zipompa
JF-Expert Member
- Aug 19, 2014
- 12,508
- 27,663
wewe wa 82 upo hapa kushabikia ujinga ujinga9 sept 2026 anaingia ofisini kijana wa 1983
Ccm ni kubwa kuliko mtu.

Mama anajaza vibenten vimzunguke ili asipate pressure kila akiamuka asubuhi asikie "shikamoo mama nchi iko shwari". Huku mwigulu huku Ndejembi.Hongera kwa Deogratius Ndejembi.
Ndejembi anachukua nafasi Emmanuel Nchimbi aliye jiuzulu hujambo nafasi ya Umakamu wa Rais na Utumishi wa Umma.
View attachment 3657631
Je, Deogratius Ndejembi ni nani?
Deogratius John Ndejembi ni mwanasiasa wa Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mbunge wa Jimbo la Chamwino, Dodoma.
Elimu:
Alisoma shule ya msingi Cannon Andrea Mwaka, kisha Kigurunyembe/Jamhuri Secondary na Merton College.
Baadaye alisoma International Relations katika University of Lincoln na kupata Advanced Diploma kutoka Institute of Administrative Management.
Siasa:
Ni mwanachama wa CCM na anaiwakilisha Chamwino Bungeni.
Tarehe 07 Julai, 2016 Hayati Magufuli alimteua Bw. Deogratius John Ndejembi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma.
Mwaka 2021 Samia aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI
Mnamo Novemba 17, 2025, Samia Suluhu Hassan, alimteua Deogratius Ndejembi kuwa Waziri wa Nishati
Kabla ya kuwa Waziri, alikuwa Naibu Waziri wa TAMISEMI.
Machi 31, 2024:
Samia Suluhu Hassan alimhamisha kutoka Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu)
MY TAKE;
Pipa na mfuniko.
Duh 😂We huoni kichwwa kama kimebumbwa huko visiwani?
Umeona eehAiseee kama Deo anaweza kuwa Rais kumbe hata Mimi ni swala la muda tu aiseeeee..
Kumbe mambo sio magumu kabisa
Ccm = dolaHuyo dogo wanamuingiza kwenye lots of complications. Wangemuacha akue na siasa mpya wazee mmalizane vizuri. Hivi hivi wanamuweka kwenye njia ngumu sanaaaa
Hongera nyingi kwake! Tunamtakia utumishi wa umma uliotukukaHongera kwa Deogratius Ndejembi.
Ndejembi anachukua nafasi Emmanuel Nchimbi aliye jiuzulu hujambo nafasi ya Umakamu wa Rais na Utumishi wa Umma.
View attachment 3657631
Je, Deogratius Ndejembi ni nani?
Deogratius John Ndejembi ni mwanasiasa wa Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mbunge wa Jimbo la Chamwino, Dodoma.
Elimu:
Alisoma shule ya msingi Cannon Andrea Mwaka, kisha Kigurunyembe/Jamhuri Secondary na Merton College.
Baadaye alisoma International Relations katika University of Lincoln na kupata Advanced Diploma kutoka Institute of Administrative Management[alisoma International Relations – University of Lincoln (2006–2009) na Advanced Diploma in Administrative Management (2009–2012)]
Siasa:
Ni mwanachama wa CCM na anaiwakilisha Chamwino Bungeni.
Tarehe 07 Julai, 2016 Hayati Magufuli alimteua Bw. Deogratius John Ndejembi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma.
Katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 alipita bila kupingwa kwani wapinzani wake wote waliemguliwa. Katika kura za maoni ndani ya CCM za kuwania ubunge mwaka 2020, Deogratius (Deo) Ndejembi alipata kura 422 katika Jimbo la Chamwino (wakati huo likiitwa Chilonwa). Alimshinda aliyekuwa Mbunge Joel Mwaka aliyepata kura 99.
Mwaka 2021 Samia aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI
Mnamo Novemba 17, 2025, Samia Suluhu Hassan, alimteua Deogratius Ndejembi kuwa Waziri wa Nishati
Kabla ya kuwa Waziri, alikuwa Naibu Waziri wa TAMISEMI.
Machi 31, 2024:
Samia Suluhu Hassan alimhamisha kutoka Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu)
MY TAKE;
Pipa na mfuniko.
