Deni la ujenzi wa reli ya SGR ni kitanzi kitakachotunyonga tusipokuwa makini

Anajua hilo ziko watalibeba warithi wake, serikali zinazokuja zitaishia kulipa madeni na mishahara, alafu wakolomije watakua wanalalamika "enzi za magufuli maendeleo yalikua yanaonekana, sasa hivi hakuna kitu ...."
 
Dah, umenifikirisha sana
This man is all about himself
Anajali ujiko wake binafsi wa muda mfupi at the expense ya mustakbali mpana zaidi wa Taifa.
Na hili ndo tatizo la kudhani maendeleo ni vitu.
Sasa tutakuwa na li SGR lakini deni kubwa balaa
 
Huyu Mzee kiukweli anazingua. Mwaka wa tano huu anatufanyia tu dhihaka sisi Wafanyakazi, kisa anajenga miundombinu!

Halafu kumbe huko kwenye hiyo miundombinu yenyewe, hela za kujengea anakopa!! Sasa hela za kodi zaidi ya tirioni 1.4 za kila mwezi anazojisifia, huwa zinafanyia nini!!

Atasemani kwa ajili ya kulipia mishahara!! Ya wafanyakazi gani? maana hakuna ajira kwa wahitimu wa vyuo kwa sasa kama ilivyokua enzi za JK, hakuna nyongeza ya mishahara wala kupandishwa madaraja kwa wakati kama ilivyokua enzi za JK, hakuna annual incriment, alitumbua kikatili zaidi ya wafanyakazi aliowaita wenye vyeti feki na hewa zaidi ya elfu 19!

Hakika Mzee ana haki ya kuminya uhuru wa kujieleza. Maswali ni mengi huku majibu yakiwa hakuna. Bora ya JK.
Ni mwendawazimu tu anayeweza kuwanyima watoto wake chakula kwa kisingizio Cha kujenga nyumba
 
Dah, umenifikirisha sana
This man is all about himself
Anajali ujiko wake binafsi wa muda mfupi at the expense ya mustakbali mpana zaidi wa Taifa.
Na hili ndo tatizo la kudhani maendeleo ni vitu.
Sasa tutakuwa na li SGR lakini deni kubwa balaa
Hivi hao wanaotamani kumpa madaraka ya urais tena hawaoni haya? Au mtu akishateuliwa kwenye nafasi fulani akili zinaruka?
 
Hii haiwezi kuwa kweli maana magufuli alituhakikishia na kutuaminisha kuwa yeye Ni mzalendo sana na anaipenda nchi hii sana hivyo hataki mikopo ya riba kubwa ndo maana akawakataa wachina,hizo figure utakuwa umezisoma kinyumenyume maana nahisi umetumwa na beberu wewe
unachukulia kutumwa na mabeberu kama defence mechanism yako
acha kulisha wAtu matango pori wewe
 
Kama ni kweli hii ni hatri sana. Ukope trillioni 2.6 halafu uje ulipe trillioni 13?.
 
Dawa ni kuwatoa mapepo tu.
Nadhani mkopaji hajui hii calculation au kafanya makusudi

Mimi naamini JIWE hayajui haya maesabu ya compound interest kwani yeye ni zaidi kwenye kuchanganya madawa; bahati mbaya sana Watu wake wa kumshauri kama Philip Mpango ndio hao opportunist ambao wanaogopa kumwambia ukweli ambao hataki kuusikia!!! Mkopo wa kujenga hiyo reli ni mzigo mzito sana kwa Taifa!!! Time will tell.
 
Hii haiwezi kuwa kweli maana magufuli alituhakikishia na kutuaminisha kuwa yeye Ni mzalendo sana na anaipenda nchi hii sana hivyo hataki mikopo ya riba kubwa ndo maana akawakataa wachina,hizo figure utakuwa umezisoma kinyumenyume maana nahisi umetumwa na beberu wewe

Soma za ukweli alafu zilete tuone wote, huenda kweli huyu ni muongo lete zako.
 
Exim ni benki ya China na si Uturuki, Uturuki haina uwezo wa kutoa mkopo wa pesa hiyo kwa Tanzania na yenyewe ina hali mbaya sana ya uchumi, fatilia hilo ujue.

Kipande cha dar es salaam-morogoro kinajengwa kwa pesa za ndani. Hilo ni kweli.

Kipande cha pili cha morogoro-makutupora ndio kinajengwa kwa pesa ya mkopo ya Exim.

