Deogratius Ndejembi akerwa na taarifa ya udanganyifu wa TANROADS Mbeya

Deogratius Ndejembi akerwa na taarifa ya udanganyifu wa TANROADS Mbeya

Makamu hana lolote. Ametoka sijui wapi huko kukimbiza mwenye anakuja kusumbua wataalam wetu. Bishanga ni msomi aliyebobea, Injinia..

Wanasema kala hela kumchafua tu. Wakandarasi wake wote hawajapewa hela, nani ataingiza mashine site kisa makamu anakuja Weekend?

Uzuri Bishanga hawezi kuchafuka sababu hakuna vocha ya mkandarasi inapita mikononi mwake kwamba kachelewesha.. Hazina watuma lot moja kwa moja kwa mkandarasi halafu leo wanaleta nywinywinywi ili wapigiwe makofi wanaonekane wanafanya kazi na serikali imetoa hela.

Kwanza Bishanga alitakiwa wamtie moyo aendelee kusimamia barabara aliyoanza nayo ya TANZAM sehemu ya Igawa hadi Tunduma inayojengwa kwa njia nne mpya, na kufanya jumla ya barabara hiyo kuwa ya njia sita na mradi umefika 50% Wanampeta kuongeza nguvu huku ili wamletee siasa.
50% ipi iliofikiwa unayoizungumzia hapa mkuu? Au wwwe ndio Bishanga. ?
 
Tanroads mbeya chini ya huyo eng.Bishanga wanamtesa sana mzee wangu ambaye ana mradi wa ujenzi wa barabara katika mojawapo ya wilaya za mkoa huo. Wanamtesa sana kuhusu malipo, vibaya mnoooo, acha limkute jambo tu
Pole sana ukitaka umfahamu vizuri Bishanga ulizia songwe. Kama hutoi posho hakulipi kwa wakati.
Kuna kampuni inaitwa Mbuya Constructors na NARMO ambayo Jana imemfukuzisha umeneja Meneja wa songwe ni kama hua wanampa mpunga mrefu jamaa.
Huyo Meneja ni Ntu ya Dili.
 
Tanroads mbeya chini ya huyo eng.Bishanga wanamtesa sana mzee wangu ambaye ana mradi wa ujenzi wa barabara katika mojawapo ya wilaya za mkoa huo. Wanamtesa sana kuhusu malipo, vibaya mnoooo, acha limkute jambo tu

Huo mradi mkilipaji mkuu ni nani ?Au naweza kusema mfadhili wa mradi ni nani?
 
Hilo liko wazi mameneja wengi Tanroad wanaendesha ofisi kama mali binafsi ukichanganya mtendaji mkuu kuwa wa kawaida ni shida tupu.

Meneja kazi yake kusaini certificate ambazo zimekamilika na kutuma kwa mlipaji atume vocha za malipo basi meneja mnamuonea bure
 
50% ipi iliofikiwa unayoizungumzia hapa mkuu? Au wwwe ndio Bishanga. ?
Hii barabara ilianza 2023, ilitakiwa ikamilike 2025 km29. Lakini hadi 2026 ilikuwa 24%. Bishanga kaenda Mbeya 2026 April. Sasa hivi ipo 50%. Barabara ilojengwa tangu 2023, kwanini lawama apewe Bishanga ambaye ana miezi 7? Mimi hoja yangu ipo hapo sio asilimia. Hata hivyo ni 45% hadi 50%. Una swali?
 
Makamu wa Rais Deogratius Ndejembi amekerwa na uzembe na taarifa zisizo sahihi zilizotolewa na Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Mkoa wa Mbeya kuhusu ufunguaji wa barabara ya njia nne.

Ndejembi ametoa kauli hiyo leo, Oktoba 17, 2026, baada ya kufanya ukaguzi wa kushtukiza eneo la Kabwe, kufuatilia utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa Oktoba 16, alipokutana na wakazi wa Mbeya Mjini.

Amehoji namna Serikali inavyotumia Sh40 bilioni katika mradi huo bila kuona matokeo yanayolingana na fedha hizo, akisisitiza kuwa kiasi hicho siyo kidogo kiasi cha kuruhusu uzembe na usimamizi dhaifu.

Makamu wa Rais amemtaka Waziri wa Ujenzi, Masanja Kadogosa kuhakikisha hatua za uwajibikaji zinachukuliwa dhidi ya Meneja wa Tanroads mkoani humo, Mhandisi Suleiman Bishanga, kwa kutoa taarifa alizozitaja kuwa za kupotosha kuhusu kuanza kufungua barabara eneo la Mdope.

Amesisitiza kuwa Serikali haitavumilia watendaji wanaotoa taarifa zisizo sahihi huku wananchi wakiendelea kukabiliwa na adha ya miundombinu
Chanzo : Mwananchi official

Kwa mara yabkwanza jabisa serikali ya Awamu ya 6 imeusemea mradi wa baravara ya njia nne Mbeya.
 
Bishanga wanamuonea bure. Huyo Waziri aseme hela kapeleka wapi. Sababu Waziri jana kaja kumpanga kwamba barabara itengenezwe usiku Makamu akija akute inafanya kazi. Usiku ule vifaa vingetoka wapi?

Waziri kamgeuka mbele ya kadamnasi

Makamu apambane na Waziri. Bishanga kasoma hotuba ya Waziri. Waziri ndo ajibu why hotuba inasema uongo. Halafu waziri anasema jana usiku ndo wamekubaliana watengeneze na maeneo mengine 32. Usiku kucha vifaa atatoa wapi?

