Mac Alpho
JF-Expert Member
- Aug 5, 2019
- 13,953
- 27,825
Hapo siwezi kukupinga mkuu,kuhusu swala la uthubu yuko vizuri sana na angeweza kuwa sehemu kubwa tu.Kuna wakati alianza kufanya vitu vya ajabu mpaka nikahisi labda kachezewa akili.Ila to be honest, ni mtu wa kuthubutu kafanya makubwa kwa age yake hata kama hayamletea matokeo.
Alishawahi kupokelewa kwenye mkutano mkubwa na Kinana na Nape wa CCM. Ingekuwa awamu hii ya machizi, probably angekuwa mkuu wa Mkoa.
Aligombea ubunge Lushoto 2010 enzi hizo ndiyo vijana wameanza kuwa moto na mageuzi. Huwezi kuitaja BAVICHA Tanga bila kumtaja jamaa.
Alikuwa kiongozi wa vijana Taifa ( NCCR Mageuzi ) na mjumbe wa Mkutano mkuu na pia kabla hajafungwa alikuwa ni mwalimu Mkolani.
Ni vijana wangapi wenye uthubutu wa aina hii nchi hii ??
Sema tu jamaa ni sijuo amechezewa, ameshindwa kabisa kutunza anachokipata.
Nilipokuwa general Manager SUMA lake zone, niliwahi kumuita ofisini tukapiga story mbili tatu, huku lengo ikiwa ni kumuonya kuhusu swala la kuikashifu serikali bila kujilinda kwa namna yoyote ile, baada ya pale nikaja kusikia kijana kakamatwa.
Nafikiri kwasasa kichwa chake hakiko vizuri, hasa nikiangalia vimbwanga anavyokuja navyo kila siku.