Tahadhari: usimwamini sana Zitto Kabwe
 
Mimi naamini JIWE hayajui haya maesabu ya compound interest kwani yeye ni zaidi kwenye kuchanganya madawa; bahati mbaya sana Watu wake wa kumshauri kama Philip Mpango ndio hao opportunist ambao wanaogopa kumwambia ukweli ambao hataki kuusikia!!! Mkopo wa kujenga hiyo reli ni mzigo mzito sana kwa Taifa!!! Time will tell.

Ukitaka kujua uzito wa hili deni, assume wewe una deni la bodi ya mikopo la elimu ya Juu, halafu ukae miaka 10 bila kulipa kisha nenda ukaangilie utakuwa unadaiwa shilingi ngapi baada ya hiyo miaka 10

Sasa mfano huo ni kwako wewe mwenye deni la vimilioni vichache, sasa what about mkopowa Matrilion mkopaji atalipa shilingi ngapi?

Njia nzuri ya kujenga hii miundo mbinu. inayohitaji riba kubwa ni kupitia mfumo wa PPP tu basi, nje ya hapo ni kuidumbukiza nchi katika kitanzi kikali cha deni, Tutakuja kujuta sana aisee!
 
Mwaka 2017, nchi yetu ilipata mkopo wa dola za kimarekani kutoka benki ya Exim ya Uturuki ya dola za kimarekani bilion 1.2 ambazo ni sawa na takriban shilingi Trillion 2.76 za kitanzania kwa ajili ya Ujenzi wa kipande cha Dar es salaam mpaka Morogoro tu.

Kwa mujibu wa tweet ya mheshimiwa Zitto ya october mwaka 2017, Ndugu Zitto aliufahamisha umma kuwa riba ya mkopo huo ni 9%
Ndugu Zitto alikuwa anashangaa aina ya mkopo huo kutoka kwa waturuki wakati Wachina hapo mwanzoni tulishakubalina nao waijenge hiyo reli kwa riba ya 1% tu na mkopo huo kutoka kwa wachina tulikuwa na unafuu wa kuanza kuulipa baada ya miaka 20 kupita kwanza!

Sasa mimi nitajikita kwenye riba ya mkopo wa kipande kifupi tu cha reli hiyo cha kutoka Dar es salaam mpaka Morogoro halafu wewe mwenyewe msomaji utajaza mwenyewe ni pesa ngapi tutalipa kwa mikopo ya kujenga vipande vingine vya reli hiyo kama kile cha kutoka Morogoro mpaka Makutopora, na Makutoora mpaka sehemu nyingine hadi mwisho

Nimechukua pesa tuliyokopa, dola bilion 1.2 kama principle, na interest ya 9% aliyoisema mheshimiwa Zitto kisha nikatumia calculator ya online kuangalia, Je deni la kipande hicho pekee cha Dar es salam Morogoro baada ya miaka 20 itakuwa shilingi ngapi?

Nimetumia calculator inayopatikana hapa:

Compound Interest Calculator - The Calculator Site

matokeo niliyopata ni kuwa jumla ya riba tutakayopaswa kulipa ni takriban dola bilion 6 sawa na shilingi Trillion 13. 8 kwa kipande kidogo tu cha Dar hadi Morogoro baada ya miaka 20.

Sasa najiuliza, Je tumejipangaje kama taifa kuja kubeba mzigo huu wa deni?

Kama kipande kifupi tu cha hiyo reli kinaweza kutupelekea kulipa shilingi Trillion 13. 8 kama riba baada ya miaka 20, Je tutalipa shilingi ngapi kwa ajili ya kulipia mikopo yote ya reli nzima?

Tunaweza kuwa tunaimba na kufurahia SGR kumbe ikageuka kuw kitanzi cha kutunyonga kiuchumi huko mbeleni.

View attachment 1541204
Huenda walitaka wafanye walichofanya Kenya, waijenga na kuishikilia reli kwa miaka hiyo mpaka tukianza lipa deni lao. Mchina hajawahi kuwa na deal zuri hivyo, cover la kitabu lake linakuwa linavutia kiichomo ni kitanzi.
 
Exim ni benki ya China na si Uturuki, Uturuki haina uwezo wa kutoa mkopo wa pesa hiyo kwa Tanzania na yenyewe ina hali mbaya sana ya uchumi, fatilia hilo ujue.

Kipande cha dar es salaam-morogoro kinajengwa kwa pesa za ndani. Hilo ni kweli.

Kipande cha pili cha morogoro-makutupora ndio kinajengwa kwa pesa ya mkopo ya Exim.

