Deogratius Ndejembi ateuliwa kuwa Makamu wa Rais

Deogratius Ndejembi ateuliwa kuwa Makamu wa Rais

Kwa hyo akirudi anabadilika kuanzia airport
 

Attachments

  • Screenshot_20260826-233312.png
    Screenshot_20260826-233312.png
    535.8 KB · Views: 14
Mimi ni mwanachama kabisa wa CCM na nalipia card yangu ya mwanachama.

Lakini ukweli CCM tuweni makini kabisa Maji yana mtindo wa kufata njia Sasa naomba maji yasifate njia mpya maana itakuwa balaa.

Aibu naona Mimi Wacha nijifiche
 
Mbona kama elimu yake ya hapa na pale?

Aiseee kama Deo anaweza kuwa Rais kumbe hata Mimi ni swala la muda tu aiseeeee..
Kumbe mambo sio magumu kabisa
Siku moja nilimtania "Tonito" kuwa yeye hana mpango na "ofisi numero uno", alichonijibu ni kuwa " Mungu ndiye apangaye".

Leo ndugu yake ni VP!
 
Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imemteua Deogratius Ndejembi kushika nafasi ya Makamu wa Rais, nafasi ambayo ilibaki wazi baada ya aliyekuwepo, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi kutangaza kujiuzulu 25, Agosti 2026.
Huo ni uvunjifu wa Katiba ya mwaka 1977.
Kwa mujibu wa Ibara ya 50(4), ni Rais anatakiwa kumteua mtu mwingine kuwa Makamu wa Rais ndani ya siku 14 tangu nafasi hiyo kuwa wazi.
Hakuna mahali kamati kuu ya chama imepewa jukumu hilo!
 
Kabla ya kuwa Waziri, alikuwa Naibu Waziri wa TAMISEMI.

Machi 31, 2024: Samia Suluhu Hassan alimhamisha kutoka Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu)
Kwenye haya maandishi hii rangi mlioweka sijui ni copy and paste haioneshi maandishi

Moderator
 
Elimu yake Sasa.... Ilibidi iwe hivi...
1988 - 1994 Drs I - VII (PEE)
1995 - 1998. Kdt I - Kdt IV (CSEE)
1999 - 2001 Kdt V - Kdt VI (ACSEE)
Kwa mtiririko huo wa usomaji, tayari tushawashwa huko. Ma-VP wengi huko nyuma ni madoctor...
Ngoja tusubiri maoni ya Mange akisema ni mpango wa Abdul...🤪🤪🤪
 
Huo ni uvunjifu wa Katiba ya mwaka 1977.
Kwa mujibu wa Ibara ya 50(4), ni Rais anatakiwa kumteua mtu mwingine kuwa Makamu wa Rais ndani ya siku 14 tangu nafasi hiyo kuwa wazi.
Hakuna mahali kamati kuu ya chama imepewa jukumu hilo!

kwani ameshaapishwa kuwa vp? au labda sijaelewa vizuri kwenye hiyo katiba? mpaka sasa hivi nafikiri siyo makamu wa raisi maadamu hajaapishwa bado, au? E.Nchimbi bado ni makamu mpaka hiyo septemba kwa jinsi nilivyoelewa ...
 
Hongera kwa Deo.

Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imependekeza na kupitisha jina la Waziri wa Nishati, Deogratius John Ndejembi, kuwa mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ndejembi anapendekezwa kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, ambaye amejiuzulu
View attachment 3657631
Je, Deogratius Ndejembi ni nani?

Deogratius John Ndejembi ni mwanasiasa wa Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mbunge wa Jimbo la Chamwino, Dodoma.

Deogratius John Ndejembi alizaliwa tarehe 12 Julai 1983.

Elimu:
Alisoma shule ya msingi 1988–1995: Cannon Andrea Mwaka, Primary School — CPEE

kisha 1996–1998: Kigurunyembe Secondary School — CSEE/Jamhuri Secondary na

2002–2004: Merton College — ACSEE

Baadaye alisoma International Relations katika University of Lincoln na kupata Advanced Diploma kutoka Institute of Administrative Management[alisoma International Relations – University of Lincoln (2006–2009) na Advanced Diploma in Administrative Management (2009–2012)]

Siasa:
Ni mwanachama wa CCM na anaiwakilisha Chamwino Bungeni.

Tarehe 07 Julai, 2016 Hayati Magufuli alimteua Bw. Deogratius John Ndejembi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma.

Katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 alipita bila kupingwa kwani wapinzani wake wote wa vyama vingine waliemguliwa.

Katika kura za maoni ndani ya CCM za kuwania ubunge mwaka 2020, Deogratius (Deo) Ndejembi alipata kura 422 katika Jimbo la Chamwino (wakati huo likiitwa Chilonwa). Alimshinda aliyekuwa Mbunge Joel Mwaka aliyepata kura 99.

Mwaka 2021 Samia aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI

Machi 31, 2024: Samia Suluhu Hassan alimhamisha kutoka Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu)

Mnamo Novemba 17, 2025, Samia Suluhu Hassan, alimteua Deogratius Ndejembi kuwa Waziri wa Nishati. Kabla ya kuwa Waziri, alikuwa Naibu Waziri wa TAMISEMI.


MY TAKE;
Pipa na mfuniko.
Hiyo nishati kasomea wapi? International Relations! Watu waliofeli wapenda kutothamini elimu kwa vile yeye amefika huko kwa bahati, na siku zote wanateua watu wasiowatishia kielimu. Waziri wa Nishati nategemea hata mambo ya mitambo ya nuklia ajue ABC zake!
 
Huyu hajasoma kabisa jamani! Mbona hivi jamani? Elimu yenyewe ni hii ya Bongo ambayo hata dokta hajui trab na trat!
Bunge lisimkubali huyu tutaingia aibu mbele za nchi! Tanzania ni nchi ya 10 Afrika Leo ina Waziri Mkuu 'functional illiterate'! Iheshimuni nchi, iheshimuni elimu.
 
Hiyo nishati kasomea wapi? International Relations! Watu waliofeli wapenda kutothamini elimu kwa vile yeye amefika huko kwa bahati, na siku zote wanateua watu wasiowatishia kielimu. Waziri wa Nishati nategemea hata mambo ya mitambo ya nuklia ajue ABC zake!
Uwaziri ni uongozi na si utaalam,wizara ina wataalam
 
Back
Top Bottom