Nguruvi3,Vile vile umezungumzia suala la informal sector and taxation; kwa mujibu wa takwimu zilizopo, informal sector in Tanzania accounts for about 50% of GDP and about 70% of total workforce, yet it largely remains untaxed; Hili ni tatizo, na sina maana kwamba poor farmers and petty traders mijini waanze kutozwa kodi; Maana yangu hapa ni kwamba serikali makini inaweza kuwajengea uwezo wote hawa kwa kuwapatia incentives mbalimbali for growth and eventually formalize them hasa on condition kwamba they register na Brela na TRA kabla ya kusaidiwa katika hatua za mbele zaidi; Umakini ukifanyika, mimi sidhani kama watanzania hawa watashindwa to comply na sheria za kodi; Mkuu bongolander, katika hoja yangu ya awali kuhusiana na leakages in the circular flow of income nchini, hoja yangu ilikuwa katika muktadha huu;
Mkuu nguruvi3, kwahiyo upo sahihi ( at least kwa mtazamo wangu) kwamba idadi ya walipa kodi Tanzania ni ndogo kuliko our potential kwani kwa mujibu wa TRA, potential number ya walipa kodi Tanzania ni watanzania milioni 15 (kumi na tano), lakini actual tax payers to-date haizidi watanzania milioni mbili. Kwa maana hii, watanzania wenye uwezo wa kulipa kodi na ambao hawalipi kodi ni zaidi ya 85%; Nguruvi3, kwa mtazamo wako, tunageuzaje takwimu hizi ili walipa kodi Tanzania wawe angalau hata 50% ya watanzania wote wenye uwezo wa kulipa kodi na tuweke targets zipi na kwa vigezo gani?
Kabla sijachangia changamoto yako ningeseama kuwa mengi mumeyajadili katika mabandiko yako Mchambuzi, Petlanding na Bongolander ambayo nakubaliana nayo kabisa.
Bandiko#50 umesema kuwa WB ilifanya reform kwasababu ukusanyaji wetu wa kodi ulikuwa mdogo.
Pamoja na mambo mengine masilahi ya TRA yaliangaliwa kwa undani. Mimi sidhani kama tatizo lipo kwa watendaji wote wa TRA. Nadhani tatizo ni interference kutoka kwa viongozi wa serikali ambao vimemo n.k. ndivyo vinachagiza ukwepaji mkubwa sana wa kodi. Mathalani, wawekezaji hawawezi kugeuza majina ya business zao kukwepa kodi bila kuwa na baraka za viongozi.
Hatua muhimu ni kuifanya TRA iwe independent. Ndivyo nchi nyingine zinavyofanya.
Kwamba, taarifa za TRA zinaweza kufanyiwa kazi na taasisi nyingine kama bunge kwa kishindo.
Na ukweli kuwa hii ni sehemu muhimu ya uchumi, uteuzi wa viongozi wake lazima upunguze uwajibikaji kwa mtu mmoja.
Kurejea katika nukuu yako hapo juu, kuna kitu umegusia kuhusu BRELA na TRA. Nilikuwa nakwenda huko.
1. Ni lazima walipa kodi wajulikane. Kama tuna estimate ya million na wanaolipa ni 2 millions tuna tatizo kubwa.
Basically ni wale wanaolipa kwa kupitia mishahara, na biashara ndogo ndogo.
2. Kuhakikisha kuwa kila shughuli inasajiliwa na BRELA kwa kushirikiana na TRA. Na umeongelea informa sector
Hapa natofautiana nawe Mchambuzi kwasababu informal sector inapaswa kujulikana na kulipa kodi hata kama ni mkulima.
Nina maana kila mtu alipe fair share kwasababu sote tunatumia huduma zile zile za umma bila kujali vyanzo vyetu vya mapato.Hili litaongeza uchungu kwa mkulima anaposikia kuna bilion 600 unaccounted for, kuna mgao wa umeme wa kutengneza n.k. kwamba ukilipa kodi you feel it na hapo ndipo uwajibikaji wa kila mtu utakapokuwa na impact katika mabadiliko ya nchi. We need to feel pain, later evening sitting watching tv we will have the courage to pity Nchemba and Lusinde for abysmal performance at our expense. Lazima kila mtu ajaisikie maumivu ya kodi kwanza.
Informal sector ina watu wenye uwezo wa kulipa kodi. Nitakupa mfano, endapo mfanyakazi wa serikali kama mesenja anakatwa kodi kila mwezi kwa mshahara wa 200,000 ni kwanini mtu mwenye gereji anayetengeneza 600,000 asamehewe.
Kama tarishi anayelipwa 200,000 anakatwa kodi kwanani mwenye genge la nyanya anayetengeneza 200,000 asilipe.
Hii ni minimum kabisa kwa ajili ya majadiliano, tukienda kwa undani tutaona ukubwa wa sekta hii.
