Deogratius Ndejembi ateuliwa kuwa Makamu wa Rais

Nina ushuhuda na hilo jambo kuhusu huyu dogo kwenye madudu yake japo wengi hawamzingatii labda kwa sababu sio mtu wa media sana ila ana uchafu mwingi sana tena hapo kwenye wizara aliyoteuliwa mwaka 2024 Ina uchafu
Njoo DM mkuu
 
Hongera kwa Deo.

Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imependekeza na kupitisha jina la Waziri wa Nishati, Deogratius John Ndejembi, kuwa mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ndejembi anapendekezwa kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, ambaye amejiuzulu
View attachment 3657631
Je, Deogratius Ndejembi ni nani?

Deogratius John Ndejembi ni mwanasiasa wa Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mbunge wa Jimbo la Chamwino, Dodoma.

Deogratius John Ndejembi alizaliwa tarehe 12 Julai 1983.

Elimu:
Alisoma shule ya msingi 1988–1995: Cannon Andrea Mwaka, Primary School — CPEE

kisha 1996–1998: Kigurunyembe Secondary School — CSEE/Jamhuri Secondary na

2002–2004: Merton College — ACSEE

Baadaye alisoma International Relations katika University of Lincoln na kupata Advanced Diploma kutoka Institute of Administrative Management[alisoma International Relations – University of Lincoln (2006–2009) na Advanced Diploma in Administrative Management (2009–2012)]

Siasa:
Ni mwanachama wa CCM na anaiwakilisha Chamwino Bungeni.

Tarehe 07 Julai, 2016 Hayati Magufuli alimteua Bw. Deogratius John Ndejembi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma.

Katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 alipita bila kupingwa kwani wapinzani wake wote wa vyama vingine waliemguliwa.

Katika kura za maoni ndani ya CCM za kuwania ubunge mwaka 2020, Deogratius (Deo) Ndejembi alipata kura 422 katika Jimbo la Chamwino (wakati huo likiitwa Chilonwa). Alimshinda aliyekuwa Mbunge Joel Mwaka aliyepata kura 99.

Mwaka 2021 Samia aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI

Machi 31, 2024: Samia Suluhu Hassan alimhamisha kutoka Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu)

Tarehe 21 Julai 2024, Ndejembi aliteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , katika mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Samia Suluhu Hassan. Alimrithi Jerry Silaa.

Mnamo Novemba 17, 2025, Samia Suluhu Hassan, alimteua Deogratius Ndejembi kuwa Waziri wa Nishati. Kabla ya kuwa Waziri, alikuwa Naibu Waziri wa TAMISEMI.

MY TAKE;
Pipa na mfuniko.
Bila shaka naye ni Mkatoliki
 
Namkumbuka wakati akiteuliwa siku ya kwanza kua waziri mama alimwambia mwanangu nakutizama nakulea kwenye siasa wewe bado kijana hajatumia ata nguvu uyo kawa vice wazee wameachwa
Pia nakumbuka alimwambia anamwona kama bishoo.
 
Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imemteua Deogratius Ndejembi kushika nafasi ya Makamu wa Rais, nafasi ambayo ilibaki wazi baada ya aliyekuwepo, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi kutangaza kujiuzulu 25, Agosti 2026.
Okay..
 
Hongera kwa Deo.

Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imependekeza na kupitisha jina la Waziri wa Nishati, Deogratius John Ndejembi, kuwa mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ndejembi anapendekezwa kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, ambaye amejiuzulu
View attachment 3657631
Je, Deogratius Ndejembi ni nani?

Deogratius John Ndejembi ni mwanasiasa wa Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mbunge wa Jimbo la Chamwino, Dodoma.

Deogratius John Ndejembi alizaliwa tarehe 12 Julai 1983.

Elimu:
Alisoma shule ya msingi 1988–1995: Cannon Andrea Mwaka, Primary School — CPEE

kisha 1996–1998: Kigurunyembe Secondary School — CSEE/Jamhuri Secondary na

2002–2004: Merton College — ACSEE

Baadaye alisoma International Relations katika University of Lincoln na kupata Advanced Diploma kutoka Institute of Administrative Management[alisoma International Relations – University of Lincoln (2006–2009) na Advanced Diploma in Administrative Management (2009–2012)]

Siasa:
Ni mwanachama wa CCM na anaiwakilisha Chamwino Bungeni.

Tarehe 07 Julai, 2016 Hayati Magufuli alimteua Bw. Deogratius John Ndejembi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma.

Katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 alipita bila kupingwa kwani wapinzani wake wote wa vyama vingine waliemguliwa.

Katika kura za maoni ndani ya CCM za kuwania ubunge mwaka 2020, Deogratius (Deo) Ndejembi alipata kura 422 katika Jimbo la Chamwino (wakati huo likiitwa Chilonwa). Alimshinda aliyekuwa Mbunge Joel Mwaka aliyepata kura 99.

Mwaka 2021 Samia aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI

Machi 31, 2024: Samia Suluhu Hassan alimhamisha kutoka Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu)

Tarehe 21 Julai 2024, Ndejembi aliteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , katika mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Samia Suluhu Hassan. Alimrithi Jerry Silaa.

Mnamo Novemba 17, 2025, Samia Suluhu Hassan, alimteua Deogratius Ndejembi kuwa Waziri wa Nishati. Kabla ya kuwa Waziri, alikuwa Naibu Waziri wa TAMISEMI.

MY TAKE;
Pipa na mfuniko.
Mtoto mdogo sana ktk nafasi ya umakamu wa Rais.
 
..ana uzoefu gani ktk serikali au chama?

..ana sifa gani za ziada kumfanya astahili kuwa VP?

..Je, yuko tayari kuwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu ikiwa Mama atashindwa kutekeleza majukumu yake?
Dah siku hizi vyeo vinachezewa sana havina heshima tena kama ilivyokuwa zamani.
Sasa nimeelewa kwa nini wakina K.majaliwa walijiweka pembeni,walishaona Disco limeingia mmasai hakuna kitu kitakachnyooka
 
Kapata atakayeweza kumkontrol anavyotaka……maskini Makonda mama hakuwaza ata kumconsider umakamo
 
Mama anajaza vibenten vimzunguke ili asipate pressure kila akiamuka asubuhi asikie "shikamoo mama nchi iko shwari". Huku mwigulu huku Ndejembi.
Yeah anafanya vitu ili kujirahisishia usalama upande wake binafsi ila sio kwa maslahi ya nchi.
Maana yake hata siku akisema nikiondoka naombeni Rais awe mtoto wangu wote watakubali hakuna wa kupinga mwenye nguvu hii alibaki Nchimbi tu ndio huyo katoka
 
Back
Top Bottom