabunge, Wanasiasa Wachumi Na Wachumi Wanasiasa

Patlending,

Nakubaliana na wewe kwamba tunaweza andika hata kontena zima la vitabu kuhusiana na suala hili na most likely hakuna kitachofanyika kuleta mabadiliko katika usimamizi mzima wa uchumi kwa manufaa ya watanzania walio wengi; Pia nakubaliana na wewe kwamba ni kweli - CCM ina wataalam wengi lakini kama tunavyofahamu, wakipewa tu nafasi za kisiasa huwa wanaishia kustaajabisha umma kwa madudu, ubabaishaji na uchwara wao katika kusimamia sera kwa manufaa ya wananchi; Je – ni kwa nini inatokea hivyo? Kuna sababu nyingi ambazo zimeshajadiliwa sana na bado zitaendelea kujadiliwa, lakini kwa madhumuni ya huu mjadala, hasa kwa sababu hoja hii imejitokeza ndani ya mjadala huu, ningependa kutoa mawazo yangu machache juu ya suala hili; Katika hili, pia nitakuwa najibu moja ya hoja za mdau mwenzetu bongolander kuhusiana na na suala zima la usimamizi mbovu wa uchumi miongoni mwa viongozi wa Tanzania;

By definition, party politics ni partisan politics, ndio maana ni kwa kiasi kidogo sana vyama vya siasa huwa vina reflect and carter for society’s interest kwani vyama hivi world all over vipo zaidi kwa ajili yaku – respond to the expediencies of power; Vyama vya siasa vina muda mdogo sana to reflect over larger social issues; Hali hii, again, ni world all over lakini kwa nchi maskini na ndogo kiuchumi kama Tanzania, tabia hii ya vyama vya siasa inakuwa felt zaidi kutokana na sababu moja tu kwamba – sisi kama jamii ya watanzania, we don’t have a firm direction of development; we don’t have a Nation and a National Vision ambayo imetokana na wananchi wenyewe, yenye kuweka priority juu ya wapi fedha ziende, kwa madhumuni gani, kwa muda gani, chini ya key performance indicators zipi n.k; Badala yake, chini ya uliberali mamboleo, tumekuwa tunafuata objectives and targets za IMF/World Bank (Patlending awali ulijadili wataalamu wa nje …) na sote tunajua historia ya sera hizi za uliberali mambobelo kwahiyo haitakuwa na maana sana kuanza kujadili kwa kina suala hili;

Ni katika muktadha wa paragraph yangu hapo juu pamoja na madhara yake ndio maana hakuna cha kustaajabisha kuona madudu kama vile – serikali kutegemea 75% ya bajeti kwa ajili ya maendeleleo zitoke kwa wahisani, huku madudu yakizidi kuwa worse pale ambapo baada ya serikali kupokea 75% ya fedha za maendeleo ya maskini kutoka kwa wahisani (nje) kama mikopo ya masharti nafuu, serikali hiyo hiyo inafanya maamuzi ya kutenga sio zaidi ya zaidi ya 35% ya bajeti ya nchi kwa ajili ya maendeleo ya wananchi kwani ni utamaduni wa muda mrefu kwa serikali kutennga 65 to 70% ya bajeti kwa ajili ya posho, mishahara, procurement na operations za kisiasa katika muktadha wa partisan politics niliojadili hapo juu; Kwa mtindo huu, ni lazima serikali itasikiliza zaidi wataalam wa nje kwani hawa ndio wanaiweka serikali mjini and as we all know, tyrants love AID, kwani without aid, I, as a ‘tyrant wanna be’ sitaona maana ya kutafuta uongozi katika nchi maskini kama Tanzania;

Patlending, kuingia zaidi katika hoja yako ya msingi kwenye bandiko namba 59 hapo juu, hasa kuhusiana na jinsi gani wataalamu kama kina anna tibaijuka n.k wanavyokuwa ineffective, nadhani ni muhimu tukaelewa kwamba mtu kama Tibaijuka au Ndullu ni properly trained individuals wenye good track record ya utendaji lakini katika mazingira, mfumo na muundo ambao ni formal (not informal), unafuata sheria na kanuni husika, ndio maana ikitokea unawaweka watu wa aina hii katika mazingira kinyume na haya, hasa mazingira ambayo politics is supreme to rationality, economics and even common sense, no matter how much they try, hawatafanikiwa kuleta a desired change;

