Kuna vitu nimeviona hapa, Fiscal discipline, deficit, debt(internal and external), Revenue,GDP and Political will.
Mkuu Mchambuzi, bandiko lako
#22 ''limeninyang'anya'' sehemu kubwa sana ya mchango wangu.
Sipendi kurudia uliyoyasema kwa undani na ukweli, ninachotaka kusema kwa uchache ni kuwa ndani ya bunge letu asilimia 95 kwa mtazamo wangu hawawezi kuongelea na wala hawajui haya ''Fiscal discipline, deficit, debt(internal and external), Revenue,GDP and Political will''
Kilichobaki kwao ni kile ulichokisema 'take care of today tomorrow will take care of itself''.
Kwanza, bungalow pili watoto watasoma wapi huko nje n.k. haya mengine ni by the way.
Watu wanaposema eti tupo katika hali nzuri kwa deni la taifa ukilinganisha na mataifa mengine inachekesha sana.
Marekani, Japan, China n.k wapo katika vita ''currency war'' kila mmoja akifanya devaluation ya currency yake katika ku-encourage export na kuweka uchumi katika hali nzuri. Nchi hizi ukiangalia GDP yake, fiscal discipline, debt management, revenue collection and political will, hatufanani hata kidogo, leo tunachukua namba 47% na kusema tunalingana nao!!
Marekani ina mzozo ndani ya senate na congress kuhusu debt ceiling. Kwamba serikali iwekewe ukomo wa kukopa hovyo ili kuleta fiscal discipline. Mtakumbuka hili ni moja ya mambo yaliyopeleke marakani kupoteza AAA katika credit rating.
Sasa tunapodhani wao wana debt to 100+% ni mbaya zaidi yetu ni kichekesho kingine kutoka kwa bunge letu
Fiscal discipline ni dira ya uongozi wa taifa lolote linalojitakia mema.
Kwamba lazima utumie kile unachopata. Ukiangalia Australia, UK, Japan, USA n.k. serikali inayokosa fiscal discipline inaondolewa madarakani haraka.Hata kwa akili za kawaida tu, huwezi kutumia zaidi ya unachokipata ukawa salama.
Kwa nchi yetu fiscal discipline hicho kitu hakuna. Kwanza hakuna mtu anayejua tunakopa wapi na kwanini na kwamba mkopo huo una return gani directly or indirectly.
Si bunge wala wananchi kwasababu juzi upinzani bungeni umeeleza kuwa deni la taifa lina uwalakini kwasababu 640 billions are unaccounted for. Sasa zilikopwa kwa kutumia sehemu gani ya utawala endapo bunge linaloidhinisha matumizi halijui?
Mambo kama hayo nduiyo yanaleta deni la taifa (internal na external).
Hata ukiangalia internal debt taarifa za CAG zimeonyesha embezzlement ya hali ya juu sana.
Hakuna mtu anayekuwa responsible kwasababu hakuna political will.
Kwa kadri deni linavyokaa ndivyo linavyokuwa na hili linakuwa mzigo kwetu sisi walipa kodi na vizazi vijavyo.
Kw vile hatuna fiscal discipline hatuwezi kuwa na effective revenue collections.
Pasco ameeleza vema scenario ambayo nadhani sote tunaijua.
Kwakukosa revenue tunaishia kuwa na deficit katika bajeti.
Na ili kufidia deficit tunalazimika kwenda kwa wajomba tukipitisha bakuli.
Wajomba wanatupa msaada sasa ni miaka 50. Dambisa Moyo katika kitabu chake ameeleza vema jinsi misaada inavyotulemaza waafrika. Alitolea mfano wa Nigeria nchi yenye utajiri wa mafuta.
Akasema tangu mwaka 1960+ hadi alipoandika kitabu chake nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta imepokea zaidi ya dollar billion 360 za msaada. Akauliza kama misaada inasiaidia iweje basi leo Nigeria iwe na idadi ya watu masikini sana?
Ukweli huo unatugusa sana kwasababu kama misaada inalenga kutuondoa katika umasikini na utegemezi kwanini basi miaka 50 sasa hakuna hata dalili ya kuweza ku-balance bajeti yetu.
Kwamba, tunaweza kujihudumia kwa basic needs kabla ya msaada.
Hapa tunarudi katika fiscal discipline. Hatuna kitu hicho kwasababu haiwezekani serikali ilete bajeti ambayo hailingani na revenue halafu wabunge wakubali tu. Wanakubali kwa kuelewa kuna mjomba na si wao kutumia akili zao na uwezo wao wa kimamlaka kuhoji.
Fiscal discipline inatakiwa iangalie mambo mengi sana.
Kwa mfano, nini kinaongeza matumizi kuliko mapato? Ni kwanini mapato hayakidhi matumizi? Je kuna njia mbadala za kuongeza mapato. Je, tunawekeza katika sehemu zinazotoa return au tunawekeza politically.
Tukiangalia kwa uchache, matumizi ni yale yanayoihusu serikali.
Inakuwaje nchi masikini kama yetu iwe na matumizi makubwa ya serikali.
Mathalani, katika mkoa mmoja wenye wilaya 5 kuna mkuu wa mkoa 1, wakuu wa wilaya 5, wabunge zaidi ya 5, maafisa tawala n.k. achilia mbali maafisa wa idara,wote hawa wanaongeza gharama zisizo za muhimu kwasababu mkuu wa mkoa mmoja ambaye ni effective anaweza kufanya kazi za wakuu wa wilaya bila tatizo.
Tuna serikali kubwa sana katika ngazi ya taifa na kila mahali.
Kibaya zaidi ukubwa huo si wa ufanisi bali sehemu za kutoa shukrani.
Tumeona ukuu wa wilaya ukigawiwa kama njugu, mawaziri na manaibu lukuki n.k.
Gharama za uendeshaji ni kubwa mmno kutokana na matumizi yasiyo ya lazima.
Ukubwa tu wa serikali unakuwa ni sababu ya kutokuwa na balanced budget na hivyo kuongeza deni hasa la ndani.
Ni vivyo hivyo katika ukusanyaji wa kodi. Serikali imebaki na kundi la wafanyakazi ambalo halina ujanja mbele ya kodi.
Makundi mengine yanapewa loophole za ima kulipa au kutolipa na hakuna anayejali.
Nilisikitika sana mwaka jana waziri wafedha aliongelea kuongeza mapato kwa kutumia kodi za simu za mikononi.
Kwamba nchi iliyojaa neema na mito, maziwa na bahari, madini, na uoto mzuri wa asili bado inategemea kodi ya text message kupata mapato. Kama ubunifu utakuwepo basi ni wa kugundua aina mpya ya soda na sigara ili kuwekewa kodi
Sasa katika fikra za namna hiyo ni nani anayejishughulisha na fiscal discipline, debt reduction, GDP,budget deficit na reveue collections.
Hebu tutue hapa kwanza kabala ya kuendelea