Tahadhari: usimwamini sana Zitto Kabwe

Tatizo mnayoelezwa kwenye majukwaa ya siasa siyo hali halisi.
Wenzako wanaposema "kwa pesa zetu" wanakuwa wanamaanisha eti kwa kuwa mkopo tutaulipa basi hizo ni pesa zetu ati!

Hebu tazama hii uone jinsi tulivyoomba mkopo kwa Waturuki!

Img-1597771946119.jpg

Kwa taarifa zaidi juu ya namna tulivyokopa kwa waturuki soma hapa:

Turkey wins bid to finance, build $1.9b second phase of Tanzania railway | The East African
 
Mwaka 2017, nchi yetu ilipata mkopo wa dola za kimarekani kutoka benki ya Exim ya Uturuki ya dola za kimarekani bilion 1.2 ambazo ni sawa na takriban shilingi Trillion 2.76 za kitanzania kwa ajili ya Ujenzi wa kipande cha Dar es salaam mpaka Morogoro tu.

Kwa mujibu wa tweet ya mheshimiwa Zitto ya october mwaka 2017, Ndugu Zitto aliufahamisha umma kuwa riba ya mkopo huo ni 9%
Ndugu Zitto alikuwa anashangaa aina ya mkopo huo kutoka kwa waturuki wakati Wachina hapo mwanzoni tulishakubalina nao waijenge hiyo reli kwa riba ya 1% tu na mkopo huo kutoka kwa wachina tulikuwa na unafuu wa kuanza kuulipa baada ya miaka 20 kupita kwanza!

Sasa mimi nitajikita kwenye riba ya mkopo wa kipande kifupi tu cha reli hiyo cha kutoka Dar es salaam mpaka Morogoro halafu wewe mwenyewe msomaji utajaza mwenyewe ni pesa ngapi tutalipa kwa mikopo ya kujenga vipande vingine vya reli hiyo kama kile cha kutoka Morogoro mpaka Makutopora, na Makutoora mpaka sehemu nyingine hadi mwisho

Nimechukua pesa tuliyokopa, dola bilion 1.2 kama principle, na interest ya 9% aliyoisema mheshimiwa Zitto kisha nikatumia calculator ya online kuangalia, Je deni la kipande hicho pekee cha Dar es salam Morogoro baada ya miaka 20 itakuwa shilingi ngapi?

Nimetumia calculator inayopatikana hapa:

Compound Interest Calculator - The Calculator Site

matokeo niliyopata ni kuwa jumla ya riba tutakayopaswa kulipa ni takriban dola bilion 6 sawa na shilingi Trillion 13. 8 kwa kipande kidogo tu cha Dar hadi Morogoro baada ya miaka 20.

Sasa najiuliza, Je tumejipangaje kama taifa kuja kubeba mzigo huu wa deni?

Kama kipande kifupi tu cha hiyo reli kinaweza kutupelekea kulipa shilingi Trillion 13. 8 kama riba baada ya miaka 20, Je tutalipa shilingi ngapi kwa ajili ya kulipia mikopo yote ya reli nzima?

Tunaweza kuwa tunaimba na kufurahia SGR kumbe ikageuka kuw kitanzi cha kutunyonga kiuchumi huko mbeleni.

View attachment 1541204
Tumechoka na mambo ya zito.
 
Exim ni benki ya China na si Uturuki, Uturuki haina uwezo wa kutoa mkopo wa pesa hiyo kwa Tanzania na yenyewe ina hali mbaya sana ya uchumi, fatilia hilo ujue.

Kipande cha dar es salaam-morogoro kinajengwa kwa pesa za ndani. Hilo ni kweli.

Kipande cha pili cha morogoro-makutupora ndio kinajengwa kwa pesa ya mkopo ya Exim.

Tahadhari: usimwamini sana Zitto Kabwe
You got it wrong,waulize Yap
 
Tatizo mnayoelezwa kwenye majukwaa ya siasa siyo hali halisi.
Wenzako wanaposema "kwa pesa zetu" wanakuwa wanamaanisha eti kwa kuwa mkopo tutaulipa basi hizo ni pesa zetu ati!

Hebu tazama hii uone jinsi tulivyoomba mkopo kwa Waturuki!

View attachment 1541439

Kwa taarifa zaidi juu ya namna tulivyokopa kwa waturuki soma hapa:

Turkey wins bid to finance, build $1.9b second phase of Tanzania railway | The East African

Hujaelewa kitu nilichoandika hapo juu. Mkopo ni kwa second phase na hapo wamesema. Kumbuka second phase ndio hiyo yenye 400km kutoka morogoro mpaka makutupora. Kipande cha kwanza ni hela za ndani dar-moro, jumla 300km
 
Back
Top Bottom