Kuna mtaalamu mmoja wa masuala ya African Politics anaitwa Giran Hyden; Mtaalam huyu amejadili sana jinsi gani African States are inherently weak kwani zinaendeshwa zaidi na informal systems kuliko formal systems; Katika moja ya makala yake anauliza swali kwamba je:

"If informal institutions are so dominant and the STATE so weak and soft, how do countries in Africa govern themselves?"

Anasema kwamba – individuals and organizations in Africa do not engage in politics to win the right to govern or influence government policy within an overall framework of legitimate rules; Instead, Politics in most African states is rather like politics in the international arena where the unsanctioned use of coercion and violence takes place in the absence of agreed – upon rules. Consequently, politics in Africa are less restrained and more personalized than in places with formalizes systems of rule; The result are higher stakes and greater risks for those who engage in the political game and greater uncertainty for the general public;

To put it in a nutshell, pengine constitutional reforms zitaweza kutusaidia katika hili ambapo wataalamu kama kina mama Tibaijuka na wengine wataondokewa na constraints katika utendaji wao kwani chini ya mfumo wa sasa wa patrimonialism – hasa huu wetu wa an imperial president, Max Webber (mtaalam mwingine mashuhuru wa masuala ya siasa) anasema kwamba:

"The patrimonial office lacks above all the bureaucratic separation of the “private” and “official” sphere. For the political administration too, is treated as a purely personal affair of the ruler, and political power is considered part of his personal property…The office and the exercise of public authority serve the ruler and the official on which the office was bestowed; They do not serve impersonal purposes;"
 
Mkuu Mchambuzi,
Bandiko lako #58 umepiga misumari mingi sana. Nitasherehesha michache! ha ha ha
Kwanza umeeleza kuhusu ongezeko la bajeti na kusema ni nominal tu. Ukweli ni kuwa ukiangalia value ya Tshs ni wazi bajeti inashuka bila hata ya hesabu. Instability ya Tshs haiwezi kutupa percentage ya maana kama ulivyonena.

Umeongelea Purchasing power. Watanzania wana tatizo la kuangalia figure na wala si purchasing power.
Hili ameliongelea Bongolander vizuri kuwa utamaduni wetu ni wa kutoanagalia masuala ya uchumi kama tatizo na hakika nakubaliana naye kabisa.

Bongolander amesema wakati wa Mwinyi watu walisema pesa ilikuwa nje nje na pengine hali ilikuwa ''nzuri''.
Wanasahau kuwa Bongoman alipokuja kupiga mziki kiingilio kilikuwa 100,000 na kila mmoja alikuwa nazo kwa ukumbi kujaa.
Hapo hakuna aliyeangalia purchasing power.

Mkapa alipoingia alibana kidogo hadi kuitwa Ukapa. Lakini nikiangalia kwa upande mwingine purchasing power ilikuwa kubwa sana. Hii middle class ilianza kuibuka kwa wingi wakati huo. Nilishangaa vyama vya wafanyakazi kulilia ongezeko la mishahara na si kuangalia inflation na purchasing power.

Hata Wabunge wetu wengi wanaangalia sana figure za mshahara na wala si factors zinazoweza kuathiri figure hizo.
Nadhani serikali ikiangalia zaidi vitu kama inflation na kurudisha chini, mshahara unaweza kuwa maana kwasababu purchasing power inakuwa na maana.

Kuhusu suala la bandari Bagamoyo, hakika ni politics tu zinafanya kazi.
Hakukuwa na thorough economic analysis.
Tatizo la bandari ya Dar es Salaam ni mismanagement kama alivyosema Bongolander.
Mismanagement ndiyo imepelekea bandari kuwa inefficient katika utendaji wake.