Mh ametufanyia Simplification sana hadhi na taasisi ya Urais...!Umeona eeh
Angeteuliwa mzee wasira hapo mngelalama kwanini wazee wanaoenda kufa muda sio mrefu wanapewa shavuHuyo dogo wanamuingiza kwenye lots of complications. Wangemuacha akue na siasa mpya wazee mmalizane vizuri. Hivi hivi wanamuweka kwenye njia ngumu sanaaaa
TOKA MAKTABA
Mzee Ndejembi : Wengi tulimuunga mkono Lowassa ndani ya CCM siyo Magufuli
Jumatatu, 27 Juni , 2016 —
View attachment 3657650
Mzee Pancras Mtemi Ndejembi
Mwanasiasa Mkongwe, Pancras Mtemi Ndejembi akizungumza alipokuwa akifanyiwa mahojiano maalum na waandishi wa gazeti la Mwananchi, nyumbani kwake mjini Dodoma, hivi karibuni. Picha na Edwin Mjwahuzi
Pancras Mtemi Ndejembi ambaye pia aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya katika miaka ya 1980 hadi 2007,
CCM wa Mkoa wa Dodoma, alisema aliamua kumuunga mkono Edward Lowassa baada ya kuona chama chake kinapotoka na kwenda mrama .. SOMA ZAIDI:
29 December 2018
Mwanasiasa mkongwe Pancras Mtemi Ndejembi afariki dunia mkoani Dodoma
View: https://m.youtube.com/watch?v=TCGZD0aLdwQ
Mwanasiasa mkongwe aliyewahi kushika wadhifa wa ukuu wa Wilaya DC kwenye Serikali ya awamu ya kwanza sambamba na kuwa mwenyekiti wa CCM mkoani Dodoma hadi mwaka 2007 amefariki dunia hii leo akiwa anapokea matibabu.
Pancras Mtemi Ndejembi amefariki katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma alikopelekwa jana Ijumaa baada ya hali yake kubadilika ghafla.
Mtoto wa Marehemu, Edna Ndejembi amesema baba yake alikuwa anasumbuliwa na kifua kubana ambapo alilazwa katika Hospitali ya DCMC ya jijini Dodoma na kuruhusiwa juzi Alhamisi akiwa ameimarika kiafya.
TOKA MAKTABA :
April 23, 2014
Kete ya Muungano imebaki mkononi mwa CCM na CUF
mwanasiasa mkongwe, Pancras Mtemi Ndejembi (82)Picha: Mwananchi
Dodoma. “Ni vyama viwili nchini kwa sasa ndivyo vilivyoshikilia suala la Muungano, kama viongozi wake wakikaa pamoja na kukubaliana, hakuna shida.
Vyama hivyo, CCM na CUF vimeshika kete na hatima ya Muungano wetu.” Haya ni maneno ya mwanasiasa mkongwe, Pancras Ndejembi.
Ndejembi (82) ni miongoni mwa wanasiasa wakongwe ambao walifanya kazi serikalini tangu kipindi cha uongozi wa awamu ya kwanza ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na ambao wamekuwa miongoni mwa wazee wanaoheshimika kwa misimamo yao.
Katika mahojiano yaliyofanyika nyumbani kwake mjini Dodoma, mwanasiasa huyo alizungumzia Muungano kwa mtazamo mpana kwamba una faida kubwa kiasi ambacho haupaswi kuvunjwa.
Katika kipindi hiki cha mchakato wa katiba mpya, kumekuwa na mjadala wenye hoja zinazopingana kuhusu Muungano, baadhi wakisema una faida na wengine wakipinga kuwa hawajaona faida zake kwa miaka hamsini ya uhai wake.
Hata hivyo, lipo kundi ambalo linapinga kauli hiyo kwa kutumia kauli ya umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu ambalo kwa sehemu ni kundi la viongozi walioko madarakani.
Pamoja nao, wapo wazee wa siku nyingi ambao katika kipindi cha Muungano walikuwepo na walishuhudia Tanganyika na Zanzibar zikiungana pamoja na kutenegeneza kitu kilichoitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katikka mazungumzo hayo, Pacras Mtemi Ndejembi anaelezea kile alichokiita kuwa siri ya kuondoa migogoro na kuimarisha Muungano, siri ambayo anasema imeshikwa na vyama vya siasa.
Muungano una kero nyingi
Hata hivyo, kabla ya mazungumzo zaidi mwanasiasa huyu anakiri kuwepo kwa kero nyingi katika Muungano, lakini bado anaamini kuwa mambo mengi yanaweza kumalizwa kwa njia ya mazungumzo.
Mahojiano kamili na Mzee Pancras Mtemi Ndejembi
Swali: Mzee Ndejembi pole na majukumu ya kila siku. Vipi habari za shamba?
Jibu: Sijapoa bado, lakini namshukuru Mungu kwamba pamoja na kuwa umri wangu ni sawa na jua la machweo, lakini najikongoja kuhakikisha mambo yanakuwa mazuri hapa nyumbani.
Swali: Tunaelekea katika maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano, unautazama vipi Muungano huo?
Jibu: Bado ni Muungano imara ambao una nguvu, lakini pia bado ni Muungano wa mfano katika maeneo mengi duniani na watu wanatakiwa kujifunza kwa hilo.
Swali: Ukiwa miongoni mwa viongozi waliokuwa mstari wa mbele kuupigania Muungano wakati wote, una lolote la kujivunia zaidi kwamba nchi imefaidika nalo.
Jibu: Kuna majaribio mengi ya kutaka kuzipindua serikali zetu hizi mbili, lakini yamekuwa yakishindikana kutokana na umoja na mshikamano tulio nao.
Swali: Unaweza kukumbuka tukio lolote ambalo unadhani bila ya kuwa na Muungano lingeisumbua zaidi nchi? Je, uwepo wa Muungano ulinusuru vipi tukio hilo.
