Deogratius Ndejembi akerwa na taarifa ya udanganyifu wa TANROADS Mbeya

carbohydates

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
260
Reaction score
607
Makamu wa Rais Deogratius Ndejembi amekerwa na uzembe na taarifa zisizo sahihi zilizotolewa na Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Mkoa wa Mbeya kuhusu ufunguaji wa barabara ya njia nne.

Ndejembi ametoa kauli hiyo leo, Oktoba 17, 2026, baada ya kufanya ukaguzi wa kushtukiza eneo la Kabwe, kufuatilia utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa Oktoba 16, alipokutana na wakazi wa Mbeya Mjini.

Amehoji namna Serikali inavyotumia Sh40 bilioni katika mradi huo bila kuona matokeo yanayolingana na fedha hizo, akisisitiza kuwa kiasi hicho siyo kidogo kiasi cha kuruhusu uzembe na usimamizi dhaifu.

Makamu wa Rais amemtaka Waziri wa Ujenzi, Masanja Kadogosa kuhakikisha hatua za uwajibikaji zinachukuliwa dhidi ya Meneja wa Tanroads mkoani humo, Mhandisi Suleiman Bishanga, kwa kutoa taarifa alizozitaja kuwa za kupotosha kuhusu kuanza kufungua barabara eneo la Mdope.

Amesisitiza kuwa Serikali haitavumilia watendaji wanaotoa taarifa zisizo sahihi huku wananchi wakiendelea kukabiliwa na adha ya miundombinu
Chanzo : Mwananchi official

Your browser is not able to display this video.
 
Bishanga wanamuonea bure. Huyo Waziri aseme hela kapeleka wapi. Sababu Waziri jana kaja kumpanga kwamba barabara itengenezwe usiku Makamu akija akute inafanya kazi. Usiku ule vifaa vingetoka wapi?

Waziri kamgeuka mbele ya kadamnasi

Makamu apambane na Waziri. Bishanga kasoma hotuba ya Waziri. Waziri ndo ajibu why hotuba inasema uongo. Halafu waziri anasema jana usiku ndo wamekubaliana watengeneze na maeneo mengine 32. Usiku kucha vifaa atatoa wapi?

Yaani ndani ya saa 24 utengeneze barabara maeneo 32 ili Makamu akija awakute wakandarasi kazini. Ingewezekanaje?

Ma CCM lolote liwakute ila kwa Bishanga hapana. Wasimletee siasa zao.
Alipokuwa Songwe alipewa Zawadi na Bashungwa kwa usimamizi mzuri wa barabara na kufanya kazi usiku nq mchana wakati wa el nino. Leo wanadai eti ndo anakwamisha miradi ya Serikali. Wakandarasi hafanyi kazi sababu hakuna hela. Helazaishia huko juu lawama zinaenda kwa anayechezea tope
 
Amehoji namna Serikali inavyotumia Sh40 bilioni katika mradi huo bila kuona matokeo yanayolingana na fedha hizo, akisisitiza kuwa kiasi hicho siyo kidogo kiasi cha kuruhusu uzembe na usimamizi dhaifu.
Wamewalea wenyewe kula urefu wa kamba
 
Tatizo ccm hawataki watu wenye akili waluo serious na maendeleonya nchi hii.
Japo sina uhakika kama huyo makamu ana akili wala kama yupo serious. Maana hawa wote ni waigizaji tu
Makamu hana lolote. Ametoka sijui wapi huko kukimbiza mwenye anakuja kusumbua wataalam wetu. Bishanga ni msomi aliyebobea, Injinia..

Wanasema kala hela kumchafua tu. Wakandarasi wake wote hawajapewa hela, nani ataingiza mashine site kisa makamu anakuja Weekend?

Uzuri Bishanga hawezi kuchafuka sababu hakuna vocha ya mkandarasi inapita mikononi mwake kwamba kachelewesha.. Hazina watuma lot moja kwa moja kwa mkandarasi halafu leo wanaleta nywinywinywi ili wapigiwe makofi wanaonekane wanafanya kazi na serikali imetoa hela.

Kwanza Bishanga alitakiwa wamtie moyo aendelee kusimamia barabara aliyoanza nayo ya TANZAM sehemu ya Igawa hadi Tunduma inayojengwa kwa njia nne mpya, na kufanya jumla ya barabara hiyo kuwa ya njia sita na mradi umefika 50% Wanampeta kuongeza nguvu huku ili wamletee siasa.
 
Me binafsi naona bado kuna madhaifu mengi kuhusu mifumo yetu, mpaka ufanye dhihara za kushutukiza ndiyo ujue madhaifu, wakae waone wanawekaje mifumo sahihi kuweza kupata taharifa mapema kabla miladi haija kwenda mbali
 
Hilo liko wazi mameneja wengi Tanroad wanaendesha ofisi kama mali binafsi ukichanganya mtendaji mkuu kuwa wa kawaida ni shida tupu.
 
Na watanzania tutakavyomsifia sasa utazani kuna la maana litafanyika.
Hiyo barabara kama walikuwa hawawezi irekebisha kwa wakati ni bora wangeacha ile ile ya zamani.

Makamu wa rais alikuwa anajua vizuri mda wa hiyo barabara toka imeanza kujengwa, nikazani atachukua hatua zozote kwa uzembe wa mkandarasi lakini hamna kitu. Saizi ni upigaji
 
Hawa wanafanya maagizo tu. Ni muda gani hiyo barabara imekuwa iklisua sua serikali inasema haina fedha?

Wajinga wote hawa, juu hadi chini. Raisi wetu raisi wetu, umbea tu wa kujipendekeza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…