Yaani ndani ya saa 24 utengeneze barabara maeneo 32 ili Makamu akija awakute wakandarasi kazini. Ingewezekanaje?

Ma CCM lolote liwakute ila kwa Bishanga hapana. Wasimletee siasa zao.
Alipokuwa Songwe alipewa Zawadi na Bashungwa kwa usimamizi mzuri wa barabara na kufanya kazi usiku nq mchana wakati wa el nino. Leo wanadai eti ndo anakwamisha miradi ya Serikali. Wakandarasi hafanyi kazi sababu hakuna hela. Helazaishia huko juu lawama zinaenda kwa anayechezea tope
Hah hah na yule mbunge wao wa Mbeya mjini na majigambo ya barabara kuwa kazi inafanyika, barabara zote za mkoa wa Mbeya ni mbovu, kule wilaya ya Kyela tuliambiwa barabara kuanzia Ibanda junction ya Kwenda Malawi hadi Kyela mjini ingefanywa kwa miezi sita na watu wakabomolewa nyumba zao ili kupisha ujenzi hadi leo hakuna cha barabara wala fidia hizo ni enzi za aliyekuwa mbunge wa wilaya Kyela Kinanasi na mkuu wa mkoa alikuwa Homera, waziri alikuwa yule mwenye maneno mengi Prof Mbalawa. Pamoja na umuhimu wake kwenye kilimo na kuwa ni lango la nchi za Malawi na Zambia mkoa wa Mbeya umeachwa nyuma sana unazidiwa na hata mkoa wa Iringa au Mkoa wa Njombe na hao akina Tulia walipokuwa kileleni walijua kufunga barabara kwa ving'ora na kuandaa matamasha ya kijinga tu na kusahau kuutetea mkoa wake, nae sasa kabaki kuimba mafumbo tu.
 
Hongera zake Ndejembi analitumikia Taifa Kwa umri sahihi kabisa ,bado ana nguvu na anaweza kuwa zaidi ya hapo
Unafikiri taarifa alizohoji alikuwa hana? Hajui hali ya miundombinu ya barabara katika jiji la Mbeya
 
Bishanga wanamuonea bure. Huyo Waziri aseme hela kapeleka wapi. Sababu Waziri jana kaja kumpanga kwamba barabara itengenezwe usiku Makamu akija akute inafanya kazi. Usiku ule vifaa vingetoka wapi?

Waziri kamgeuka mbele ya kadamnasi

Makamu apambane na Waziri. Bishanga kasoma hotuba ya Waziri. Waziri ndo ajibu why hotuba inasema uongo. Halafu waziri anasema jana usiku ndo wamekubaliana watengeneze na maeneo mengine 32. Usiku kucha vifaa atatoa wapi?

Yaani ndani ya saa 24 utengeneze barabara maeneo 32 ili Makamu akija awakute wakandarasi kazini. Ingewezekanaje?

Ma CCM lolote liwakute ila kwa Bishanga hapana. Wasimletee siasa zao.
Alipokuwa Songwe alipewa Zawadi na Bashungwa kwa usimamizi mzuri wa barabara na kufanya kazi usiku nq mchana wakati wa el nino. Leo wanadai eti ndo anakwamisha miradi ya Serikali. Wakandarasi hafanyi kazi sababu hakuna hela. Helazaishia huko juu lawama zinaenda kwa anayechezea tope
Tena watuachie my wetu waache upumbavu, alafu wakati huo ni kumtafuta mkandarasi maana Tanroads hawana machines wala operators wa kusema watagawa watendakazi wagawanyike huku na huko, na wananchi wajue kabla ya kuongea inamaana Eng Bishanga amewasiliana na waziri mwenye dhamana atajibu nini! Hata iyo umbwa enye kuuliza inajua kila kitu maana vikao vya budget wanakaa pamoja iweje leo ajifanye hajui lolote
 
Hilo liko wazi mameneja wengi Tanroad wanaendesha ofisi kama mali binafsi ukichanganya mtendaji mkuu kuwa wa kawaida ni shida tupu.
Umewahi kufanya kazi Tanroads? Umewahi kujua meneja wa Tanroads anafanyaje kazi? Umewahi kujua fedha zinaingiaje kwa ajili ya miradi? Ungefyata tu ndugu yangu yule jamaa alisema "no research no right to speak"
 
Huyo ndejembi Hana muda nakuhakikishieni hanganya Hua hapendi watu wa kuhoji hoji yeye anataka kama mmeamua muwe wezi basi Ni kuiba kwenda mbele mambo ya kuhoji hoji ili kujisafisha kisiasa hataki

Hata mwigulu Kazi anayo unajifanya mzalendo kwa hanganya
 
Tanroads mbeya chini ya huyo eng.Bishanga wanamtesa sana mzee wangu ambaye ana mradi wa ujenzi wa barabara katika mojawapo ya wilaya za mkoa huo. Wanamtesa sana kuhusu malipo, vibaya mnoooo, acha limkute jambo tu
Na hujui Eng Bishanga anafanya kazi chini ya waziri na katibu wake? Unahisi meneja wa mkoa atapokea pesa ya mradi na asilipe makandarasi? Ukipewa nafasi ya meneja wa mkoa wa Mbeya Tanroads bora hata ukae HQ ukasome magazeti kuliko kuitwa meneja wa Tanroads mkoa wa Mbeya...amepokea mkoa barabara zote vipengele na bado fedha haziji kwa wakati na vikao wanakaa na hao hao mawaziri situation yote wanaijua usione anaropokewa pale ni basi tu
 
Back
Top Bottom