Huyu Mzee kiukweli anazingua. Mwaka wa tano huu anatufanyia tu dhihaka sisi Wafanyakazi, kisa anajenga miundombinu!
Halafu kumbe huko kwenye hiyo miundombinu yenyewe, hela za kujengea anakopa!! Sasa hela za kodi zaidi ya tirioni 1.4 za kila mwezi anazojisifia, huwa zinafanyia nini!!
Atasemani kwa ajili ya kulipia mishahara!! Ya wafanyakazi gani? maana hakuna ajira kwa wahitimu wa vyuo kwa sasa kama ilivyokua enzi za JK, hakuna nyongeza ya mishahara wala kupandishwa madaraja kwa wakati kama ilivyokua enzi za JK, hakuna annual incriment, alitumbua kikatili zaidi ya wafanyakazi aliowaita wenye vyeti feki na hewa zaidi ya elfu 19!
Hakika Mzee ana haki ya kuminya uhuru wa kujieleza. Maswali ni mengi huku majibu yakiwa hakuna. Bora ya JK.