DENZEL OMONDI ambaye kwenye list ambayo walishirki kujipost bungeni huko kenya naye amefariki na kutupwa

Kama inafaa kugharamia mabadiliko wala sioni ajabu. Yeye ni sehemu ya hiyo gharama na ninaamini hata na wao walijua kuwa watakuwa na gharama ya kulipa. Siku mabadiliko wanayoyalenga yakipatikana majina ya wahanga hawa yataandikwa kwa wino wa dhahabu.
Hata wakati watu wanapigania kujikomboa na kujitawala kutoka kwa wakoloni,wapo waliokuwa wanaona harakati hizo hazikuwa na maana lakini leo sio wao tu bali vizazi vyao vyote vinafurahia matunda ya sadaka ya uhai iliyotolewa na wapambania uhuru waliokufa katika mchakato.
 
Sawa nakukubalia lakini kweli kuwahukumu kwa uhai? ndio italipia hiyo hasra?
Walichofanya sio poa ile ni hasara ya mabillion , haya mambo usipenda kujiweka mbele mbele na conscious za kishamba utapotea .


Kuna jamaa walisababisha mgomo na vurugu pale udsm miaka ya 90's mpaka leo vyeti vyao vina alama kila wanapoenda wanashindwa kusoma Masters , sio wote ila wale walijifanya waratibu wa mgomo kwa kukaa mbele.
 
kama umesoma iki kitabu kuna sehemu anasema "chembe ya ngano bila kufa iwezi kuzaa ngano zengine"
 
kama umesoma iki kitabu kuna sehemu anasema "chembe ya ngano bila kufa iwezi kuzaa ngano zengine"
. View attachment 3038350
Nilitaka nimpe huu mfano, grain of wheat, nikahofia pengine ninkizazi cha dot com ambao fasihi kwao ni mtihani.
Anahofia gharama za items zilizoharibika wakati ruto anaharibu ndoto za kizazi chote kwa tamaa zake za kisiasa
 
Sioni kama kuharibu items za mabilion inalingana na gharama za kuharibu maisha ya wanachi wote,
Kodi na tozo zinaumiza jamii nzima ndo maana hata polisi huko wanaungana na waandamanaji maana ugumu wa maisha asiyeguswa ni mtawala peke yake.
 
A usual african with blaming game
 
Ww kwenu kuna majizi yako bungeni yanaiba na unayalipa mshahara kwa kodi yako na bado yanakutingia sheria za kipuuzi na tozo kibao je umeyashughulikia 🤯
 
tatizo lako unaona kama sifa ila wananchi wakiamua hata wewe ungeshauliwa kwa maneno yako.
unajua mapinduzi yakianza mpaka na chuki na visasi vinawakuta watu kama nyie mkifa
Mapinduzi yakianza..... Jibu swali, ni nani anayefaidika na mapinduzi; ni yule anayekufa wakati wa mapinduzi au ni wale wachache watakaounda Serikali???

Mimi binafsi siko tayari kufa na kujitoa muhanga ili "wapumbavu" wengine waingie Ikulu.

Hii dunia imejaa wapumbavu wengi sana, mkimtoa yule mmoja aliyeko Ikulu ataingia mwingine naye atafanya upumbavu mwingine.
 
nimekosa cha kukujibu maana sijui kama walikufikisha hapo ulipo leo unaona uhuru wa nchi yako
 
Baada ya wakoloni kuondoka, dhiki, umaskini, maradhi na ujinga waliondoka navyo?

Mbona mpaka leo tunalia shida, umaskini, maradhi nk.

Ninachotaka kusema, hakuna Serikali yoyote ya wanadamu itakayomaliza shida na kuondoa kero zote za wananchi isipokuwa Serikali ya MUNGU.

Tumeona mabadiliko ya Serikali kwenye nchi zingine, mfano wa karibu kabisa ni hapo Kenya. Tokea mwaka 2000 mpaka leo wameshabadili Serikali mara 3, lakini hakuna cha ziada walichopata. Matatizo yao bado yanaongezeka kila uchwao.

Sasa jiulize tena hili swali, unajitoa muhanga kwa faida ya nani?? Kwa faida yako au kwa faida ya yule anayeingia IKULU????
 
Changamoto kenya wapo nayo ni kuwa hawana kiongozi mkuu wa maandamano, kila mtu anayeandamana yupo level moja na mwingine.

Wakiamua kufanya hivi watamaliza waandamanaji wote.
Na Nchi itatumbukia mahala ambako kuitoa itakuwa vigumu sana , hata majirani hatutakuwa salama maana ni lazima tuwapokee wasio na nguvu za kujitetea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…