carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Makamu wa Rais Deogratius Ndejembi amekerwa na uzembe na taarifa zisizo sahihi zilizotolewa na Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Mkoa wa Mbeya kuhusu ufunguaji wa barabara ya njia nne.
Ndejembi ametoa kauli hiyo leo, Oktoba 17, 2026, baada ya kufanya ukaguzi wa kushtukiza eneo la Kabwe, kufuatilia utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa Oktoba 16, alipokutana na wakazi wa Mbeya Mjini.
Amehoji namna Serikali inavyotumia Sh40 bilioni katika mradi huo bila kuona matokeo yanayolingana na fedha hizo, akisisitiza kuwa kiasi hicho siyo kidogo kiasi cha kuruhusu uzembe na usimamizi dhaifu.
Makamu wa Rais amemtaka Waziri wa Ujenzi, Masanja Kadogosa kuhakikisha hatua za uwajibikaji zinachukuliwa dhidi ya Meneja wa Tanroads mkoani humo, Mhandisi Suleiman Bishanga, kwa kutoa taarifa alizozitaja kuwa za kupotosha kuhusu kuanza kufungua barabara eneo la Mdope.
Amesisitiza kuwa Serikali haitavumilia watendaji wanaotoa taarifa zisizo sahihi huku wananchi wakiendelea kukabiliwa na adha ya miundombinu
Chanzo : Mwananchi official