Bandari haifanyi kazi kama inavypaswa, imekuwa na political interference nyingi na kumekuwa hakuna innovation.
Sababu kubwa ni kuwa watendaji wa bandari hawapatikani kwa merits bali ''technical know who''

Kijiografia bandari ya Dar ilitakiwa iwe the main gate ya East na central Africa. Ni jambo la kushangaza kuwa Watanzania wana opt kutumia bandari ya Mombasa kwasababu ya uzembe uliokithiri katika bandari zetu.
Endapo wizi wa vifaa umetamalaki na hakuna mwenye solution nani ataendelea ku-risk au ku-venture katika business na irresponsible harbor kama ya Dar es Salaam.

Tatizo si ukosefu wa bidhaa ni political interference Ukisoma project ya kupanua bandari ya Dar there is nothing except corruption inayowahusu viongozi wakubwa wa serikalini. Ni corruption hiyo pia inahusu vimemo, kukwepa kodi n.k.

Sasa mtu anapotaka kuniamnisha kuwa bandari ya Bagamoyo ita solve matatizo hayo sikubaliani naye hata kwa bahati mbaya.

Nasema hivyo kwasababu tumeshindwa ku-run Tazara ni kwanini tuamini kuwa bandari mpya itafanya kazi.
Mchambuzi kaeleza kuwa kuna sababu zipi za kiuchumi ambazo zita justify uwepo wa bandari ya Dar es Salaama na ya Bagamoyo 100 KM apart. Haya ni mambo tunayopaswa kuyafahamu na si kubambikiwa deni tu.

Lakini pia bajeti hii ilipaswa kuhoji, ule upanuzi wa bandari uliotengewa fedha miaka ya nyuma umefikia wapi na unaelekea wapi. Kama umesitishwa nini economic benefit zitokanazo na nini disadvantage za kufanya hivyo. Cost ambazo tume incur nani anakuwa responsible.

Kuhusu Matumizi ya maendeleo na yale ya kawaida, utashangaa kuwa current expenditure is staggering so as to speak.
Nchi haiwezi kutegemea wafadhili katika maendeleo. Kwa maana kuwa bajeti yetu ni hand to mouth sasa lini tutafanya maendeleo!!

Bado naiangalia bajeti nasikitika. Hatuwezi kuwa na serikali kubwa kiasi tulicho nacho huku tukiwa hatuna uwezo wa kukusanya kodi halafu tuka balance bajeti.

Angalia pesa zilizotengwa kwa ajili ya bunge mwaka 2011-2012 halafu linganisha na miradi mingine muhimu ya jamii.
Inawezkeanaje kuwa ''administrative business'' zika out pace investment! wapi hii iliwezekana.
Investment inaweza kuwa katika mambo yote hata social service. Sasa tafuta bajeti ya bunge halafu linganisha na bajeti ya Hospital 4 za rufaa.

Tatizo linaanzia hapo na ndiyo maana wabunge hawawezi kuangalia nje ya masilahi yao.
Nasi wananchi lazima tuelewe kuwa uchumi ni sehemu ya maisha yetu, hatutakiwa kuwa zealous katika politics tukiacha mambo ya uchumi yaende kama yalivyo. Ni kujidanganya

Otherwise nakubaliana sana na hoja zenu wakuu
 
Hawa ndio wachumi wanasiasa, na tofauti na wanasiasa wanasiasa wachumi kama mwigulu nchemba ni kama hakuna kwani wote ni useless kwa maendeleo ya wananchi walio wengi; huyu mwigulu angekuja humu na digrii yake ya uchumi daraja la kwanza ambayo ni kwa manufaa ya watanzania daraja ya kwanza, nadhani angetusaidia zaidi kutuelimisha wananchi nje ya daraja la kwanza, vinginevyo ni dhahiri hawezi thubutu kuja humu kujadili uchumi wetu kwa hoja

Wakuu nawasalimu, nimevutiwa na mada lakini michango ni mingi na yakina- hongereni, nasoma na kutafakari mliyosema nione kama ninalo la kuchangia ila kwa hili la Mh Mwigulu niwakumbushe maneno ya Einstein kuhusu education - he said "education is what is left after you have forgotten what you learned at school" need i say more .... what we are getting from him(Mwigulu) is his true education level not the first class.
 
Back
Top Bottom