3. Kuwe na incentive kwa mlipa kodi, mathalani mtu mwenye rekodi za kulipa kodi hasa wale wa informal sector apewe unafuu ili naye alazimike kulipa kodi au kumlazimisha mwajiri wake kulipa kodi. Mfano mdogo tu kama mtu yupo informal sector basi akikata bima ya afya binafsi apunguziwe asilimia kadha endapo ana ushahidi wa kulipa kodi kutoka TRA.
4. Adhabu kali kwa wakwepa kodi. Kwa nchi za wenzetu mtu anapata unafuu wa adhabu ya kuiba pesa ofisini kuliko kukwepa kodi. Kukwepa kodi ni kosa linalofunga business yoyote ile. Waajiri wanaogopa sana kwasababu adhabu yake ni tatizo kubwa sana.Je, sisi tunafanya nini? Unakumbuka kesi za matycoon wa America.
5. Tuwe na ''sunshine'' list hasa ya makampuni. kwamba, mtu yoyote yule anaweza kuona kampuni gani inalipa kiasi gani.
6. Misamaha ya kodi isiwe suala la mtu mmoja au wawili. Iwekwe wazi katika taarifa za mwaka na sababu zake na jinsi gani misamaha hiyo imekuwa na manufaa au ilitarajiwa kuboresha kwa namna moja huduma za uchumi au za jamii kwa taifa. Msamaha ulitolewa na mamlaka ipi kwa kuzingatia vigezo gani.
Namna ya kuongeza mapato.
Kila mkoa upewe malengo ya ukusanyaji kodi, na hiyo iwe reflected katika mgao kutoka hazina kwa maendeleo au shughuli za uendeshaji wa mikoa husika. Nina maana pesa za kodi zisizambazwe tu bali zirudi kufanya kazi kule kuliko tarajiwa na zilikopatikana.
Kutumia mbinu za kisasa za kubaini walipa kodi, ikiwa ni pamoja na nguvu kazi ya formal na informa sectors.
BRELA na TRA ziwe huru na uongozi upatikane kwa vetting na siyo appointment.
Zipewe malengo na sio kujipangia malengo.
Mwaka juzi TRA ilisema wamekusanya 110% ya malengo, sasa inakuwaje tuna watu 13 milion wasiolipa kodi.
Malengo hayo yamefikiwa vipi na kwa hesabu gani. Huu ni udanganyifu wa kupeana bonus kwasababu wao ndio wanaopanga malengo. Haiwezekani kukawa na 110% huku 13Million hawakulipa kodi.
Kuangalia na kuziba mianya katika sehemu kuu za uchumi kama bandari, migodi n.k.
Kuziba leakage katika miradi inayotumia fedha zaidi ya ilivyokadiriwa.
Kuweka malengo ya kumalizika miradi bila kuwa na bajeti ya ziada.
Kama mradi umetengewe bilioni 120 kusiwe na bajeti ya ziada baada ya hapo.
Kuondoa ruzuku kwa miji na majiji. Hivi kwanini Jiji la Dar lipewe ruzuku na si kutoa kwa serikali.
Something is wrong! Ondoa ruzuku kila mmoja asimame kwa miguu yake. Asiyeweza akae pembeni.
Kuwaagiza TRA kutafuta vyanzo vingine vya mapato zaidi ya bia na sigara.
Kwamba kila bajeti mpya lazima kuwe na ubunifu. Hiwezekani tusubiri kodi ya vocha za simu wakati sekta ya utalii ina uwezo mkubwa sana wa kukusanya kodi pengine zaidi ya hiyo. Tunafanya nini na mito ya maji, bahari na maziwa ambayo ni resource nzuri sana za revenue.
Iweje kuwe na taifa linalotegemea uvuvi nasi tushindwe tukiwa tumezungukwa na maziwa makubwa dunia na bahari kama wenzetu. Tunafanya nini kupata mapato kutoka sekata ya uvuvi?
Kwanini nchi za wenzetu kama Kenya na Uganda remittance za diaspora ziwe sehemu muhimu ya kuongeza mapato sisi tuache tu akina western union wakusanye kwa niaba yatu. Kunafanyika nini katika ku-tap kodi zitokanazo na remittance.
Mtu anaweza kudhani ni kiasi kidogo, lakini angalia kodi za makampuni halafu linganisha na income inayoweza kupatikana.
Kupunguza matumizi ya serikali ikiwa ni pamoja na ukubwa wake.
Kupunguza miradi isiyo ya lazima kwanza na kuhakiki ile iliyopo inakamilika.
Juu ya yote ni kuwa na political will na hiyo ni kazi ya wananchi.
Kwamba serikali isipo deliver ni kuiweka pembeni haraka.
Nimeona nchi moja ya magharibi, kulikuwa na mradi ambao kwasababu zisizojulikana ulizidi kwa dollar 150,000.
Hili lilikwenda na maji na waziri mkuu aliyekuwepo madarakani ingawa hakuhusika.
Niseme kama hakuna fiscal discipline, known source of income, good tax collection, na political will, tutaendelea kukopa, interest inaongezeka na siku moja watakuja tena na kusema kama rais wenu hatapanga chumba manzese ili kumwachia mwekezaji nafasi magogoni hatuwapi. Tutafanya nini!