Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Mwaka 2017, nchi yetu ilipata mkopo wa dola za kimarekani kutoka benki ya Exim ya Uturuki ya dola za kimarekani bilion 1.2 ambazo ni sawa na takriban shilingi Trillion 2.76 za kitanzania kwa ajili ya Ujenzi wa kipande cha Dar es salaam mpaka Morogoro tu.
Kwa mujibu wa tweet ya mheshimiwa Zitto ya october mwaka 2017, Ndugu Zitto aliufahamisha umma kuwa riba ya mkopo huo ni 9%
Ndugu Zitto alikuwa anashangaa aina ya mkopo huo kutoka kwa waturuki wakati Wachina hapo mwanzoni tulishakubalina nao waijenge hiyo reli kwa riba ya 1% tu na mkopo huo kutoka kwa wachina tulikuwa na unafuu wa kuanza kuulipa baada ya miaka 20 kupita kwanza!
Sasa mimi nitajikita kwenye riba ya mkopo wa kipande kifupi tu cha reli hiyo cha kutoka Dar es salaam mpaka Morogoro halafu wewe mwenyewe msomaji utajaza mwenyewe ni pesa ngapi tutalipa kwa mikopo ya kujenga vipande vingine vya reli hiyo kama kile cha kutoka Morogoro mpaka Makutopora, na Makutoora mpaka sehemu nyingine hadi mwisho
Nimechukua pesa tuliyokopa, dola bilion 1.2 kama principle, na interest ya 9% aliyoisema mheshimiwa Zitto kisha nikatumia calculator ya online kuangalia, Je deni la kipande hicho pekee cha Dar es salam Morogoro baada ya miaka 20 itakuwa shilingi ngapi?
Nimetumia calculator inayopatikana hapa:
Compound Interest Calculator - The Calculator Site
matokeo niliyopata ni kuwa jumla ya riba tutakayopaswa kulipa ni takriban dola bilion 6 sawa na shilingi Trillion 13. 8 kwa kipande kidogo tu cha Dar hadi Morogoro baada ya miaka 20.
Sasa najiuliza, Je tumejipangaje kama taifa kuja kubeba mzigo huu wa deni?
Kama kipande kifupi tu cha hiyo reli kinaweza kutupelekea kulipa shilingi Trillion 13. 8 kama riba baada ya miaka 20, Je tutalipa shilingi ngapi kwa ajili ya kulipia mikopo yote ya reli nzima?
Tunaweza kuwa tunaimba na kufurahia SGR kumbe ikageuka kuw kitanzi cha kutunyonga kiuchumi huko mbeleni.