Deni la ujenzi wa reli ya SGR ni kitanzi kitakachotunyonga tusipokuwa makini

Deni la ujenzi wa reli ya SGR ni kitanzi kitakachotunyonga tusipokuwa makini

Ulisema Dar hadi Moro tunajenga kwa pesa za ndani, now source hii uliyoleta inasema kuna mkopo wa standard chartered unacover kuanzia Dar mpaka Makutopora.
Hizo pesa za ndani ni zipi sasa?

Kuna kitu serikali hii haitoi taarifa za kutosha kuhusu financing ya huu mradi maana naona inarukaruka katika kutafuta financiers
Propaganda haijawahi shinda ukweli
 
Hii miradi utekelezaji wake utazamwe upya.
 
Huyu Mzee kiukweli anazingua. Mwaka wa tano huu anatufanyia tu dhihaka sisi Wafanyakazi, kisa anajenga miundombinu!

Halafu kumbe huko kwenye hiyo miundombinu yenyewe, hela za kujengea anakopa!! Sasa hela za kodi zaidi ya tirioni 1.4 za kila mwezi anazojisifia, huwa zinafanyia nini!!

Atasemani kwa ajili ya kulipia mishahara!! Ya wafanyakazi gani? maana hakuna ajira kwa wahitimu wa vyuo kwa sasa kama ilivyokua enzi za JK, hakuna nyongeza ya mishahara wala kupandishwa madaraja kwa wakati kama ilivyokua enzi za JK, hakuna annual incriment, alitumbua kikatili zaidi ya wafanyakazi aliowaita wenye vyeti feki na hewa zaidi ya elfu 19!

Hakika Mzee ana haki ya kuminya uhuru wa kujieleza. Maswali ni mengi huku majibu yakiwa hakuna. Bora ya JK.
Aisee
 
Back
Top Bottom