Jibu: Kinachoniuma zaidi ni mauaji ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Abeid Aman Karume (1972). Jaribio la kupindua Serikali la mwaka 1970 na lile la Zanzibar 1984 pamoja na uvamizi katika nchi yetu uliofanywa na Idd Amin aliyekusudia kuimega ardhi yetu mwaka 1978.
Haya yote tulifanikiwa kwa umoja, kwani bila umoja hata lile la njaa ya mwanzoni mwa miaka ya 1970 bado lingeweza kutusumbua zaidi. Udugu na mshikamano tuliokuwa nao ndio umetufikisha hapa leo.
Swali: Kuna tetesi kwamba Muungano huu umepoteza mwelekeo wake na baadhi wanapendekeza kuwa uvunjwe ili kila mshiriki achukue kilicho chake. Ni nini ukweli kuhusu hili?
Jibu: Sioni sababu za kuwa na uamuzi wa kuuvunja Muungano. Katika nchi za Afrika watu wanataka kuungana ili kutengeneza nguvu ya kupambana na maadui, halafu sisi wa damu moja tuvurugane?
Muungano ukivunjika Watanzania watarudi nyuma hatua nyingi na kuanza kusonga mbele itakuwa ni tatizo tena.
Swali: Lakini hili jambo la kwamba wengine wanaburuzwa ndani ya Muungano unalizungumziaje wakati huu?
Jibu: Siwezi kusema wanaburuzwa, lakini ninachokiamini ziko changamoto nyingi ambazo wao wanaita ni kero za muungano ambazo zinaweza kutatuliwa kama watu wataamua kukaa pamoja.
Unajua mwandishi, hakuna jambo ambalo linashindikana kama mtu akiamua kulimaliza mwenyewe kwa hiyari na utashi wake, lakini wao wanataka kumaliza kwa taratibu za kisheria ambazo wengi wanahisi ni kulamishwa.
Swali: Uhiyari upi unaouzungumzia wewe ambao unadhani ukitumika unaweza kuondosha kelele na kama utaratibu huo haujawahi kutumiwa?
Jibu: Unajua walioshikilia masuala ya Muungano kama nilivyosema awali ni Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF) vilivyopo katika malumbano ya kihistoria.
Swali: Kwa nini unataja CUF na CCM wakati kuna vyama vingine ambavyo vina wawakilishi hadi bungeni na vinaonekana kukubalika kwa wananchi wengi.
Jibu: Angalieni historia wanangu, vyama hivyo ndivyo vilivyokamata kila kitu kutokana na historia yake kwani hakuna chama kingine kinachoweza kupinga muundo wa muungano kuwa na nguvu kuliko CUF?
Swali: Mzee Ndejembi, hawa watu wamekuwa wakikutana mara zote na kuzungumza kiasi cha kukubaliana hadi kuingia katika serikali ya umoja, je, kuna mazungumzo mengine zaidi ya hayo?
Jibu: Hawa watu wamekuwa wakikutana kutafuta mwafaka wa kuondoa migogoro inayotokana na chaguzi za visiwani sio kwamba wamekuwa wakizungumzia masuala ya Muungano, hapana.
Ndugu zetu hawa wanakutana na kufanya mazungumzo yao huko. Ingawa watu wa Tanzania Bara wanashiriki, ukweli ni kwamba hawazungumzii Muungano zaidi.
Kuwaweka pamoja CCM na CUF ni sawa na kukubaliana kwa Tanganyika, Pemba na Unguja kuwa wanaweza kuishi pamoja kama ndugu wa baba mmoja.
Swali: Kwani kitu gani zaidi unachoona kinasumbua na kuwapa watu mashaka juu ya Muungano wetu?
Jibu: Hali ya kutoaminiana katika kada ya viongozi, wako wale wasioupenda Muungano na pengine wangependa usiwepo. Mambo ya udini, ukabila, ukanda, utaifa kwa maana ya Utanganyika na Uzanzibari ambayo yote yanabomoa misingi ya Muungano wetu.
Hata hivyo, Ndejembi anazungumzia pengo kubwa la wenye nacho na wasio nacho ambalo pia linapaswa kuangaliwa kwenye masuala ya muundo wa Muungano.
Anashauri suala la ajira liangaliwe siyo tu katika utengenezaji wa katiba bali hata katika muundo wa Muungano ili vijana wa Tanzania waweze kufaidi kwa pamoja matunda ya Muungano wao.
Mkongwe huyo, ambaye aliwahi kuwa mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Dodoma na mwenyekiti wa wenyeviti wa chama hicho Tanzania, anashauri dhamira ya dhati iwepo kwa viongozi katika kuondoa chuki na migogo ya udini na ukabila inayoanza kuota mizizi kwa wananchi wan chi hii.
Bado anayakumbuka maneno ya Mwalimu Nyerere aliyosema miaka michache kabla ya uhuru kuwa ni heri uhuru wa Tanganyika ucheleweshwe ili nchi za Afrika Mashariki zipate uhuru kwa pamoja kwa lengo la kuuda shirikisho la pamoja.
Chanzo: Mwananchi
Na ndio nalpKwaiyo rais akikata moto uyo ndio atakua pelezident?