Deo Kisandu kafungwa jela?

Deo Kisandu kafungwa jela?

Jamii haipo informed.
Masikini mama yake, huyu mama kwa uzoefu wangu alikaa na ndugu wakaamua kumfungulia hii kesi kwa nia njema kabisa ya kumuokoa, kwa uzoefu nilio nao, itakuwa Deo alianza kuwa violent mtaani kiasi watu walishapanga kumfanya vibaya au hata kumuua kabisa.
Kitendo cha huyu mama kumfungulia hii kesi ilikuwa ni mkakati wake kumuondoa mtaani akafungwe akiamini huko atakuwa salama zaidi.
Kumuanzishia matibabu mgonjwa wa akili nchini Tanzania ni kati ya vitu vigumu sana kuwezekana. Mtu anakuwa violent mnaenda kumpeleka mnashangaa jioni au kesho yake wamemuachia na amerudi nyumbani, wakiwa wamemfungashia dawa. Labda uwe na connections otherwise ni ngumu sana mgonjwa wako kupokewa na kupewa huduma stahiki. Hivyo kwenye issue ya Kisandu ndipo wanafamilia hukutana na kujadili na ili kumuokoa na kuhakikisha ndugu yao anakuwa salama huona ni afadhali wamtungie hata kesi ili afungwe aondolewe mitaani maana huko watampoteza haraka sana.
Keako Dkt. Gwajima D tunaomba uliangalie hili pia, kuna mahala jamii inakwama. Shirikiana na Waziri wa Afya mtafute namna ya kuwasaidia watu wanaokumbea na changamoto za afya ya akili.
I don't buy the story, waulize waliokaa jela kama unaweza kuthubutu kumpeleka ndugu yako jelar kwa sababu yoyote ile.
 
Ni kweli Kisandu aliwekwa ngome ,akatoka .Kwa sasa akili haiko sawa ni wakufungwa kamba .Na haeleweki anapatikana wapi.Hizi taarifa kanipa bro mmoja wa maskani huko.Nikirudi likizo ntafatilia zaidi.Huyu homeboy kasoma na wajomba zangu .Inasikitisha sana.
 
Wakuu, kwema?
Nimemkumbuka mwamba Deo Kisandu na namna aliburudisha hapa jukwaani na ikabidi ni Google taarifa zake. Nimekutana na hukumu ya mahakama kuwa alifungwa miaka Saba jela kwa kosa la kumtukana mama yake kuwa ni mchawi baada ya kukatazwa kuuza kitanda alipo kuwa akiishi na mama yake kahama.

Natamani nikamsalimie, naomba mwenye taarifa za magereza aliopo atujuze.
 

Attachments

  • Screenshot_20211123-125139.png
    Screenshot_20211123-125139.png
    130.7 KB · Views: 8
Alifukuzwa kazi mwaka 2017 nadhani na akashtakiwa kutukana mtandaoni Facebook, akafungwa miaka mitatu, 2020 alitoka ndio kafungwa tena 2022 miaka Saba kwa kumtangaza mama yake mchawi baada ya kikatazwa kuuza kitanda alocho kua analalia kwa mama yake
Wanaosema kuwa alifia gelezani??
 
Back
Top Bottom